MEM 104 Online

download MEM 104 Online

of 5

Transcript of MEM 104 Online

  • 8/20/2019 MEM 104 Online

    1/9

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali

    kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizar a ya Nishati na MadiniWasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263

    au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    HABARI ZA

    NISHATI &MADINI

    Toleo No. 104 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Januari 28 - Februari 3, 2016Bulletinews

     

    http://www.mem.go.tz

     

    S o m a hab ar i  U k . 3 

    GST yapata Tuzo Maalum ya SAG kutoka Marekani

    MSINUNUEeneo la mradi wa Gesi – TPDC

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya PetroliTanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio

  • 8/20/2019 MEM 104 Online

    2/9

    2   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Veronica Simba

    Serikali kupitia Shirika laMaendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) imewataka wananchikujiepusha na ununuzi wamaeneo yaliyotengwa kwa

    miradi yenye manufaa kwa Taifa hususanMradi wa kuchakata na kusindika gesiasilia uliopo mkoani Lindi.

    Taarifa iliyotolewa hivi karibunikwa Vyombo vya Habari na Ofisi yaMkurugenzi Mtendaji wa TPDC,imeeleza kuwa ni kinyume cha sheriaza nchi, mtu yeyote kununua, kujigawiaau kuvamia maeneo ya kiwanja Namba1 kilichopo katika Kitalu “A” Likong’o,

    Manispaa ya Lindi kwani eneo hilo kwasasa linamilikiwa kisheria na Serikalikwa ajili ya Mradi wa kuchakata na

    kusindika gesi asilia.Taarifa imeeleza bayana kuwa

    hakuna malipo yoyote yatakayofanyikakwa mtu yeyote atakayethibitikakuvamia eneo husika kwa minajili yakujipatia kipato.

    Aidha, Taarifa hiyo imeeleza kuwazoezi linaloendelea sasa ni la uhakikikwa waliokuwa wakazi katika eneo hilo,kwa lengo la kujiridhisha na idadi yakaya ambazo zitaathirika na mradi huopamoja na mazao, ili walipwe fidia nakuhamishiwa sehemu nyingine.

      “Ulipaji wa fidia utafanyika kwamujibu wa sheria za nchi. Nia na

    mategemeo ya Serikali ni kuhakikishakila mkazi anapata haki yake kwawakati na kama anavyostahili kisheria,”

    imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, zoezi la

    uhakiki linatarajiwa kumalizika Januari30 mwaka huu, na kwamba uhakikiunaofanyika sasa ni kwa kuzingatiaripoti ya tathmini iliyokwishafanywaawali na Wizara ya Ardhi, Nyumba naMaendeleo ya Makazi.

    Vilevile, taarifa imefafanua kuwa,Januari 19 mwaka huu, TPDC ilifanyakikao kazi na uongozi wa Serikali yaMkoa wa Lindi. Kikao hicho kilihusishaKatibu Tawala wa Mkoa, Wakuu waWilaya, Wakurugenzi wa Halmashauriza Mkoa wa Lindi na Wawakilishi wa

    Kampuni za kimataifa za mafuta nagesi ambazo ni wabia na TPDC katika

    Mradi husika kwa lengo la kutoa elimuna faida zitokanazo na mradi huo.Imeelezwa kuwa, pamoja na

    elimu hiyo, viongozi wa Mkoa waLindi walitaarifiwa kuhusu uwepo wawataalam kutoka Ofisi ya Rais, Taasisiya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Wizara ya Nishatina Madini, Wizara ya Ardhi, Nyumbana Maendeleo ya Makazi pamoja naTPDC, ambao wanaendesha zoezi lauhakiki wakishirikiana na wataalam waardhi kutoka Halmashauri ya Manispaaya Lindi.

    Msinunue eneo la mradi wa gesi – TPDC

    Na Coleta Njelekela-STAMICO

    Shirika la Madini la Taifa(STAMICO) linaandaamwongozo wa majadilianokatika miradi ya uwekezajikatika mfumo wa ubia, ili

    kudhibiti wawekezaji wababaishaji,

    kuboresha mgawanyo wa hisa na kuletatija kwa Taifa.

    Kaimu Mkurugenzi wa Utafitina Uchorongaji Alex Rutagwelelaalisema hayo hivi karibuni, baada yakushiriki ziara ya Waziri wa Nishatina Madini Profesa Sospeter Muhongoalipotembelea Mgodi wa Makaaya Mawe wa Kiwira unaotarajiwakuzalisha umeme kiasi cha megawati200.

    Rutagwelela alisema mwongozohuo wa majadiliano utajenga uwezo

    wa wataalam wa Shirika hilo katikakubaini wawekezaji wababaishaji nawasio na uwezo wa kifedha, kiteknolojiapamoja na uzoefu wa kutosha, katikakutekeleza miradi ya ubia ikiwemo yautafiti na uchimbaji madini.

    “Wakati sasa umefika kwawataalam wa STAMICO kuendeleakufanya kazi kwa bidii zaidi nakuendesha majadiliano ya miradi yauwekezaji kitalaam zaidi; hatua hiiitawezesha kuachana na wawekezajiwababaishaji wa ndani na nje ya nchi,”alifafanua Rutagwelela.

    Hivi karibuni Waziri wa Nishatina Madini Profesa Sospeter Muhongoalifanya ziara kwenye mgodi wa Kiwirana kuitaka STAMICO kukamilisha

    hatua za zabuni za kumpata mwekezajimbia katika mradi husika ili uwezekuanza mara moja na kuwanufaisha

    Watanzania.Profesa Muhongo alisema mara

     baada ya kumbaini mbia husika,STAMICO haina budi kurudi mezanina kujiridhisha kwa uhakika juu yauwezo wa mwekezaji huyo na uzoefukatika kuendesha migodi ya makaa yamawe na uzalishaji umeme kwa makaaya mawe.

    Mgodi wa Kiwira ulianzishwamwaka 1988 ukiwa na mashapo yamakaa (Economical reserve) ya mawetani milioni 35.14, mashapo ya kisanifu(Proved reserve) tani milioni 22.14 namashapo yanayoweza kuvunwa kwafaida (Mineable reserve) tani milioni14.64 za makaa ya mawe.

    Mgodi huo unamilikiwa na Serikalikwa asilimia 100 kupitia Shirika laMadini la Taifa (STAMICO).

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akitoamaelekezo kwa Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) baadaya kukamilisha ziara yake ya kutembelea Mgodi wa Makaa ya Mawe waKiwira hivi karibuni. Wa kwanza kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi waUtati na Uchorongaji wa STAMICO Alex Rutagwelela. Wa tatu kutokakulia ni Meneja wa Huduma za Kihandisi katika Mgodi wa Kiwira,Mhandisi Aswile Mapamba.

    Wawekezaji wasio na uwezohawakubaliki- STAMICO

    Kaimu Mkurugenzi wa Utati na Uchorongaji wa STAMICO, AlexRutagwelela (wa kwanza kushoto) akipokea taarifa kuhusu Mgodi waMakaa ya Mawe wa Kiwira, kutoka kwa Boazi Masatu (aliyeinama katika

    meza), wakati alipotembelea mgodi huo hivi karibuni. Wa pili yake niMeneja Mkuu wa Kampuni ya KCPL Evans Mponjoli na wa tatu kutokakulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Senyamuwe.

  • 8/20/2019 MEM 104 Online

    3/9

    3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    TahaririMEM

      Na Badra Masoud

    FIVEPILLARS OFREFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI

    MHARIRI MKUU: Badra MasoudMSANIFU: Lucas Gordon

    WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, GreysonMwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,

    Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

    INCREASE EFFICIENCY 

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OFTHE CLIENT

    SATISFACTION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OFSHAREHOLDERS

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Tuepuke tamaa kuhodhimaeneo ya Serikali

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    GST yapata Tuzo Maalumya SAG kutoka Marekani

    Katika Toleo hili, tumechapisha taarifa kutoka Shirikala Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kuhusu zoezila uhakiki kwa ajili ya kulipa fidia kwa waliokuwa wakazikatika maeneo ya Mradi wa kuchakata na kusindika gesiasilia.

    Aidha, tumeandika habari inayotokana na taarifahusika, yenye kichwa cha habari “Msinunue eneo la Mradiwa Gesi – TPDC.”

    Katika taarifa hiyo, pamoja na mambo mengine, TPDCimewaasa wananchi kujiepusha na ununuzi wa maeneo

    ya Kiwanja Namba 1, Kitalu “A” Likong’o, kilichopoManispaa ya Lindi kwani eneo hilo kwa sasa linamilikiwakisheria na Serikali kwa ajili ya Mradi wa kuchakata nakusindika gesi asilia.

    Taarifa imeeleza bayana kuwa haitawajibika kutoamalipo kwa yeyote atakayethibitika kuvamia eneo husikakwa minajili ya kujipatia kipato.Hii ni kwa sababu nikinyume cha sheria za nchi kwa mtu yeyote kununua,kujigawia au kuvamia maeneo yanayomilikiwa kisheria naSerikali.

    Kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kutokakwa baadhi ya wananchi kuhusu Serikali kutowalipafidia ipasavyo pale inapochukua maeneo kwa ajili yakuendeshea miradi mbalimbali ya maendeleo.

    Kwa upande mwingine, kuna taarifa kuwa kuna baadhiya wananchi wenye tabia ya kufanya udanganyifu kwa

    kujimilikisha au kuhodhi maeneo isivyo halali ambayoSerikali inayamiliki na kisha kudai fidia kutoka kwaSerikali.

    Udanganyifu huo wa baadhi ya wananchi huhusishapia kumilikisha watu wengine au kuwauzia maeneoambayo tayari Serikali imeyafanyia tathmini na kufanyataratibu za fidia kwa wahusika.

    Kutokana na hali hiyo, tunaunga mkono taarifailiyotolewa na TPDC ikiwataka wananchi kuwa makinina kujiepusha na kununua ama kuhodhi isivyo halali,maeneo ambayo yanamilikiwa kisheria na Serikali kwaajili ya kuendeshea miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

    Ikumbukwe kuwa maeneo yanayochukuliwa naSerikali kwa lengo la kuendeshea miradi hiyo, ni kwa faidaya Taifa zima kwa ujumla. Aidha, kufanya udanganyifu waaina yoyote kwa ajili ya kuhodhi maeneo hayo ili kujipatiafaida binafsi ni kosa kisheria na husababisha migogoroisiyo ya lazima.

    Tunawaasa wananchi waliokuwa wakazi wa maeneoya Mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia huko Lindi,watoe ushirikiano unaostahili katika zoezi linaloendeleala uhakiki ili hatimaye waweze kulipwa fidia stahiki kwamujibu wa sheria.

    Ikumbukwe kuwa lengo la Serikali siku zote ni kutendahaki kwa wananchi wake, hivyo ushirikiano kutoka kwawananchi husika ni muhimu sana.

    Serikali inatarajia kuwepo na uaminifu na ushirikianokutoka kwa wananchi wakazi wa eneo husika ili kwaupande wake iweze kuhakikisha kila mkazi anapata hakiyake kwa wakati na kama anavyostahili kisheria.

    Tuisaidie Serikali yetu kufanikisha malengo ya kuondoa

    umaskini nchini mwetu kupitia utekelezaji wa miradimbalimbali ya maendeleo kwa ufanisi.Tuwe wazalendo na tuipende nchi yetu.

    Na Samwel Mtuwa - GST

    Wakala wa Jiolojia Tanzania(GST) umepata tuzomaalum ijulikanayo kamaSpecial Achievement ofGIS (SAG) kutokana na

    utumiaji mzuri wa programu ya uchoraji nauchakataji wa Ramani za Jiolojia ijulikanayokama ArcGIS kutoka kwa taasisi miliki yaprogramu hiyo iitwayo Environment SystemResearch Institute (ESRI) yenye makaomakuu nchini Marekani.

    Meneja wa Uchoraji Ramani naUchakataji taarifa za Jiosayansi wa GST,Terence Ngole alisema hayo hivi karibunimjini Dodoma wakati akizungumza na Jaridahili.

    Ngole alisema kuwa GST imepata Tuzo

    hiyo kwa mwaka 2015 kutokana na uzoefuna ubingwa wa matumizi ya teknolojia yaprogramu hiyo tangu mwaka 2004.

    Aidha, alitaja sababu nyingine iliyochangiaGST kutunukiwa Tuzo hiyo kuwa, ni kuwezakutumia leseni 29 za ArcGIS zilizogawanywakatika sehemu mbili ambazo ni leseni 10zinazotumiwa na watu wengi kwa wakatimmoja pasipo kuingiliana (concurrent license)pamoja na leseni 9 zinazotumiwa na mtummoja tu (single use license).

    “Leseni hizo hutumiwa na GST katikaviwango vya aina Tatu ambavyo ni kiwangocha juu, kiwango cha kati na kiwango chachini (Advanced, Standard & Basic).”

    Ngole aliongeza kuwa, utumiaji waprogramu hiyo katika hali ya ubora naumakini katika pande zote yaani uchoraji na

    uchakataji wa taarifa za jiosayansi (Mapingtool and Analytical tool) ni sababu nyingine yaGST kupata tuzo hiyo.

    Akifafanua kuhusu matumizi ya programuhusika, Ngole alisema kuwa inatumikakatika uchakataji na uchambuaji wa taarifaza jiosayansi lakini kuna moduli nyingine yaprogramu hiyo inayotumika kutunza taarifaza jiosayansi.

    Kuhusu faida zinazotokana na utumiajiwa programu ya ArcGIS, Ngole alizitaja

     baadhi ya faida kuwa ni pamoja na kuwezeshauchoraji wa kisasa wa ramani za jiosayansi,kuwezesha uchakataji na uhifadhi wa taarifaza jiosayansi katika mfumo wa kisasa nakuwezesha kusambazwa kwa taarifa kwawadau katika hali ya ubora zaidi yaani (GIS

     based web-portal).

    Alitaja faida nyingine kuwa ni pamojana programu husika kuwezesha wepesi waupatikanaji, usambazaji na ushirikishaji wataarifa za jiosayansi ukilinganisha na kipindicha miaka ya nyuma kabla ya matumizi yaprogramu hiyo.

    Tuzo za SAG zilianza kutolewa mwaka2004 na hutolewa mwishoni mwa kila mwaka.Katika Tuzo za Mwaka 2015, Kampuni 97za Marekani na 77 kutoka nje ya Marekanizilipata tuzo hizo katika sekta mbalimbali zamaendeleo kama vile gesi, umeme, madini namazingira.

    Meneja wa Uchoraji Ramani naUchakataji taarifa za Jiosayansi katikaWakala wa Jiolojia Tanzania (GST)Terence Ngole, akionesha tuzo maalumya SAG iliyotolewa na Taasisi yaEnvironment System Research Instituteya Marekani (ESRI) kwa mwaka 2015.

  • 8/20/2019 MEM 104 Online

    4/9

    4   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

     Asteria Muhozya naRhoda James

    K atika kudhihirisha kilealichokuwa akikielezakatika ziara zakealipotembelea miradiya kuzalisha umeme,

    maeneo ya tafiti na miradi ya Makaaya Mawe hivi karibuni katika Mikoaya Njombe, Ruvuma na Mbeya,Waziri wa Nishati na Madini, ProfesaSospeter Muhongo akisisitiza marakadhaa kuhusu dhamira ya Serikali

    ya kuhakikisha Tanzania inakuwana umeme wa kutosha kutokavyanzo mbalimbali vya Nishativinavyopatikana nchini ikiwemo GesiAsilia, Nishati Jadidifu, Maji, Makaaya Mawe, Jua, na Upepo.

      Katika kila kituo cha kuzalishaumeme au miradi ya umeme, Prof.Muhongo hakuacha kulitaka Shirikala Umeme Nchini (TANESCO),kufanyakazi kwa karibu na WazalishajiWadogo, Wa Kati na Wakubwa waumeme na kueleza kuwa, wazalishajihao watasaidia kuongeza kiwangocha umeme nchini, jambo ambalo pialitasaidia kuongeza kiasi cha umemekatika gridi ya Taifa kwakuwa,wazalishaji hao pia wataliuzia Shirika

    hilo umeme badala ya Shirika hilokuwa mzalishaji pekee na hivyokuondoa changamoto ya nishati hiyo

    nchini.Prof. Muhongo alieleza kuwa

    mbali na kuingiza umeme katika Gridiya Taifa, lakini pia kwa kushirikianavizuri na Shirika hilo kutakuwa na kasiya usambazaji umeme katika maeneo

    ambayo miradi hiyo inaendeshwa nahivyo kuongeza kasi ya usambazajiumeme nchini kupitia TANESCOau kupitia Wakala wa Nishati Vijijini(REA), jambo ambalo pia litawezeshakutekeleza Ilani ya Chama ChaMapinduzi (CCM), ambayo inasemahadi ifikapo mwaka 2020 , wananchiwaliounganishwa na umeme wafikieasilimia 60 na kiwango cha uzalishajikifike megawati 4915.

    Katika kuonesha kwamba, ProfesaMuhongo anamaanisha kile ambachopia kimeelezwa katika Dira yaMaendeleo ya Taifa kuwa Tanzaniainakuwa miongoni mwa nchi zenyeUchumi wa Kati ifikiapo mwaka2025. Prof. Muhongo anataka Sekta ya

    Nishati itoe mchango mkubwa kufikiauchumi huo kwa kuwa rasilimali zakufikia lengo hilo kupitia nishati zipokinachotakiwa ni dhamira, na kasiya kutekeleza kwa kuwa, awali Diraya Maendeleo ya Taifa ilieleza kuwa,ifikapo mwaka 2015 uunganishajiumeme ufikie asilimia 30; lakinikutokana na utekelezaji madhubutiwa dira hiyo kiwango hicho kilivukwakufikia asilimia 40 mwaka 2015.Vivyo hivyo, Dira ya Maendeleo yaTaifa inaeleza kuwa, ifikapo mwaka2025 ifikie asilimia 50 na mwaka 2033asilimia 70.

    Prof. Muhongo katika hiloanaamini kwamba, nishati ya umemeni chachu kubwa ya maendeleo na

    moja ya nyenzo kuu za ukuaji uchumi

     Jitihada za Prof. Muhongo kuongeza

    uzalishaji umeme ziungwe mkono

    Waziri wa Nishati na Madini, akilakiwa na baadhi ya Askari wa Chuo Cha Magereza, Tukuyu alipokakatika eneo hilo ambapo Kampuni ya ea- power iko kwenye mchakato wa kuzalisha umeme kutokana na

    bwawa ambalo liko ndani ya eneo la Magereza. Nyuma ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mwalimu ZainabuMbusi.

    Meneja Mkuu wa Kampuni ya kuzalisha umeme kwa kutumia mabaki ya miti ya Miwati, Dkt. RayeerSingh (aliyenyoosha mikono), akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongona Ujumbe wake walipotembelea Kampuni hiyo.

    >>Inaendelea Uk. 5

  • 8/20/2019 MEM 104 Online

    5/9

    5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

     Jitihada za Prof. Muhongo kuongeza uzalishaji umeme ziungwe mkono

    ambao una mchango mkubwa katikakuongeza kipato cha mtu mmojammoja na pato la taifa na uwezekano

    wa kufikia asilimia 60 ifikapo mwaka2020 upo . Aidha, jambo hilo pialilisukuma ziara za Prof. Muhongokuangalia hali ya uzalishaji umemekatika maeneo kadhaa ikiwemomabwawa ya kuzalisha umeme yaMtera, Kihansi, Nyumba ya Mungu,Hale, Kidatu , Pangani na piaalitembelea mikoa ya Mwanza naKagera.

    Ziara hizo pekee ni kiashiriatosha kwamba, Prof. Muhongoamedhamiria kuifanya Tanzaniainakua na umeme wa kutosha nawa uhakika. Aidha, jambo hili pialinadhihirika pale ambapo, katika ziarahizo hakusita kuwataka wazalishajiwadogo kueleza changamotozinazowakabili katika utekelezajiwa majukumu yao, lengo likiwa nikuhakikisha Serikali inashirikiana kwakaribu na wazalishaji hao wawezekuzalisha, kuongeza viwango vyaovya uzalishaji na hatimaye kuiuziaTANESCO umeme wa bei nafuuambao pia hautakuwa mzigo kwawananchi.

    Mifano hii ni michache tu kati yamaeneo mengi aliyotembelea ambapoaliitaka kampuni ya TANWATiliyopo Mkoani Njombe inayozalishaumeme kwa kutumia Mabaki yaMiti ya Miwati, kuongeza uwezo wa

    uzalishaji kutoka Megawati 2.5 kufikia10, huku akiitaka kampuni hiyokueleza changamoto zitakazozuia

    uzalishaji huo kufikiwa. Vilevile, katikaKituo cha kuzalisha umeme chaTulila, kinachomilikiwa na Watawawa Kanisa Katoliki wa Shirika laMtakatifu Agnes Chipole, ProfesaMuhongo aliwataka Wataalam waTANESCO kuendelea kuwapamafunzo wazalishaji hao kwa kipindicha mwaka mmoja ili wawezekumudu vizuri zaidi shughuli zauzalishaji umeme.

    Prof. Muhongo alieleza umuhimuwa wazalishaji hao kuliuzia Shirikahilo umeme kwa bei nafuu akiaminikwamba, unafuu huo wa beiutaliwezesha Shirika hilo kujiendeshakibiashara bila kutegemea ruzuku zaSerikali. Aidha, Prof. aliongeza kuwa,ikiwa TANESCO itanunua umemekwa bei ghali, italazimika kuuzakwa bei nafuu kuepuka kuwaumizawatumiaji hususani wananchi jambo

    ambalo linafanya shirika hilo kuwategemezi.Inawezekana kabisa kuna baadhi

    ya wananchi wanadhani kuwaProfesa Muhongo anavyozungumziawazalishaji wadogo anamaanishakwamba TANESCOwatanya’nganywa majukumu yakeya kuzalisha na kusambaza umeme.

    Dhana hiyo si kweli , taarifasahihi kuhusu jambo hilo ni kwamba,upo Mkakati wa mwelekeo wakurekebisha sekta ndogo ya umeme(EISI- RSR) ambayo MweziJuni 2014, Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania ilipitisha nakuchapisha mkakati wa mageuzi wa

    Electricity Supply Industry ReformStrategy and Roadmap (ESI-RSR)2014 – 2025. Lengo la msingi wa

    mkakati huo ni kuboresha mazingiraya uwekezaji wa sekta binafsi katikanyanja za uzalishaji na usambazaji,na kuongeza uunganishaji wa umemekatika ngazi zote.

    Utekelezaji wa mpango huoambao unatarajiwa kutekelezwakatika kipindi cha miaka kumi namoja (11) umegawanyika katikavipindi vikuu vitatu ambavyo ni mudamfupi, wa kati na muda mrefu.

    Mkakati wa muda mfupi nikutenganisha shughuli za Uzalishajiili zifanywe na Kampuni Tanzu yaTANESCO. Umiliki wa uzalishaji,usafirishaji na usambazaji chini yaawamu hii itaendelea kuwa chini yaSerikali, kama mbia moja.

    Mkakati wa muda wa kati unahusukutenganisha sehemu ya usambazajikutoka kwenye usafirishaji. KatikaAwamu hii, Kampuni za uzalishaji,

    usafirishaji na usambazaji zitaendeleakuwa chini ya umiliki wa Serikali.Mkakati wa muda mrefu

    utahusisha Ofisi za Kanda kujihusishana usambazaji wa huduma za umemeambazo pia zitagawanywa kulinganana uwezo wa kujiendesha. Katikakipindi hicho cha muda mrefu,kampuni binafsi za usambazajiumeme zitaendelea kushiriki katikashughuli za uzalishaji na usambazajiumeme kwa ajili ya kuchocheaushindani na ufanisi kwenye soko.

    Aidha, ili kujua undani wa sualahilo ni vema wadau wakapata fursaya kusoma mkakati wa mageuziujulikanao kama Electricity Supply

    Industry Reform Strategy andRoadmap (ESI-RSR) 2014 – 2025ambao unapatikana katika tovuti ya

    wizara kwa anuani ya www.mem.go.tz.

     Aidha, ni vema tukatambua nakuunga mkono juhudi zinazofanywana Wizara chini ya Profesa Muhongokwa kuwa anataka Tanzania yenyeumeme mwingi wa kutosha utakaochochea ukuaji wa Viwanda kamailivyo Kaulimbiu ya Serikali yaAwamu ya Tano ya kuifanya Tanzaniaya viwanda vikubwa na vidogo.

    Mara baada ya ziara hiyo,hatimaye tarehe 8 Februari, 2016,Profesa Muhongo atakutana nawazalishaji binafsi wadogo wa umemewa maji chini ya Megawati 20, lengola mkutano huo ni kuimarishaushirikiano, kutumia utaalam, uzoefuna miundombinu ya TANESCO, nakujadili namna ya kuongeza uzalishajiwa mitambo ya wazalishaji wadogo.

    Mkutano huo wa wazalishaji

    wadogo unaotarajia kufanyika katika bwawa la kuzalisha umeme kwamaji la Mtera, unaonesha dhamirasafi aliyonayo Waziri Muhongo naWizara ya kuhakikisha kwambaTanzania inakuwa na umeme wakutosha ambao utakuwa kichocheocha ukuaji wa viwanda na shughulinyingine za kiuchumi zinazotegemeanishati hiyo, ikiwemo kupanua wigowa ajira.

      Hivyo, wananchi na wapendamaendeleo hawana budi kuungamkono jitihada hizo za Wizaraya Nishati na Madini badala yakuwanyooshea vidole viongoziambao wameonesha nia ya dhati ya

    kuendeleza sekta ya Nishati ili iwezekutoa mchango unaotarajiwa kwakizazi cha sasa na kijacho.

    Waziri wa Nishti na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akimweleza jambo, Meneja wa Bwawa la kuzalisha umeme kwa Maji la Kihansi,Mhandisi Pakaya Sakaya (wa Kwanza kulia), walipotembelea bwawala kuzalisha umeme la Uwemba, Njombe ambalo liko chini ya Bwawala Kihansi.

    Prof. Sospeter Muhongo na Ujumbe wake, wakimsikiliza Mtaalam waKituo cha kuzalisha umeme Tulila, kinachomilikiwa na Watawa waKanisa Katoliki wa Shirika la Mtakatifu Agnes Chipole wakati wa ziarayake.

    >>INATOKA Uk. 4

    MAKALA

  • 8/20/2019 MEM 104 Online

    6/9

    6   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Mwandishi wetu 

    Wakala wa Ukaguziwa MadiniTanzania (TMAA)umekusanya wastaniwa shilingi milioni

    40 kila mwezi kufuatia ukaguzi wauzalishaji na mauzo ya dhahabukutoka kwa wamiliki wa mitambo yauchenjuaji dhahabu wanaoyeyushamabaki (tailings) ya wachimbajiwadogo.

    Akizungumza na MEM Bulletinhivi karibuni jijini Dar es Salaam, AfisaMahusiano wa Wakala huo, YisambiShiwa alisema ukaguzi wa aina hiyoulianza rasmi mwezi Agosti, 2012katika mikoa ya Mwanza na Geitakwa kushirikiana na Ofisi za Madinikatika maeneo husika.

    Alisema TMAA ilibuni nakuanzisha ukaguzi wa uzalishajina mauzo ya dhahabu kutoka kwawamiliki wa mitambo ya uchenjuajidhahabu wanaoyeyusha mabaki yawachimbaji wadogo kupitia mitamboya upembuaji wa marudio ya mashapoya wachimbaji wadogo ijulikanayokama vat leaching plants.

    “Ukaguzi huu uliiwezesha Serikalikupata takwimu halisi za uzalishajikutoka kwa wahusika ambapo wastaniwa kilo 15 za dhahabu zilizalishwana kuiwezesha Serikali kukusanyamrabaha wastani wa Shilingi milioni40 kila mwezi,” alisema.

    Akizungumzia kuhusu mitambohiyo ya kuchenjulia dhahabu, Yisambialisema kadri siku zilivyopita watuwengi zaidi walijenga mitambo husikaya elution sehemu mbalimbali nchinina hivyo kufanya idadi ya mitambohiyo kuongezeka kutoka mitambo 11iliyokuwa ikikaguliwa mwaka 2012katika mikoa ya Mwanza na Geitahadi kufikia zaidi ya mitambo 100inayokaguliwa hivi sasa.

    Anasema kutokana na kuongezekakwa mitambo hiyo, uzalishajiwa dhahabu umeongezeka hadikufikia wastani wa kilo 120 ambapo

    mrabaha unaolipwa Serikalini naoumeongezeka sawia hadi kufikiatakribani Shilingi milioni 320 kwa

    mwezi.Yisambi alisema teknolojiaya uchenjuaji wa dhahabu kwakuyeyusha mabaki yatokanayo nauchimbaji mdogo na kisha kutumiacarbon kuchenjua dhahabu (elutioncolumn) iliingia nchini hususan kandaya Ziwa Viktoria ikitokea nchiniZimbabwe na imewezesha wachimbajiwadogo kuuza mabaki zao ambazotayari walikwishazichenjua na kwawachimbaji hao huhesabika kamataka.

    Alisema muunganiko huo wakimahitaji baina ya wachimbajiwadogo na wa kati, uliongeza mfumkowa shughuli za uchimbaji na biasharaya madini katika mikoa mingi ya

    Tanzania kwa kutumia teknolojia hiyompya.Aliongeza kuwa, baada ya

    wachimbaji wa kati kuanza kutumiateknolojia hiyo ya kuchenjuamarudio yaliyokuwa yameachwana wachimbaji wadogo na wa kati,changamoto kubwa iliyojitokezailikuwa ni jinsi ya kubaini na kudhibitimfumko huo wa uzalishaji.

    Ili kukabiliana na changamotohiyo, Yisambi alisema Wakala ulibuniutaratibu wa kudhibiti mapato yaSerikali yatokanayo na biashara yadhahabu inayozalishwa kwenyemitambo ya uchenjuaji wa marudiokatika Kanda ya Ziwa hususan katikamikoa ya Geita na Mwanza.

    “Ili kudhibiti usafirishaji wa carbon,Wakala uliandaa vibali maalumkwa ajili ya kutumiwa kusafirishacarbon kutoka vat leaching kwendakwenye elution plant”; vibali hivyovinaainisha uzito wa carbon, kiasicha dhahabu kilichomo na mitamboambayo carbon hizo zinapelekwaikiwa ni pamoja na namba ya leseni yamuhusika,” alisema.

    Aliongeza kuwa, kutokanana hatua mbalimbali za udhibitizilizochukuliwa na Wakala kwakushirikiana na Ofisi za Madini, katika

    kipindi cha mwezi Disemba 2015,udhibiti huo umewezesha ukusanyajiwa shilingi milioni 321.14 kamamrabaha kutoka kwa wachenjuajiwa marudio katika mikoa ya Geita,Mwanza na Mbeya ambapo jumla yakilo 130 za dhahabu zilizalishwa.

    Alisema, Wakala umeweza kufikiamafanikio hayo katika kuwezeshaukusanyaji wa maduhuli yatokanayo

    na shughuli za uzalishaji na biasharaya madini nchini kutokana na kufanyakazi kwa ushirikiano na weledi.

    Vilevile, Yisambi alisema TMAAimekuwa ikitoa elimu shirikishi kwawamiliki wa mitambo ya kuchenjuadhahabu ili kuwaongezea uelewa washughuli za Wakala na Ofisi za Madinina vilevile kuhusu sheria, kanuni nataratibu zinazopaswa kutekelezwana wamiliki wa mitambo hiyo kablana baada ya kuanzisha shughuli na

     biashara ya madini.“Mafanikio yote hayo yametokana

    na ubunifu na ushirikiano mkubwa baina ya watendaji wa Wakala, Ofisiza Madini pamoja na wananchiwaliowezesha upatikanaji wa taarifahusika.”

    Akizungumzia kuhusuchangamoto, alisema kuwa baadhiya wamiliki wa mitambo husikasio waaminifu kwani wanafungana kuendesha mitambo hiyo kwa

    siri kitendo ambacho kinaikoseshaSerikali mapato yake yatokanayo nashughuli husika.

    Aidha, alisema katika kukabilianana changamoto hiyo, Wakalaumeendelea kufanya kaguzi zakushitukiza kwa kushirikiana na Ofisiza Madini na vilevile anasema Wakalaunatoa wito kwa wananchi kufichuana kutoa taarifa kwa Wakala, Ofisi yaMadini au Polisi ili hatua stahiki ziwezekuchukuliwa kwa watakaogundulikawakifanya shughuli hizo kinyume naSheria ya Madini ya Mwaka 2010.

    TMAA kuimarisha usimamizi wa mapato ya uchenjuaji wa marudio

    Marudio yakipakiwa kwenye gari tayari kwa ajili ya kupelekwa kwenyematanki ya kuyeyushia dhahabu iliyopo ndani ya marudio hayo

    Elution column zikiwa zimewekewa lakiri za Serikali

  • 8/20/2019 MEM 104 Online

    7/9

    7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    PROFESA MUHONGO:UMEME NI INJINI YA UCHUMI

    Na Mohamed Saif

    Ikiwa ni takriban mwezi mmojatangu ameapishwa kuwa waziriwa Nishati na Madini, ProfesaSospeter Muhongo amekuwagumzo kubwa kwa juhudi na

    kasi yake katika kuhakikisha tatizo laumeme nchini linamalizika.

    Mara tu baada ya kuapishwa,Profesa Muhongo alikutana naMenejimenti ya Shirika la UmemeTanzania (TANESCO) na kutakamajawabu ya kisayansi ya maswalimakuu manne ambayo alisemayatasaidia katika kutatua tatizo la mudamrefu la nishati ya umeme nchini.

    Maswali ambayo yaliulizwa ni:kwa namna gani tatizo la kukatika

    umeme mara kwa mara litamalizika;pili ni vipi wamejipanga kuhakikishakunakuwepo na umeme mwingi,wa kutosha na wa uhakika; tatuni vipi watahakikisha gharama zaumeme (bei) zinapungua kutokana namatumizi ya gesi asilia katika kuzalishaumeme na swali la nne ni kwambavipi wamejipanga kuondokana namalalamiko ya wateja katika kutoahuduma bora kwa wananchi.

    Mbali na maswali hayo, WaziriMuhongo aliwaagiza kuandaamkakati madhubuti utakaotumikakuhakikisha makusanyo ya mapatoyatokanayo na huduma ya nishati yaumeme yanaongezeka mara mbili yamalengo yaliyokuwapo awali.

    Alisema wananchi wanahitajiumeme wa bei nafuu ili wawezekujikwamua na umasikini hukuakieleza kwamba ni wakati mwafakasuala hilo likatazamwa kwani bei yahuduma ya umeme ikishuka bidhaanyingine pia zitashuka.

    Profesa Muhongo alisema lengo laSerikali ya Awamu ya Tano ni kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda na ilikufikia azma hiyo, anasema inatakiwakuwepo na umeme mwingi na wauhakika.

    Vilevile Profesa Muhongoaliwataka watendaji hao kujieleza nikwanini umeme umekuwa ukikatikamara kwa mara ikiwa ni pamojana kuwataka waeleze wao kama

    Menejimenti ya Shirika hilo ni hatuazipi ambazo tayari wamezichukuakuhakikisha hali hiyo haijirudii.

    Siku ya pili baada ya kuapishwakwake, Waziri Muhongo alianzaziara ya kukagua miundombinu namitambo ya uzalishaji umeme ambapoalieleza umuhimu wa kutembeleamaeneo hayo na kujionea hali halisiiliyoko kwenye maeneo ya uzalishajiumeme nchini.

    “Kukaa ofisini hakuwezi kutatuatatizo la umeme nchini; nimeamuakufanya ziara nchi nzima ili kukaguahali halisi ya uzalishaji wa umeme,”alisema.

    Waziri Muhongo alianza ziarayake ya kukagua vyanzo vya kuzalisha

    umeme kwa nguvu ya maji ambapoalitembelea Kituo cha Hale, NewPangani vya Mkoani Tanga na siku

    hiyo hiyo alitembelea kituo cha

    Nyumba ya Mungu cha MkoaniKilimanjaro.Baada ya hapo Waziri Muhongo

    aliendelea na ziara yake kwakutembelea Mikoa ya Morogoro naIringa ambapo alikagua uzalishajiumeme katika vituo vya Mtera,Kihansi na Kidatu na kujionea hali yamitambo ya kuzalisha umeme katikavituo hivyo pamoja na hali halisi yamaji kwenye mabwawa ya vituo hivyo.

    Katika majumuisho ya ziara yakekatika vituo hivyo vya kuzalishaumeme vilivyotajwa hapo juu, WaziriMuhongo alisema amebaini kwambasababu kuu iliyopelekea kupunguakwa kina cha maji katika mabwawahayo ni mfumo duni wa umwagiliaji

    usio zingatia taratibu za matumizisahihi ya maji.Alisema mfumo wa umwagiliaji

    unaotumika kwenye mashambayanayotumia maji ya mito inayotiririkakwenye mabwawa ya kuzalishaumeme ni wa kienyeji sio wa kitaalamuna hivyo aliagiza matoleo ya maji yakumwagilia kwenye mashamba hayoyafungwe.

    Kufuatia agizo hilo, tayariimeelezwa kuwa kina cha majikwenye mabwawa husika kimeanzakuongezeka; hata hivyo WaziriMuhongo ameelekeza kuacha majihayo yaongezeke ili kuwa na uzalishajiumeme wenye tija zaidi kwa kipindichote.

    Suala lingine ambalo WaziriMuhongo aliliwekea mkazo katikaziara zake ni taratibu za manunuzi yamitambo ya kuzalisha umeme ambaoalionyesha kutoridhishwa nao.

    Waziri Muhongo amelitakaShirika la Umeme Tanzania(TANESCO), kuwa makini wakatiwa kuingia mikataba na Wakandarasiili kuepuka kuuziwa mitambo hafifuna kusababisha hasara na migogoroisiyo ya lazima.

    Agizo hilo limefuatia ukaguziwake kwenye mitambo ya kuzalishaumeme ambapo alikuta mitambokadhaa ikiwa imeharibika na hivyokushindwa kuzalisha umeme na huku

     baadhi ya mitambo ikiwa haina muda

    mrefu tangu imefungwa na mingineimesimama kutokana na kukosaukarabati.

    Katika kituo cha kuzalisha umemecha Hale ilielezwa kwamba kituokinayo mitambo miwili ambayoilifungwa mwaka 1964 ikiwa nauwezo wa kuzalisha umeme wa kiasicha megawati 21 ambapo kila mtambo(kati ya mitambo miwili) katika kituohicho una uwezo kuzalisha umemewa kiasi cha megawati 10.5.

    Kilichomshangaza WaziriMuhongo ni kwamba ukarabati wakwanza wa mitambo hiyo ulifanyikamwaka 1986 na kuwa ilipofika mwaka2008 mtambo mmoja uliharibika nahivyo kusababisha mtambo mmoja tu

    kufanya kazi.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akikagua vipulivilivyoharibika vya mitambo ya kuzalisha umeme ya Nyakato ya jijiniMwanza.

    Baadhi ya mitambo ya kuchakata Gesi Asilia ya Kituo cha Madimbaambacho kilitembelewa na Waziri wa Nishati na Madini, ProfesaSospeter Muhongo.

    Moja ya mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta uliopokatika kituo cha Nyakato cha jijini Mwanza.

    >>Inaendelea Uk. 8

    MAKALA

  • 8/20/2019 MEM 104 Online

    8/9

    8   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Profesa Muhongo: Umeme ni Injini ya UchumiAkionekana kukasirishwa na

    taarifa hiyo, Profesa Muhongo alihoji

    ni kwanini ukarabati wa mtambo huoumechukua muda mrefu na hivyokuagiza mtambo huo kufungwa harakaili uweze kuzalisha nishati ya umeme.

    Hali kama hiyo alikutana nayoalipotembelea kituo cha kuzalishaumeme cha Somanga Fungu cha Kilwa,Mkoani Lindi ambapo alikuta mtambommoja kati ya mitatu iliyopo kituonihapo umeharibika na haufanyi kazitangu mwaka 2012 na huku kituo hichokilizinduliwa rasmi mwaka 2010.

    Halikadhalika waziri Muhongoalifanya ziara kwenye kituo cha kuzalishaumeme cha Nyakato, mkoani Mwanzachenye uwezo wa kuzalisha megawati60 ambapo alijionea mitambo mitatukati ya mitambo kumi imeharibika na

    huku kituo hicho kikiwa kimezinduliwamwezi Novemba mwaka 2013.Profesa Muhongo alisema

    alichogundua tangu ameanza ziaraya kukagua mitambo ya kuzalishaumeme maeneo mbalimbali nchini nikuwa Shirika hilo linaonekana kutumiawatu wa kati katika kununua mitamboyake na vilevile ukarabati wa mitambohaufanyiki inavyopaswa.

    “Ilipaswa wataalamu wafanyeuchunguzi wa mitambo na kujiridhishakabla mitambo hiyo haijaletwa nchini; napia msisubiri hadi mitambo inaharibika

    ndiyo mnafanya ukarabati,” alisema.Alisema haoni sababu ya Shirika hilokununua mitambo yake kutoka kwenyekampuni ambazo hazina viwanda vyakutengeneza mitambo husika wakatizipo kampuni mahiri duniani zenyekutengeneza mitambo bora.

    “Hawa inaonekana wanatumia watuambao hawatengenezi mitambo nandio maana tunashuhudia tunauziwamitambo hafifu ambayo katika kipindikifupi tangu imeanza uzalishaji baadhiimeharibika,” alisema.

    Mbali na suala la umakini kwenyeununuzi, Profesa Muhongo alisemawataalamu wanapaswa kufuata taratibuza uendeshaji wa mitambo na hivyoaliwaasa kuwa makini muda wote

    wakati wa kuendesha mitambo hiyo.Baada ya kujionea hali halisi yaumeme maeneo aliyotembelea, WaziriMuhongo alikutana na watendajikutoka taasisi mbalimbali zilizo chini yaWizara ya Nishati na Madini hususanzinazojishughulisha na masuala yanishati ya umeme.

    Baada ya tathmini ya uzalishajiumeme, Profesa Muhongo amesema

    unahitajika uwekezaji mkubwa katikauzalishaji umeme ili kuwa na umememwingi na wa uhakika na hivyo kueleza

    kwamba wawekezaji wanakaribishwakatika uzalishaji umeme kwa kutumiavyanzo mbalimbali.

    >>INATOKA Uk. 4

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) marabaada ya kuapishwa alika Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) na kuzungumza na Menejimenti ya Shirika hilo. Kulia niMkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba.

    Na Zuena Msuya Singida.

    Mkurugenzi Mkuu waWakala wa Nishati Vijijini(REA), Dkt. LutenganoMwakahesya ameshauri

    kuwa fomu za kuomba huduma yakuunganishiwa umeme ziwekwekatika ofisi za Serikali za Mitaa ilikuwaondolea adha ya kutembeaumbali mrefu wananchi kufuata fomuhizo.

    Ushauri huo aliutoa hivi karibuni

    Mkoani Singida kwenye ziara yakeya kukagua miradi ya Umeme Vijijiniinayotekelezwa na wakala huo nakusimamiwa na Shirika la UmemeTanzania (TANESCO).

    Dkt. Mwakahesya alisema kuwahatua hiyo itahamasisha wananchikujiunga na huduma ya umemewa REA kwa kuwa itawaondoleausumbufu wa kutembea umbali mrefukufuata fomu hizo katika ofisi zaTANESCO ambazo alisema nyinginezipo maeneo ambayo inamlazimumwananchi kutumia gharama kubwahadi kufika eneo husika.

     “Fomu hizi ni bei ndogo, ni shilingielfu sita tu; lakini unakuta mwananchianatumia zaidi ya fedha hiyo kwa

    ajili ya nauli kufuata fomu; sasaTANESCO iangalie namna ambavyoitaweza kuwasaidia wananchi

    kupata fomu hizo kwa urahisi nakupunguza malalamiko,” alisemaDkt. Mwakahesya.

    Vilevile Mkurugenzi huyo,aliwataka wananchi waishio katikavijiji ambavyo viko katika miradiya REA kuchangamkia fursa hiyokwa kuwa huduma hiyo ya umemehutolewa kwa bei nafuu tofauti nakuunganishiwa huduma hiyo moja

    kwa moja na TANESCO.Katika hatua nyingine, Dkt.

    Mwakahesya aliwaasa vijana,kutumia nishati ya umeme kwakujipatia kipato kwa kujiajiri kwakufanya kazi zinazotumia nishatihiyo kama vile kuchomelea vifaa vyachuma, kuuza vinywaji baridi na hatashughuli za muziki ili kupunguzauhalifu na vilevile kuepuka kujiingiza

    katika makundi mabaya ya mitaani.“Eneo ambalo umeme umefika

    maendeleo huwa makubwa sana kilammoja hujitahidi kuutumia ili kubadilimaisha yake na hata wale wasiokuwanao pia wananufaika kwa kupatahuduma za haraka zinazotumiaumeme kama kusaga nafaka; vijanawamekuwa wabunifu wakubwakatika matumizi ya umeme sasa nivyema wale waliojiunga na hudumahiyo watoe ushauri kwa wengine ilikukuza ajira za vijana,” alisema.

    Dkt. Mwakahesya aliongeza kuwasera ya Taifa inaeleza kuwa kufikiamwaka 2025, Tanzania itakuwa katikauchumi wa kati kutokana na kuwepokwa umeme wa uhakika kutoka katikavyanzo mbali vya umeme na hivyokila Mtanzania ajitahidi kuendanana kasi ya sera hiyo ili kuharakishaMaendeleo ya Taifa.

    Katika ziara hiyo, Dk. Mwakahesyaaliambatana na Mkurugenzi waUfundi wa REA, Mhandisi BengielMsofe pamoja na Afisa Mahusianowa wakala huo, Jaina Msuya ambapowalitembelea miradi mbalimbali yaREA katika mikoa ya Kilimanjaro,Arusha, Singida, na Manyara ambapo

    wakandarasi wanaotekeleza miradihiyo wametakiwa kukamilisha kamawalivyokubaliana.

    Fomu za kuomba huduma ya umeme ziwepo

    kwenye Ofisi za Serikali za Mitaa- REA

    Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),Dkt. Lutengano Mwakahesya

    MAKALA

  • 8/20/2019 MEM 104 Online

    9/9

    9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

     

    Maonesho ya 5 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha

     yenye aina mbalimbali za vito zikiwemoTanzanite, Ruby, Sapphire, Tsavorite,

    Rhodol ite, Spessart ite, Tourmaline,

    Chrysobery l na Almasi yanatarajiwa kuvutia  

    Zaidi ya kampuni 100 za wafanyabiashara na

     wachimbaji madini ya Vito kutoka Tanzania na

    nchi zingine za Afrika Mashariki, Kati na Kusini;

    na  zaidi ya wanunuzi 500 kutoka zaidi ya nchi 25

    ulimwenguni

     Jisajili na Ushiriki Sasa!!! 

     Wasiliana na: Kamati ya Maandalizi AGF 

    Simu: +255 784352299 or +255 767106773 

    Barua pepe: [email protected]

    :ama Ofisi za Madini za Kanda

     Yameandaliwa na Wizara ya Nishati na Madinikwa kushirikiana na

    Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA) 

    ZOEZI LA UHAKIKI KWA AJILI YA KULIPA FIDIA KWA WALIOKUWA WAKAZI KATIKA MAENEO YA MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKA GESI ASILIA 

    (LIQUEFIED NATURAL GAS - LNG) MKOANI LINDI

    SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI

    TANZANIA (TPDC)

    TAARIFA KWA UMMA

    Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)linatoa taarifa kwa umma juu ya zoezi linaloendeleala uhakiki kwa ajili ya kulipa fidia kwa waliokuwawakazi katika maeneo ya Kiwanja Na. 1 Kitalu “A”Likong’o, Manispaa ya Lindi. Itakumbukwa kwambamwezi Desemba mwaka 2015 TPDC ilitoa taarifa yakupata hati miliki ya ardhi tajwa kwa ajili ya mradihuu. Baada ya kupata hati miliki, sheria inaelekezammiliki kuwalipa wahusika fidia kulingana na

    tathmini itakayofanywa na Mtathmini Mkuu waSerikali.

    Tarehe 19 Januari 2016, TPDC ilifanya kikao kazina uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Lindi. Kikaohiki kilihusisha Katibu Tawala wa Mkoa, Wakuu waWilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa waLindi na wawakilishi wa kampuni za kimataifa zamafuta na gesi (IOC’s) ambazo ni wabia na TPDCkatika mradi wa LNG. Lengo kuu la kikao kazi hichoilikua ni kutoa elimu juu ya mradi wa LNG na faida

    zitokanazo na mradi huu ili kuweza kujiandaa nafursa na changamoto zinazoambatana na mradi.Pamoja na elimu hiyo Viongozi wa Mkoa waLindi walitaarifiwa uwepo wa wataalamu kutokaOfisi ya Rais, TAKUKURU, Wizara ya Nishati naMadini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleoya Makazi na TPDC ambao wanaendesha zoezi lauhakiki wakishirikiana na wataalam wa ardhi kutokaHalmashauri ya Manispaa ya Lindi.

    Zoezi hili la uhakiki linategemea kumalizika tarehe30 Januari 2016. Nia ni kujiridhisha na idadi yakaya ambazo zitaathirika na mradi huu pamoja namazao, ili walipwe fidia na kuhamishiwa sehemunyingine (resettlement). Ikumbukwe kuwa tayaritathimini ilishafanywa na Wizara ya Ardhi, Nyumbana Maendeleo ya Makazi hapo awali hivyo uhakikiunaofanyika sasa ni kwa kuzingatia ripoti ya tathminihiyo ya mwanzo. Ulipaji wa fidia utafanyika kwamujibu wa sheria za nchi.

    Nia na mategemeo ya Serikali ni kuhakikisha kilamkazi anapata haki yake kwa wakati na kamaanavyostahili kisheria.

    Serikali kupitia TPDC inatoa wito kwa wananchikujiepusha na ununuzi wa maeneo ya kiwanja Na.1-Kitalu “A” Likong’o, Manispaa ya Lindi kwani eneohili limetengwa kwa miradi yenye manufaa kwa Taifana hivyo kujigawia au kuvamia itakuwa ni kinyume

    cha sheria za nchi. Ni vema ikaeleweka kuwa hakunamalipo yeyote yatakayofanyika kwa mtu yeyoteatakayethibitika kuvamia eneo hili kwa minajili yakujipatia kipato.

    Imetolewa na;Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,

    Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania,P.O.Box 2774,

    Dar-es-Salaam.Tanzania.