MEM 118 Online

download MEM 118 Online

of 15

Transcript of MEM 118 Online

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    1/15

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali

    kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizar a ya Nishati na MadiniWasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263

    au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM)

    HABARI ZA

    NISHATI &MADINI

    Toleo No. 118 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Mei 5 - 11, 2016Bulletinews

     

    http://www.mem.go.tz

     

    Taarifa Leseni zaMadini sasa kwa SMS

    Ujenzi bomba la mafuta kuanza karibuni >>UK. 5

    Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Wizara yaNishati na Madini, Francis Fungameza

    Kaimu Kamishna wa Madini,Mhandisi Ally Samaje

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    2/15

    BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    2

    Teresia Mhagama na Asteria Muhozya

    Imeelezwa kuwa, Wizara yaNishati na Madini imeendeleakurahisisha utoaji wa hudumaza leseni za madini ambaposasa wamiliki wa Leseni hizo

    wanaweza kupata taarifa za ada yaleseni kwa njia ya ujumbe wa simu(SMS).

    Mkuu wa Kitengo cha TEHAMAkatika Wizara ya Nishati na Madini,Francis Fungameza alisema kuwaili mteja aweze kupata huduma hiyoanatakiwa kuandika neno MEM,aache nafasi , kisha aandike Nambaya Leseni na kutuma kwenda 15341.

    Fungameza alisema kuwa hizo nihabari njema kwa wamiliki wa lesenikwani sasa wataweza kupata taarifa

    hizo kwa wakati na hivyo kulipia adaza leseni hizo kwa wakati.Gharamaya huduma hiyo ni shilingi 250.

    Aidha Fungameza alisemakuwa Wizara imekuwa ikibuni njiambalimbali ili kuhakikisha kuwahuduma za utoaji wa leseni za madinipamoja na taarifa mbalimbali kuhusuleseni hizo zinapatikana kwa urahisina kwa uharaka tofauti na ilivyokuwahapo awali.

    “Kwa mfano kwa sasa tayari kunamfumo wa kielektroniki ujulikanaokamaOnline Mining CadastreTransactional Portal (OMCTP)ambao unawawezesha wateja kufanyamasuala mbalimbali ikiwemo kufanyamalipo ya leseni na mrabaha, wateja

    waliosajiliwa kutuma maombi yaleseni, kuhakiki taarifa za leseniwanazomiliki na kutuma taarifa zautendaji kazi .

    Aliongeza kuwa Mfumo wa

    OMCTP pia unawawezesha watejakupata taarifa mbalimbali za Sekta yaMadini zikiwamo ramani za kijiolojiana taarifa za migodi mikubwa.

    Fungameza alieleza kuwa hapoawali, mfumo wa utoaji leseniulifanyika kwa njia ya mkono(manually) na ulitegemea utumaji wakaratasi (paperwork based) na hali hiyoilichangia kuchelewesha utoaji lesenina kuongeza kuwa utoaji huo waleseni ulitegemea hali ya mawasilianokama ya telegram na rejesta.

    “ Vilevile upimaji na uchorajiramani za kijiolojia ulifanyika kwanjia ya mkono na ulitegemea umahiriwa mtu na mara nyingine makosayalifanyika na kusababisha migogoroau waombaji kukosa leseni kwasababu zisizo za msingi,” aliongezaFungameza.

    Anasema kuwa mfumo huo

    wa awali ulileta changamoto kwaniWizara ilikuwa na wakati mgumukuhakikisha kuwa kumbukumbu zaleseni zinatunzwa vizuri bila kupotea,pia kulikuwa na kazi ngumu yakuchambua nyaraka za leseni kwa njiaya mkono (manually) ili kufuatilia uhaiwa leseni, malipo ya ada na utendajiwa wamiliki wa leseni.

    Aliongeza kuwa leseni nyingihazikuweza kuchambuliwa na halihiyo iliathiri ubora wa utendaji waWizara na pia kasi ya kuwahudumiawananchi ilikuwa ndogo.

    Alisema kuwa mfumo wakieletroniki unaotumika sasa katikaleseni za madini unakuwa kamakituo kimoja (one-stop-centre)

    kinakachotumiwa na wadau wa Sektaya Madini walio nchini na nje ya nchikuweza kujipatia huduma za leseni bilakulazimika kusafiri kwenda kwenyeofisi ya Madini, pindi wanapokuwa

    wamesajiliwa ndani ya mfumo huo.Alisema kuwa OMCTP ina faida

    mbalimbali ikiwemo, kuongeza uwazina kasi ya utoaji wa leseni za madini naWateja kuingiza maombi ya leseni waowenyewe hivyo kupunguza tatizo lamlundikano wa maombi kwenye ofisiza madini.

    Aliongeza kuwa Wateja na Serikaliwatakuwa na uhakika na maombi

    yote yatakayowasilishwa (yakiwamomaombi ya sihia (transfer), kuhuishaleseni na pia kuwa na uhakika namalipo yote yatakayofanywa kupitiamfumo wa OMCTP.

    “ Kupitia mfumo huu, Watejapia wanapata taarifa za leseni zaokila wakati na kujua wanapotakiwakufanya malipo ya leseni auwatakapotakiwa kutuma taarifa zautendaji kazi na pia kurarahishamawasiliano kati ya Wizara nawamimiki wa leseni,” alisemaFungameza.

    Aidha alisema kuwa Wateja

    wataweza kuhuisha taarifa za lesenizao za madini kama vile anuanina namba za simu kupitia mfumowa OMCTP pindi taarifa hizozitakapobadilishwa.

    Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Wizara ya Nishati na Madini, FrancisFungameza

    Taarifa za Leseni za Madini sasa kwa SMS

    Zaidi ya shilingi Bilioni 8 kutumikakwa Ruzuku ya Wachimbaji WadogoTeresia Mhagama na Mohamed Saif 

    Benki ya Dunia (WB) imeahidi kutoaDola za Marekani milioni 4 sawa nazaidi ya shilingi Bilioni 8, kwa ajili yaRuzuku katika shughuli za uchimbajimdogo wa madini nchini.

    Hayo yamebainishwa hivi karibuni jijini Dar esSalaam na Waziri wa Nishati na Madini, ProfesaSospeter Muhongo mara baada ya kumalizakikao na Watendaji Wakuu wa Benki ya Duniawanaosimamia Miradi ya Sekta ya Madini.

    Profesa Muhongo alisema kuwa sehemu yafedha hizo za Ruzuku ambayo ni ya Awamu yaTatu zitatolewa mwezi Septemba, 2016.

    Aliongeza kuwa fedha hizo zitatumikakufadhili uendelezaji wa vituo Saba vya mfano

    vya utafutaji na uchimbaji mdogo wa madiniambavyo vitachaguliwa na Wizara baada yakufanya tathmini ya maeneo yanayowezakuwekwa vituo hivyo.

    “Sio hivyo tu, Fedha hizi za Benki ya Duniazinalenga kuwafadhili wanawake kwenyeshughuli za uchimbaji mdogo wa madini,ukataji na uchongaji wa madini ya vito ili idadiya wanawake wanaojishughulisha na Sekta yaMadini iongezeke,” alisema Profesa Muhongo.

    Aidha, Profesa Muhongo alitoa witokwa wataalam wote wanaosimamia miradiinayofadhiliwa na Benki ya Dunia katika Sektaya Madini kuhakikisha kuwa utekelezaji wamiradi hiyo uende kwa kasi ili kuleta matokeoyaliyotarajiwa.

    Benki ya Dunia kupitia Wizara ya Nishatina Madini imeendelea kutoa Ruzuku katika

    Uchimbaji madini mdogo ambapo katika mwakawa Fedha 2015/16 zilitengwa takribani Shilingi

     bilioni 7.2 ambazo zilitolewa kwa vikundi 111vya wachimbaji wadogo na watoa hudumambalimbali katika sekta ya uchimbaji madinimdogo.

    Vilevile, katika mwaka wa Fedha 2013/2014,Fedha za Ruzuku zilizotolewa kwa WachimbajiWadogo zilikuwa ni Dola za Marekani 500,000sawa na takribani Shilingi Bilioni 1 zilizotolewakwa waombaji 11. Fedha hizi ziliwalengawachimbaji madini wadogo pekee tofauti naawamu zilizofuata.

    Utoaji huo wa Ruzuku unaenda sambambana utoaji wa elimu na mafunzo kwa wachimbajiwadogo wa madini waliopata ruzuku husika ilikuhakikisha kuwa shughuli zilizopata ufadhilizinaleta tija.

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    3/15

    3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    FIVEPILLARS OFREFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI

    MSANIFU: Lucas Gordon

    WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, GreysonMwase, Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,

    Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

    INCREASE EFFICIENCY 

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OFTHE CLIENT

    SATISFACTION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OFSHAREHOLDERS

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Huduma ya SMS mkombozikwa Wachimbaji Madini

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Profesa Muhongo kuzurumikoa ya Mara, Geita

      Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikitoa taarifa zaleseni za utafutaji na uchimbaji madini kwa njia mbalimbali ikiwani pamoja na vyombo vya habari kama vile redio, televisheni,magazeti, tovuti yake na mitandao ya kijamii lengo likiwa nikuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwawanakuwa na taarifa sahihi zinazohusu masuala ya madini

    Kama njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa wachimbajimadini wanapata taarifa kwa urahisi zaidi, Wizara imeanzautaratibu wa utoaji taarifa za madini ambapo kuanzia sasawamiliki wa leseni hizo wanaweza kupata taarifa za ada za lesenikwa njia ya ujumbe wa simu (SMS).

    Akizungumzia huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo chaTEHAMA katika Wizara ya Nishati na Madini, FrancisFungameza alisema kuwa ili mteja aweze kupata huduma hiyoanatakiwa kuandika neno MEM, aache nafasi, kisha aandikeNamba ya Leseni na kutuma kwenda namba 15341.

    Baada ya hapo mteja ataweza kupata ada halisi ya leseni yakeinayostahili kulipwa kwa gharama ya shilingi 250. Tunaaminikuwa hizo ni habari njema kwa wamiliki wa leseni kwaniwataweza kupata taarifa hizo kwa muda mfupi na hivyo kulipiaada za leseni hizo kwa wakati.

    Mbali na huduma hiyo kwa njia ya SMS, Wizara imekuwaikitoa huduma za leseni kwa njia ya mfumo wa kielektronikiujulikanao kama Online Mining Cadastre Transactional Portal(OMCTP) ambao unawawezesha wateja kufanya masualambalimbali ikiwemo kufanya malipo ya leseni na mrabaha,wateja waliosajiliwa kutuma maombi ya leseni, kuhakiki taarifaza leseni wanazomiliki na kutuma taarifa za utendaji kazi .

    Mfumo wa OMCTP pia unawawezesha wateja kupata taarifambalimbali za Sekta ya Madini zikiwamo ramani za kijiolojia nataarifa za migodi mikubwa.

    Ikumbukwe kuwa, hapo awali mfumo wa utoaji leseniulifanyika kwa njia ya mkono (manually) na ulitegemeautumiaji wa karatasi (paperwork based) na hali hiyo ilichangiakuchelewesha utoaji leseni ambapo utoaji huo wa leseniulitegemea hali ya mawasiliano kama ya telegram na rejesta.

    Katika kipindi hicho, upimaji na uchoraji ramani za kijiolojiaulifanyika kwa njia ya mkono na ulitegemea umahiri wa mtu namara nyingine makosa yalifanyika na kusababisha migogoro auwaombaji kukosa leseni kwa sababu zisizo za msingi.

    Mfumo huo wa awali ulileta changamoto kwani Wizarailikuwa na wakati mgumu kuhakikisha kuwa kumbukumbuza leseni zinatunzwa vizuri bila kupotea, pia kulikuwa na kazingumu ya kuchambua nyaraka za leseni kwa njia ya mkono(manually) ili kufuatilia uhai wa leseni, malipo ya ada na utendajiwa wamiliki wa leseni.

     Mfumo huu ulipelekea leseni nyingi kutoweza kuchambuliwana kuathiri ubora wa utendaji wa Wizara na pia kasi yakuwahudumia wananchi ilikuwa ndogo.

    Mfumo wa kieletroniki unaotumika sasa katika leseniza madini unakuwa kama kituo kimoja (one-stop-centre)kinachotumiwa na wadau wa Sekta ya Madini walio nchini nanje ya nchi kuweza kujipatia huduma za leseni bila kulazimikakusafiri kwenda kwenye ofisi ya Madini, pindi wanapokuwawamesajiliwa ndani ya mfumo huo.

    Mfumo wa OMCTP una faida mbalimbali ikiwemo,kuongeza uwazi na kasi ya utoaji wa leseni za madini na Watejakuingiza maombi ya leseni wao wenyewe hivyo kupunguza tatizola mlundikano wa maombi kwenye ofisi za madini.

    Tunapongeza hatua kubwa iliyofikiwa na Idara ya Madinikwa kushirikiana na Kitengo cha TEHAMA katika kuhakikishakuwa wamiliki wote wa leseni za madini nchini wanapata taarifambalimbali za madini kwa urahisi na kwa wakati.

    Wito wetu kwa wachimbaji madini ni kuchangamkia

    huduma hii mpya ambayo ni rafiki kwani wataweza kupatataarifa za leseni za madini kwa muda mfupi na kulipia leseni zaokwa wakati.

    Leo tarehe 5 Mei, 2016, Waziriwa Nishati na Madini, ProfesaSospeter Muhongo anaanza safariya kikazi kuelekea katika mikoa yaMara na Geita.

    Akiwa mkoani Mara, atafanya shughulimbalimbali ambapo tarehe 6/5/2016atafanya mazungumzo na Uongozi waHalmashauri ya Musoma Vijijini na kutoamadawati 100 katika shule ya MsingiKisiwani iliyo katika kijiji cha Rukubawilayani Musoma Vijijini.

    Tarehe 7/5/2016, Profesa Muhongoatazindua Tovuti ya Jimbo la MusomaVijijini katika kijiji cha Saragana. Kazi hiiitafanyika Saa Tisa mchana.

    Akiwa mkoani Mara, atakutana naWawakilishi wa Wachimbaji Wadogo ilikujadili changamoto zao.

    Mnamo tarehe 9/5/2016 atakuwamkoani Geita, kwa ajili ya kujadilichangamoto za Wachimbaji Wadogo wamkoa huo.

    TAHARIRI

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    4/15

    4   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    AfDB yaipongeza Tanzania kwa

    mradi wa Bomba la MafutaNa Teresia Mhagama

    Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) imeipongeza Tanzania

     baada ya Uganda kuamuahivi karibuni kuwa Bomba laMafuta Ghafi lenye kipenyo

    cha inchi 24 kutoka Hoima nchiniUganda litapita katika ardhi ya Tanzaniahadi bandari ya Tanga.

     Pongezi hizo zilizotolewa naMwakilishi Mkazi wa Benki hiyo, ToniaKandiero wakati alipofika katika MakaoMakuu ya Wizara ya Nishati na Madini

     jijini Dar es Salaam na kuzungumzana uongozi wa Wizara ukiongozwa naWaziri wa Nishati na Madini, ProfesaSospeter Muhongo pamoja na watendajiwa Taasisi zilizo chini ya Wizara.

    “Tunawapongeza sana kwa kupatamradi huu muhimu kwa nchi yaTanzania, napenda kukutaarifu kuwaBenki ya Maendeleo ya Afrika ipo tayarikufanya kazi nanyi ili mradi huo uwezekutekelezeka kama ilivyopangwa,”alisema Kandiero.

    Akizungumzia utekelezaji wa bomba hilo la mafuta litakalokuwana urefu wa kilometa 1403, ProfesaSospeter Muhongo alisema kuwa, hatuainayofanyika sasa ni majadiliano yawataalam kutoka nchi hizo mbili juu ya

    mpango wa utekelezaji wa mradi huoikiwemo masuala ya fedha na watatoataarifa yao kwa viongozi wa juu wa nchihizo.

    Alisema kuwa pia kitajengwa

    kiwanda kwa ajili ya kusafisha mafutaghafi katika eneo la Hoima nchiniUganda ambapo mradi huo utagharimuDola za Marekani bilioni 4.7 na kila nchimwanachama wa Jumuiya ya AfrikaMashariki atakuwa na hisa ya asilimia8 na kuwajibika kuchangia Dola zaMarekani milioni 150.4 ili kutekelezamradi huo.

    “ Sisi kama nchi tunajipangakuchukua asilimia zote Nane (8) zahisa hizo na fedha ambazo tunapaswakutoa kwenye mradi huu zinawezakutoka Serikalini au Sekta Binafsi hivyo

    tunaweza kuja AfDB kuzungumzia sualahili,” alisema Profesa Muhongo.Aidha katika kikao hicho, AfDB

    iliipongeza TANESCO kwa kutekelezamikakati mbalimbali inayopelekea deni laShirika kupungua.

     Watendaji wa Benki hiyo yaMaendeleo ya Afrika pamoja Wizarapia walijadiliana masuala mbalimbaliyaliyolenga kuendeleza miradi yaNishati nchini pamoja na upunguzajiwa deni la TANESCO ili kuliwezeshaShirika hilo kufanya kazi zake kwaufanisi.

    Aidha Mwakilishi Mkazi wa Benkihiyo, alieleza kuwa AfDB inatoakipaumbele katika uendelezaji wamiradi ya Nishati ili kuliwezesha Bara

    la Afrika kuwa na nishati ya umeme yauhakika na kwamba wataendelea kutoaushirikiano kwa Wizara ya Nishati naMadini ili kuendeleza miradi ya Nishatipamoja na mafunzo.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia)akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB), Tonia Kandiero (kushoto) mara baada ya kumaliza kikao

    kilichofanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, jijini Dar es Salaam. Kikao kilijadili masuala mbalimbali ya uendelezajiwa Sekta ya Nishati nchini.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwana watendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) walioka katika

    Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini, jijini Dar es Salaam ilikujadili masuala mbalimbali ya uendelezaji wa Sekta ya Nishati nchini.Kutoka kushoto ni Prosper Charle, Chidozie Emenupa, Stella Mandagona Mwakilishi Mkazi wa AfDB, Tonia Kandiero.

    Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati naMaji (EWURA), Felix Ngamlagosi, Mkurugenzi wa Sheria, Wizara yaNishati na Madini, Justus Mulokozi na Mkurugenzi wa Ufundi kutokaWakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Bengiel Msofe, wakiwakatika kikao kati ya Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini naTaasisi zake na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (kushoto),Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikiaNishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa pili kushoto) na KamishnaMsaidizi wa Nishati anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, JamesAndilile,( wa Tatu kushoto) wakiwa katika kikao na Watendaji wa Benkya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ili kujadili uendelezaji wa Sekta yaNishati nchini.

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    5/15

    5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Greyson Mwase,Dar es Salaam

    U jenzi wa bomba la mafutakutoka Hoima nchiniUganda hadi katika

     bandari ya Tanga nchiniTanzania unatarajiwa

    kuanza hivi karibuni baada ya timu yawataalam kutoka nchi ya Tanzania naUganda kuanza kukutana jijini Dar esSalaam kwa ajili ya kupanga mikakatiya ujenzi wa bomba hilo.

    Akizungumza na waandishiwa habari hivi karibuni jijini Dar esSalaam mara baada ya kumalizikakwa mkutano wa kwanza kati yake naWaziri wa Nishati na Maendeleo yaMadini Nchini Uganda, MhandisiIrene Muloni aliyeambatana naujumbe wake katika mkutano huo,Waziri wa Nishati na Madini ProfesaSospeter Muhongo alisema kuwalengo la mkutano huo lilikuwa nikujadili mpango wa ujenzi wa bombala mafuta kutoka Hoima nchiniUganda hadi katika bandari ya Tanganchini Tanzania.

    Profesa Muhongo alifafanua kuwamkutano huo ulikutanisha wataalamkutoka nchi zote mbili, ambao ni waardhi, miundombinu, ujenzi, uchumi,

    maji, barabara pamoja na makampuniya mafuta.

    Profesa Muhongo alisema kuwamara baada ya Marais wa Tanzaniana Uganda kukubaliana kuanzakwa ujenzi wa bomba la mafuta,kinachofuatia ni utekelezaji wa kasiya ajabu ambapo tayari wameanzakukutana na kuunda kamati ndogondogo zitakazokuwa na wataalammbalimbali kwa ajili ya kuanza maramoja kwa utekelezaji wa mradi huo.

     Profesa Muhongo alisemakuwa Serikali za nchi zote mbilizimejipanga katika kuhakikisha kuwaujenzi huo unakwenda kwa kasikubwa, ikiwezekana ujenzi ukamilikemwishoni mwa mwaka 2019 badalaya mwaka 2020 kama ilivyopangwa.

    Aliongeza kuwa Serikali yaUganda inatarajia kujenga kiwandakwa ajili ya kusafisha mafuta ghafiHoima ambapo wametoa hisa 40zenye thamani ya Dola za Marekani

     bilioni 4.7 kwa nchi zilizomo ndaniya Jumuiya ya Afrika Masharikiambapo kila nchi itaweza kununuaasilimia nane ya hisa hizo na kusisitizakuwa Tanzania ipo tayari kununua

    hisa nane kwa thamani ya Dola zaMarekani milioni 150.4

    Aliendelea kusema kuwa hisazitanunuliwa na serikali pamoja nawawekezaji binafsi watakaoonesha niaya kununua hisa ili waweze kunufaikana mradi huo.

    Hata hivyo aliongeza kuwa nchiya Uganda pamoja na nchi nyinginezilizomo ndani ya Jumuiya ya AfrikaMashariki wameomba kununua gesikutoka nchini Tanzania na kusemakuwa kwa kuanzia serikali inatarajiakujenga bomba la gesi hadi nchiniUganda ili waweze kunufaika na gesihiyo.

    Alisema kuwa bomba la gesilitasambazwa katika mikoa yakaskazini na mingineyo ili uchumiwa nchi uweze kukua kwa kasi naTanzania kuwa nchi yenye kipato chakati ifikapo mwaka 2025 kama Diraya Maendeleo ya Taifa inavyofafanua.

    “ Kila sehemu yenye gesiya kutosha, lazima tuhakikishetunaweka bomba la gesi ambalo nimkombozi wa uchumi wa nchi,”

    alisisitiza Profesa Muhongo.Wakati huo huo Waziri wa Nishati

    na Maendeleo ya Madini NchiniUganda, Mhandisi Irene Muloni,aliishukuru serikali ya Tanzania kwakuwa tayari kushirikiana na Ugandakwa ajili ya mradi mkubwa wa ujenziwa bomba la mafuta.

    Alisema kupitia uzoefu waTanzania katika ujenzi wa mabombaya gesi na mafuta pamoja nawataalam waliobobea anaaminikuwa mradi huu utakwenda kwa kasikubwa na kukamilika kwa wakati.

    Aliiomba nchi ya Tanzaniapamoja na wadau mbalimbali ikiwani pamoja na makampuni ya mafuta,

     jamii itakayopitiwa na miundombinuya bomba la mafuta kutoa ushirikianoili mradi uweze kukamilika kwawakati kama ilivyopangwa.

    Alisema kuwa mkutano wa piliunatarajiwa kufanyika Hoima nchiniUganda tarehe 27 Mei, mwakahuu na kuendelea kufanyika katikamaeneo mbalimbali yatakayopitiwana bomba la mafuta.

    Ujenzi Bomba la Mafuta kuanza

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini NchiniUganda, Dk. Fred Kaliisa (kushoto) akifafanua jambo katika kikao hicho.Kulia ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda,Mhandisi Irene Muloni.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikiamadini Profesa James Mdoe (wa kwanza kushoto, waliokaa mbele);Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikianishati Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa pili kushoto waliokaambele) pamoja na wataalam wengine wa Wizara ya Nishati na Madiniwakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri waNishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi IreneMuloni (hayupo pichani) katika mkutano kati ya Tanzania na Ugandalengo likiwa ni kujadili mpango wa ujenzi wa bomba la mafuta kutokaHoima, Uganda hadi katika bandari ya Tanga nchini Tanzania.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi

    wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi katikabandari ya Tanga nchini Tanzania. Kulia ni Waziri wa Nishati naMaendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati)akielezea uzoefu wa Tanzania kwenye ujenzi wa miradi ya mabombaya gesi na mafuta katika mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishatina Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni nakulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa JustinNtalikwa.

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    6/15

    6   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Madini Kanda ya Ziwa Victoria

    Magharibi yakusanya bilioni 42.5

    Na Greyson Mwase,Morogoro

    Imeelezwa kuwa Serikalikupitia Wizara ya Nishati naMadini – Kanda ya Madiniya Ziwa Victoria Magharibiimekusanya jumla ya shilingi

    42,505,024,512.66 kati ya kipindi chamwezi Julai mwaka jana na Aprili29, mwaka huu.

    Hayo yalielezwa na KamishnaMsaidizi wa Madini Kanda ya ZiwaVictoria Magharibi Mhandisi DavidMulabwa, alipokuwa akizungumzakatika mkutano wa makamishnawa madini nchini na Katibu Mkuuwa Wizara ya Nishati na MadiniProf. Justin Ntalikwa na watendajiwa Wizara uliofanyika hivi karibunimjini Morogoro. Lengo la mkutanohuo lilikuwa ni kujadili mafanikio

    na changamoto mbalimbali katikasekta ya madini ikiwa ni pamoja na

    kuweka mikakati ya kukabiliana nachangamoto hizo.Mhandisi Mulabwa alisema

    kuwa kiasi hicho cha fedhakilitokana na tozo mbalimbalizilizolipwa kutokana na shughuli zamadini katika mikoa ya Mwanza,Geita na Kagera inayohudumiwa naofisi yake.

    Aliongeza kuwa, ofisi yakeimeweka mikakati madhubuti yaukusanyaji wa tozo na kuhakikishakuwa inavuka lengo la makusanyoili sekta ya madini iweze kuwa namchango katika ukuaji wa uchumiwa nchi.

    Alieleza mafanikio menginekatika kanda hiyo kuwa ni pamoja

    na uanzishaji wa mfumo wa hati zamauzo ya madini katika Wilaya za

    Bukoba na Kyerwa pamoja na eneomoja kuainishwa na kupendekezwakutengwa kwa wachimbaji wadogowilayani Kyerwa.

    Aliongeza kuwa mafanikiomengine ni pamoja na utoaji wamafunzo juu ya biashara ya madinina uchimbaji salama wilayaniKyerwa yaliyoshirikisha wachimbajipamoja na wafanyabiashara wamadini.

    “Elimu juu ya Sheria ya Madiniya mwaka 2010 na kanuni zakekwa Viongozi wa Wilaya tano(5),Halmashauri sita (6) na vitongojivyake ulifanyika katika mkoa

    wa Kagera,” alisema MhandisiMulabwa.

    Mhandisi Mulabwa aliendeleakutaja mafanikio mengine kuwa nipamoja na kaguzi kufanyika katikamaeneo ya leseni tatu za uchimbajimkubwa, leseni 18 za uchimbajiwa kati na leseni 586 za uchimbajimdogo, leseni za uchenjuaji 71,maghala ya baruti 21,stoo za baruti10 na leseni za utafutaji wa madini 8.

    Akielezea changamoto katikautekelezaji wa shughuli za madinikatika kanda hiyo MhandisiMulabwa alisema kuwa ni pamojana ofisi ya Mwanza kutokuwa na

     jengo lake na hivyo kupanga kwenye jengo la TBA wanaotoza bei kubwa

    kwa pango na soko la madini ya batikutokuwa na uhakika kwa kuwa

    Tanzania haijajiunga na mfumowa ununuzi wa madini ya bati kwanchi za Maziwa Makuu na hivyokusababisha wachimbaji kushindwakusafirisha bati nje ya nchi.

    Akielezea mikakati ya kuboreshashughuli za madini katika kandahiyo Mhandisi Mulabwa alielezakuwa ofisi ya kanda imewekamkakati wa kufanya kaguzi zamara kwa mara kwenye maeneoya uchimbaji na uzalishaji madini,kutoa hati za makosa kwa wakati nakufuta leseni zinazokiuka taratibukwa wakati.

    Alisisitiza kuwa ofisi itaendeleakushirikisha wadau wa sektambalimbali kukabiliana na tatizola uchafuzi wa mazingira pamojana kushirikiana na jeshi la polisi naviongozi katika serikali za mitaana vikundi vya wachimbaji kupigavita biashara haramu ya madini nakudhibiti uchimbaji bila kuwa naleseni.

    Aliongeza kuwa ofisi itaendeleakuelimisha wachimbaji wadogo wamadini juu ya wajibu wa kufanyashughuli za madini kwa tija na njiambalimbali wanazoweza kutumia ilikukuza mtaji kwa kazi zao pamojana muda mwafaka wa kuachanana shughuli za uchimbaji pale

    wanapoona shughuli za uchimbajihazina tija tena.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madinianayeshughulikia madini, Prof. James Mdoe (kulia) akibadilishanamawazo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof.

     Justin Ntalikwa (katikati). Kushoto ni Kamishna Msaidizi waMadini Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka

    Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria Magharibi,Mhandisi David Mulabwa akielezea mafanikio ya sekta ya madinikatika kanda yake.

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    7/15

    7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Greyson Mwase,Morogoro

    Wizara ya Nishati naMadini inatarajiakusambaza

    watumishi wa kadambalimbali kwenyeofisi zake za madini zenye upungufuwa wafanyakazi ili kuongeza kasi yautendaji katika sekta ya madini nakuwa na mchango katika ukuaji wauchumi wa nchi.

    Hayo yalielezwa na Mkurugenziwa Utawala na Usimamizi waRasilimali Watu kutoka Wizaraya Nishati na Madini, MrimiaMchomvu katika mkutanounaokutanisha makamishna wamadini nchini na Katibu Mkuuwa Wizara ya Nishati na MadiniProf. Justin Ntalikwa na watendajiwa Wizara unaoendelea mjiniMorogoro. Lengo la mkutano huo ni

    kujadili mafanikio na changamotombalimbali katika sekta ya madiniikiwa ni pamoja na kuweka mikakatiya kukabiliana na changamoto hizo.

    Alisema kuwa katika utekelezajiwake, ofisi yake itashirikiana naOfisi ya Kamishna wa Madiniili kubaini mahitaji ya ofisi zamadini za kanda kabla ya kuanzakwa mchakato wa kuhamishawataalam hao ili kuhakikisha kuwakila kituo kinakuwa na wataalamwanaohitajika kituoni

    Hata hivyo, Mrimia aliwatakawatumishi kujiendeleza kielimuna kuwa wabunifu ili kuwezakupandishwa vyeo muda unapofikia.

    “ Miundo ya maendeleo ya

    utumishi wa umma ina utaratibuwa kupandisha watumishi vyeokulingana na muda waliotumikiavyeo vyao pamoja na sifa za kielimuzinazohitajika,” alisisitiza Mchomvu.

    Aliendelea kusema kuwa kwawatumishi wanaopenda kuendeleana mafunzo wanatakiwa kuhakikishakuwa wanajiendeleza katika fanizilizomo ndani ya miundo husikana zitakazoboresha utendaji kazi.

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa(mbele) akifafanua jambo katika mkutano huo.

    Waliokaa mbele kutoka kushotoMeneja Mradi wa UsimamiziEndelevu wa Rasilimali za Madini(SMMRP) Mhandisi Idrissa Yahya;Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini Prof. JustinNtalikwa; Naibu Katibu Mkuuwa Wizara ya Nishati na Madinianayeshughulikia madini Prof.

     James Mdoe na Kaimu Kamishnawa Madini Nchini, Mhandisi AllySamaje wakiwa katika picha yapamoja na washiriki mara baadaya ufunguzi wa mkutano huo.

    Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu,Mrimia Mchomvu akisisitiza jambo katika mkutano huo.

    Waliokaa mbele kutoka kulia Mkurugenzi wa Idara ya Utawalana Usimamizi wa Rasilimali watu, Mrimia Mchomvu, Kamishna

    Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Magharibi, HumphreyMmbando, wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwazinawasilishwa katika mkutano huo.

    Wizara kugawa watumishi

    kwenye ofisi za madini

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    8/15

    8   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa(wa pili kutoka kulia) akisalimiana na Kamishna Msaidizi wa Madini

     – Maendeleo ya Uchimbaji Madini Mdogo, Julius Sarota (katikati)mara baada ya kufungua mkutano huo.

    Kaimu Kamishna wa MadiniNchini, Mhandisi Ally Samajeakisisitiza jambo katika mkutanohuo.

     Vituo vya mafunzo kwa wachimbaji wadogo kuanzishwa nchini

    Na Greyson Mwase,Morogoro

    Imeelezwa kuwa Wizara yaNishati na Madini kupitia Mradiwa Usimamizi Endelevu waRasilimali za Madini (SMMRP)inatarajia kuanzisha vituo vya

    mafunzo kwa ajili ya wachimbajiwadogo wa madini.

    Hayo yalisemwa na MenejaMradi wa Usimamizi Endelevu waRasilimali za Madini (SMMRP)Mhandisi Idrissa Yahya alipokuwaakizungumza katika mkutano wamakamishna wa madini nchini naKatibu Mkuu wa Wizara ya Nishatina Madini Prof. Justin Ntalikwa nawatendaji wa Wizara unaoendeleamjini Morogoro. Lengo la mkutano

    huo ni kujadili mafanikio nachangamoto mbalimbali katikasekta ya madini ikiwa ni pamoja na

    kuweka mikakati ya kukabiliana nachangamoto hizo.

    Alisema kuwa awali kabla

    ya mpango huo walibaini kuwawachimbaji wadogo wa madiniwalikuwa wanakabiliwa nachangamoto mbalimbali ikiwa nipamoja na teknolojia duni, ukosefuwa mafunzo ya nadharia na vitendo,ukosefu wa mitaji, masoko, nakutokukusanywa kwa maduhuli yakutosha.

    “ Wachimbaji wengi wamekuwawakichimba madini kwa kubahatisha

     bila ya kuwa na taarifa za kijiolojia,hivyo tunaamini kuwa vituovitakavyojengwa vitawapatia elimuya madini ikiwa ni pamoja na taarifaza kijiolojia ili uchimbaji wao uwe natija na endelevu,” alisema MhandisiYahya.

    Mhandisi Yahya aliendelea kusemakuwa lengo la ujenzi wa vituo hivi nikuwafundisha wachimbaji wadogo

    teknolojia ya kisasa ya uchimbajimadini kwa nadharia na vitendo,kupata uelewa wa taarifa za kijiolojia

    kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania(GST) na kuzalisha zaidi.

    Alifafanua kuwa tathmini yaawali ilifanywa na timu iliyoundwana wataalam kutoka Idara yaMadini, Shirika la Madini la Taifa(STAMICO), Wakala wa JiolojiaTanzania (GST) na Wakala waUkaguzi wa Madini Nchini (TMAA)

    Alisema kuwa mara baada yatathmini ya awali kufanyika, maeneoyaliyopendekezwa kwa ajili yaujenzi wa vituo hivyo yalikuwa nipamoja na Kyerwa mkoani Kagera,Kaparamsenga mkoani Katavi,Mbesa mkoani Ruvuma, Mishindomkoani Lindi, Katente mkoani Geita,Buhemba mkoani Mara na Itumbi

    mkoani Mbeya.Akifafanua vigezo vilivyotumika

    kupendekeza maeneo hayo Mhandisi

    Yahya alitaja kuwa ni pamoja nauwepo wa kutosha wa wachimbaji,athari za mazingira na maeneo rafikikwa mradi kama vile umeme, maji, namiundombinu.

    Vingezo vingine ni pamoja namaeneo hayo kuwa na uchimbajiwa muda mrefu, na kupata faidaendelevu.

    Akielezea matokeo ya vituohivyo kwenye uchimbaji madini,Mhandisi Yahya alisema kuwa elimuitakayotolewa kwa wachimbajimadini itawawezesha kuchimba kwakufuata sheria na kanuni za uchimbajiwa madini ikiwa ni pamoja nautunzaji wa mazingira.

    Alieleza matokeo mengine kuwa nipamoja na kuongezeka kwa maduhuli

    yatakayotokana na wachimbajiwadogo kuzalisha zaidi kwa kufuatateknolojia mpya.

    Asa kutoka Mradi wa UsimamiziEndelevu wa Rasilimali za Madini(SMMRP) Veronica Nangaleakichangia mada katika mkutanohuo.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikiamadini, Prof. James Mdoe (kushoto), akielezea mikakati ya Serikali katikakukuza sekta ya madini katika mkutano huo. Kulia ni Katibu Mkuu waWizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa.

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwaakifungua mkutano huo. Wengine waliokaa kutoka kushoto ni KaimuKamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Ally Samaje, Naibu KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini Prof.

     James Mdoe. Kulia ni Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu waRasilimali za Madini (SMMRP) Mhandisi Idrissa Yahya.

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    9/15

    9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikiamasuala ya nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (pichani) akisisitizajambo katika kikao hicho.

    Wataalam kutoka Idara ya Nishati kutoka kushoto, Mussa Abbas naAthur Lyatuu wakinukuu hoja mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa katikakikao hicho.

    Wataalam kutoka Idara yaNishati iliyopo chini ya Wizaraya Nishati na Madini wakifuatiliakwa makini mada mbalimbalizilizokuwa zinawasilishwa katikakikao hicho

    DK. MHANDISI JULIANA PALLANGYO AKUTANA NA WATENDAJI WA TPDC KUJADILI MATUMIZI YA GESI ASILIA 

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk. James Mataragio(mbele) akielezea mikakati ya shirika hilo juu ya matumizi ya gesi asilia inayozalishwa kwa ajili yamatumizi ya majumbani na nyingine kuuzwa katika soko la nje. Kikao hicho kilichowakutanishaNaibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dk.Mhandisi Juliana Pallangyo na watendaji wa TPDC kilifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

    Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili matumizi ya gesi iliyogunduliwa nchini katika matumizi yandani na nyingine kuuzwa nje ya nchi.

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    10/15

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    11/15

    11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na. Samwel Mtuwa –GST

    Waziri wa Nishati naMadini, Profesa

    Sospeter Muhongoamemteua ProfesaShukrani Manya kuwa

    Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakalawa JiolojiaTanzania (GST).

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewana Bodi hiyo hivi karibuni, Prof. Manyaanachukua nafasi iliyoachwa wazina Profesa Justin Ntalikwa ambayealiteuliwa na Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Dkt. JohnPombe Magufuli kuwa Katibu Mkuuwa Wizara ya Nishati na Madini.

     Imeelezwa kuwa, kwa sasa Prof.Manya ni Mkurugenzi anayesimamiaMasuala ya Utafiti na Machapishokatika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).

    Profesa Manya pia amewahikushika nyadhifa mbalimbali katikaChuo hicho ikiwemo Ukuu wa Idara yaJiolojia katika Chuo Kikuu cha Dar essalaam (UDSM) kuanzia mwaka 2012Hadi 2015.

    Aidha, taarifa hiyo ilieleza kwamba,Mwaka 2005 mpaka 2009, Profesa

    Manya alikuwa Mhadhiri katika chuoKikuu cha Dar es Salaam, Idara yaJiolojia.

    Mwaka 2009-2014 alikuwaMhadhiri Mwandamizi katika Idara yaJiolojia chuo kikuu cha DSM.

    Vilevile Mwaka 2001 mpaka 2005Profesa Manya alikuwa Mhadhiri

    Msaidizi katika Idara hiyo.Sambamba na uteuzi huo Prof.Manya amekuwa Mjumbe katika Bodimbalimbali, ikiwamo Mjumbe katikaGeochemical Society tangu mwaka2008 , Mjumbe katika GeologicalSociety of Tanzania tangu 2012 ,Mjumbe katika bodi ya ushauri wa

    Madini ya Taifa (National Mining

    Advisory Board -2012).Mpaka sasa Profesa Manyaameandika machapisho ya utafitizaidi ya 25 katika taaluma ya Jiolojia,Jiokemia , na milipuko ya Volkano.

     Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi,Uteuzi huo umeanza rasmi mweziMachi 2016.

    BODI YA USHAURI YA GST YAPATA MWENYEKITI MPYA

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    12/15

    12   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    MATUKIO YA MEI MOSI PICHANI

    Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini Wakiimba wimbo wa ‘Mshikamanoni Umoja’ katika Sherehe hiyo ya Maadhimisho ya Wafanyakazi Duniani.

    Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani.

    Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (hayupo pichani) katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani.

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    13/15

    13BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Wafanyakazi wa Osi ya Madini Kanda ya Kati, wakiwa katika Uwanjawa mpira wa Namfua mkoani Singida katika maadhimisho ya Siku yaWafanyakazi Duniani yaliyofanyika tarehe 1 Mei, 2016.

    Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe akimpa

    mkono wa pongezi Tantao A. Tantao kwa kuchaguliwa kuwaMfanyakazi bora wa Osi ya Madini, Kanda ya Kati Singida.

    PICHA Na. 1-3 ni Watumishi wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)wakiwa katika maandamano kuelekea katika Uwanja wa Jamhuri mjini

    Dodoma katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani kwamwaka 2016. Maadhimisho hayo yalifanyika kitaifa mkoani Dodoma

    MATUKIO YA MEI MOSI PICHANI

    2

    3

    SINGIDA - KANDA YA KATI GST1

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    14/15

    14   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Watumishi wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI) wakiwa katikamaandamano ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi duniani kwamwaka 2016 iliyofanyika tarehe 1, Mei. Maandamano yalianzia

    Viwanja vya Bunge kuelekea katika Uwanja wa Jamhuri mjiniDodoma.

    MATUKIO YA MEI MOSI PICHANI

    Wataalam kutoka Chuo cha Madini Dodoma (MRI), wakiwa katikamaadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani kwa mwaka 2016iliyofanyika tarehe 1, Mei. Maadhimisho hayo yalifanyika kitaifamkoani Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri. Kushoto ni EmmanuelGuffu, kulia ni Reuben Mdoe na aliyesimama ni Sunday Brown. Kifaakinachoonekana (chenye rangi ya njano) ni Theodolite ambacho

    hutumika katika upimaji wa ardhi (measuring angle in both verticaland horizontal planes).

    Mkufunzi kutoka Chuo cha Madini Dodoma (MRI), GeofreyAnyandwile akitoa maelezo kuhusu uchimbaji madini kwa njia ya wazi(open pit) katika miamba isiyokuwa imara katika maonesho hayo.

    CHUO CHA MADINI (MRI)

  • 8/17/2019 MEM 118 Online

    15/15

    15BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati - Petroli, Erasto Simon (kulia)akisalimiana na Osa kutoka Ubalozi wa Uganda Nchini TanzaniaNyiransanziyera Fredah (kushoto) aliyewasili katika Uwanja waKimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kumpokea Waziri waNishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni.

    Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati - Petroli, Erasto Simon (kushoto)akibadilishana mawazo na Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, DorothyHyuha (kulia) mara baada ya Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini

    Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni, kuwasili katika Uwanja waKimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ujumbe wake.

    Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati - Petroli, Erasto Simon (kulia)akibadilishana mawazo na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masualaya ujenzi wa mabomba kutoka Uganda, Habumugisha Johnbosco(kushoto) aliyeambatana na ujumbe wa Waziri wa Nishati naMaendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni.

    Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati - Petroli, Erasto Simon (kulia)akizungumza na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini

    Uganda, Mhandisi Irene Muloni (kushoto) mara baada ya Waziri huyopamoja na ujumbe wake kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa waMwalimu Julius Nyerere.

     WAZIRI WA UGANDA ALIPOWASILI NCHINI

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Dk. Fred Kaliisa(kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, Dorothy Hyuha (kulia)

    mara baada ya Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni,kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere pamoja na ujumbe wake.