MEM 105 ONLINE.pdf

download MEM 105 ONLINE.pdf

of 14

Transcript of MEM 105 ONLINE.pdf

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    1/14

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali

    kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizar a ya Nishati na MadiniWasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263

    au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    HABARI ZA

    NISHATI &MADINI

    Toleo No. 105 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Februari 4 - 10, 2016Bulletinews

    http://www.mem.go.tz

    SomahabariUk.3

    Sweden waridhishwa na miradi ya REA

    MgomoTanzaniteOnewamalizika

    Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha, inayoratibu Udhibiti wa Utoroshaji wa Madiniya Tanzanite, Amos Makalla akiongea jambo na Wafanyakazi wa mgodi wa Tanzanite One kutoa mrejesho wa madai yao 14 yaliyowasilishwa kwaKamati hiyo kupitia kwa Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi Mgodini Tawi la TanzaniteOne (TAMICO).

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    2/14

    2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Asteria Muhozya,Arusha

    Mgomo uliopangwakufanyika kwamuda usioelewekawa Wafanyakaziwa Kampuni ya

    TanzaniteOne umefanikiwa kumalizwana Kamati za Ulinzi na Usalamaza Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro naManyara chini ya Mwenyekiti wakeAmos Makalla ambaye pia ni Mkuuwa Mkoa wa Kilimanjaro.

    Hayo yamethibitishwa baadaya kikao cha kutatua mgomo huokilichokutanisha Kamati za Ulinzi naUsalama za Mikoa hiyo, ambayo piainaratibu Udhibiti na Utoroshaji waMadini ya Tanzanite, Menejimenti yaMgodi na Viongozi wa Chama Cha

    Wafanyakazi Migodini (TAMICO),Tawi la Tanzanite One kwa niaba yawafanyakazi wa Tanzanite One.

    Mgomo huo ulianza tarehe1 Februari, 2016, na ulikuwauendelee hadi pale uongozi wamgodi utakapotimiza madai 14 yawafanyakazi yaliyowasilishwa naMwenyekiti wa TAMICO Tawi laTanzanite One Hagai Daniel, kwaniaba ya wafanyakazi katika kikao chakamati ya Ulinzi na Usalama.

    Baadhi ya madai hayo ni Upigajiwa nguzo zinazoweka uimara mgodini;kutolipa Bima ya Afya katika Mfuko waBima ya Afya wakati fedha zinakatwana fedha za NSSF zinazokatwa katikamishahara kutokupelekwa katika

    mfuko huo, mazingira mabaya yakazi, pamoja na uchakavu wa vifaa, naWafanyakazi kusachiwa kwa kuvuliwanguzo zote kila wanapotoka mgodini.

    Baada ya kusikiliza madai yapande zote, Mwenyekiti wa kamatihiyo, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoawa Kilimanjaro Amos Makalla

    alisema mgomo huo umetokana nakutokuwepo kwa mawasiliano mazuribaina ya Menejimenti ya mgodi nawafanyakazi na hivyo kuutaka uongozina wafanyakazi kuondoa tofauti hiyoili kurejesha mahusiano na maelewanomazuri ikiwemo pia kuwezeshashughuli za uchimbaji wa Tanzanitekuendelea kwa maslahi ya pande zoteyanayohusisha Serikali kupata mapatostahiki, wafanyakazi kuendelea na ajirazao na kuhakikisha mgodi unabakisalama.

    Kamati imejiridhisha kwambahakukuwa na mawasiliano mazurikwa pande zote. Tunataka kikao hikikiwe chanzo cha kurejesha mahusianomazuri. Watumishi watekeleze wajibu

    wao lakini pia Menejementi itekelezesehemu yake ikiwemo kutatua kero zawafanyakazi kwa busara na kukutanamara kwa mara. Lakini pia, baada yakikao hiki, asifukuzwe mtumishi hatammoja kutokana na mgomo huu,alisisitiza Makalla.

    Wakati huo huo, Makalla alisisitizasuala la udhibiti wa utoroshaji wa madiniya Tanzanite na kusema kuwa, zoezi laudhibiti wa madini hayo litaendelea ilikuiwezesha Serikali kupata kodi kupitiamadini hayo, ikiwemo pia kuhakikishakwamba wageni wanaofanya kazikatika mgodi huo ni wale tu wenyevibali halali.

    Kwa upande wake, Naibu KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,

    Profesa James Mdoe, alisisitiza kuwa,mawasiliano mabaya ndio chanzo chamgomo na kuzitaka pande zote kuwana lengo moja la kujenga mgodi huo

    kwa manufaa ya taifa, kuwa wawazina kuhakikisha kuwa pande zotezinakutana mara kwa mara ili tatizolililokuwepo awali lisijirudie.

    Kwa niaba ya Menejimenti yaTanzanite One, Faizar Shabahi,alisema kuwa, uongozi wa mgodiutatekeleza maagizo yaliyotolewa naSerikali ikiwemo kupunguza tofautiiliyokuwepo ambayo ndiyo imekuwachanzo cha mgomo huo.

    Mgodi wa Tanzanite unamilikiwana Kampuni ya Wazawa ya SkyAssociates inayomilikiwa kwaushirikiano na Shirika la Madini laTaifa (STAMICO) kila moja ikiwa nahisa asilimia 50. Mgodi huo upo katikaeneo la Merelani, Wilayani Simanjiromkoani Manyara.

    Kamati ya Ulinzi na Usalama

    yamaliza Mgomo TanzaniteOne

    Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mikoa mitatu yaKilimanjaro, Manyara na Arusha inayoratibu Udhibiti na Utoroshaji waMadini ya Tanzanite, Amos Makalla (katikati) akijadiliana jambo na NaibuKatibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe(Kulia) na Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia masuala yaUchumi na Biashara ya Madini, Salim Salim (kushoto) mara baada yakikao kati ya Menejimenti ya mgodi wa TanzaniteOne na Wafanyakazi .

    UTATUZI WA MGOMO WA TANZANITEONENo MADAI YA

    WAFANYAKAZITANZANITE ONE

    UTATUZI WA MGOMO

    1 Upigaji nguzozinazoweka uimara

    mgodini

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madinianayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe,

    alimwagiza Kamishna wa Madini kufanyaukaguzi wa mgodi na kuchukua hatua stahikibaada ya ukaguzi.

    2 Kutolipa Bima ya Afyakatika Mfuko wa Bimaya Afya wakati fedhazinakatwa

    Ndani ya kipindi cha wiki moja tangukufanyika kwa kikao hicho, kiasi cha Milioni 14kiwe kimelipwa kwa Mfuko wa Bima ya Afya.

    3 Fedha za NSSFzinazokatwakatika mishaharakutokupelekwa katikamfuko huo

    Menejimenti ya mgodi waoneshe namnawatakavyolipa fedha hizo na kwa kipindi ganikwa kuzingatia umuhimu na uharaka wa jambohilo.

    4 Kutokulipwa fedha zakazi za ziada

    Fedha za overtime kwa masaa 168 kiasi chashilingi milioni 30, zilipwe baada ya uhakikikwa ushirikiano na viongozi wa TAMICO

    5 Kutolipa fedha zaChama Cha wafanyakazikwa muda wa miakamitatu

    Katibu Tawala Manyara atashughulikia sualahilo

    6 Kutolipwa mshara wamwezi Disemba kamailivyoainishwa katikaMkataba

    Mshahara huo utalipwa pamoja na mshaharawa mwezi Aprili mwaka huu.

    7 Mazingira mabayaya kazi, pamoja nauchakavu wa vifaa

    Uongozi wa mgodi kuboresha mazingiraya kazi na ununuzi wa vifaa vya uchimbajivinavyokidhi mahitaji ya shughuli hizo.

    8 Manyanyaso kwawafanyakazi kutoka kwabaadhi ya viongozi

    Barua ya kusimamishwa kazi kwa mudakwa Mwenyekiti wa TAMICO, Hagai Danielkutenguliwa na kurudishwa kazini haraka.

    9 Kuwapa watu wasiowawekezaji wala wasiowafanyakazi kuchimbandani ya kampuni

    Taarifa kuhusu jambo lolote linaloendeleamgodini litolewa kwa wafanyakazi ili kuwa nauelewa wa pamoja.

    10 Wafanyakazikutokuongezwamshahara Mgodi na Uongozi wa Wafanyakazi watajadili

    suala hilo kwa kushirikiana na Katibu Tawalawa Mkoa wa Manyara11 Kutokujadili sehemu

    iliyobaki ya mkataba wahali bora

    12 Wafanyakazi kusachiwakwa kuvuliwa nguzozote kila wanapotokamgodini

    Chama cha Wafanyakazi, Menejimenti wajadilikuona namna bora ya udhibiti wa madini.Udhibiti usidhalilishe utu wa watu. Wizaraihusike katika kutoa mwongozo sahihi wakupata Scanner haraka na isiyo na madharakwa binadamu.

    13 Wageni kufanyakaziambazo Watanzaniawana uwezo wa kufanyatena kwa umahiri

    Jambo hili litaongezwa katika taarifailiyowasilishwa awali kwa Kamati ya Ulinzi naUsalama.

    14 Kampuni kuwa namikataba miwili tofauti Uongozi kufuata maadili na kuheshimu Sheriaza Kazi.

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    3/14

    3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    FIVEPILLARS OFREFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI

    MHARIRI MKUU:Badra MasoudMSANIFU: Lucas Gordon

    WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, GreysonMwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,

    Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

    INCREASE EFFICIENCY

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OFTHE CLIENT

    SATISFACTION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OFSHAREHOLDERS

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Tuepuke tamaa kuhodhimaeneo ya Serikali

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Sweden waridhishwa na miradi ya REA

    Katika Toleo liliopita, tulichapisha taarifa kutoka Shirikala Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kuhusu zoezila uhakiki kwa ajili ya kulipa fidia kwa waliokuwa wakazikatika maeneo ya Mradi wa kuchakata na kusindika gesiasilia.

    Aidha, tuliandika habari inayotokana na taarifa husika,yenye kichwa cha habari Msinunue eneo la Mradi waGesi TPDC.

    Katika taarifa hiyo, pamoja na mambo mengine, TPDCiliwaasa wananchi kujiepusha na ununuzi wa maeneo

    ya Kiwanja Namba 1, Kitalu A Likongo, kilichopoManispaa ya Lindi kwani eneo hilo kwa sasa linamilikiwakisheria na Serikali kwa ajili ya Mradi wa kuchakata nakusindika gesi asilia.

    Taarifa ilieleza bayana kuwa haitawajibika kutoa malipokwa yeyote atakayethibitika kuvamia eneo husika kwaminajili ya kujipatia kipato.Hii ni kwa sababu ni kinyumecha sheria za nchi kwa mtu yeyote kununua, kujigawia aukuvamia maeneo yanayomilikiwa kisheria na Serikali.

    Kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kutokakwa baadhi ya wananchi kuhusu Serikali kutowalipafidia ipasavyo pale inapochukua maeneo kwa ajili yakuendeshea miradi mbalimbali ya maendeleo.

    Kwa upande mwingine, kuna taarifa kuwa kuna baadhiya wananchi wenye tabia ya kufanya udanganyifu kwa

    kujimilikisha au kuhodhi maeneo isivyo halali ambayoSerikali inayamiliki na kisha kudai fidia kutoka kwaSerikali.

    Udanganyifu huo wa baadhi ya wananchi huhusishapia kumilikisha watu wengine au kuwauzia maeneoambayo tayari Serikali imeyafanyia tathmini na kufanyataratibu za fidia kwa wahusika.

    Kutokana na hali hiyo, tunaunga mkono taarifailiyotolewa na TPDC ikiwataka wananchi kuwa makinina kujiepusha na kununua ama kuhodhi isivyo halali,maeneo ambayo yanamilikiwa kisheria na Serikali kwaajili ya kuendeshea miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

    Ikumbukwe kuwa maeneo yanayochukuliwa naSerikali kwa lengo la kuendeshea miradi hiyo, ni kwa faidaya Taifa zima kwa ujumla. Aidha, kufanya udanganyifu waaina yoyote kwa ajili ya kuhodhi maeneo hayo ili kujipatia

    faida binafsi ni kosa kisheria na husababisha migogoroisiyo ya lazima.

    Tunawaasa wananchi waliokuwa wakazi wa maeneoya Mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia huko Lindi,watoe ushirikiano unaostahili katika zoezi linaloendeleala uhakiki ili hatimaye waweze kulipwa fidia stahiki kwamujibu wa sheria.

    Ikumbukwe kuwa lengo la Serikali siku zote ni kutendahaki kwa wananchi wake, hivyo ushirikiano kutoka kwawananchi husika ni muhimu sana.

    Serikali inatarajia kuwepo na uaminifu na ushirikianokutoka kwa wananchi wakazi wa eneo husika ili kwaupande wake iweze kuhakikisha kila mkazi anapata hakiyake kwa wakati na kama anavyostahili kisheria.

    Tuisaidie Serikali yetu kufanikisha malengo ya kuondoa

    umaskini nchini mwetu kupitia utekelezaji wa miradimbalimbali ya maendeleo kwa ufanisi.Tuwe wazalendo na tuipende nchi yetu.

    Na ZuenaMsuya,Manyara

    Shirika la Kimataifa la Maendeleo laSweden (SIDA) limeridhishwa na

    utekelezaji wa miradi ya umemevijijini inayotekelezwa na Wakalawa Nishati Vijijini (REA) kwa

    kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania(TANESCO) katika mikoa mbalimbalinchini.

    Mkuu wa Shirika la Kimataifa laMaendeleo la Sweden (SIDA) MariaBerlekom alisema hayo hivi karibuni baadaya kuona maendeleo ya wanavijiji waliopatahuduma ya umeme wakati alipofanya ziara yakukagua miradi hiyo katika baadhi ya mikoaya Kanda ya Kaskazini.

    Berlekom alisema kuwa wao kamawafadhili wanaridhika na kufurahi palewanapoona kile wanachokifadhili hasamasuala ya maendeleo yanafanikiwa kwakiasi kikubwa hivyo kutoa motisha kwao yakuendelea kufadhili miradi husika.

    Mkuu huyo wa SIDA alisemaameridhishwa na namna ambavyo wanavijijiwamebadili maisha yao kutoka hatua mojakwenda nyingine kama kutoka kutumiavibatari hadi nishati ya umeme; Pia kupatahuduma bora za kijamii kama vile huduma zaafya pamoja na elimu.

    Wananchi wanasema sasa hiviwanajifungua katika zahanati ya kijiji

    bila kulipia fedha za mafuta ya taa kama

    ilivyokuwa awali, wanapata huduma yakusaga nafaka zao pamoja na kufungua

    biashara ndogo ndogo kutokana na uwepowa huduma ya umeme, alisema Berlekom.

    Berlekom aliongeza kuwa wataendeleakushirikiana na Serikali ya Tanzania katikakufadhili miradi ya maendeleo ili kutimizaazma ya kuiwezesha Tanzania kufikia katikauchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

    Mmoja wa wanakijiji wa Kwedizingamkoani Tanga ambaye anamiliki mashine yakusaga nafaka alisema kuwa alikuwa na ndotoya kufungua mashine hiyo lakini hakuwezakutimiza ndoto yake kutokana na kukosekanakwa huduma ya umeme.

    Alisema kuwa mbali na mashine hiyokumsaidia kuongeza kipato pia imesaidiawanakijiji wenzake kupata huduma kaributofauti na hapo awali kwani walikuwawanatembea umbali mrefu kufuata hudumahiyo na hivyo kuzorotesha shughuli zamaendeleo ambazo kwa sasa zimeimarika.

    Aidha mmoja wa wanawake katikakijiji cha Kwedizinga alisema kuwa zamaniwalipokuwa wakienda kujifungua walikuwawakitozwa fedha za mafuta ya taa au betrikwa ajili ya kurunzi (tochi) ili waweze kupatahuduma hiyo.

    Tunashukuru REA sasa hivi unaendahospitali na kujifungua bila kudaiwa chochotelakini wakati najifungua mtoto wangu wakwanza na wa pili nililipia gharama hizo ilakwa huyu wa tatu haikuwa hivyo, AlisemaFatuma.

    Mhandisi Elneema Mkumbo kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) akitoamaelezo kuhusu moja ya nyumba za mabanzi zilizounganishwa na umeme namashirika ya maendeleo ya SIDA na GIZ wanaofadhili miradi ya umeme vijijiniwakati wa ziara ya kukagua miradi ya umeme mkoani Manyara.

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    4/14

    4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Wadau wahamasishwa kuwekeza katika uongezaji thamani madiniNa Asteria Muhozya, Arusha

    Serikali kupitia Wizara yaNishati na Madini imetoa witokwa wawekezaji wa ndani na

    nje katika Sekta ya Madinikuwekeza kwa Kuanzisha

    Vituo vya Uongezaji Thamani Madiniili kuendeleza fani hiyo iweze kutoamchango wa kiuchumi kwa manufaa yaTaifa.

    Wito huo ulitolewa hivi karibuni jijiniArusha na Naibu Katibu Mkuu, Wizaraya Nishati na Madini anayeshughulikiaSekta ya Madini, Profesa James Mdoewakati wa Mahafali ya Pili ya Ukataji naUngarishaji Madini ya Vito iliyofanyikaKituo cha Jemolojia Tanzania (TGDC)kilicho chini ya Wizara ya Nishati naMadini.

    Profesa Mdoe alisema kuwa,uongezaji thamani madini unalenga

    kuongeza fursa ya ajira kwa Watanzaniawatakaofanya kazi katika vituo hivyo,ikiwemo pia kutoa fursa za wataalamuwa sekta hiyo kujiajiri na hivyo kuongezamapato kwa Serikali jambo ambalo pia

    litasaidia kuongeza mchango wa sektahiyo katika Pato la Taifa.Aliongeza kuwa, Kituo hicho kina

    historia ya pekee katika Sekta ya Madinikwa kuwa kimekuwa cha kwanzana pekee kuanzishwa hapa nchini,na kuongeza kuwa, uwepo wake nikielelezo sahihi cha kazi za ubunifu nauongezaji thamani madini ya vito.

    Vilevile, Profesa Msofe alisemakuwa, kituo hicho kinatarajia kuwachachu katika kutoa wataalam borawatakaotumika kufanya kazi katika vituovya kukata madini ya vito na usonarahapa nchini pamoja na kutoa elimuna ujuzi kwa wachimbaji wadogo wamadini ili waweze kuboresha shughulizao.

    Pia alisema kuwa, kuanzishwa kwakituo hicho ni moja ya hatua za Serikaliza kutimiza malengo yaliyomo katikaSera ya Madini ya Mwaka 2009 yenyelengo la kuongeza mchango wa Sekta ya

    Madini katika Pato la Taifa na ajira kwawatanzania kupitia uongezaji thamanimadini, ikiwa pamoja na mafunzo yaJemomojia, ukataji na ungarishaji wamadini ya vito , utengenezaji wa bidhaaza mapambo na uchongaji wa vinyagovya mawe.

    Aidha, Profesa Msofe alitoa witokwa Kampuni zinazofanya biasharaya madini ya vito na wadau wenginekuchangia maendeleo ya Kituo hichoili kiwe kitovu cha kutoa Wataalamwanaokidhi mahitaji ya tasnia ya madiniya vito nchini.

    Akizungumzia zuio la mwaka 2010la kusafirisha Tanzanite ghafi inayozidigramu moja nje ya nchi, alisema lengo lazuio hilo lilikuwa ni kuhamasiaha ujenzi

    wa vituo , vyuo, taasisi na viwanda vyakuongeza thamani ya madini hayo nchinina kuongeza kuwa, jambo hilo pia ndilolililopelekea Serikali kwa kushirikiana naBenki ya Dunia kuanzisha kituo hicho.

    Aliongeza kuwa, agizo la kuzuiausafirishaji wa madini ghafi pialiliwezesha kuanzishwa kwa vyuo vyamafunzo ya ukataji na usanifu wa madiniya vito na kuvitaja kuwa ni pamoja navyuo vya Arusha Technical College(ATC), Arusha Gemolojical and JewelryVocational Training centre (AGJVTC),VETA Shinyanga, na Arusha MineralResources Training College.

    Pamoja na utoaji mafunzo yauongezaji thamani madini, aliutakauongozaji wa kituo hicho kupanuawigo wake wa mafunzo kwa kuangaliauwezekano wa kuwa na somo la maadilina ujasiriamali na kuongeza kuwa,

    >>Inaendelea Uk. 5

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikiaSekta ya Madini, Profesa James Mdoe akisisitiza jambo wakati waMahafali ya Pili ya Mafunzo ya Ukataji na Ungarishaji Madini ya Vitokatika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikiaSekta ya Madini, Profesa James Mdoe (katikati), akiwa katika picha yapamoja na baadhi ya Wafanyabiashara wa Madini wa Jijini Arusha katikaMahafali ya Pili ya Mafunzo ya Ukataji na Ungarishaji Madini ya Vitoambapo jumla ya wanafunzi 14 wamehitimu mafunzo hayo.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikiaSekta ya Madini, Profesa James Mdoe akiangalia madini mbalimbali kupitiakifaa kinachotumika kukuza mawe ya madini ili yaweze kuonekanavizuri ikiwemo kubaini kasoro. Kabla ya kutunuku vyeti Wahitimu 14wa Mafunzo ya kungarisha na kukata madini ya Vito, Prof. Mdoe alipatafursa ya kuangalia bidhaa mbalimbali za mapambo zilizotengenezwana wahitimu hao ikiwemo vifaa vinavyotumika wakati wa mafunzo.Anayemwonesha kushoto ni Mtumishi katika cha Jemolojia Tanzania,

    Salome Tilumanywa (kushoto). Wa kwanza kulia ni Kaimu Mratibu waKituo hicho John Mushi, anayefuata ni Kamishna Msaidizi wa Madinianayeshughulikia masuala ya Uchumi na Biashara ya Madini, Salim Salim.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia

    Sekta ya Madini, Profesa James Mdoe (katikati) katika picha ya pamojana baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kutokaMakao Makuu na walio katika osi za Madini za Arusha na Moshi naKituo cha Jemolojia Tanzania, wakati wa Mahafali ya Pili ya Mafunzo yaUkataji na Ungarishaji Madini ya Vito.

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    5/14

    5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    UONGEZAJI THAMANI MADINI

    Picha N0. 1, 2 na 3 ni baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Ukatajina Ungarishaji Madini ya Vito wakitumia mashine mbalimbali zaKuchonga maumbo mbalimbali na kungarisha madini ya Vito.

    Mmoja wa Walimu katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), RamadhanHaizer (kushoto) akimwonesha mfano wa mapambo ya vito ambayoWahitimu wamepata mafunzo ya kutengeneza katika maumbo mbalimbaliatika fani za Ungarishaji na uchongaji madini ya vito Naibu Katibu Mkuu

    wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesaames (wa pili kushoto). Katikati ni Kaimu Kamishna wa Madini Tanzania,Mhandisi Ally Samaje.

    aminifu ni kitu muhimu kwa kuwahughuli za ukataji madini zinabeba

    madini yenye gharama kubwa. Niizuri wahitimu watakaotoka kwenyeituo hiki wafanye kazi kwa weledi naadilifu mkubwa, alisistiza Mdoe.

    Awali, akisoma risala kwa niaba yawahitimu wa mafunzo hayo, MonicaLaiton, alisema kuwa, mafunzo hayoamewapa ujuzi wa kukata madini yaina tofauti ikiwemo Tanzanite katika

    maumbo mbalimbali na kuongezakuwa, ujuzi huo utawawezesha

    kuajiriwa au kujiajiri na kuongezakuwa, mafunzo hayo yamedhihirishawazi kuwa, wanawake wanawezakufanya kazi katika sekta hiyo tofautina dhana iliyokuwepo awali kwambashughuli za sekta hiyo zinafanywa nawanaume pekee.

    Awali, akitoa historia ya Kituo hicho,Kaimu Kamishna wa Madini, MhandisiAlly Samaje alisema kuwa, ukarabatiwa majengo ya kituo ulifanywa kupitia

    Mradi wa Usimamizi Endelevu waRasilimali Madini (SMMRP), chiniya ufadhili wa Benki ya Dunia, lengolikiwa ni kuhamasisha uongezajithamani madini na kuboresha sekta yamadini ii iweze kuchangia zaidi pato lataifa ikiwemo kupanua wigo wa ajira.

    Aidha, Mhandisi Samaje aliongezakuwa, Jumla ya Wahitimu 14, katiya 18 wamehitimu mafunzo hayoyaliyochukua kipindi cha miezi sita,chini ya ufadhili wa Kamati inayoandaaMaonesho ya Kimataifa ya Vito ya

    Arusha (Arusha Gem Fair) kupitiaMfuko wa kuendeleza Wanawakekatika tasnia ya madini.

    Maonesho ya Arusha huandaliwana Chama cha Wafanyabiashara waMadini Tanzania (TAMIDA) kwakushirikiana na Wizara ya Nishatina Madini, ambapo hufanyika kilamwaka. Mwaka huu maonesho hayoyatafanyika jijini Arusha katika Hotelya Mount Meru kuanzia tarehe 19- 21,Aprili, 2016.

    >>Inatoka Uk. 4

    1

    2

    3

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    6/14

    6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Zuena Msuya na DevotaMyombe, Dar Es Salaam

    Imeelezwa kwamba, tathmniniya utekelezaji wa Mpangowa Umeme (Power Africa)unaotekelezwa na Serikali yaMarekani kwa nchi za Afrika

    imekamilika.

    Hayo yalielezwa hivi karibunijijini Dar es Salaam, na Naibu KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati naMadini anayeshughulikia Nishati,Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyowakati akifungua kikao cha kujadilitathmini ya utekelezaji wa mradi huonchi sita za Afrika ikiwemo Tanzania.

    Dkt. Pallangyo alisema, Tanzaniainahitaji umeme katika shughuli zakeza maendeleo ili kutimiza lengo lakufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka2025; hivyo kuna umuhimu wakutekeleza mipango ya kufanikishaazma hiyo na kuongeza juhudi zaidikatika kuibua miradi mipya ya umemeAlisema, Mpango wa Umeme wa

    Afrika ambao ulizinduliwa mwaka2013 na Rais Barrack Obama waMarekani alipofanya ziara yake kwamara ya kwanza kwa nchi za Afrikaikiwemo Tanzania,ulikuwa na lengola kuzijengea uwezo nchi za Afrikahasa zinazoendelea pamoja nakuimarisha upatikanaji na usambazajiwa huduma ya umeme katika mataifahayo.

    Aidha,alieleza kuwa malengomengine ya Mpango huo kuwa nipamoja na kuzijengea uwezo nchihusika kwa kuwawezesha wawekezaji

    binafsi kuzalisha umeme, ili kuongezakasi ya usambazaji wa huduma hiyokwa wananchi wake.

    Tulipewa kazi ya kuandaamikakati ya utekelezaji wa mradihuo na kubainisha namna ambavyoutatekelezwa katika maeneo

    mbalimbali nchini kwa maana yauzalishaji, usambazaji na usafirishaji,kazi hiyo tumeitekeleza kwa kiasikikubwa.alisema Dkt. Pallangyo.

    Aidha katika mkutano huo,Taasisi zilizo chini ya Wizara yaNishati na Madini, ziliwasilishautekelezaji wa maagizo waliyopewaambapo Naibu Mkurugenzi Mtendajiwa Shirika la Umeme Tanzania

    (TANESCO),anayeshughulikiaUwekezaji,Mhandisi DecklanMhaiki alisema shirika hilo linasubirikuanza kwa mradi husika kamailivyoelekezwa na Serikali kwani tayariwamejiandaa vya kutosha.

    TANESCO ndio wenye

    dhamana ya kusambaza umeme nchinzima hivyo tuko tayari muda wowoteili kutimiza lengo na azma ya Serikaliya kufikia uchumi wa kati kufikiamwaka 2025 na endelea kuboreshamiundombinu ya usambazaji,alisema

    Kwa upande wake, MkurugenziMkuu wa Mamlaka ya Udhibitiwa Huduma za Nishati na Maji

    (EWURA), Felix Ngamlagosialisema EWURA ilipewa majukumumbalimbali ikiwemo taratibu za njiaya usafirishaji wa umeme jamboambalo limekamilika.

    Mradi wa umeme Afrikaunatekelezwa katika nchi sita ikiwemoTanzania, Liberia,Kenya,Ethiopia,Nigeria na Ghana.

    Tathmini ya mpango wa umeme Afrika yakamilika

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. JulianaPallangyo, akifungua mkutano wa Tathmini ya Mpango wa UmemeAfrika, uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt.Juliana Pallangyo (watatu kutoka kulia) na

    Kamishna Msaidizi wa Nishati, James Andilile (Kulia kwa Naibu Katibu Mkuu), wakiwa na wawakilishikutoka Serikali ya Tanzania na Serikali ya Marekani katika mkutano wa Tathmini ya Mpango wa UmemeAfrika. Mkutano ulifanyika hivi karibuni, jijini Dar es Salaam.

    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati naMaji, Felix Ngamlagosi akizungumza katika mkutano wa Tathmini yaMpango wa Umeme.

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    7/14

    7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    1 2

    5 6

    3 4

    MGOGORO TANZANITEONE

    1 na 2. Baadhi ya Wawakilishi wa Menejimenti ya Mgodi wa TanzaniteOne wakijibu madai ya Wafanyakazi wa mgodi huokwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mikoa Mitatu Kilimanjaro, Manyara na Arusha inayoratibu Udhibiti na Utoroshaji waMadini ya Tanzanite.

    3. Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akifafanua jambo wakati wa kikao kati ya Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mikoa Mitatu Kilimanjaro, Manyara na Arusha inayoratibu Uthibiti na Utoroshaji wa Madini ya Tanzanite,Menejimenti ya Mgodi na wawakilishi wa Chama cha Wafanyakazi Mgodini Tawi la TanzaniteOne (TAMICO).

    4. Katibu wa Chama cha Wafanyakazi Mgodini Tawi la TanzaniteOne (TAMICO), Richard Nyanginywa akiongea jambowakati akiwasilisha madai 14 ya Wafanyakazi wa mgodi wa Tanzanite One mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya MikoaMitatu Kilimanjaro, Manyara na Arusha inayoratibu Udhibiti na Utoroshaji wa Madini ya Tanzanite.

    5 na 6. Baadhi ya Wafayakazi wa Mgodi wa TanzaniteOne wakifuatilia mkutano wa wazi kati yao na Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mikoa Mitatu Kilimanjaro, Manyara na Arusha inayoratibu Udhibiti na Utoroshaji wa Madini ya Tanzanite naMenejimenti ya mgodi.

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    8/14

    8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Tano wakujadili namna ya kuboresha masuala ya kijamii na kiuchumikwa wachimbaji wadogo baina ya Tanzania na Canadawakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa mkutano.

    Mmoja wa Wajumbe wa kikao hicho Bubelwa Kaiza akichangia madakatika mkutano huo.

    Baadhi ya Wajumbe wa mkutano wakimsikiliza Mgeni rasmi NaibuKatibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Masualaya Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo (hayupo pichani) wakati akifunguakikao hicho.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikiaMasuala ya Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo akifungua mkutanouiliohusisha wadau wa sekta ya madini kilichokuwa kikijadili namna yakurasimisha sekta ya wachimbaji wadogo wa madini

    Mwezeshaji wa kikao cha kujadili namna ya kuboresha masualaya kijamii na kiuchumi kwa wachimbaji wadogo baina ya Tanzaniana Canada Dkt. Wilson Mutagwaba akiongea jambo kabla yakuwakaribisha wachangia mada wakati wa mkutano huo

    Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia ufunguzi wa mkutano

    URASIMISHAJI UCHIMBAJI MDOGO WA MADINI

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    9/14

    9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Maonesho ya 5 ya Kimataifa yaVito ya Arusha

    yenye aina mbalimbali za vito zikiwemo

    Tanzanite, Ruby, Sapphire, Tsavorite,Rhodol ite, Spessart ite, Tourmaline,

    Chrysobery l na Almasiyanatarajiwa kuvutia

    Zaidi ya kampuni 100 za wafanyabiashara na

    wachimbaji madini ya Vito kutoka Tanzania na

    nchi zingine za Afrika Mashariki, Kati na Kusini;

    nazaidi ya wanunuzi 500 kutoka zaidi ya nchi 25

    ulimwenguni

    Jisajili na Ushiriki Sasa!!!

    Wasiliana na: Kamati ya Maandalizi AGF

    Simu: +255 784352299 or +255 767106773

    Barua pepe: [email protected]

    :ama Ofisi za Madini za Kanda

    Yameandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini

    kwa kushirikiana naChama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA)

    MKUTANO WA WAZALISHAJI WADOGO WAUMEME WA MAJI (MINI-HYDROS)

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    Wizara ya Nishati na Madini inawakumbushaWazalishaji wadogo wa umeme wa Maji

    (chini ya Megawati 20) kuhudhuria mkutanoutakaofanyika siku ya Jumatatu tarehe 8Februari, 2016 katika ukumbi wa Mtera,Dodoma.

    Mameneja wote wa TANESCO wa Kandanao wanasisitizwa kuwepo katika kikao hichobila kukosa.

    Kikao kitaongozwa na Waziri wa Nishati

    na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongokuanzia saa 2:00 Asubuhi

    Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na;

    Naibu Katibu Mkuu, NishatiSimu: 2110426Barua pepe: [email protected]

    Au

    Mkuu wa Mawasiliano SerikaliniSimu: 2110490 au 2110389Barua pepe: [email protected]

    Imetolewa na;Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    10/14

    10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    8000 MW energy gaps in next 10years opens an opportunity for privatesector to partner with government to

    invest on the existing gaps in generation,Transmissions and distribution. PublicPrivate Patrnerships( PPPs) in theenergy sector come in different shapes,

    sizes and structures, generations andTransmissions are usually associatedwith capital intesity investments and

    technology capacity unlike distributionsnetwork. The electricity Supply industryreform Strategy and roadmap (ESI-RSR) opens up opportunities for the

    private sector to work together withgovernment to meet power vision 2025.Gas Availability, unutilized Renawable

    Energy like Hydro, Wind, Geothermal,biomass, Solar) other Sources like coalprovides much needed fuels for electricitygeneration in Tanzania. The Ministry

    of energy has also opened investment

    inquiry desk in an effort to boost private

    investment enthuism in energy sectorby providing first hand information and

    contacts.

    BUSINESS PERSPECTIVE

    By Salum Mnuna: MBA, Certied PPP specialist based in Dar es SalaamCan be reached via email [email protected] or WhatsApp 0767457817

    The views in the article are solely based on the knowledge of the author and should

    not be associated with his employer.

    Email: [email protected]

    2025 Power Vision, 10GW Target and PPPpie on meeting the Energy Targets

    2025 vision targets includesHigh Quality lively hood,Good governance and Rule ofLaw, Strong and Competitiveeconomy whilst many other

    documents in an efforts to implement thevision 2025 have been drawn includingfive years Development Plan, long termperspective plan (LTPP) and sectorialstrategic plans all these documentsfocusing on detailing implementation

    strategy to work on meeting targets tocontribute in building the economy andsocial economic development of ourpeople and Country to reach an overalltarget of becoming a middle incomecountry. In 2025 Vision Developmentof mindset and empowering culture,Competence and competitivenesstogether with Good governance andrule of law have been pinpointed asthe drivers surrounding the journey to

    see the vision become a reality. Underthe current country administrationleadership the five years development

    focuses on building industrial Tanzania,like what again the President, Iterated onhis visit to Arusha on 22 January 2016,he was quoted saying the new Tanzaniais under way when speaking to admirerson his way to Monduli, but also remindedthe Tanzania Peoples Defense forces(TPDF) on the need to focus on buildingthe economy during peace times allthese in an efforts to mobilize maximumresources at his exposure to meet certainlevel of economic growth.

    Industrial economy is directly linkedto value creation and addition withinthe country to create jobs and increasevalue of the exported products throughmanufacturing and Agriculture. In order

    for these to happen the country needs tomeet and exceed its targets in electricitygeneration, transmission and distributions

    networks to increase both accessibilityand connectivity to fuel development ofindustrial economy. Electricity Supplyindustry reform Strategy and road maphas outlined powering vision 2025 tohave 10GW (10,000MW) installed and50% connectivity and 75% access levelfrom the existing capacity of less than1.5 GW (1500MW) installed capacity,24% connection level and 36% accesslevel.In simple arthmetic the countryhave more 8000 MW gaps to reach themagic number of 10000 MW (10GW)envision energy capacity by 2025 tosustain country energy needs and fuelindustrial economy.

    Private Sector Opportunity in Electricity infrastructure

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    11/14

    11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Asteria Muhozya,Merelani

    Kamati ya Ulinzi na Usalamaya Mikoa Mitatu (3) yaKilimanjaro, Arusha naManyara hivi karibuniilifanya mkutano wa

    hadhara na wachimbaji wadogo waMadini ya Tanzanite, wanunuzi nawafanyabiashara ya madini wa lengoa kupokea maoni ya wadau hao waSekta ya madini, ambapo pia Kamatihiyo ilieleza kuhusu suala la Udhibiti,Utoroshaji wa madini ya Tanzanite naukusanyaji kodi.

    Akizungumza katika mkutanohuo, Mwenyekiti wa Kamati hiyona Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,

    Amos Makalla alisisitiza kuhusu sualaa udhibiti wa utoroshaji wa madini nakuongeza kuwa, Kampuni zisizolipa

    kodi zitafutiwa leseni za madini.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya

    Nishati na Madini, anayeshughulikia

    Madini, Profesa James Mdoe, akijibuhoja ya upatikanaji wa vifaa vyauchimbaji, alieleza kuwa, Serikaliitatengeneza utaratibu wa namna yakupata vifaa hivyo na kuongeza kuwa,Serikali imedhamiria kumaliza migogoroya wachimbaji ikiwemo kutekeleza yaleiliyoahidi.

    Kwa upande wake, KaimuKamishna wa Madini, Mhandisi AllySamaje alisema kuwa, Wafanyabiasharawa Madini (Dealers) hawaruhusiwikununua madini mgodini, badalayake wanaopaswa kununua mgodinini Mawakala (Brokers) na kuongezakuwa, Mfanyabiashara wa Madini

    atakayekamatwa akitenda kinyume,madini yake yatataifishwa na kupigwaMnada na Serikali.

    MKUTANO WA HADHARA MERERANI

    Picha N0. 1,2,3 ni baadhi ya wachimbaji, wauzaji na wafanyabiashara wamadini wa Mererani wakifuatilia mkutano kati yao na Kamati ya Ulinzina Usalama yaMikoa mitatu ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Lengo lamkutano huo ilikuwa kusikiliza maoni kuhusu Sekta ya Madini hususanMadini ya Tanzanite.

    Mmoja wa wadau katika mkutano wa hadhara kati ya Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mikoa mitatu ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara akiuliza swaliwakati wa mkutano huo.

    Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi akiongea jambowakati wa mkutano wa hadhara wa Kamati ya Ulinzi na Usalama yaMikoa mitatu ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara na wachimbaji, wauzajina wafanyabiashara wa madini, Merelani. Kutoka kushoto ni KatibuTawala wa Mkoa wa Arusha Severine Kahitwa, Naibu Katibu Mkuu waNishati na Madini, Profesa James Mdoe, na Mwenyekiti wa Kamati yaUlinzi na Usalama ya Mikoa Mitatu ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha,Amos Makala

    1

    2

    3

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    12/14

    12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    MAHAFALI KITUO CHA JEMOLOJIA ARUSHA

    Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Ukataji na Ungarishaji wa Madini yaVito katika Kituo cha Jemolojia wakifuatilia tukio la Mahafali jijini Arusha

    Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuuwa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Sekta ya Madini,Profesa James Mdoe (katikati) na baadhi ya viongozi wa ChamaCha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA) Wa kwanza na wa pilikushoto. Wa kwanza kulia ni Mkufunzi wa Mafunzo na anayefuata niKaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.

    Baadhi ya wageni walioka katika Mahafali ya Pili ya Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) wakiangalia vifaa na vitabu vinavyotumiwa na wanafunzikatika mafunzo ya Ukataji na Ungarishaji wa Madini ya Vito.

    Naibu Katibu Mkuu waWizara ya Nishati naMadini anayeshughulikiaSekta ya Madini,Profesa James Mdoe,akipokea zawadi yaKinyago kilichochongwakutokana na madiniya Mawe katika Kituocha Jemolojia Tanzania(TGC), kutoka kwaAsa kutoka Osi zaMadini Arusha, HalimaHussein wakati waMahafali ya Pili yaMafunzo ya Ukataji naUngarishaji madini yavito. Wanaoshuhudiakatikati ni KaimuKamishna wa Madini,Mhandisi Ally Samajena wa kwanza kuliani Kaimu Mratibu waKituo cha TGC, JohnMushi.

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    13/14

    13BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    MAHAFALI KITUO CHA JEMOLOJIA ARUSHA

    Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania(TAMIDA), Sam Molel (kushoto), akijadiliana jambo na Kamishna Msaidiziwa Madini anayeshughulikia masuala ya Uchumi na Biashara za Madini,Salim Salim (Kulia) Wanaofuatilia kushoto ni Mtumishi wa Kituo Chaemolojia Tanzania (TGC) Salome Tilumanywa, Wa pili kulia ni KaimuKamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Ally Samaje na Asa MadiniMkazi wa Merarani Mhandisi Henry Mditi

    Monica Laiton kushoto akisoma risala kwa niaba ya wahitimu 14 waMafunzo ya Ukataji na Ungarishaji wa Madini ya Vito.

    Naibu Katibu Mkuu waWizara ya Nishati naMadini Profesa James Mdoeakimkabidhi Cheti mmojawa Wahitimu wa Mafunzoya Ukataji na Ungarishajiwa Madini ya Vitoyaliyofanyika hivi karibunikatika

    Pichazinazooneshamadini ya ainambalimbalina mapamboyanayotengenezwana Kituo chaJemolojia Tanzania(TGC) kutoka namadini ya Mawe .

  • 7/25/2019 MEM 105 ONLINE.pdf

    14/14

    14 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    NAFASI ZA MAFUNZO YA UKATAJI VITO KWA WANAWAKE

    TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MKUTANO NA WAWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA NISHATITAREHE 15 18 FEBRUARI, 2016

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    Kamati ndogo ya kusimamia Mfukowa Maendeleo ya Wanawake (WomenFoundation Fund) iliyo chini ya Kamati yaMaandalizi ya Arusha Gem Fair (AGF)inatangaza nafasi 18 za mafunzo ya mudamfupi katika fani ya ukataji na usanifu wamadini ya vito (lapidary training course).Mafunzo hayo yatatolewa katika Kituo chaJemolojia Tanzania (TGC), kilicho chini ya

    Wizara ya Nishati na Madini, kilichoko eneola Themi, Jijini Arusha kuanzia mwezi Machi,2016. Atakayechaguliwa kujiunga atalipiwaada na posho ya kujikimu kumuwezeshakuhudhuria mafunzo kila siku. Hata hivyo,atajitegemea malazi kwa muda wote.

    Lengo la Mafunzo

    Lengo la mafunzo haya ni kuwawezeshawanawake kujiajiri au kuajiriwa katika fani yaukataji na usanifu madini ya vito ili kuongezathamani ya madini hayo.

    Muda wa Mafunzo

    Muda wa mafunzo ya cheti cha LapidaryTechnology utakuwa miezi sita (6).

    Sifa za Mwombaji- Awe mwanamke Mtanzania mwenye

    umri usiozidi miaka 30; na- Awe na elimu ya kidato cha nne na

    kuendelea mwenye kufaulu Kingerezana Hisabati.

    Barua za maombi, CV na vyeti vitumwekwa: - Mwenyekiti, Kamati ya AGF Women

    Foundation Fund, S. L. P. 641, Arusha; auyaletwe kwa mkono katika ofisi za MadiniKanda ya Kaskazini zilizopo Themi, Njiro.Kwa maelekezo zaidi piga simu Namba 027254 4079. Mwisho wa kupokea maombi nitarehe 22/02/2016.

    Itakumbukwa kuwa tarehe 20 Desemba,2015, Wizara ya Nishati na Madini ilitoaMwaliko kwa Wawekezaji wa ndani na njeya nchi kuwasiliana na Wizara ya Nishatina Madini kwa ajili ya kuwekeza katikauzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia,maporomoko ya maji, makaa ya mawe nanishati jadidifu (jotoardhi, upepo, nguvu yajua, tungamotaka, mawimbi (tides & waves)).Lengo la kuhamasisha uwekezaji kwenyevyanzo hivyo ni kuhakikisha nchi inakuwa naumeme wa kutosha, wenye uhakika na wa beinafuu.

    Wizara inapenda kuzitaarifu Kampunizilizoonesha nia ya kuwekeza nchini pamoja

    na wananchi kuwa, hadi tarehe 26 Januari,2016jumla ya Kampuni 100 zimeonesha niaya kuwekeza katika Sekta ndogo ya Umeme.Kabla ya kuanza utaratibu rasmi wa kupataWawekezaji wenye uwezo wa rasilimalifedha, teknolojia na kutoa huduma husikandani ya kipindi kifupi, Wizara imeandaaMkutano wa Wawekezaji kuanzia tarehe 15hadi 18 Februari, 2016. Wawekezaji wote wandani walioomba wametakiwa kuja na wabiawao katika Wizara ya Nishati na Madini.

    Lengo la Mkutano huo ni kuwawezeshaWawekezaji kupata maelezo ya kina kuhusufursa zilizopo nchini na pia kuiwezesha Wizarakupata maelezo kutoka kwa Wawekezaji

    kuhusu uwezo wao wa kutekeleza miradi

    wanayokusudia. Ili kutimiza lengo hilo, kilaMwekezaji amepangiwa tarehe na muda wakukutana na Viongozi wa Wizara ya Nishatina Madini pamoja na Taasisi zake chini yauenyekiti wa Waziri wa Nishati na MadiniMhe. Prof. Sospeter Muhongo.

    Washirika wote wanaombwa kuhudhuriaMkutano huo bila kukosa na kamawalivyopangiwa kupitia barua za mialiko.

    Imetolewa na: Kitengo cha MawasilianoSerikalini

    WIZARA YA NISHATI NA MADINI