MEM Bulletin 51

download MEM Bulletin 51

of 12

Transcript of MEM Bulletin 51

  • 8/9/2019 MEM Bulletin 51

    1/12

    BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali

    kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizar a ya Nishati na MadiniWasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263

    au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    HABARI ZA

    NISHATI &MADINI

    Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - 23-29 Januari , 2015

    JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

    Waziri wa Nishatina Madini, ProfesaSospeter Muhongo

    Naibu Waziri wa Nishati naMadini, anayeshughulikiaMadini Stephen Masele

    Naibu Waziri wa Nishati naMadini anayeshughulikiaNishati, Charles Kitwanga

    Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO,Mhandisi FelchesmiMramba

    Mkurugenzi Mkuu waREA, Dk. LutenganoMwakahesya

    Wabunge

    SomahabariUk.2

    Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

    WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO-Uk2

  • 8/9/2019 MEM Bulletin 51

    2/12

    2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    NISHATI/MADINI

    Na Asteria, Muho-zya, Dar es Salaam

    N

    aibu Waziri waNishati na Ma-dini, StephenMasele amesema

    kuwa bado kunafursa nyingi za uwekezaji ka-tika sekta ya madini kutokanana Tanzania kuwa na rasilimalinyingi za madini ambayo badohayajafikiwa.

    Naibu Waziri Masele ali-yasema hayo mwishoni mwawiki wakati wa kikao na wawak-ilishi wa kampuni ya dhahabuya Rand Gold ya Afrika Kusiniwaliofika wizarani ili kufahamukuhusu fursa za uwekezaji ka-tika sekta hiyo.

    Aidha, Masele aliongezakuwa, kutokana na mazingiramazuri ya uwekezaji yaliyopokatika sekta hiyo, yamewezesha

    uwepo wa kampuni nyingi zauwekezaji madini nchini.

    Wawekezaji wapo, tuna

    kampuni mbalimbali kubwaza uchimbaji madini na hii nikutokana na mazingira ma-zuri ya uwekezaji, lakini piatuna taasisi kwa ajili ya kusi-mamia shughuli za madinikama Shirika la Madini la Taifa(STAMICO),alisisitiza Masele.

    Vilevile alisema kuwa, badoserikali inahitaji kampuni zaidikuwekeza katika sekta hiyo nakuongeza kuwa, tuna mifumomizuri ya uwekezaji, tunatakawawekezaji zaidi,majadilianoyanayowezekana, na rasilimaliza madini zipo, aliongezaMasele.

    Kwa upande wake MenejaUtafiti wa kampuni ya Rand-Gold, Jono Lawrence alielezakuwa, kampuni hiyo iko tayarikwa majadiliano zaidi kuhusukuwekeza katika uchimbajiwa madini ya dhahabu nchinina kuongeza kuwa, tunatakaTanzania, tunataka kuwekezakatika sekta hii, tunataka kutafitina kuwekeza katika maeneomapya, alisema Jono.

    Aidha, Jono aliongeza

    kuwa, kampuni hiyo imevutiwakuwekeza nchini kutokana namazingira mazuri ya uwekeza-

    ji. Tanzania ni nchi rafikikwa mazingira ya uwekezaji,serikali imeweka mazingiramazuri,tunataka kuwekezahapa ili sote, jamii na sisi tunu-faike, alisisitiza Jono.

    Bado kuna fursa nyingi sekta ya madini: Masele

    Wabunge waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

    Na Leonard Mwakalebela

    Wajumbe wa Kamati ya kudu-mu ya Bunge ya Nishati naMadini pamoja na wale waKamati ya Bajeti wameim-wagia sifa na pongezi lukuki

    Wizara ya Nishati na Madini, Shirika laUmeme nchini (TANESCO) na Wakalawa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi nzuri yakusambaza umeme nchini. Kila aliyesima-ma kuzungumza alianza na pongezi!

    Wabunge hao walitoa pongezi hizobaada ya kupokea taarifa za utekelezaji wamiradi mbalimbali ya umeme hususan yakupeleka umeme vijijini iliyowasilishwa naTANESCO pamoja na REA kuhusiana nautekelezaji wa majukumu yao kwa Kamatiza Kudumu za Bunge za Nishati na Madini

    na Bajeti jijini Dar es Salaam wiki hii.Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM)Andrew Chenge alisema Wizara ya Nishatina Madini pamoja na taasisi zake hasa REAna TANESCO wamefanya kazi nzuri yakupeleka umeme kwa Watanzania waliopovijijini licha ya changamoto zilizokuwa ziki-wakabili ikiwamo ya ukosefu wa fedha zakutosha za kutekeleza miradi hiyo.

    Mwenye macho haambiwi tazamakazi yenu inaonekana na kwa hakikatunawapongeza kwa kuleta mabadiliko namapinduzi kwa watanzania wa vijijini hivyosisi wabunge tunaopenda maendeleo tutaku-wa ni wakala wa kuleta mabadiliko hayo,alisema Chenge.

    Naye Mbunge wa Bariadi Mashariki(UDP) John Cheyo aliimwagia sifa Wizaraya Nishati na Madini, TANESCO na REAkwa kujituma na kufanya kazi kwa weledi ili

    kuhakikisha Watanzania wa vijijini wanaku-wa na maisha bora.

    Yale maisha bora kwa kila Mtanzaniahususan wa vijijini yameanza kuonekanakutokana na Wizara ya Nishati na Madinikuyabadilisha kutokana na kupeleka umemevijijini kwa kweli umeme ni kila kitu,

    Kule kwangu maisha yamebadilika ka-bisa shule ya Wilaya yangu imefanya vizurina kuwa ya kwanza kutokana na uwepo waumeme kwani vijana wetu wanajisomea,alisisitiza Cheyo.

    Mbunge wa Bukoba Mjini (CCM)Khamis Kagasheki naye hakusita kusemakwamba wananchi wa vijijini kwenye jimbolake wamefarijika kwani hakuna mtu anay-etafuta au kutembea umbali mrefu kuchajisimu.

    Mbunge wa Sumve (CCM) RichardNdasa aliisifu TANESCO kwa kazi nzuri yakuwaunganishia umeme wananchi na aliasakuwa jitihada hizo zisikwamishwe na mtu

    yeyote.Mimi nawasifu sana, haki yao wapeni,jitihada zao zisikwamishwe na wababaishaji.Kuna watu kazi yao kuimba ufisadi, ufisadi,hivi sasa hata mtu ukifanya jambo zuri un-aitwa fisadi.

    Wizara, TANESCO, REA mnafanyakazi kubwa sana, msikatishwe tamaa, kama-ti yetu ipo pamoja nanyi. Kete yetu wote niumeme alisisitiza.

    Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mar-tha Mlata ameitaka Wizara ya Nishati naMadini, TANESCO na REA kutosikilizakelele za watu na kuendelea kuchapa kazikwani Taifa linawategemea.

    Naomba sana Wizara na taasisi zakemsonge mbele, msijali kelele za watu, msio-gope, fanyeni kazi, Taifa linawategemeaalisisitiza.

    Zamani nyumba nzuri kijijini kwetu ili-

    kuwa yangu lakini baada ya REA kupelekaumeme, yangu ndio mbaya alisema Mlata.

    Hii ni kueleza kwamba umeme huoumepelekea pia wananchi kuboresha maka-zi yao.

    Aliishauri TANESCO kutafuta njiambadala ya kulinda miundombinu yakeili kuepuka hasara kubwa inayotokana nauharibifu wa miundo hiyo.

    Kwa upande wake, Mbunge wa MulebaKaskazini (CCM) Charles Mwijage aliisifuWizara, TANESCO na REA kwa usamba-zaji wa umeme kila kona nchini.

    Aidha aliishauri serikali kuangalia upyasuala la fidia kwa ajili ya kupisha miradi mi-kubwa ya maendeleo kama umeme.

    Huwezi kuzuia mradi mkubwa wamaendeleo kwa sababu ya fidia, tuangalienchi za wenzetu wanavyoshughulikia sualakama hili aliongeza.

    Ushauri huo ulifuatia malalamikoyaliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa

    TANESCO Bw. Felchesmi Mramba kuwagharama za fidia ni mkubwa mno na hivyozinakwamisha utekelezaji wa miradi yaumeme.

    Viwango vya fidia vimeongezeka sana,mfano kuna mradi mmoja gharama za fidiatu ni Bilioni 217, sasa utekelezaji wa mradihuu unakuwa mgumu alisema Bw Mram-

    ba. Wabunge wengine walioimwagia sifa

    wizara, TANESCO na REA ni pamoja naJuma Njwayo (CCM-Tandahimba), RizikiLulida (CCM-Viti Maalum) na DevothaLikokola (CCM-Viti Maalum).

    Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Je-rome Bwanausi (CCM-Lulindi) aliipongezaTANESCO na REA na kuzitaka taasisi hizokuwasilisha kwa kamati taarifa kamambe(comprehensive) kuhusu taasisi hizo kwahatua zaidi.

    Hata hivyo, Viongozi wa Wizara yaNishati pamoja na Taasisi zake wakipokea

    pongezi hizo kutoka kwa wabunge wamese-ma kwamba pamoja na pongezi hizo wa-taendelea kufanya kazi kwa bidii na weledimkubwa ili kuhakikisha Watanzania wengihususan wale wa vijijini wanapata umemekwani nchi zote zilizoendelea zilitokana nakupeleka umeme vijijini.

    Nchi kama Marekani iliendelea baadaya umeme kupelekwa vijijini, alisema

    Mkurugenzi Mtendaji wa REA, Dk. Luten-gano Mwakahesya.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madinianayeshughulikia Madini, StephenMasele, (katikati) akizungumza

    jambo wakati wa kikao kati yakena wawakilishi wa kampuni yauchimbaji madini ya dhahabu yaAfrika Kusini ya RandGold. Kushotoni wawakilishi wa kampuni hiyona kulia ni baadhi ya watendaji wawizara ambao ni Kaimu MkurugenziMtendaji wa Shirika la Madini la

    Taifa (STAMICO), Mhandisi EdwinNgonyani (wa kwanza kulia) naKamishna Msaidizi wa MadiniMenejimenti ya Baruti, Oforo Ngowi.

    n Akaribisha wawekezaji zaidi

    Meneja Utafiti wa kampuni ya RandGold, Jono Lawrence (Wa pili kushoto )akizungumza wakati wa kikao kati yao na Naibu Waziri wa Nishati na Madinianayeshughulikia Madini, Stephen Masele (hayupo pichani). Kampuni hiyo ilifikawizarani kufahamu fursa za uwekezaji nchini.

    Nao wasema hawatalewa na sifa bali watachapa kazi!!

    Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini Mhandisi NgosiMwihava

  • 8/9/2019 MEM Bulletin 51

    3/12

    3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    MAONI

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    FIVEPILLARS OFREFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    INCREASE EFFICIENCY

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OFTHE CLIENT

    SATISFACTION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OFSHAREHOLDERS

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    GSTyafanya upimaji na utafiti wajiosayansi kwa asilimia 84.7

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    WIKI hii tumeshuhudia Wizara ya Nishati na Madini nataasisi zake ikikutana na kamati za kudumu za Bungela Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Wizara na taasisi zake zimekutana na kamati zakudumu za Bunge za Nishati na Madini; Uchumi, Viwanda na Bi-

    ashara na kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti.Vikao kati ya kamati hizi na Wizara na taasisi zake vililenga ku-wapatia wabunge wa kamati husika taarifa za utekelezaji wa miradina programu mbalimbali na masuala mengine yaliyohusu sekta zaNishati na Madini.

    Katika masuala yaliyochukua nafasi kubwa katika vikao hivyoni utekelezaji wa miradi ya umeme hususani usambazaji wa umemevijijini.

    Wabunge wengi waliochangia mada hii waliimwagia sifa Wizaraya Nishati na Madini, Shirika la Umeme nchini (TANESCO), naWakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi nzuri ya utekelezaji wamiradi ya umeme kwa kasi kubwa.

    Katika kuonyesha hisia zao kali za pongezi walidiriki kutoa mi-fano ya jinsi ya usambazaji umeme vijijini ulivyobadilisha maisha yawananchi vijijini kiuchumi na kijamii.

    Kuna wananchi walikuwa wanatembea kilomita hadi Tanokwenda kuchaji simu za mkononi na hivyo kutumia hadi siku nzima

    bila kufanya shughuli yoyote ya maendeleo.

    Baadhi ya shule vijijini zilikuwa hazina umeme na hivyo wa-nafunzi kushindwa kusoma muda wa jioni, maabara kushindwa ku-fanya kazi na walimu kuwa na changamoto katika ufundishaji kuto-kana na kukosekana kwa umeme.

    Baadhi ya wabunge walidiriki hata kusema upatikanaji waumeme umesaidia uzazi wa mpango katika maeneo yao!

    Wabunge hao wamekiri kuwa upatikanaji wa umeme hivi sasamaeneo ya vijijini umechochea upatikanaji wa maji safi, huduma

    bora za afya, kilimo na ufugaji wa kisasa, ujenzi wa nyumba bora naumechochea maendeleo ya shughuli za kiuchumi na kuongeza ajirana kujiajiri kama vile baadhi ya wananchi wa vijijini kufungua saluniza nywele, mashine za nafaka n.k.

    .Tunawashukuru sana waheshimiwa wabunge kwa pongezi zaokwetu na thamani waliyotupatia kutokana na utekelezaji wa miradiya umeme kwa mafanikio makubwa.

    Pongezi na shukrani zao kwetu zimetupa moyo sana na sisitunawaahidi kuwa hatutabweteka na hatutawaangusha kwa sababutuna jukumu na dhamana ya kuhakikisha watanzania wanaishi

    maisha bora ambayo ni pamoja na kuwa na umeme wa uhakika nanafuu.Kwa mujibu wa takwimu za TANESCO na REA, utekelezaji

    wa miradi ya umeme umefanya idadi ya wateja wa TANESCOkuongezeka maradufu huku maombi mengi sana ya maeneo yanyongeza (additional scope) yakizidi kupokelewa.

    Mahitaji haya yanakwenda sambamba na kasi kubwa ya kuun-ganisha wateja wengi kwenye huduma ya umeme ambayo inalengakuongeza idadi ya wateja kutoka asilimia 25 ya wateja wanaopataumeme hadi kufikia kati ya asilimia 30 na 35 ifikapo mwishoni mwamwaka huu.

    Tunatoa rai kwa wafanyakazi, Wizara ya Nishati na Madinina taasisi zake, kuwa sifa na pongezi tulizopewa na waheshimiwawabunge ziwe chachu na kichocheo cha kufanya kazi kwa nguvuzote kuhakikisha malengo ya serikali katika usambazaji umemeyanafikiwa.

    Tumeweza na tutaweza, waheshimiwa wabunge na watanzaniawote kwa ujumla asanteni kwa kutuunga mkono na tunaahidi ku-

    towaangusha.Safari yetu ya umeme kuelekea vijijini imeshika kasi!!!!

    Na Samwel Mtuwa -Dodoma

    Wakala wa Jiolojia Tanzania(GST)umefanya upimaji nautafiti wa Jiosayansi kwaasilimia themanini na nnenukta saba (84.7%) ya eneo

    la nchi nzima.Akizungumza katika mahojiano maalum

    na mwandishi wa habari hizi, Mtaalamu waJiolojia kutoka GST, Faustine Nyanda Petroalisema kuwa kazi ya utafiti na upimaji ilianzatangu miaka ya 1930 wakati huo Wakala uki-julikana kama Idara inayojitegemea ya upi-maji wa Jiolojia chini ya Mamlaka ya Utawalawa Makoloni ya Nje ya Serikali ya kikoloni yaMuingereza uliojulikana kama British Over-seas Management Authority (BOMA) ulioan-zishwa mwaka 1925.

    Faustine alieleza kuwa GST imeendeleana kazi hizo, ambapo hadi sasa wamefikiajumla ya eneo la kilomita za mraba 938,952sawa na Quarter Degree Sheet (QDS) 322.Kati ya hizo, QDS 305 ambazo ni sawa naasilimia 84.7 tayari zimeshafanyiwa utafiti naupimaji wa Jiosayansi.

    Alisema kutokana na utafiti na upimajihuo GST imeweza kuchapisha ramani zaJiosayansi 175 katika vipimo vya skeli ya1:250,000, 1:125,000, 1: 100,000, na ramani

    130 sawa na asilimia 40.4% bado hazijachap-ishwa.

    Akizungumzia kuhusu dira ya GST, Faus-tine alisema kulingana na ubora wa kazi una-vyoongezeka, dira ya GST ni kuwa moja yataasisi mashuhuri katika Afrika inayotoa tak-wimu na taarifa sahihi za kijiosayansi ifikapomwaka 2025.

    Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa namwandishi wa habari hizi kupitia takwimuna taarifa zilizopo GST, amegundua kuwampaka sasa zimebaki QDS 17 tu ambazo nisawa na kilomita za mraba 49,572 sawa naasilimia 5.3% ambazo hazijafanyiwa utafitina upimwaji, kulingana na ukubwa wa eneolililobakia ambapo wataalamu wa Jiosayansiwa GST watatumia miaka minne hadi mi-tano kukamilisha utafiti na upimaji kwa nchinzima.

    Naye mtaalamu wa Jiolojia GST, PeterLaizer akizungumzia juu ya ufanisi wa maen-deleo ya ukamilishaji wa utafiti na upimaji waJiosayansi alisema kuwepo kwa Mradi waUsimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini(SMMRP) kumewezesha kuongeza kiwangocha utafiti na upimaji kutokana na kutumiateknolojia ya kisasa ya ndege ujulikanao kwajina la (Airborne Geophysical Survey) ulio-wezesha kufanya utafiti na upimaji wa QDS48 katika mgawanyo ufuatao Jiolojia QDS 18, Jiokemia QDS 9 , na Jiofizikia QDS 41.

    BODI YA UHARIRI

    MHARIRI MKUU:Badra Masoud MHARIRI : Leonard Mwakalebela

    MSANIFU: Essy OgundeWAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase

    Teresia Mhagama, Mohamed Saif na Nuru Mwasampeta

    Waheshimiwa

    Wabunge tumewasikia

    Wataalam wa JiosayansiYusto Joseph na PeterLaizer wakimuelezeamwandishi wa habarihizi ( katikati) juu yamaendeleo ya utafiti naupimaji wa jiosayansinchini Tanzaniaunaotekelezwa na GST.

    Umeme utawaka kila kijiji!!!!!

  • 8/9/2019 MEM Bulletin 51

    4/12

    4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo Msimbati

    Mkuu wa Mkoa waMtwara, Halima Dendegu(wa kwanza kushoto)akiwaongoza Wajumbewa Kamati ya Kudumuya Bunge ya Nishati naMadini kuangalia uharibifuuliofanywa kutokana na majiya bahari kuingia jirani namahali ulipo mtambo wakuchakata gesi asilia eneola Msimbati, Mtwara. Wa pilikulia ni Waziri wa Nchi, Ofisiya Waziri Mkuu, Tawala za

    Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI), Hawa Ghasiaaliyeiwakilisha Serikali.

    Kaimu Mwenyekiti waKamati ya Kudumu yaBunge ya Nishati na Madinina Mbunge wa Jimbo laSumve (CCM), RichardNdasa, akiongea navyombo vya habari , marabaada ya kukagua eneolililoharibiwa na mvua kubwailiyoambatana na upepo,

    Msimbati Mtwara jirani nailipo mitambo ya kuchakatagesi asilia.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikiaNishati, Charles Kitwanga ( wa kwanza kushoto)akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikala Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. JamesMataragio (kulia), nyuma yao ni Meneja Mradi waUjenzi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba(TPDC),wakiwa katika eneo palipotokea uharibifu jiranina mahali ilipo mitambo ya kuchakata gesi asilia eneo

    la Msimbati kutokana na mvua kubwa iliyoambatana naupepo.

    u

    u

    u

    Na Asteria Muhozya, Mtwara

    Kamati ya Kudumu ya Bunge yaNishati na Madini imepongeza

    juhudi zilizofanywa na Jeshila Wananchi wa Tanzania

    (JWTZ) na vikosi vingine vya ulinzi ku-nusuru mtambo wa kuchakata gesi asiliakatika eneo la Msimbati Mkoani Mtwara.

    Pongezi hizo zilitolewa na KaimuMwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge waJimbo la Sumve (CCM), Richard Ndasaaliyeambatana na wajumbe wa kamatihiyo, kutembelea eneo hilo ili kukaguauharibifu uliojitokeza, ambapo Jeshi hilolimenusuru uharibifu uliotokana na majiya bahari kuingia jirani na eneo la mtambo

    huo unaochakata gesi asilia kwa ajili yakuzalisha umeme unaotumiwa na mikoaya Lindi na Mtwara.

    Jeshi hilo lilipeleka takribani askari 300kufanikisha zoezi la kuzuia mmomonyokokatika kingo za bahari ya Hindi baada yamvua kubwa kunyesha ikiambatana naupepo mkali.

    Kasi ya maji ni kubwa, bila yauwepo wenu hali ingekuwa tofauti,tunawapongeza sana kwa uzalendo wenumliouonesha, lakini pia tunaipongeza Seri-kali kwa kutoa fedha za kuanza kushughu-likia suala hili, alisema Ndasa.

    Aidha, Ndasa alitumia fursa hiyo kui-taka serikali kuongeza kasi ya kudhibitimaji ili yasiweze kufika eneo la mitambohiyo ikiwemo kuongeza kikosi cha jeshi ili

    kufanikisha zoezi hilo.Serikali lazima ifanye haraka kutoa

    maamuzi katika suala hili, suala hili sio lakisiasa, wapiganaji wapo, hakuna sababuza kuchelewa kuchukua hatua. Thamaniya mitambo hii ni kubwa sana, lazimautekelezaji wa kuzuia mmomonyokoufanywe haraka, alisisitiza Ndasa.

    Kwa upande wake Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoana Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), HawaGhasia akizungumza kwa niaba ya serikalialisema kuwa, serikali inalitambua tatizohilo, hivyo, itaongeza juhudi zaidi ku-hakikisha kwamba tatizo la kuzuia mmo-monyoko usiendelee linatatuliwa haraka.

    Aidha, aliutaka mkoa wa Mtwarakufanya makadirio halisi ili kuwezesha

    shughuli hiyo kufanyika kikamilifu nakuongeza kuwa, bajeti iliyopangwa hivisasa ya kiasi cha shilingi milioni 700 hai-toshi kuondoa tatizo hilo.

    Ninaomba Mkoa wa Mtwara mfanyetena makaridio ya kushughulikia jambohusika. Taarifa ya hali halisi kuhusu jambohili, itafikishwa serikalini, alisistiza Gha-sia.

    Wakati huo huo, wakichangia kuhusunamna ya kunusuru tatizo hilo wajumbewa kamati hiyo walipendekeza kuwa ju-kumu zima la kusimamia shughuli likabi-dhiwe kwa JWTZ.

    Aidha, wajumbe wa Kamati hiyowalitoa ushauri kwa Shirika la Maende-leo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuonaumuhimu wa kuwa na mipango ya baadae

    ya kuhamisha mitambo hiyo.

    nNi wa kuchakata gesi asilianKamati ya Nishati, Madini yataka nguvu zaidi

    Sehemu ya Vikosi ya ulinzi vikijumuisha Jeshi lawananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Magerezana Polisi wakiwa eneo palipotokea uharibifuuliofanywa kutokana na maji ya bahari kuingia jiranina mahali ulipo mtambo wa kuchakata gesi asiliaeneo la Msimbati, Mtwara.

    u

  • 8/9/2019 MEM Bulletin 51

    5/12

    5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    WaziriwaNishati na Madini, ProfesaSospeterMuhongo (katikati) akiwapongeza Wajumbe

    wa Bodi mpya ya TANESCO mara baadayakuizindua Bodihiyo jijini Dar es Salaamna

    kutoa vipaumbele vyautekelezaji wamajukumu.Wanaoshuhudia ni viongozi wa Wizaraya

    Nishati na Madini wakiongozwanaNaibuWaziri, Stephen Masele(kushotokwa Waziri) na

    Kaimu Katibu Mkuu,Eng. Ngosi Mwihava(wa nne kulia).

    Wajumbe wa Bodi ya TANESCO wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dkt.Mighanda J. Manyahi (wa sita kutoka kushoto) wakimsikiliza Kaimu KatibuMkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng.Ngosi Mwihava (wa tano kulia) marabaada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati)

    kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.Wajumbe wengine wa Bodi hiyo(kutoka kushoto) ni Dkt. Nyamajeje C. Weggoro, Eng. Boniface C. Muhegi,Dkt. Mutesigwa I. Maingu, Bw. Shaaban S. Kayungilo, na Dkt. Haji H. Semboja.Wajumbe wengine (kutoka kulia) ni Bibi. Kissa Vivian Kilindu, Bw. Felix G.Kibodya na Eng. Juma F. Mkobya.

    Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Dkt. Mighanda J.Manyahi (aliyesimama) akizungumza mara baada ya Waziri wa Nishati naMadini, Profesa Sospeter Muhongo kuizindua Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.Wanaomsikiliza ni Waziri, Profesa Muhongo (kulia) na Mjumbe wa Bodi hiyo,Dkt. Haji H. Semboja (kushoto).

    WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUARASMI BODI YA TANESCO

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kutoka kushoto), NaibuWaziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa tatu kutoka kushoto), Kaimu Katibu MkuuWizara ya Nishati na Madini, Eng.Ngosi Mwihava (wa nne kutoka kushoto) na Mkurugenzi

    Mtendaji wa TANESCO, Eng. Felchesmi Mramba (wa pili kulia), wakimsikiliza mmoja wawajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO (haonekani pichani) wakati wa hafla yauzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dares Salaam. Wa kwanza kulia ni mmoja wa wajumbe wa Bodi hiyo, Eng. Juma Mkobya.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo mara baadaya kuzindua Bodi mpya ya TANESCO katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.

    Wanaomsikiliza ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele (wa tatu kutoka kushoto), KaimuKatibu Mkuu, Eng.Ngosi Mwihava (wa nne kutoka kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Eng.Felchesmi Mramba (wa nne kulia). Wengine katika picha ni Wajumbe wa Bodi hiyo, Eng. Juma Mkobya,(watatu kulia), Bw. Felix G. Kibodya (wa pili kulia), Bibi. Kissa Vivian Kilindu (wa kwanza kulia), pamoja na watendajimbalimbali wa TANESCO (waliokaa mstari wa nyuma).

    Asisitiza siku za kuunganisha umeme kupungua

    Na Teresia Mhagama

    Waziri wa Nishati naMadini, ProfesaSospeter Muhongoamezindua rasmi

    Bodi mpya ya Wakurugenzi waShirika la Umeme nchini (TANE-SCO) na kuipa vipaumbele vyautekelezaji wa majukumu vitakavy-otekelezwa na Bodi hiyo kabla yakufikia ukomo wake mwaka 2017.

    Uzinduzi wa Bodi hiyo uli-fanyika hivi karibuni katika MakaoMakuu ya Wizara ya Nishati naMadini, jijini Dar es Salaam, na

    kuhudhuriwa na viongozi wa Wiz-ara ya Nishati na Madini akiwemoNaibu Waziri wa Nishati na Ma-dini, Stephen Masele, Kaimu KatibuMkuu, Mhandisi Ngosi Mwihavana Menejimenti ya TANESCO.

    Waziri Muhongo aliieleza Bodihiyo kuwa ina jukumu kubwa lakuliongoza Shirika hilo kwa ufanisina kuhakikisha kuwa Shirika hilolinajitegemea na hivyo kupunguzautegemezi wa fedha kutoka serika-lini.

    Kwa kipindi kirefu, Serikali im-ekuwa inatoa fedha nyingi kuisaidiaTANESCO kutekeleza miradi kati-ka maeneo ya uzalishaji, usafirishajina usambazaji wa umeme hivyo

    Bodi hii ionyeshe jinsi mtakavyoli-badilisha Shirika hili ili hii misaadakutoka serikalini ipungue na ifikemahala Shirika hili lijitegemee,alisema Profesa Muhongo.

    Kuhusu madeni ambayo TA-NESCO inadai kutoka kwa Taasisiza Umma, binafsi na watu binafsi,Waziri Muhongo aliiagiza Bodi hiyokulisimamia suala hilo na kutoka namkakati utakaoliwezesha Shirika

    hilo kukusanya madeni hayo kwanilengo la Serikali ni kuona Shirikahilo linakusanya madeni kutoka kwawadeni wake wakubwa na wadogoili Shirika hilo liweze kulipa madenilinalodaiwa na wadau wake.

    Suala la wananchi kufungiwaumeme ndani ya siku 30 mara wa-napopeleka maombi hayo Tane-sco lilimkera Profesa Muhongo nakuiagiza Bodi hiyo kulishughulikiasuala hilo ili siku hizo zipungue.

    Bodi simamieni maombi yakufungiwa umeme ambayo sasa ya-naelezwa kushughulikiwa ndani yasiku 30, hii lazima ibadilike, watan-zania lazima wapewe umeme ndaniya wiki, zaidi ya hapo haikubaliki.EWURA waelezwe kuhusu sualahili ili kuona namna ya kupunguzahizi siku sababu wao wanahusikakatika suala la upangaji wa siku husi-ka, alisisitiza Profesa Muhongo.

    Vilevile, Profesa Muhongoaliiagiza Bodi mpya ya Tanescokuhakikisha kuwa Shirika hilo lina-shirikiana na sekta binafsi katika mi-radi yake ya uzalishaji, usafirishaji nausambazaji umeme ili kufanikishalengo la Serikali la kuzalisha umemewa kiasi cha megawati 10,000 ifika-po mwaka 2025.

    Profesa Muhongo alieleza kuwakulingana na sera zilizopo, uende-lezaji wa sekta ya umeme unahitajiushirikishwaji wa sekta binafsi kwakuwa uwekezaji katika sekta hiyounahitaji kiasi kikubwa cha fedhaza kigeni, kiwango ambacho kinahi-taji ushirikiano na sekta hizo kupitiamitindo ya IPP na PPP.

    Alisema Tanesco inapaswakuonesha nia thabiti ya kuungamkono juhudi za serikali za kuka-milisha majadiliano na wawekezaji

    na waendelezaji wa miradi bila ku-wakatisha tamaa.

    Awali Naibu Waziri wa Nishatina Madini, Stephen Masele aliielezaBodi hiyo kwamba serikali ina imanikuwa uzoefu na weledi wa Mwe-nyekiti na wajumbe wa Bodi hiyoutasaidia katika kutatua changa-moto zinazoikabili sekta ya nishati ilisekta hiyo muhimu ichangie katikakuipeleka nchi kwenye uchumi wakati. Aidha aliwaasa Wajumbe haokuhakikisha kuwa taaluma walizon-azo wanazitumia katika kuliboreshaShirika la Umeme nchini.

    Akiongea wakati wa uzinduziwa Bodi hiyo, Kaimu Katibu Mkuuwa Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Ngosi Mwihava aliiasaBodi hiyo kufanya kazi kwa uadilifu,uzalendo na kuwa wabunifu ili bid-haa ya umeme inayozalishwa nchiniiweze kupata soko katika Jumuiyaya Afrika Mashariki na Soko laPamoja la Mashariki na Kusini mwaAfrika (COMESA).

    Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyoDkt. Mighanda Manyahi ameelezakuwa majukumu waliyokabidhiwaya kuisimamia Tanesco ni makub-wa lakini kwa kutumia taaluma zaowatahakikisha wanayatimiza ili ku-hakikisha nchi inakuwa na umemewa uhakika kwa kuwa nchi ina ra-silimali za kutosha zinazowezeshakutimiza lengo hilo.

    Mwenyekiti huyo wa Bodi yaWakurugenzi wa Tanesco anaon-goza wajumbe Nane ambao ni Bibi.Kissa Vivian Kilindu, MhandisiJuma Mkobya, Dkt. Haji H. Sem-

    boja, Bw. Shaaban Kayungilo, Dkt.Mutesigwa Maingu, Mhandisi Bon-iface Muhegi, Bw. Felix Kibodya, naDkt. Nyamajeje Weggoro.

  • 8/9/2019 MEM Bulletin 51

    6/12

    6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Mkurugenzi Mpya Shirika la Maendeleo yaPetroli Tanzania (TPDC) apokewa rasmi

    Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, (wa pili kushoto) akisalimianana Mhandisi, Joyce Kisamo, mara alipowasili katika ofisi za TPDC kuanza kutekelezamajukumu yake na kupokelewa na baadhi wa wafanyakazi, makao makuu ya TPDC

    jijini Dar es Salaam.

    Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Michael Mwanda, (mwenye tainyekundu) pamoja na wadau wa TPDC wakimsikiliza MkurugenziMtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (hayupo pichani), katikahafla fupi ya kumkaribisha Mkurugenzi huyo jijini Dar es Salaam.

    Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, akizungumzana wafanyakazi (hawapo pichani) wa TPDC katika mkutano wautambulisho wa mkurugenzi huyo kwa wafanyakazi hao jijini Dar esSalaam.

    Wafanyakazi wa TPDC wakimsikiliza MkurugenziMtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. James Mataragio (hayupopichani) katika hafla ya utambulisho wa Mkurugenzi huyokwa wafanyakazi.

    Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Michael Mwanda (kushoto)akimtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. JamesMataragio, (katikati) mbele ya wadau wa TPDC katika hafla

    fupi ya kumkaribisha Mkurugenzi huyo jijini Dar es Salaam,kulia ni aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa TPDC, JamesAndilile.

    Wafanyakazi, Wajumbe wa Bodi ya TPDC na wadau wa TPDC wakimsikiliza MkurugenziMtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumkaribishaMkurugenzi huyo jijini Dar es Salaam.

    Picha zote na Augustino Kasale

  • 8/9/2019 MEM Bulletin 51

    7/12

    7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Kutoka kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati naMadini Mhandisi Ngosi Mwihava, Naibu Waziri wa Nishati naMadini, Charles Kitwanga na Makamu Mwenyekiti wa Kamati yaKudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Jerome Bwanausi.

    Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,Jerome Bwanausi (wa pili kulia) akisisitiza jambo wakati Kamati hiyo ilipokutanana Watendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) mwishoni mwa wiki jijiniDar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, CharlesKitwanga akifuatiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Mhandisi Ngosi Mwihava.Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Kamati hiyo, Stanslaus Kagisa. Wenginepichani ni baadhi ya wajumbe wa Kamati husika.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Stephen Masele, (katikati) akipitiataarifa kuhusu ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Afrika Kusini ya RandGold ambao wameoneshania ya kuwekeza katika uchimbaji wa madini ya dhahabu nchini. Wengine wanaosoma taarifa hizokulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mhandisi Edwin Ngonyani (wakwanza kulia) na Kamishna Msaidizi wa Madini Menejimenti ya Baruti, Oforo Ngowi, wanaofuatiliakushoto ni baadhi ya wawakilishi wa kampuni ya uchimbaji madini ya RandGold.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mhandisi EdwinNgonyani, akiwasilisha taarifa kuhusu mgodi wa TanzaniteOne na uuzwaji wa hisazake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini (Baadhihawapo pichani). Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Jerome Bwanausi na anayemfuatia ni Mjumbe wa Kamati hiyo, David Lusinde.

    Eneo la ardhi ambalo limemomonyoka na kuzama baharinikutokana na mvua kubwa na mawimbi katika eneo la Msimbatimkoani Mtwara

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (anayeelekeza) akishauriana na Meja JeneraliR. S. Laswai (wa pili kutoka kulia) kuhusu kudhibiti Mmomonyoko katika lango la bahari mkoaniMtwara uliotokea kutokana na mvua kubwa na mawimbi katika eneo lililo karibu na mtambo wakuchakata gesi asilia wa Msimbati.

  • 8/9/2019 MEM Bulletin 51

    8/12

    8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Na Mohamed Saif

    Serikali imedhamiria ku-dhibiti mmomonyokowa ardhi uliotokea ka-tika kijiji cha Msimbati,Mkoani Mtwara ili ku-

    nusuru eneo hilo ikiwa ni pamojakukinusuru Kiwanda cha Kusafi-sha gesi cha Maurel and Prom (P& M) kilichopo karibu na maeneoambayo yamekumbwa na kadhiaya mmomonyoko wa ardhi.

    Hayo yalielezwa na NaibuWaziri wa Nishati na Madini,

    Charles Kitwanga hivi karibunimara baada ya kutembelea eneohilo na kufafanua kuwa mmomo-nyoko huo umesababishwa namvua kubwa iliyoambatana naupepo mkali.

    Hali niliyoiona katika eneohilo si nzuri na imenibidi nikutanena Kamati ya Ulinzi na Usalamaya Mkoa wa Mtwara na tume-kubaliana kwamba tutashirikianaili kuhakikisha tunaudhibiti mmo-monyoko huu, alieleza Kitwanga.

    Alisema Serikali imelazimikakutumia Jeshi la Wananchi Tan-zania (JWTZ), Polisi, Magereza

    na wataalamu mbalimbali ili ku-dhibiti hali hiyo isiendelee hasaikizingatiwa kuwa utabiri wa haliya hewa unabainisha kuwa ni kip-indi cha mvua kubwa.

    Wenzetu wa Mamlaka yaHali ya Hewa wanatueleza kwam-ba hiki ni kipindi cha mvua kubwa,hivyo tunapaswa kuchukua hatuaharaka iwezekanavyo ili kuzuiammomonyoko huu usiendelee,alisisitiza Kitwanga.

    Kitwanga alisema kuwaendapo mmomonyoko huoutashindwa kudhibitiwa mapema,utasababisha Kiwanda hicho cha

    kusafisha gesi cha P & M kuzima mitambo yake, hali itakayosababishaMikoa ya Lindi na Mtwara kuingia gizani.

    Hatupo tayari kuona kiwanda hiki kinazima mitambo yake kutokanana umuhimu wake katika kuchakata gesi inayotumika kufua umeme unao-tumika katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. Kwa sababu hii, tutatumia kilanjia kuhakikisha tunaudhibiti mmomonyoko huu ili usiendelee, alisisitizaNaibu Waziri Kitwanga.

    Aidha, Kitwanga alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo wa Mtwarakutoa ushirikiano kwa Serikali ili kuhakikisha kazi hiyo inakamilika mape-ma bila kuleta athari kwenye eneo hilo.

    Hili ni janga letu sote, ni vyema tukashirikiana na pia tukatoa ushiriki-

    ano wa hali na mali kwa vikosi ambavyo vitakuwa vinafanya kazi kwenyeeneo la tukio ili kwa pamoja tuweze kudhibiti hali hii isiendelee, alisisitizaKitwanga.

    Naye Meneja wa Kampuni ya P & M, Mhandisi Peter John alisematukio hilo la kudidimia kwa ardhi lilitokea usiku wa tarehe 13 mwezi huu.

    Kulikuwa na upepo mkali na tulisikia vishindo. Tulivyotoka nje yakiwanda kuona nini kimetokea ndipo tulipobaini kuwa ardhi inatitia nandani ya takriban saa nne, eneo la ardhi kama mita 100 zilikuwa zimetitiabaharini, alieleza Mhandisi John.

    Serikali kuwanusuru Wana-Mtwara

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (anayeelekeza) akishauriana na Meja Jenerali R. S.Laswai (wa pili kutoka kulia).

    Baadhi ya Wanajeshi wakiendelea na zoezi la kuthibiti mmomonyoko.

    nNi kwa juhudi za kudhibiti mmomonyoko wa ardhi

    nJWTZ, Polisi na Magereza washirikiana kuweka mambo sawa

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga alipotembeleaeneo ambalo limeathirika na mmomonyoko wa ardhi uliotokana namvua iliyoambatana na upepo mkali

  • 8/9/2019 MEM Bulletin 51

    9/12

    9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Hakikisheni Kahama

    inapata umeme wakutosha- MuhongoNa Mohamed Saif

    Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongoameliagiza Shirika la UmemeTanzania (TANESCO) kuha-rakisha mkakati wa kuhakiki-

    sha wilaya ya Kahama inakuwa na umeme wakutosha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za ki-maendeleo wilayani humo.

    Akizungumza hivi karibuni ofisini kwake nawatendaji kutoka TANESCO, Profesa Muhongoalisema wilaya ya Kahama ni miongoni mwawilaya ambazo zinakua kwa kasi na hivyo ina-hitaji kuwa na umeme mwingi ambao utakidhimahitaji ya watumiaji na hasa ikizingatiwa kuwawilaya hiyo ina wawekezaji wengi ambao wana-hitaji nishati hiyo kwa ajili ya shughuli zao za kilasiku.

    Wilaya ya Kahama inakua kwa kasi kubwana wawekezaji wengi wanaongezeka wilayanihumo hivyo kusababisha mahitaji ya umeme

    kuongezeka. Inabidi tujitahidi kuhakikisha ku-nakuwepo na umeme wa kutosha ili wawekezajihao waendelee kuwapo hapo na pia kuvutiawawekezaji wengi zaidi katika wilaya hiyo,alisisitiza Profesa Muhongo.

    Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikala Umeme Tanzania (TANESCO), MhandisiDecklan Mhaiki, alieleza kuwa shirika hilolimeanza mazungumzo na Mgodi wa Buzwagi ilikuangalia namna mgodi huo unavyoweza kush-irikiana na shirika hilo katika kuhakikisha wilayahiyo inakuwa na umeme wa kutosha.

    Tanesco iliona kuwa ili mradi huu utekelezweharaka, mazungumzo lazima yafanyike, mradiugharamiwe na mgodi wa Buzwagi na baadayegharama hizo zirudishwe kwa utaratibu maalumkupitia Ankara za kila mwezi kama ilivyofanyikawakati wa ujenzi wa laini ya umeme wa 220kV nakituo cha Buzwagi hapo nyuma, alisema.

    Mhandisi Mhaiki alieleza kwamba uamuzi wakuutumia mgodi wa Buzwagi ulifikiwa kutokanana uharaka wa suala hilo, ufinyu wa bajeti na piakwakuwa mitambo itakayofungwa inafanana na

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

    ile inayotumiwa na mgodi huo.Kwa upande wake Meneja Mwandamizi (Mauzo na Masoko) wa

    TANESCO, Mhandisi Nicholaus Kamoleka ambaye ni Mwenyekiti waMajadiliano ya kuboresha umeme Kahama kati ya Barrick Gold Minesna TANESCO alisema kuwa wanatarajia kukutana na uongozi wa mgodihuo kwa mazungumzo zaidi mapema iwezekanavyo kwa ajili ya kuha-rakisha kuanza kwa kazi ya kupanua Kituo cha Buzwagi ili umeme huoutumiwe na Wananchi wa Kahama na vitongoji vyake.

    TANZANITE KUWANUFAISHA ZAIDI WATANZANIAnKuuzwa kwa wazawa kwanza ili kukidhi soko la ndanin

    Kutangazwa duniani kuwa chimbuko lake ni TanzaniaNa Veronica Simba

    Watanzania wa-natarajia kunu-faika zaidi namadini ya Tan-zanite kutokana

    a kuboreshwa kwa mazingira yadhibiti na uendelezaji wa mgodia TanzaniteOne Mining Limited

    TML), pamoja na biashara nzimaa Tanzanite.

    Manufaa hayo kwa Taifa yana-kana na maboresho katika mka-

    ba baada ya Kampuni ya wa-alendo ya Sky Associates Groupimited kuwa mbia mpya wahirika la Madini la Taifa (STA-

    MICO) katika umiliki wa leseni yachimbaji wa madini ya Tanzaniteupitia kampuni ya TML huko

    Mirerani.Hayo yamebainishwa wakati

    TAMICO ikiwasilisha taarifa yatekelezaji wa majukumu yakewa Kamati ya Kudumu ya Bungea Nishati na Madini.

    Akiwasilisha taarifa kuhusumgodi wa TanzaniteOne na uu-waji wa hisa zake, Kaimu Mku-ugenzi Mtendaji wa STAMICO,

    Mhandisi Edwin Ngonyani alise-

    ma wanahisa hao wapya wamea-di kufanya maboresho kwenyemkataba wa ubia uliopo kati yahirika lake na TML na kwamba

    STAMICO iliwataka kuwasilishaahadi zao zote kwa maandishi,

    jambo ambalo wamelitekeleza.Kimsingi, Bodi ya STAMICO

    imeridhia Sky Associates kuwambia mpya wa TML na kinacho-subiriwa ni idhini ya MheshimiwaWaziri wa Nishati na Madini,alieleza Mhandisi Ngonyani.

    Akifafanua zaidi, MhandisiNgonyani alisema taratibu zoteikiwa ni pamoja na zile za kisheriazimefuatwa na hatua inayosubiri-wa ni Waziri wa Nishati na Madinikuridhia ili utekelezaji uanze.

    Alitaja maeneo yaliyokubalika

    kuboreshwa kwenye mkataba nambia mpya, kuwa ni pamoja nakuuza madini ya Tanzanite kwawazawa kwanza ili kukidhi soko landani pamoja na kuongeza uwazikatika mauzo kwa kuhusisha STA-MICO kwa asilimia 100 katikahatua zote za uchambuzi mpakauuzaji.

    Mhandisi Ngonyani alitajamakubaliano mengine kuwa nikuongeza thamani ya madini yaTanzanite hapa nchini kabla yakuyauza, hali ambayo itasaidiakuongeza ajira kwa Watanzania.

    Maeneo mengine yamakubaliano ni kuitangaza Tan-zanite duniani na kuonesha kuwa

    chimbuko la madini hayo ni Tan-zania na hazina ya nchi. Vilevilewabia hao wamekubaliana kuten-geneza mazingira ya mgodi kuwa

    kivutio cha utalii na mafunzo sam-bamba na kuboresha maisha yajamii inayozunguka mgodi kwa ku-jenga Zahanati pamoja na kukara-bati Shule zilizopo eneo la mgodikuwa za kisasa.

    Kwa upande wake, Kamishnawa Madini nchini, Mhandisi PaulMasanja alisema ni jambo la kutiamoyo kwamba Kampuni ya Rich-land Resources Ltd iliyouza hisazake kwa Sky Associates imefuatataratibu zote kisheria ikiwa nipamoja na kuwalipa wafanyakazi

    wake na hivyo hakuna malalamiko.Baada ya kupokea taarifa hiyo,

    Makamu Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Nishatina Madini, Jerome Bwanausi, al-ipongeza makubaliano mazuri yali-yofikiwa baina ya pande hizo mbilina kusisitiza kuwa yatekelezwe ilikulinufaisha Taifa. Naye mmojawa Wakurugenzi wa Kampuni yaSky Associates, Bwana Faisal JumaShahbhat, alisema kwamba dhami-ra ya kampuni yake ni kuhakiki-sha maendeleo yatakayopatikana

    yanamgusa kila Mtanzania. Tu-naahidi kuwa mfano wa kuigwana kampuni nyingine za uwekezajihapa nchini, alisisitiza Faisal.

    STAMICO ina hisa ya asil-imia 50 katika umiliki wa leseniya uchimbaji madini ya Tanzanitekatika Kitalu C huko Mirerani,Arusha ambapo husimamia kwaukaribu maslahi yake kwa niaba yaWatanzania katika ubia wa umilikiwa leseni hiyo na Kampuni ya Tan-zaniteOne Mining Limited (TML).

    Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Paul Masanja akifafanua jambo wakati Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)lilipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini (hawapo pichani) na kuwasilisha taarifa yautekelezaji wa majukumu yake. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Mhandisi Edwin Ngonyani.

  • 8/9/2019 MEM Bulletin 51

    10/12

  • 8/9/2019 MEM Bulletin 51

    11/12

    11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Jacqueline Mattowo & God-frey Francis -Biharamulo

    Mwenyekiti wa bodi ya Shirikala Madini la Taifa (STAM-ICO) Balozi Alexander Mu-ganda mwishoni mwa juma

    alitembelea mgodi wa STAMIGOLDuliopo wilayani Biharamulo na kuzun-gumza na wafanyakazi wa mgodi kwa niaya kufahamu mwenendo wa kampuni kiu-tendaji pamoja na changamoto mbalimbalizinazowakabili ili kuongeza ufanisi zaidi kwamaendeleo ya Shirika na taifa kwa ujumla.

    Akizungumza wakati wa ufunguzi wakikao na wafanyakazi Balozi Mugandaalieleza kuwa lengo la kukutana na wa-fanyakazi ni kufuata maagizo kutoka kwaWaziri wa Nishati na Madini Prof. SospeterMuhongo aliyewaagiza kuzungumza na wa-

    fanyakazi wa mgodi ili kufahamu mwenen-do wa utendaji wa kampuni pamoja nachangamoto mbalimbali wanazokabiliananazo katika kutimiza malengo yao ya kilasiku ili ziweze kupatiwa ufumbuzi yakinifukwa ustawi bora wa mgodi na shirika kwaujumla.

    Tuko hapa kwa lengo kubwa la kusiki-liza hoja zenu, mapendekezo yenu pamojana changamoto mbalimbali mnazokabiliananazo katika kufikia malengo mliyojiwekeahivyo kila mmoja wenu awe huru ili kwapamoja tuweze kujadili mwendendo wakiutendaji wa mgodi wetu na vile vile yaleyatakayohitaji kupatiwa ufumbuzi zaidi basitutayachukua na naahidi tutayafanyia kazimara moja Alieleza balozi Muganda.

    Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa

    ni pamoja na muundo mpya wakiutendaji wa kampuni (neworganizational structure)ulioidhinishwa na bodi yaSTAMICO katika kikao kili-chofanyika mwanzoni mwamwezi Desemba 2014 jijinidar es salaam uliolengakuleta ufanisi zaidi katikakampuni. Mengine yali-yojadiliwa ni pamoja nawafanyakazi takribani 10

    watakaopoteza nafasi zaoza kazi (redundancy) baadaya muundo mpya kuondoa

    baadhi ya nafasi katika idarazilizoonekana kuwa na wa-

    fanyakazi wengi ukilinganisha

    na kazi chache zilizopo. Wafan-yakazi wote watapatiwa seminakutoka kwa maafisa wa Idara yakazi na baadae wale walioachish-

    wa kazi watapatiwa barua na taratibu zoteza kisheria kufuatwa ili kuhakikisha zoezizima linatendeka kwa haki.

    Kwa upande mwingine wafanyakaziwalitumia nafasi hiyo kuuliza maswali nakutoa mapendekezo mbalimbali yakiwemowafanyakazi kutopunguzwa na kupatiwaajira mbadala hasa zile zinazohitajimafunzo kidogo kuzielewa mfano uderevawa mitambo, mgodi kutafutiwa mtaji ilikukabiliana na ufinyu wa mtaji unaochangiakupata changamoto nyingi za kifedha nahasa gharama katika vifaa vya uchimbaji,kusamehewa kufuata taratibu za manunuziza serikali (tendering procedure) ambazo hu-chukua muda mrefu hali inayoweza kuathirimalengo ya kiuzalishaji pamoja na kushaurikila idara kupitia upya matumizi yake nakuja na mpango mkakati wa jinsi ya kupun-guza gharama ili kuhakikisha matumizi ya-naendana na gharama za uzalishaji pamoja

    na faida inayopatikana.Wakati huohuo, Kaimu Mkurugenzi

    Mtendaji wa Shirika la Madini la taifaMhandisi Edwin Ngonyani aliyeambatanana mwenyekiti huyo wa bodi alitumia fursahiyo kuwapongeza wafanyakazi kwa ku-weza kufanya kazi kwa bidii pamoja na ku-kabiliwa na hali ngumu kifedha hasa katikamwezi wa Disemba 2014 na kuongeza kuwamgodi umeonyesha kuwa watanzania tunauwezo wa kuendesha migodi kwa ufanisi

    bila ya kuwa na wawekezaji kutoka nje yanchi na alisisitiza wafanyakazi waendeleekufanya kazi kwa bidii na shirika lipo nao

    bega kwa bega kuhakikisha STAMIGOLDinaendelea kufanya vizuri na kuwa mfanokwa miradi mingine iliyo chini ya shirikahilo na taifa kwa ujumla.

    Mbali na kikao cha wafanyakazi vion-gozi hao wa Shirika waliweza pia kuku-tana na Menejimenti ya mgodi na kuwezakuzungumza nao maswala mbalimbaliyaliyozungumzwa wakati wa kikao chawafanyakazi kama ambavyo mheshimiwaWaziri wa Nishati na Madini alivyoele-keza vikao hivyo vifanyike sehemu tofautipamoja na kujadiliana namna ya kuongezaufanisi katika utendaji kwa ustawi bora wakampuni.

    Hii ni mara ya kwanza kwa Mwenyekitiwa bodi ya STAMICO kuzungumza na wa-fanyakazi wa mgodi tangu kushika wadhifahuo alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kik-wete katikati ya mwaka 2014 mara baadaya aliyekuwa mwenyekiti wa bodi hiyo

    Mjiolojia Rumisha Kimambo kufikia mudawake wa kustaafu.

    Kamishna wa Madini

    kuongezewa makaliNa Mwandishi Wetu

    Wizara ya Nishati naMadini imempelekeaMwanasheria Mkuuwa Serikali mareke-

    bisho ya Sheria ya Ma-dini ya mwaka 2010 ili sheria hiyo ikidhimahitaji na mazingira ya sasa.

    Pamoja na mambo mengine, mareke-bisho hayo yamelenga kumpa nguvu zakisheria Kamishna wa madini kuyataifi-sha na kuyauza madini yaliyokamatwa

    kwa kukiuka sheria.Kamishna wa Madini Mhandisi Paul

    Masanja ameiambia Kamati ya Bungeya Uchumi, Viwanda na Biashara kuwamarekebisho hayo yatasaidia kuongezamapato yatokanayo na madini.

    Tumepeleka marekebisho ya she-ria ya madini kwa AG (MwanasheriaMkuu) ili Kamishna wa Madini awezekutaifisha pale pale na kunadi madiniyaliyokamatwa kwa kukiuka sheria bilakwenda mahakamani.

    Utaratibu kama huu unatumika kwamazao ya misitu ambayo yakikamatwayanataifishwa palepale alisema.

    Mhandisi Masanja alibainisha kuwautaratibu wa sasa ni mrefu, wa gharamana unatoa nafuu kwa mtuhumiwa.

    Kuna madini ya mamilioni ya-likamatwa Arusha lakini mtuhumiwaakapigwa faini ya Milioni Tatu, mareke-

    bisho haya yatafanya jukumu la kwendamahakamani liwe la mwenye kosa asi-poridhika alisisitiza.

    Kamishna huyo wa Madini alitajamkakati mwingine wa kuongeza mapatokatika sekta ya madini kuwa uanzishwajiwa vocha kwenye madini ya ujenzi.

    Miaka ya nyuma, tulikuwa tuna-pata Milioni Mbili kwa mwaka kamamrabaha kutokana madini ya ujenzilakini sasa tunakusanya zaidi ya Bil-ioni 1.7 kwa mwaka alisema MhandisiMasanja.

    Aidha alitaja mikakati mingine kuwani kuanza kutumia madalali kwa ajili ya

    kukusanya madeni na ujenzi wa jengolitakalojulikana kama Madini Houseambapo biashara yote ya madini ita-fanyika katika jengo hilo.

    Jengo hili litajengwa mjiniArusha na litakuwa na vitu vy-ote muhimu kwa biashara yamadini yakiwemo mabenki,lengo baadaye ni kuanzishamajengo kama haya katikamikoa minginealisemaMhandisi Masanja.

    Alizitaja changa-moto zinazopunguzaongezeko la mapato

    yatokanayo na madini kuwa ni pamojana kushuka kwa bei ya dhahabu katikasoko la Dunia na kufungwa kwa migodimiwili ya dhahabu.

    Kwa mujibu wa Kamishna Masanja,changamoto nyingine ni wachimbajiwadogo kutolipa mrabaha, utoroshajiwa madini nje ya nchi na Wakala waUjenzi wa Barabara (TANROADS) naokutolipa mrabaha.

    Wachimbaji wadogo wanazali-sha tani 20 za madini lakini ni asilimia2 tu ndio zinakuwa captured (zina-

    patikana) katika kumbukumbu zaserikalialibainisha.Mhandisi Masanja alitaja changa-

    moto nyingine kuwa ni watu kuhodhileseni (licence speculators) bila kuende-leza maeneo ya madini na hivyo serikalikutopata mapato iliyostahili.

    Kwa upande wao, wajumbe wakamati ya Uchumi, Viwanda na Biasha-ra walisifu mipango inayotekelezwa nawizara katika kuongeza mapato yatoka-nayo na madini.

    Aidha, Mwenyekiti wa kamati Lu-haga Mpina (CCM-Kisesa) aliisifu taar-ifa hiyo ya Wizara ya Nishati na Madinina mikakati yake.

    Nakupongeza (Kamishna) kwataarifa nzuri sana, tunawapongeza sana

    Wizara, TMAA (Wakala wa Ukaguziwa Madini nchini) na TEITI (Mpangowa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji ka-tika Tasnia ya Uziduaji) kwa kazi nzurialiongeza.

    Sheria

    Ni ya kutaifisha na kuuza madini

    Kamishna wa MadiniMhandisi Paul Masanja

    MWENYEKITI WA BODI YA STAMICOAZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI STAMIGOLD

    Kaimu MkurugenziMtendaji waShirika la Madinila Taifa MhandisiEdwin Ngonyani(aliyesimama)akifafanua jambowakati wa kikao nawafanyakazi (hawapo

    pichani) wa mgodi waSTAMIGOLD mwishonimwa juma. Wengine niMratibu wa Rasilimaliwatu David Nyagiro(kulia) Mwenyekiti wabodi ya STAMICOAlexander Muganda(kushoto) na Kaimumeneja Mkuu wamgodi Bi. Enea Minga.

  • 8/9/2019 MEM Bulletin 51

    12/12