MEM 98 Online

download MEM 98 Online

of 6

Transcript of MEM 98 Online

  • 8/20/2019 MEM 98 Online

    1/11

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali

    kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizar a ya Nishati na MadiniWasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263

    au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    HABARI ZA

    NISHATI &MADINI

    Toleo No. 98 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Desemba 18 - 24, 2015Bulletinews

     

    http://www.mem.go.tz

     

    n  TANESCO nayokufumuliwa

    n  Ni kwa kushindwakupata ufumbuzitatizo la umeme

    Prof. Sospeter Muhongo

    Idara NishatiWizarani

    kufumuliwa

     

    S o m a hab ar i  U k . 9 

    Prof. Muhongo atema cheche

    TATIZO LA UMEME NCHINI

    Naibu WaziriDkt. Medard Kalemani

    Katibu MkuuEng. Omar Chambo

  • 8/20/2019 MEM 98 Online

    2/11

    2   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Teresia Mhagama

    Naibu Waziri wa Nishatina Madini, Dkt. MedardKalemani amelitakaShirika la Umemenchini (TANESCO)

    kukamilisha mradi wa uzalishajiumeme kwa kutumia gesi wa KinyereziI ifikapo Januari 2016 ili nchi iweze

    kuwa na umeme wa uhakika.Naibu Waziri alitoa maagizo hayowakati alipofanya ziara ya kutembeleamitambo hiyo katika eneo laKinyerezi jijini Dar es Salaam ambapoaliambatana na Katibu Mkuu Wizaraya Nishati na Madini, MhandisiOmar Chambo na watendaji wenginewa Wizara ya Nishati na Madini naTANESCO.

    Dkt. Kalemani alitoa agizo hilo baada ya watalaam wa TANESCOwanaosimamia mradi huo kumuelezakuwa kwa sasa kituo hicho kinazalishaumeme wa kiasi cha megawati 70 kati yamegawati 150 na kwamba megawati 80zilizobaki zipo katika hatua ya mwishoya utekelezaji ambapo zitakuwa tayari

    ifikapo mwezi Februari 2016.

    Kinyerezi I kukamilisha Megawati150 ifikapo Januari 2016

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia) akiwa katika eneo ambalolitajengwa mitambo mingine ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi (Kinyerezi II) Wengine katika pichani Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa pili kulia), Wa kwanza kuliani Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, Wa Pili kulia ni Kamishna Msaidizi wa Nishati – Maendeleo ya Nishati, James Andilile, Wa kwanza kushoto ni Shoji Watanabe, Mtendaji kutoka kampuni yaSumitomo ya nchini Japan itakayohusika na ujenzi wa mitambo ya kituo hicho.

    >>INAENDELEA UK. 4

     Idara Nishati Wizarani kufumuliwaMwandishi Wetu 

    Waziri wa Nishati naMadini Prof. Muhongoamemwagiza NaibuWaziri kushirikiana naKatibu Mkuu pamoja

    na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini kuifumua mara mojaIdara ya Nishati ya Wizara na kuisukaupya kutokana na kushindwa kupataufumbuzi wa kuwapatia Watanzaniaumeme wa kutosha, uhakika na wa beinafuu.

    Sambamba na agizo hilo amesemakwamba hataishia kuifumua Idara hiyoya Nishati pekee, bali atafanya mabadikomakubwa kwa kuwabadilisha Watendajiwa Shirika la Umeme Tanzania.

    (TANESCO)“Lazima tuwe na wataalam wa

    Nishati ambao ni ‘Innovative andProductive’ na si kuwa na watalaamuambao wanashindwa hata kupataufumbuzi wa kero na tatizo la umemeambalo miaka yote hakuna mabadiliko,”alisema Prof. Muhongo.

    Prof. Muhongo alitoa maagizohayo aliporipoti katika ofisi ya Wizaraya Nishati na Madini na kukutana naMenejimenti ya Wizara hiyo AlhamisiDesemba 17, 2015.

    Tangu alipoteuliwa na kuapishwaDesemba 12, 2015 alikuwa hajaripoti

    katika ofisi ya Wizara hiyo kutokana nakutoridhishwa na hali ya umeme nchinina hususan kukatika kwa umeme marakwa mara. Hivyo kujikuta akianza kazizake kwa kutembelea ofisi za TANESCOmara baada ya kuapishwa na hatimayekwenda kukagua mabwawa ya majiyanayotumika kuzalisha umeme.

    Waziri Muhongo alipomalizakukutana na Menejimti ya TANESCO,alitembelea mabwawa ili kujioneauwezo wa kuzalisha umeme .Mabwawa ni pamoja na Hale (21MW), New Pangani Falls (68MW), Nyumbaya Mungu (8MW), Mtera (80MW),Kidatu (204MW), Kihansi (180MW)ambapo alikuta hali mbaya ya uzalisha

    umeme kutokana na kutokuwa namaji. Mabwawa hayo yote kwa sasayanazalisha umeme MW 100 ambayoni asilimia 20 ya uzalishaji kwa sasa.

    Mara baada ya kurejea kutokakwenye mabwawa hayo Prof. Muhongondipo aliripoti ofisini kwa mara yakwanza tangu alipoapishwa nakukutana na Watendaji wa Wizara hukuakiwa amechukizwa na suala la tatizo laumeme wa uhakika jambo lililomfanyaashindwe kujizuia na kusema kwambaIdara ya Nishati ya Wizara imeshindwa

    kutekeleza majukumu yake ipasavyo.Alisema Idara hiyo lazima

    ifumuliwe na kusukwa upya kutokanana kushindwa kutoa ushauri mzurikwa Serikali pamoja na kuisimamiavizuri Shirika la TANESCO ili wawezekutatua kero ya kutokuwa na umemewa uhakika kwa Watanzania.

    “Mimi lazima niwe mkweli nawala sina ugomvi au kumchukia mtuyeyote nataka kusema kwamba Idaraya Nishati imetuangusha kwani miakanenda miaka rudi mambo ni yale yale nawatu ni wale wale ambao wameshindwakuleta mabadiliko katika sekta ya umemenchini,” alisema Prof. Muhongo.

    Alisema umefika wakati sasa kwaIdara hiyo kufanyiwa mabadilikokwa maslahi na manufaa ya umma ili

    watakaowekwa waweze kuendana nakasi iliyopo ya Serikali ya awamu ya tanoyenye kauli mbiu ya “Hapa Kasi tu”.

    Kwa upande mwingine alisemaIdara hiyo ambayo inaonekana kuwa nawataalam mbalimbali wamekuwa piawakiipotosha Serikali kwa kutoa ushauriusio na tija katika sekta ya umeme nchini.

    Prof. Muhongo alisema Idara hiyoimekuwa ikija na miradi lukuki lakinihaitekelezeki na matokeo yake sikuzinakwenda Watanzania hawaoni haliya umeme ikiwa imeboreshwa.

    Prof. Muhongo aliigeukiwa piaIdara ya Madini ambayo ameitaka

    kurekebisha mapungufu yote yaliyopokatika sekta hiyo ikiwamo suala la Wizina utoshwaji wa madini hususan yaTanzanite.

    “Imetosha sasa!!! sitakubali kusikiamadini ya Tanzanite yanatoroshwanchini huku taifa likikosa mapato yakutosha. Nasema hata madini ya almasinataka nayo yaangaliwe kwa umakinimkubwa,” alisema Prof Muhongo.

    Wakati huo huo Prof. Muhongoamepiga marufuku kwa watendaji wotewaandamizi wa Wizara na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Nishati na Madinihususan TANESCO hakuna kwendalikizo ya krismasi.

    Siku ya Jumamosi Desemba 19,2015 Prof. Muhongo atafanya mkutanona Menejimenti ya Wizara ya Nishatipamoja na Menejiment ya TANESCOwakiwamo Mameneja wa Kanda zaTANESCO nchini kujadili na kutafutamajawabu ya namna ya kupatikanakwa ufumbuzi wa tatizo la umemenchini. Katika kikao hicho Mhe. Waziriameagiza hakuna Mtendaji yeyotekutuma mwakilishi lazima ahudhurieyeye mwenyewe.

  • 8/20/2019 MEM 98 Online

    3/11

    3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    TahaririMEM

      Na Badra Masoud

    FIVEPILLARS OFREFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI

    MHARIRI MKUU: Badra MasoudMSANIFU: Lucas Gordon

    WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, GreysonMwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,

    Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

    INCREASE EFFICIENCY 

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OFTHE CLIENT

    SATISFACTION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OFSHAREHOLDERS

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Tuyafanyie kazi maagizo

     ya Prof. Muhongo

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Maombi ya siku za nyuma, uunganishajiUmeme na Luku ukomo Januari 15.

    Desemba 12, 2015 mara baada ya kuapishwa Wazirialiyepangiwa kusimamia Sekta ya Nishati na Madini Mhe. Prof.Sospeter Muhongo na Naibu wake Dk. Medard Kalemani basihawakusubiri hata dakika ipite, moja kwa moja walianza kazikwa kuelekea ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)ili kuona kinachoendelea pamoja na kuangalia kulikoni katikashirika hili ambalo ndilo linawajilika moja kwa moja kuwapatiaWatanzania umeme lakini kwa muda mrefu sasa kumekuwapona malalamiko ya kutokuwa na umeme wa uhakika.

    Mara baada ya kuwasili katika Shirika hilo, watendajiwaliokuwapo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa

    TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba walikutana naWaziri na Naibu wake ambapo pamoja na mambo mengineProf. Muhongo alitaka kujua sababu za kukatika kwa umememara kwa mara.

    Hata hivyo, majibu ambayo aliyopewa kwamba kuna baadhi ya changamoto zinalikabili shirika hilo ikiwamo sualala uchakavu wa miundo mbinu, kupungua kwa kiasi kikubwakwa maji katika mabwawa yanayotumika kuzalisha umemelakini bado majibu hayo hayakumridhisha Waziri Muhongona kuamua yeye mwenyewe kuanza safari ya kutembeleamabwawa yote yanayotumika kuzalisha umeme ikiwamoHale, New Pangani, Nyumba ya Mungu, Kihansi, Kidatu naMtera.

    Baada ya kurejea kutoka katika mabwawa hayo Prof.Muhongo ndipo aliporipoti ofisini kwake rasmi na kukabidhiwaofisi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo ambaye kwa sasa niWaziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachaweneambapo mara baada ya kukabidhiwa ofisi aliagiza kukutana

    na Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Madini ili kuwaelezayaliyo moyoni mwake katika suala zima la upatikanaji waumeme nchini.

    Prof. Muhongo alifunguka bila kuuma maneno kwambainaonekana Idara ya Nishati ya Wizara imeshindwa kuwapatiaufumbuzi wa tatizo la umeme Watanzania na kuagizakupangwa upya kwa idara hiyo.

    Hata hivyo, Prof. Muhongo hakuishia katika Idara yaNishati pekee bali aligusa Idara karibu zote za Wizara ya Nishatina Madini ikiwamo Idara ya Madini hasa katika suala zima lautoroshwaji wa Madini ya Tanzanite jambo ambalo hata RaisJohn Magufuli aliligusia na kuonekana kumkera kwamba iwejeTanzania ndiyo nchi pekee inayochimba madini hayo duniani,lakini wanaofaidika na madini hayo ni nchi nyingine akitoleamfano Kenya na India ambazo hazichimbi Tanzanite.

    Halikadhalika Prof. Muhongo aliitaka Idara hiyo piakuangalia upya suala zima la madini ya almasi ambayo ndiyomadini yenye thamani duniani ili kuhakikisha taifa linapata

    mapato ipasavyo.Pamoja na mambo mengine Waziri Muhongo aliwataka

    watendaji wote wa Wizara kujipima upya utendaji, kamawanaoweza kuendana na kasi hii ya Serikali ya Awamu yaTano ya Rais John Magufuli hususan katika kufikia malengona matarajio waliyonayo Watanzania kwa Serikali yao.

    Prof. Muhongo aliongeza kusema kwamba hatamvumiliamtumishi yeyote mzembe, mla rushwa na ambaye hatajalimaslahi ya umma na taifa kwa ujumla.

    Tunasema kwamba tumeyapokea maagizo na maelekezo yaWaziri wetu ambayo kwa hakika tunayaheshimu na tunaahidikwa pamoja kuyafanyia kazi kwa vitendo kwa maslahi ya taifaletu

    Halikadhalika tunaahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwaProf. Muhongo, Naibu Waziri Dk. Medard Kalemani, KatibuMkuu Eng. Omar Chambo na Naibu Katibu Mkuu Eng. PaulMasanja kwamba tutafanya kazi kwa mshikamano kama timumoja katika kuhakikisha tunatatua kero za watanzania ikiwamo

    ya umeme.Mungu Ibariki Wizara ya Nishati na Madini!!!Mungu Ibariki Tanzania!!

    Na Mohamed Saif 

    Mameneja wa Kanda waShirika la Umeme Nchini(TANESCO) wametakiwakuhakikisha kuwa ifikapotarehe 15 Januari mwakani

    kazi ya kuwaunganishia Umeme na Lukuwaombaji wa muda mrefu iwe imekamilika.

    Agizo hilo limetolewa na Waziri waNishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongokwenye Kituo cha kuzalisha umeme chaKihansi mkoani Iringa wakati alipokutana naMameneja wote wa Kanda wa Shirika hilo.

    Alionya kuwa Meneja yoyoteatakaeshindwa kutimiza agizo hilo awe tayarikuacha ama kuachishwa kazi.

    “Ikitokea Watanzania wakalalamikakucheleweshewa huduma kufikia tarehe15 mwezi ujao, muwe tayari kuacha kazi,”alisisitiza.

    Profesa Muhongo alisema Watanzaniawamechoshwa na utendaji duni wa Tanescona kuagiza wahakikishe wanabadilika kwakuwatumikia vyema wananchi.

    Alisema kumekuwepo na malalamikomengi kutoka kwa wananchi huku kubwazaidi ikiwa ni kukatika kwa umeme marakwa mara na kucheleweshewa huduma yakuunganishiwa umeme na Luku.

    Alisema kwa sasa anazungukia mitamboyote ya uzalishaji umeme nchini kufanyatathmini ili kuelewa hali halisi ya umeme na

    kuwataka kukomesha mara moja hali yaukatikaji wa umeme mara kwa mara ambayoimekuwa kero kubwa kwa wananchi.

    Vilevile Profesa Muhongo aliwaelezaMameneja hao kuwa ifikapo siku yaJumamosi ya tarehe 19 mwezi huu wawe namajibu ya kero mbalimbali za umeme nchini.

    Alisema siku hiyo atakutana na Mamenejahao pamoja na watendaji wa taasisimbalimbali zinazojishughulisha na masualaya nishati nchini.

    “Nimewaeleza hawa Mameneja kuwasiku ya jumamosi nitakuwa na kikao naopamoja na watendaji wengine. Nataka wajena majibu ya kisayansi,” alisema ProfesaMuhongo.

    Jambo jingine ambalo Waziri huyoanataka kutoka kwa Mameneja hao nimkakati waliouandaa kuhakikisha bei yaumeme nchini inashuka.

    “Watanzania wanauliza vipi tutafaidika

    na gesi yetu? Nataka mje na mkakatiwa kupunguza bei ya umeme,” alisemaMuhongo.

    Aidha, alizungumzia suala la kuongezamakusanyo ya mapato ya huduma ya umemeambapo aliwaagiza Mameneja hao kuongezamara mbili ya malengo ya ukusanyaji mapatowaliyokuwa wamewekewa hapo awali.

    Waziri Muhongo tayariamekwishatembelea vituo vya kuzalishaumeme vya Hale, Pangani, Nyumba yaMungu, Mtera, Kihansi na Kidatu.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumzana Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Kihansi mkoani Morogorowakati alipotembelea kituo hicho.

  • 8/20/2019 MEM 98 Online

    4/11

    4   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Dkt. Kalemani akutana nawatendaji wa Wizara, TaasisiTeresia Mhagama na

     Asteria Muhozya

    Naibu Waziri wa Nishatina Madini, Dkt. MedardKalemani amekutanana watendaji wa Wizaraya Nishati na Madini na

    Taasisi zake na kutoa maagizo ambayowatendaji hao wanapaswa kuyatimizaili kuleta ufanisi katika Sekta za Nishatina Madini.

    Upatikanaji wa Umeme -Naibu Waziri aliwataka watendajiwanaohusika na sekta ya umemewahakikishe kuwa wananchiwanapata umeme wa uhakika hivyo

    wahakikishe nishati hiyo inapatikanakwa kutumia vyanzo mbalimbaliikiwemo gesi, jua, upepo, joto ardhi,makaa ya mawe na vyanzo vinginevya nishati vinavyopatikana nchini.

    Usambazaji Umeme - alielezakuwa, usambazaji wa umeme mijinina vijijini ufanyike kwa ufanisi nakwamba mtu yeyote atakayezembeakwa sababu zisizo za msingiatachukuliwa hatua. “Kama vitendeakazi vya usambazaji umeme vipomfano nguzo na mita halafu mtuakazembea, hilo suala halitakubalika,”alisema Kalemani.

    Ukatikaji wa Umeme -  Dkt.Kalemani alitoa maelekezo kuwakama kuna mitambo mibovu

    ya uzalishaji umeme, ifanyiwematengenezo ili kusiwe na sababuzozote za wananchi kupata mgawowa umeme, alisisitiza kuwa mgawohaukubaliki.

    Uunganishaji umeme kuchukuamuda mrefu - Naibu Waziri alisemakuwa kumekuwa na tabia kwa baadhiya watendaji wa Tanesco kuchukuamuda mrefu katika kuwaunganishiawananchi umeme ilhali vifaa vyakuunganisha umeme vipo. Alisisitizawatumishi wenye tabia hiyohawatavumiliwa.

    Wizi wa umeme - Hapa aliagizawatendaji wa Shirika la Umeme nchini(TANESCO) wamkabidhi ripoti yatakwimu za wizi wa umeme na hatua

    zilizochukuliwa na Shirika hilo dhidiya watu waliobainika kuiba umeme.“Tunabebesha mzigo wananchiwengine wakati wengine wanaiba,wezi wa umeme ni lazima tuwabainina tuwatumbue majipu,” alisisitizaDkt. Kalemani.

    Semina - Naibu Waziri aliwatakawatendaji hao kupunguza uhudhuriajiwa semina na badala yake wajikite zaidikatika kuhakikisha kuwa kunakuwana kasi kubwa ya usambazaji umemenchini.

    Mchango wa madini katika Patola Taifa - Naibu Waziri alieleza kuwa

     bado mchango wa Sekta ya Madinikatika Pato la Taifa hauridhishi hivyoaliwataka watendaji wanaosimamia

    Sekta hiyo kuhakikisha kwambawanakuwa wabunifu kubaini vyanzovya mapato katika sekta hiyo ili

    mchango wa sekta hiyo uongezeke.Wachimbaji wadogo -  Naibu

    Waziri alieleza kuwa wachimbajiwadogo waendelee kutengewa maeneoya uchimbaji madini na kuelezakuwa hii itasaidia pia ukusanyaji wakodi mbalimbali kwani wachimbajihao watakuwa wakipatikana katikamaeneo yanayotambulika na Serikali.

    Ukaguzi wa madini -  Dkt.Kalemani aliutaka Wakala waUkaguzi wa Madini (TMAA)kuhakikisha kuwa wanafanya ukaguzimakini wa shughuli za uzalishajikwenye migodi mikubwa na biasharaya madini ili Serikali ipate mapatostahiki kutoka katika rasimali hiyo,“Suala la watu kuleta udanganyifukatika kile kinachozalishwa lisiwepo,ni lazima muongeze jitihada katikaukaguzi,” alisisitiza Dkt. Kalemani.

    Aidha Naibu Waziri aliwatakawatumishi wa Wizara na Taasisi zakekufanya kazi kwa kufuata maadili,kubana matumizi yasiyo ya lazima(magari, samani) bila kuathiri utendajikazi, kutochelewesha mikatabambalimbali na kila mtumishianapaswa kwenda na kasi iliyopo yautendaji kazi.

    Kwa upande wake, Naibu KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati naMadini, Mhandisi Paul Masanjaaliahidi kusimamia utekelezaji wamaagizo hayo na kueleza kuwa,yatasaidia kuongeza kasi ya utendajikazi .

    Pia, Mhandisi Masanja alimuombaDkt. Kalemani kusaidia kuharakishauteuzi wa Wajumbe wa Bodi zataasisi mbalimbali zilizo chini yaWizara ambazo zitasaidia kuongezakasi ya utendaji. Aidha, alimuombakuwezesha Shirika la UmemeTanzania (TANESCO) kulipwamadeni yake kutoka taasisi mbalimbaliza Serikali zinazodaiwa na shirika hilo.

    Baadhi ya taasisi za Wizarazilizohudhuria mkutano huo niTANESCO, Wakala wa NishatiVijijini (REA), Wakala wa Ukaguzi waMadini Tanzania (TMAA), Shirikala Madini la Taifa (STAMICO),Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma zaMaji na Nishati (EWURA), Shirikala Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) na Mpango wa UhamasishajiUwazi katika Tasnia ya uziduaji(TEITI).

    Dkt. Medard Kalemani

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini , Dkt. Medard Kalemani (katikati)akiongoza kikao chake na Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Madini,Wakuu wa Taasisi za REA, TPDC, EWURA, STAMICO, , TANESCO,

    TMAA NA TEITI. Katika kikao hicho Naibu Waziri Dkt. Kalemaniamewataka Watendaji wa Wizara na Taasisi kutatua kero za wananchikwa kasi na asiyejipanga ajiondoe mwenyewe.

    Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje (wa kwanza kulia)akizingumza wakati wa kikao na Naibu Waziri wa Nishati na Madini ,Dkt. Medard Kalemani (katikati) na Menejimenti ya Wizara ya Nishatina Madini, Wakuu wa Taasisi za REA, TPDC, EWURA, STAMICO, ,TANESCO ,TMAA na TEITI. Katika kikao hicho Naibu Waziri Dkt.

    Kalemani amewataka Watendaji wa Wizara na Taasisi kutatua kero zawananchi kwa kasi na asiyejipanga ajiondoe mwenyewe.

    “Kwa sasa tunazalisha megawati70 kati ya 150, hizi hazitoshi, tujitahidikuzalisha zaidi ya hizi kabla ya mweziFebruari, kwani wananchi wamechokana hili suala la ukatikaji wa umemewa mara kwa mara, mmesema gesiipo ya kutosha hivyo lazima mitamboizalishe umeme kama inavyotakiwa,”alisema Kalemani.

    Awali Katibu Mkuu Wizara yaNishati na Madini, Mhandisi OmarChambo alimweleza Naibu Wazirikuwa mitambo miwili kati ya minnendiyo inayofanya kazi katika eneo hilola Kinyerezi I na kuzalisha megawati70 zinazoingizwa katika gridi ya Taifa.

    Alieleza kuwa kwa sasa serikali

    imeamua kujenga mitambo mingineya kuzalisha umeme katika eneohilo (Kinyerezi I extension) ambayoitakuwa na uwezo wa kuzalishamegawati 185 ili nchi iweze kuwa naumeme wa uhakika unaotokana nanishati ya gesi asilia.

    Aidha kazi ya ujenzi wa mitambohiyo ya megawati 185 inatarajiwakuanza mwanzoni mwa mwaka2016.

    Naibu Waziri wa Nishatina Madini pia alitembelea eneoitapojengwa mitambo ya umeme wagesi (Kinyerezi II) ambayo itazalishaumeme wa kiasi cha megawati 240

     baada ya kukamilika kwake ambapomradi huo utagharimu Dola za

    Marekani milioni 344 na serikaliitachangia Dola milioni 52 ya gharamahizo.

    Akiwa katika eneo hilo, Dkt.Kalemani aliiagiza Tanesco kuhakishakuwa eneo hilo ambalo mitambohiyo itajengwa liendelee kuwa ndaniya uzio ili lisiingiliane na shughulinyingine za wananchi na kuletamigogoro isiyokuwa na tija.

    Ili mradi huo ukamilike kwa harakana kuweza kuzalisha umeme, NaibuWaziri alieleza Wizara ya Nishati naMadini na Tanesco inafuatilia kwakaribu upatikanaji wa Fedha kutokaWizara ya Fedha ili zitolewe ndani yawakati na mradi uanze mara moja.Mpaka sasa Serikali imetoa Dola

    za Marekani milioni 13.7 ya fedhaambazo serikali inapaswa kuzitoakatika mradi wa Kinyerezi II.

    Kinyerezi I kukamilishaMegawati 150 ifikapo

     Januari 2016

    >>INATOKA UK. 2

  • 8/20/2019 MEM 98 Online

    5/11

    5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Mohamed Saif, Mtera

    Waziri wa Nishati naMadini, ProfesaSospeter Muhongoamewaagiza wataalamkutoka Wizara ya

    Nishati na Madini, Wizara ya Majia Umwagiliaji, Kituo cha Kuzalisha

    Umeme cha Mtera na wataalamu kutokaBodi ya Maji- Bonde la Rufiji kukutanai kujadili namna bora ya matumizindelevu ya maji yanayoelekea katika

    Bwawa la Uzalishaji Umeme la Mtera.

    Profesa Muhongo aliyasema hayo baada ya kukagua Bwawa hilo lililopompakani mwa mikoa ya Iringa naDodoma ambalo kwa sasa limesitishauzalishaji wa umeme kutokana kina chamaji katika bwawa hilo kupungua kwakiwango kisichoruhusu uzalishaji waumeme kuendelea.

    Profesa Muhongo alisema kuwakwa wakati huu kituo hicho chaMtera kinachozalisha megawati 80kimesimamisha uzalishaji akitajasababu kuwa ni upungufu wa majiuliosababishwa na matumizi mabaya ya

    maji yanayoelekea katika Bwawa hilokutoka mto Ruaha mkubwa, Mto RuahaMdogo na mto Kisigo.

    Alisema kuwa utatuzi wa upungufuwa maji kwenye Bwawa hilo unawezakutatuliwa kwa watalamu kukutana nakujadili namna bora ya matumizi yamaji.

    Mbali na hilo, Profesa Muhongoalitaja utatuzi mwingine kuwa nikuongeza vyanzo vingine vya kuzalishaumeme mbali na kutegemea maji ili

    kuruhusu mabwawa hayo kufikia kinakinachohitajika.“Tumeita ndugu zetu wa Bodi

    ya Bonde la Rufiji ili tusaidiane naokutekeleza suala hili kwa sababu hayamaji tunayayoyatumia kuzalishaumeme, wakulima na wafugaji naopia wanayatumia na lengo letu ni kilammoja afaidike nayo,” alisema Profesa

    Muhongo.Profesa Muhongo pia aliiagiza Bodi ya

    Maji - Bonde la Rufiji kumpatia takwimuza matumizi ya maji kwa wakulima waliona vibali vya kutumia maji ya bwawa hiloili kuelewa ni wakulima wangapi waliona vibali vilevile kuelewa kiasi cha majiwalichoruhusiwa kutumia.

    “Nimewaagiza hawa ndugu zetu waBonde la Rufiji waniletee takwimu leohii, Tanesco wanatumia mita 94 kwasekunde ili wazalishe umeme lakini jewakulima nao waliopewa vibali vyakutumia maji je wameruhusiwa kutumiakiasi gani?” alihoji Muhongo.

    Profesa Muhongo alisema ameamuakutembelea vyanzo vyote vya uzalishajiwa nishati ya umeme ili atakapokutanana wataalamu wa Idara ya Nishati naTanesco suluhisho la kudumu la matatizoya umeme nchini lipatikane.

    “Hatuwezi tukakaa na kutafutasuluhisho bila kujionea hali halisi. Ndiyomaana tumeamua kutembelea mitamboyote inayofua umeme,” alisema ProfesaMuhongo.

    Profesa Muhongo anaendelea naziara yake ya kukagua vyanzo vya nishatiya umeme na anatarajiwa kukutanana wakulima wanaotumia bwawahilo la Mtera na baadaye atakutana nawataalamu wa Idara ya Nishati pamojana Tanesco ili kujadili hatua za kuchukuaili kuwe na matumizi endelevu ya maji.

    Profesa Muhongo aagiza

    Wataalam kujadili matumiziendelevu ya Maji Mtera.

    Muonekano wa Bwawa

    la Mtera kwa hivi sasaikionesha kupungua kwa kiasikikubwa kwa kina cha maji.

    Waziri wa Nishati na Madini, ProfesaSospeter Muhongo (katikati)akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji waShirika la Umeme Nchini (Tanesco),Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia)wakati alipotembelea Bwawa laUzalishaji Umeme la Mtera. Kushotoni Meneja wa Kituo cha KuzalishaUmeme cha Mtera, MhandisiAbdallah Ikwase.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)kimsikiliza mtaalamu kutoka Bodi ya Maji- Bonde la Ruji, David Muginyakulia) akielezea kuhusu mikakati ya matumizi bora ya maji yanayoelekeaatika Bwawa la Uzalishaji Umeme la Mtera.

  • 8/20/2019 MEM 98 Online

    6/11

    6   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Mohamed Seif 

    Serikali imeagiza matoleo yamaji ya kumwagilia mashambayanayotumia maji ya mitoinayotiririsha kwenye mabwawaya kuzalisha umeme ya Mtera na

    Kidatu yafungwe.

    Agizo hilo limetolewa leo na Waziriwa Nishati na Madini, Profesa SospeterMuhongo alipotembelea Bwawa la Kidatuna kujionea namna ambavyo kina chamaji kwenye bwawa hilo kilivyopungua.

    Waziri Muhongo alisema tatizokubwa la uzalishaji mdogo wa umeme wamaji nchini ni umwagiliaji usio zingatiataratibu za matumizi sahihi ya maji.

    Alisema mfumo wa umwagiliajiunaotumika ni wa kienyeji sio wakitaalamu. “Nimeshuhudia mtu anazuiamaji kutiririka kwa kutumia mawe,magogo ama viroba vya mchanga; hii siosahihi,” alisema.

    Akizungumzia umeme unaozalishwakwa nguvu ya maji, Waziri Muhongoalisema kwa hivi sasa ni asilimia ishirini

    Waziri wa Nishatina Madini, ProfesaSospeter Muhongo(kushoto)akizungumza

     jambo wakati waziara yake kwenyekituo cha kuzalishaumeme cha Kidatu.Katikati ni Menejawa Kituo hicho chaKidatu, Mhandisi

     Justus Mtolera naanayemfuatia niMeneja wa Kituocha kuzalisha

    umeme cha Mtera,Mhandisi AbdallahIkwasa. Bwawa la maji la kuendeshea mitambo ya kuzalisha umeme la

    Kidatu likionekana katika hali ya kupungukiwa na maji

    tu inayozalishwa kutoka kwenyevyanzo vya maji nchini.

    Alisema jumla ya uwezo wa

    mitambo yote ya maji (installedcapacity) ni Megawati 561.84ambapo wastani wa uzalishaji kwasasa kutoka kwenye mitambo hiyoni Megawati 110 hiyo ni kuanziatarehe 13 hadi tarehe 16 mwezi huu.

    “Nimetembelea Nyumba yaMungu, Hale, Pangani, Mtera,Kihansi na Kidatu na kugunduakwamba tatizo sugu ni umwagiliajina siyo tabianchi,” alisema.

    Alisema mashamba yaumwagiliaji yanaongezeka MikoaniMbeya, Iringa na Morogoro.

    Aliongeza kuwa vibali vyaumwagiliaji vimetolewa kienyeji bilakutafakari athari itakayotokea.

    Profesa Muhongo alisema

    kipindi hiki ni cha mvua hivyowenye mashamba ya umwagiliajiwatumie maji ya mvua badala yakuendelea kutumia mito.

    Alisema wakati mazungumzoyanaendelea, Bodi ya Maji- Bondela Rufiji wahakikishe wanakaguamifereji yote ya umwagiliajiinayoingiza maji kwenye Mtowa Ruaha mkuu na kuifunga ilikuruhusu bwawa la Mtera kupatamaji.

    Alieleza kwamba kwa kufungamifereji hiyo ndani ya siku nnehadi tano maji yatakua yameingiakwenye bwawa la Mtera na hivyokuweza kuendesha mitambo.

    Awali akimueleza Waziri hali

    halisi ya uzalishaji umeme kwenyekituo hicho cha Kidatu, Menejawa Kituo, Mhandisi Justus Mtoleraalisema umeme unaozalishwakituoni hapo kwa sasa ni megawati50 wakati kituo hicho kinao uwezowa kuzalisha jumla ya megawati204.

    Mhandisi Justus alisema kituohicho kinayo mitambo minne yakuzalisha umeme lakini kutokanana tatizo la maji, mitambo miwili tuinafanya kazi ambapo kila mmojaunazalisha kiasi cha Megawati 25.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akimsikiliza Meneja wa Kituo cha KuzalishaUmeme cha Kidatu cha Mkoani Morogoro, Mhandisi Justus Mtolera wakati wa ziara yake kituoni hapo lengolikiwa ni kujionea uzalishaji umeme wa kituo hicho.

    Muhongo Aagiza kufungwa

    matoleo ya umwagiliaji

  • 8/20/2019 MEM 98 Online

    7/11

    7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Serikali kuanza kutumia Nguzo za ZegeRhoda James

    Wizara yaNishati naM a d i n ikupitia Shirikala Umeme

    Tanzania (Tanesco) iko mbionikuanza kutumia Nguzo zakusambazia Umeme za Zegeli kuondokana na nguzo zamiti ambazo zina changamotokadhaa ikiwa ni pamoja nakuvunjika, kuoza kwa kuliwana wadudu na kuanguka hivyokusababisha usumbufu kwawananchi kukosa hudumamuhimu ya umeme.

    Hayo yalielezwa na KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati

    na Madini, Mhandisi OmarChambo alipokutana naUjumbe kutoka UjerumaniOfisini kwake hivi karibuni jijiniDar es Salaam.

    Ujumbe huo uliongozwa naBalozi wa Ujerumani nchini,Egon Kochanke ulimtembeleaMhandisi Chambo kwa niaya kuwasilisha maombi yakuwekeza katika sekta ya nishatikupitia mradi wa kujenga nguzo

    za kusambazia umeme za zege.Akizungumza kwa niaba ya

    ujumbe huo Balozi Kochankealisema endapo maombi yaoyatakubaliwa, watatoa ajirakwa wazawa na kuwajengeauwezo ili waweze kuendelezamradi huo pindi watalaamuhao watakapomaliza mkatabana kurejea kwao.

    Katibu Mkuu Chamboalisema, “Ni vizuritukaondokana na teknolojia yazamani ya kutumia nguzo zakusambazia umeme za miti nakuhamia teknolojia ya kisasaya nguzo za zege ambayoinatumika nchi mbalimbalizikiwemo za Umoja wa Ulayana Mashariki ya Kati kama

    vile nchi ya Oman ambao kwasasa tayari wanatumia nguzo zazege.

    Aliongeza kuwa ni muhimukuzigatia taratibu za manunuziserikalini katika kuchaguaKampuni zenye sifa stahikizinazojumuisha wawekezajiWazawa na waotoka Njeya nchi kwa ajili ya kazi yakutengeneza nguzo hizo.

      Akizungumzia faida za

    kutumia nguzoza zege MhandisiChambo alisema,

    “Nguzo zinazojengwa kwa

    kutumia zege ni imara na uhaiwake ni zaidi ya miaka 100,ukilinganisha na nguzo za mitiambazo uhai wake hauzidimiaka 20 hali inayochangiamatumizi ya nguzo za mitikuwa na gharama kubwa.

    Kwa upande wake KaimuNaibu Mkurugenzi Mtendajiwa Usambazaji na Hudumakwa Wateja Kutoka Tanesco,Mhandisi Sophia Mgonjaalisema wakati mwingineTanesco hulazimika kukataumeme kwa lengo lakubadilisha nguzo ambazozinakuwa zimeoza na haliinayosababisha kukatika kwa

    umeme mara kwa mara hivyokuleta usumbufu kwa wananchina kuingia gharama kubwa.

    Aidha, Mgonja alisemakuwa Tanesco inategemeakuanza kutumia nguzo za zege

     baada ya kumaliza maandaliziyote muhimu na kwamba nimatumaini yake kuwa ifikapomwanzoni mwa mwaka 2016watakuwa wamefikia hatuanzuri.

    n Utoaji Tenda uzingatie sifa stahiki: Chambo

    Chambo ataka Mradi wa Lwamgasa uendeleeNa Nuru Mwasampeta,Dar es Salaam

    Katibu Mkuu wa Wizaraya Nishati na Madini,Mhandisi Omar Chambo,amewaagiza Watendaji katikaSekta ya Madini kuhakikishakuwa mradi wa KuwasaidiaWachimbaji Wadogo wamadini wa Lwamgasa uliopoMkoani Geita, unaendeleakufanyakazi baada yakusimama kwa takribanikipindi cha mwaka mmojatangu kuanzishwa kwake.

    Chambo alitoa agizohilo hivi karibuni wakati wakikao baina yake na watendajihao, kilichohudhuriwa piana Mwakilishi wa Benki yaDunia ambaye pia ni kiongoziwa Mradi wa UsimamiziEndelevu wa Rasilimali Madini(SMMRP) wa benki hiyoMamadou Barry.

    Katibu Mkuu pia alimtakaMeneja Mradi, wa SMMRP,Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Idrisa Yahyakuhakikisha anafuatilia hatuazote za utekelezaji wa mradihuo ambao unawawezeshawachimbaji wadogo kuchenjuadhahabu kisasa badala ya

    kutumia zebaki ambayo ilikuwaikisababisha wachimbaji haokupoteza dhahabu nyingi nakuathirika kiafya.

      “Mradi huu ni mkubwa

    na kufanikiwa kwake nikufanikiwa kwa watanzaniawenye maisha ya chini, lakinipia ni kufanikiwa kwa taifa kwasababu utawezesha kuongezapato la taifa,”alisema Chambo.

    Kwa upande wake,Mwakilishi wa Benki ya Duniana kiongozi wa mradi waSMMRP, Mamadou Barry,alieleza dhumuni la ujio wakeWizarani hapo kilikuwa nikupongeza uteuzi wa viongoziwa Wizara ya Nishati naMadini wakiwemo KatibuMkuu na Naibu KatibuMkuu kwa kuteuliwa kwao

    kuongoza wizara na kutakakuendeleza ushirikiano wakikazi ili kufanikisha utekelezajiwa miradi inayosimamiwa naBenki ya Dunia katika sekta yamadini.

    Aliongeza kuwa, sifa yaTanzania ni nzuri katikautekelezaji wa miradi yaBenki hiyo, jambo ambalo pialiliwezesha kupitishwa kwamradi wa Lwamgasa baada yakuridhishwa na mchanganuowa utekelezaji wake.

    Mamadou, aliishauri wizarakuhakikisha inasimamia nakuharakisha utekelezaji wa

    mradi huo ili kuweza kutimizamalengo ya mradi huo kamailivyokusudiwa kutokana naumuhimu wake.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi OmarChambo (mbele) na Ujumbe kutoka Ujerumani wakiongozwana Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke (watatu kulia)wakiwa osini kwa Katibu Mkuu jijini Dar es Salaam kuwasilishamaombi yao ya kuwekeza katika ujenzi wa nguzo za kusambaziaumeme za zege.

    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi OmarChambo akiwa amesimama kuangalia mfano wa Nguzo hizo,anayemuonesha ni Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke.Katikati ni Naibu Balonzi wa Ujerumani, John Reyels.

    Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, Omar Chambo akitoamaelekezo kwa Meneja Mradi wa SMMRP, Idrisa Yahya (wa pilikulia) wakati wa kikao kilichofanyika osini kwa Katibu Mkuu.

    Katikati ni Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Mamadou Barry.

    MhandisiOmar ChamboakimsikilizaKaimu Kamishnawa Madini,Mhandisi AllySamaje (katikati),anayesikilizani KamishnaMsaidiziwa MadinianayeshughulikiaWachimbajiWadogo, Julius

    Sarota (wakwanza kulia).

  • 8/20/2019 MEM 98 Online

    8/11

    8   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Asteria Muhozya,Dar es Salaam

    Serikali imetangazakuwa kuanzia tarehe 10Disemba, 2015, watejawa leseni za madiniwameanza kufanya

    malipo ya ada za leseni kwa njia

    za mitandao ya simu (M-Pesana Tigo Pesa), Maxmalipo nakwa kutumia kadi za benki zaVISA na Mastercard.

    Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuzinduliwa kwamfumo wa kielektroniki waleseni za Madini ujulikanaokama Online Mining CadastreTransactional Portal (OMCTP),ambao tangu kuanzishwakwake, umewezesha watejawaliosajiliwa kutuma maombiya leseni, kuhakiki taarifa zaleseni wanazomiliki na kutumataarifa za utendaji wa kazikielektroniki.

    Akizungumza nawaandishi wa habari katikaukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO), hivi karibuni,

    Kamishna Msaidizi wa Madinianayeshughulikia Leseni,

    Mhandisi John Nayopaalisema kuwa, mfumo huopia utawawezesha waombajikuhamisha fedha kupitia benki

    (EFT) na kuwawezesha kupatataarifa za kijiolojia na takwimumbalimbali za madini.

    “Wizara inapendakuwahakikishia watumiaji wamfumo huo kuhusu usalama

    wa fedha zao wanapofanyamalipo kwa njia ya mtandao.Malipo ya ada za lesenihayatapokelewa kwa njia yakawaida, bali ofisi zetu zitatoamsaada kwa wateja wanaohitajimaelekezo kuhusu matumiziya mfumo huo. Kama ilivyokwa huduma nyingine za lesenizitolewazo kwa njia ya mtandao,wateja wetu wanakumbushwakujisajili kwenye ofisi zetu zaMadini ili waendelee kutumia

    huduma hizo, ikiwa ni pamojana huduma hii ya malipo kwanjia ya mtandao.”alisisitizaNayopa.

    Akizungumzia zaidi kuhusumfumo huo, Mhandisi Nayopaalieleza kuwa, hadi kufikiasasa, Wizara imefanikiwakusajili jumla ya leseni 8,205 zamadini nchini katika mfumowa OMCTP, idadi ambayoinajumuisha leseni za kampuni,vikundi na watu binafsi.

    Aliongeza kuwa, kati yaleseni hizo, idadi ya leseni haiza uchimbaji mkubwa na wakati zilizosajiliwa ni 2,971 na

     jumla ya maombi ya leseniyaliyosajiliwa ni 621. Vilevile,alieleza kuwa, leseni hai zauchimbaji mdogo zilizosajiliwa

    kwenye huduma hiyo ni 1,206na kwamba maombi ya leseni zauchimbaji mdogo yaliyosajiliwakwenye mfumo mpya ni 533.

    “Leseni za utafutaji wamadini zilizosajiliwa hadikufikia sasa, ni leseni 1,618na maombi 82 ya leseni zautafutaji yamesajiliwa. Jumla yaKampuni hai 313 zimesajiliwana idadi ya ya wateja ambao

     barua pepe walizosajili

    zinasubiri uhakiki ni 348”,alisema.Akieleza malengo ya

    mfumo huo alisema kuwa,umelenga katika kuongezauwazi na kasi ya utoaji wa leseniza madini, kupunguza tatizola mlundikano wa maombikwenye ofisi za madini,kurahisisha upatikanaji wataarifa za leseni kila wakati nakujua malipo ya leseni au taarifaza utendaji kazi zinazohitajika.

    Aidha, aliyataja malengomengine kuwa ni pamoja nakurahisisha mawasiliano kati yaWizara na wamiliki wa lesenipamoja na kurahisisha uhakikina usimamizi wa leseni nautoaji wa taarifa za madini kwawakati.

    Na Mohamed Saif, Iringa

    Wananchi wa kijiji

    cha Kigozi wilayaniIringa wamempokeakwa shangwe Waziriwa Nishati na

    Madini, Profesa Sospeter Muhongoalipotembelea kijijini hapo kwa lengola kujadiliana nao kuhusu matumiziendelevu ya maji kutoka Mto Ruahaambao unapeleka maji katika Bwawa lauzalishaji umeme la Mtera.

    Mara baada ya Profesa Muhongokutambulishwa kwa wakulima hao na

    Mkuu wa Wilaya ya Iringa, RichardKasesela wananchi walishindwa kuzuiahisia zao kwa kumshangilia Profesa

    Muhongo na huku kila mmoja akitakakupeana naye mkono.Mmoja wa wakulima hao, Amos

    Mahinga alisema amefurahishwa sanana ujio wa Waziri huyo kijijini hapokwani hakuwahi kumuona na amekuwaakimsikia tu kwenye vyombo vya habari.

    “Nimefurahi sana kumuona huyuWaziri maana kupitia juhudi zaketumepata umeme,” alisema Mahiga.

    Akizungumza na wakulima hao,Profesa Muhongo aliwaagiza kuachana

    na matumizi mabaya ya maji kutokaMto Ruaha kwani kufanya hivyokumesababisha mitambo ya kuzalisha

    umeme ya Mtera kushindwa kufanyakazi.“Nadhani mmeona namna ambavyo

    umeme umekuwa ukikatika mara kwamara, hii ni sababu mmeshindwa kuwana matumizi endelevu ya maji na hivyokusababisha bwawa la Mtera kukauka,”alisema Profesa Muhongo.

    Profesa Muhongo alijionea namnawakulima hao wanavyozuia majikwenye mtoa Ruaha mdogo na hivyokusababisha Bwawa la Mtera kukosa

    maji.Baada ya kujionea hali hiyo, Waziri

    Muhongo aliiomba Ofisi ya Mkuu wa

    Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Iringakuitisha kikao na wadau wa mto huoambao ni Bodi ya Maji- Bonde la Rufiji,TANAPA, Tanesco na Ofisi ya Mkuuwa Mkoa wa Mbeya ili kujadili sualahilo ili lipatiwe ufumbuzi.

    Vilevile aliwaagiza Tanesco na Bodiya Maji - Bonde la Rufiji kuhakikishawanawapatia mafunzo wakulimahao juu ya matumizi bora ya maji bilakuathiri maji yaendayo kwenye Bwawala Mtera.

    Muhongo apokelewa kwa shangwe Kigozi

    Mkuu wawilaya ya Iringa,Richard Kaseseraakieleza jambokwa Waziri waNishati na Madini,Profesa SospeterMuhongo (hayupopichani) wakatiWaziri huyoalipoka katikakijiji cha Kigozimkoani Iringaili kujadilianana Wakulimakuhusu matumiziendelevu yamaji yam toRuaha ambao piahupeleka majikatika Bwawa la

    uzalishaji Umemela Mtera.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa katika

    kijiji cha Kigozi mkoani Iringa wakati alipoka kijijini hapo ili kujadiliana naWakulima kuhusu matumizi endelevu ya maji ya mto Ruaha ambao pia hupelekamaji katika Bwawa la uzalishaji Umeme la Mtera.

    Ulipaji Leseni za Madini warahisishwa

    Kamishna Msaidizi wa Madini, anayeshughulikia Leseni,Mhandisi John Nayopa (Kulia) akisisitiza jambo wakatiakizungumza na waandishi wa habari kuhusu malipo yaada za leseni kuanza kutumika kwa njia za mitandao yasimu (M-Pesa na Tigo Pesa), Maxmalipo, kwa kutumia kadiza benki za VISA na Mastercard. Anayemsikiliza kushotoni Mkurugenzi Msaidizi wa habari, Idara ya Habari(MAELEZO), Tiganya Vicent.

  • 8/20/2019 MEM 98 Online

    9/11

    9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

     

    Maonesho ya 5 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha

     yenye aina mbalimbali za vito zikiwemo

    T anzanite, Ruby, Sapphire, Tsavorite,Rhodolite, Spessartite, Tourmaline,

    Chr  ysober  yl na Almasi yanatarajiwa kuvutia  

    Zaidi ya kampuni 100 za wafanyabiashara na

     wachimbaji madini ya Vito kutoka Tanzania na

    nchi zingine za Afrika Mashariki, Kati na Kusini;

    na  zaidi ya wanunuzi 500 kutoka zaidi ya nchi 25

    ulimwenguni

     Jisajili na Ushiriki Sasa!!! 

     Wasiliana na: Kamati ya Maandalizi AGF 

    Simu: +255 784352299 or +255 767106773 

    Barua pepe: [email protected]

    :ama Ofisi za Madini za Kanda

     Yameandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini

    kwa kushirikiana na

    Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA) 

    Na Mohamed Saif

    Serikali imeliagiza Shirikala Umeme Tanzania(TANESCO) kuacha maramoja tabia ya kukata umeme

     bila sababu za msingi.Agizo hilo limetolewa jijini Dar

    es Salaam na Waziri wa Nishati naMadini Profesa Sospeter Muhongo naNaibu wake, Dkt. Medard Kalemaniwalipofanya ziara ya kushtukizakwenye Makao Makuu ya Taasisihiyo mara tu baada ya kuapishwa naRais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufulina kuzungumza na Menejimenti yaShirika hilo.

    Profesa Muhongo alisemawananchi wamechoshwa na tabia ya

    shirika hilo ya kukata umeme marakwa mara bila kuwepo na sababu yamsingi ya kufanya hivyo.

    “Haiwezekani kila mwaka matatizoni yaleyale na nyie bado mpo ofisini, hilihalikubaliki na halivumiliki. Ninatakatutengeneze historia ya kutatua matatizoya umeme nchini. Umeme ukiendeleakukatikakatika lazima muondoke,”alisema Profesa Muhongo.

    Alisema wananchi wanahitajiumeme wa bei nafuu ili wawezekujikwamua na umasikini huku

    akieleza kwamba ni wakati mwafakasuala hilo likatazamwa kwani bei yahuduma ya umeme ikishuka bidhaa

    nyingine pia zitashuka.Mbali na hilo, Profesa Muhongo

    aliwataka watendaji hao kujieleza nikwanini umeme umekuwa ukikatikamara kwa mara ikiwa ni pamojana kuwataka waeleze wao kamaMenejimenti ya Shirika hilo ni hatuazipi ambazo tayari wamezichukuakuhakikisha hali hiyo haijirudii.

    Vilevile aliwataka waeleze ni kwanini huwa wanachelewa kufika maeneoambayo kumetokea hitilafu hali yakuwa wananchi wanatoa taarifa maratu wanavyoona hitilafu husika.

    “Huduma zenu haziridhishi,unakuta transfoma imeharibika amanguzo imeanguka na taarifa mnaletewaniambieni ni kwanini huwa hamfiki

    kwa wakati,” alihoji Profesa Muhongohuku akiwasisitiza wabadilike.

    Alisema lengo la Serikali ya Awamuya Tano ni kuifanya Tanzania inakuwanchi ya viwanda na hivyo inatakiwakuwa na umeme wa uhakika.

    Profesa Muhongo alisema tanguametangazwa amepokea simu nyingikutoka kwa Watanzania wakisikitishwana hali ya umeme nchini.

    “Nimepokea simu kwa wananchiwa mikoa mbalimbali nchini hususanArusha na Mwanza wakinilalamikia

    kuhusu kukosekana kwa huduma yaumeme kwenye mikoa hiyo. Natakaleo hii mnipe jibu tatizo ni nini,” alihoji

    Profesa Muhongo.Alisema ni wakati sasa viongozi hao

    wawe wabunifu vinginevyo Serikalihaiwezi kuwaelewa kwani kila kukichatatizo la umeme linaonekana kuendeleakuwa palepale.

    “Kwa miaka yote mliyofanya kazihapa Tanesco naona mmeshindwakubuni mbinu zitakazolipeleka shirikakule ambapo wananchi wanataka.Ninawaagiza kujitathmini kama kwelimnafaa kuendelea na majukumuyenu,” alisema Muhongo.

    Alisema wananchi wamechokakusikiliza maneno bila kuona vitendona hivyo kuwaagiza kuhakikishawanabadilika haraka iwezekanavyokabla Serikali haijachukua hatua

    zingine.Akizungumza wakati wa kikao

    hicho, Naibu Waziri Dkt. MedardKalemani alisema kazi kubwa yashirika hilo ni kuwapelekea wananchihuduma ya umeme na si vinginevyo.

    Alisema ilani ya Chama ChaMapinduzi (CCM) imebainisha lengola Serikali ya kuhakikisha wananchiwanapelekewa huduma ya umeme nasio ahadi na maneno yasiyokuwa natija.

    Aliwaagiza kuhakikisha katika

    utendaji wao wanazingatia uadilifu,uwajibikaji na kuzingatia taaluma

     badala ya kufanya kazi kwa mazoea.

    Akizungumzia suala la wizi waumeme, Dkt. Kalemani alisemawatumishi wasio waadilifu washirika hilo nao wanahusika kwanamna moja ama nyingine na hivyokuwaagiza watendaji hao kuhakikishasuala hilo linashughulikiwa mapemaiwezekanavyo.

    “Tubadilike, tutafsiri mipango yetukwa vitendo, tupange na tutekeleze.Hakuna muda wa kuendeleakuzungumza mipango bila utekelezaji.Wananchi wanahitaji kuona utekelezajiunafanyika,” alisema Dkt. Kalemani.

    Naye Mkurugenzi Mtendaji waShirika hilo, Mhandisi FelchesmiMramba aliahidi kuendeleza

    ushirikiano na viongozi hao ili kutatuachangamoto mbalimbali za sekta yaumeme.

    “Tumefurahi na uteuzi huukwani mnaielewa vizuri sekta hii yanishati; tupo tayari kufanya kazi natunawahakikishia kuzingatia maagizoyenu bila kuchelewa,” alisema Mramba.

    Katika ziara hiyo ya kushtukizailihudhuriwa pia na Katibu MkuuWizara ya Nishati na Madini, MhandisiOmar Chambo na Naibu Katibu MkuuMhandisi Paul Masanja.

    Prof. Muhongo atema cheche

  • 8/20/2019 MEM 98 Online

    10/11

    10   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    1 2

    5 6

    3 4

    SIMBACHAWENE AKABIDHI OFISI

    1. Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mbele), Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. MedardKalemani na Naibu katibu Mkuu, Mhandisi Paul Masanja (aliyesimama), akitoa shukurani katika kikao.

    2. Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, George SimbaChawene (aliyesimama), Waziri wa Nishati na Madini, Prof.Sospeter Muhongo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani na Naibu katibu Mkuu, Mhandisi PaulMasanja wakiwa wanamsikilia Mheshimiwa Simbachawene wakati akihutubia katika kikao hicho.

    3-6. Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia makabiziano hayo.

  • 8/20/2019 MEM 98 Online

    11/11

    11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandaoya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya ‘Nishati na Madini’ Karibu tuhabarishane na

    tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

    Profesa Muhongo aiagiza Tanesco kuandaampango madhubuti wa utiririshaji maji

    Na Mohamed Saif

    Shirika la Umeme Nchini(Tanesco) limetakiwakuandaa mpangomadhubuti wa utitirishajimaji kutoka kwenye

     bwawa la Nyumba ya Mungu ilikuwepo na maji ya kutosha yakuzalisha umeme kwenye vituovya Hale na New Pangani.

    Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo alitoaagizo hilo wakati wa ziara yakekatika mabwawa ya kuzalishiaumeme ya Hale na Panganiyaliyoko mkoani Tanga na bwawala Nyumba ya Mungu la mkoani

    Kilimanjaro.Agizo hilo alilitoa baada ya

    kujionea namna ambavyo kina chamaji kwenye mabwawa ya Hale naPangani kimepungua kutokanana mipango hafifu ya utiririshajimaji kutoka bwawa la Nyumbaya Mungu ambalo ni chanzokikuu cha upelekaji maji katikamabwawa hayo yaliyoko mkoaniTanga.

    “Nimeamua kufanya ziarakatika vyanzo vyote vya uzalishajiumeme nchini ili baada ya hapatuangalie jinsi tutakavyoboreshahali ya uzalishaji umeme nawananchi wetu wapate umeme wauhakika na wa bei nafuu,” alisemaProfesa Muhongo.

    Meneja wa Kituo cha kuzalishaumeme wa maji wa Pangani,Mhandisi John Skauk alisemakuwa mitambo ya Hale ilifungwamwaka 1964 ikiwa na uwezo wakuzalisha umeme wa kiasi chamegawati 21 ambapo kila mtambo(kati ya mitambo miwili) katikakituo hicho una uwezo kuzalishaumeme wa kiasi cha megawati10.5.

    Aliongeza kuwa ukarabatiwa kwanza wa mitambo hiyoulifanyika mwaka 1986 na kuwailipofika mwaka 2008 mtambommoja uliharibika na hivyo

    kusababisha mtambo mmoja tukufanya kazi hadi sasa.Akionekana kukasirishwa na

    taarifa hiyo, Profesa Muhongoalihoji ni kwanini ukarabati wamtambo huo umechukua mudamrefu na kuagiza mtambohuo kufungwa haraka ili uwezekuzalisha nishati ya umeme.

    Profesa Muhongo pia alisisitizakufanyika kwa ukarabati wamara kwa mara wa mitambo yauzalishaji umeme huku akielezea

    kuwa kuchelewa kwa ukarabati wamitambo hiyo ni sababu mojawapoya matatizo ya umeme nchini.

    Kwa upande wa kituo chauzalishaji umeme cha NewPangani ilielezwa kuwa mitamboiliyopo ina uwezo wa kuzalishaumeme wa megawati 68 hatahivyo kutokana na upungufu wamaji kwenye bwawa la Panganimitambo hiyo inazalisha megawati17 hadi 50 kwa siku.

    “Mitambo hii ya Panganiiko vizuri haina hitilafu yoyoteisipokuwa tu ni suala la kutopatamaji ya kutosha kutoka kwenyechanzo kikuu ambacho niNyumba ya Mungu,” alisemaMhandisi Skauk.

    Aidha, akizungumzia Kituocha Nyumba ya Mungu, MhandisiSkauk alieleza kuwa kituo kinauwezo wa kuzalisha umeme wakiasi cha Megawati Nane nakwamba wanashindwa kutiririshamaji ya kutosha kwenda katikavituo vya Hale na Pangani kwakuwa watasababisha mafurikokwenye baadhi ya maeneo ambapo

    maji hayo yanapita.Akizungumzia suala la

    uzalishaji umeme kwa kutumiamaji, Profesa Muhongo alisemakuwa changamoto ya uzalishajiumeme wa maji nchini inatokanapia na mabwawa mengi kujengwakwa kutumia teknolojia ya zamanihivyo Serikali imedhamimiriakuwa na vyanzo vingi zaidi vyakuzalisha nishati hiyo ya umemembali na maji.

    “Lazima tuwe na vyanzo vingi,umeme upatikane, usikatikekatike.Tunafanya tathmini ya vyanzovyote tuone uzalishaji wake, ziarahii ni muhimu kwani bila kufanya

    hivi nisingejionea kwamba kunamtambo haufanyi kazi tangumwaka 2008,” alisema ProfesaMuhongo.

    Alisema alichokiona Kandaya Kaskazini ni kuwa maji yapoya kutosha isipokuwa hakunamipango madhubuti ya kutiririshamaji kutoka kwenye chanzo kikuuhadi kufika kwenye mabwawaya uzalishaji umeme ya Hale naPangani.

    “Habari ya kuwa mnawaambia

    wananchi kwamba huku hakunamaji sio sahihi. Maji yapoisipokuwa hakuna mipangomizuri ya mtiririko wa maji kutokaNyumba ya Mungu kwenda Halena Pangani,” alisema.

    “Hili suala la maji linatia aibu;tunataka tutathmini ndani yasiku kumi tubaini wapi tuongezenguvu zaidi, Tanesco inapaswaiingie gharama ya kutengenezamiundombinu ya maji,” alisemaProfesa Muhongo.

    Aliliagiza Shirika hilo laUmeme kufanya kikao na Bodiya Bonde la Pangani ili kuandaampangilio mzuri wa kuruhusumaji kutoka bwawa la Nyumbaya Mungu hadi Hale na Pangani

     bila kuleta uharibifu kwa kuwawananchi pia wanahitaji maji hayokwa matumizi mbalimbali.

    Aliagiza kikao hicho kifanyiketarehe 15 mwezi huu (Jumanne)asubuhi na makubaliano ya kikaoyapelekwe Wizara ya Nishati naMadini na kwa wakuu wa wilayawa maeneo husika ili hatua zaharaka zichukuliwe.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza Mhandisi JohnSkauk kutoka TANESCO, (kulia)wakati wa ziara yake kwenye kituo cha kuzalisha umeme chaHale mkoani Tanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco),Felchesmi Mramba. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kujionea shughuli za uzalishaji umemezinazoendelea kwenye mabwawa ya Hale, New Pangani Falls na Nyumba ya Mungu.