Mem Bulletin 75

9
 Ofi si ya Mawasiliano Serik alini inapokea habar i za m atukio mbalimbali kwa ajili ya News Bul lettin hii na Jar ida la Wizar a ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] HABARI ZA NISHATI &MADINI  To leo No. 75 Lime sa mb az wa kwa Ta asisi na Idara zote MEM Julai 10 - 1 6, 2015 Bulletin  e w s  http://www.mem.go.tz  Neema kwa wa chimba ji wadogo  Neema kwa wac himbaji wadogo  Kamishna wa Madini Tanzania,Mhandisi Paul Masanja Mmoja wa akina mama anayejishughulisha na shughuli za uchimbaji madini akichambua madini aina ya Rubi nchini. Baadhi ya Wachimbaji Wadogo wa Madini wakiendelea na shughuli za utafutaji madini aina ya Rubi katika moja ya migodi inayomilikiwa na wachimbaji wadogo nchini. >> Kiwango cha Ruzuku chaongezeka  S o m a  h a b a r i U k .  2 Bunge lapitisha Miswada ya Sheria za Petroli na TEITI iliyosomwa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene. Soma Miswada hiyo www.mem.go.tz

description

JARIDA WIKI TOLEO LA 75 LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Transcript of Mem Bulletin 75

Ofisi ya Mawasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali
kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizar a ya Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]
HABARI ZA
NISHATI &MADINI
 Toleo No. 75 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Julai 10 - 16, 2015
Bulletin
Mmoja wa akina mama anayejishughulisha na shughuli za uchimbaji madini akichambua madini aina ya Rubi nchini.
Baadhi ya Wachimbaji Wadogo wa Madini wakiendelea na shughuli za utafutaji madini aina ya Rubi katika moja ya migodi inayomilikiwa na wachimbaji wadogo nchini.
>>  Kiwango cha Ruzuku chaongezeka
U k . 2 
Bunge lapitisha Miswada ya Sheria za Petroli na TEITI iliyosomwa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene. Soma Miswada hiyo
www.mem.go.tz
Na Veronica Simba, Dar es Salaam
W achimbaji madini wadogo nchini wanatarajiwa kunufaika zaidi na awamu ya pili ya ruzuku inayotarajiwa
kutolewa na Serikali hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine, kiwango cha fedha pamoja na idadi ya walengwa vimeongezwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati inayoshughulikia maombi ya ruzuku ya wachimbaji madini wadogo awamu ya pili, jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Kamishna wa Madini Mhandisi Paul Masanja alisema kiwango cha fedha kwa Awamu ya Pili kimeongezeka kufikia Dola za Marekani milioni tatu (3) na Shilingi za Kitanzania bilioni 1.7 kutoka Dola za Marekani 500,000 zilizotolewa awamu ya kwanza.
Aidha, Kamishna Masanja aliongeza kuwa idadi ya walengwa wa ruzuku kwa awamu ya pili imeongezwa kutoka 11 katika awamu ya kwanza hadi 70 kwa awamu ya pili.
“Kwa awamu hii ya pili ya ruzuku, kiwango cha juu kwa kila mlengwa ni Dola za Marekani 100,000 kutoka Dola za Marekani 50,000 zilizotolewa kwa kila mlengwa kwa awamu ya kwanza,” alifafanua Kamishna Masanja.
Akizungumzia mwitikio wa walengwa kuomba ruzuku, Kamishna alisema kumekuwa na mwitikio mkubwa sana ambapo jumla ya maombi 750 yamewasilishwa kupitia Ofisi za Madini za Mikoa na Kanda zilizoko nchini kote. Katika awamu ya kwanza ya utoaji ruzuku, maombi yaliyopokelewa hayakuzidi 50.
Kamishna Masanja alisema mambo mengine yaliyoboreshwa katika awamu ya
pili ya utoaji ruzuku ni pamoja na kupanua malengo ambapo Ruzuku ya Awamu ya Pili imelenga pia kusaidia vikundi vya akina mama.
Aliongeza kuwa hata vigezo vya kupata washindi vimepanuliwa na kuwa wazi zaidi ambapo kutakuwa na tathmini ya awali na tathmini ya kina.
Vilevile, Kamishna Masanja alisema tofauti na ilivyokuwa katika awamu ya kwanza, ambapo Benki ya TIB ndiyo ilikuwa na wajibu wa kutoa ruzuku pamoja na ufuatiliaji wa utendaji wa walionufaika, katika awamu ya pili ufuatiliaji utafanywa na Idara ya Madini iliyo chini ya Wizara na TIB itabaki na wajibu wa kutoa ruzuku.
“Mabadiliko yote haya yanalenga kuboresha zoezi la utoaji ruzuku ili liwe lenye tija zaidi,” alisema Kamishna Masanja na kuongeza kuwa wanufaika wataingia Mkataba na TIB lakini Idara ndiyo itakuwa inatoa maelekezo ya utoaji ruzuku kwa muhusika.
Kwa upande wa zoezi la tathmini ya kuondoa wale ambao hawatakuwa na sifa, Kamishna Masanja alitaja masuala ya msingi yatakayozingatiwa katika hatua ya kwanza kuwa ni pamoja na Fomu iliyojazwa kwa usahihi na kusainiwa na mwombaji, Fomu iliyopokelewa na kusainiwa na Makamishna Madini Wasaidizi wa Mikoa na Kanda, iliyoambatishwa na risiti ya ulipaji wa mrahaba na vinginevyo.
Alitaja masuala mengine ya kuzingatiwa kuwa ni shughuli zinazoendana na lengo la utoaji ruzuku kama vile kupanua uchimbaji, uchenjuaji, kuongeza thamani madini na shughuli mbadala hasa za kina mama.
Katika hatua ya pili ya kuwapata watakaopendekezwa kupata ruzuku, Kamishna Masanja alisema vipengele vinavyotumika kwenye tathmini ni vile vilivyotokana na Mwongozo wa Ruzuku (Grant Manual) uliotayarishwa kati ya Wizara na Benki ya Dunia.
Masanja alivitaja vipengele hivyo kuwa ni pamoja na kuendana na gharama halisi ya vifaa vilivyoombwa, wenye kuongeza kipato cha mchimbaji, wenye kuongeza ajira kwa jamii na wenye mahitaji muhimu kwa jamii. Vingine ni uzoefu usiopungua miaka miwili na pia ambao mwombaji amechangia gharama za uendeshaji.
Alisema kuwa, hatua ya mwisho katika uchambuzi wa kuwapata wenye vigezo vya kupata ruzuku ni pamoja na kuwatembelea kwenye maeneo yao ya uchimbaji wale watakaokidhi vigezo vyote vilivyoainishwa ili kujiridhisha iwapo mahitaji waliyoyaomba yanaendana na yataweza kutimiza lengo la Wizara la kuwasaidia wachimbaji wadogo.
Utaratibu huo wa kutoa ruzuku kwa wachimbaji madini wadogo, ulianzishwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kama njia mojawapo ya kuboresha mazingira ya uchimbaji mdogo nchini na kuwawezesha wachimbaji wadogo kukuza vipato vyao na kuweza kujikimu kimaisha pamoja na kuchangia kukuza uchumi wa nchi.
Awamu ya kwanza ya utoaji Ruzuku ilifanyika mwaka 2013/2014. Maandalizi ya Awamu ya pili yalikwishaanza ambapo Ruzuku hiyo itatolewa ndani ya mwaka wa fedha 2015/2016.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja akizungumza katika moja ya Maonesho ya Kimataifa ya Vito (AGF) yanayofanyika kila mwaka jijini Arusha, Tanzania. Wa tatu kutoka kulia ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava
Baadhi ya Wachimbaji Wadogo wa Madini wakiendelea na shughuli za utafutaji madini aina ya Rubi katika moja ya migodi inayomilikiwa na wachimbaji wadogo nchini.
 
BODI YA UHARIRI
WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James
na Nuru Mwasampeta
msibweteke!
H ivi karibuni, Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Paul Masanja alizindua rasmi Kamati ya Maombi ya Ruzuku ya Wachimbaji Madini wadogo, Awamu ya Pili.
Katika hotuba yake ya uzinduzi, Kamishna Masanja alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini (ambao ndiyo
waratibu na wasimamizi wa utoaji Ruzuku), inalenga kuendelea kuwasaidia Wachimbaji Madini wadogo kwa kuboresha mazingira yao ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi na Ruzuku.
Alisema katika Awamu ya Kwanza ya Ruzuku iliyotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2013/14, kulikuwa na mafanikio lakini pia changamoto kadhaa zilijitokeza na hivyo alisema Serikali imejipanga kukabiliana na changamoto husika katika Awamu ya Pili ili zoezi la utoaji Ruzuku liwe na tija zaidi.
Miongoni mwa mambo yaliyoboreshwa katika zoezi la utoaji Ruzuku kwa Awamu ya Pili ni kuongeza kiwango cha fedha pamoja na idadi ya walengwa.
Kiwango cha fedha kwa Awamu ya Pili kimeongezeka kufikia Dola za Marekani milioni tatu (3) na Shilingi za Kitanzania bilioni 1.7 kutoka Dola za Marekani 500,000 zilizotolewa awamu ya kwanza. Aidha, idadi ya walengwa wa ruzuku kwa awamu ya pili imeongezwa kutoka 11 katika awamu ya kwanza hadi 70 kwa awamu ya pili.
Kwa mujibu wa Kamishna Masanja, kiwango cha juu kwa kila mlengwa kitakuwa Dola za Marekani 100,000 kutoka Dola za Marekani 50,000 zilizotolewa kwa kila mlengwa kwa awamu ya kwanza.
Vilevile, mwitikio wa walengwa kuomba ruzuku umekuwa mkubwa sana ambapo jumla ya maombi 750 yamewasilishwa kupitia Ofisi za Madini za Mikoa na Kanda zilizoko nchini kote kutoka maombi yasiyozidi 50 katika Awamu ya Kwanza.
Pia, Awamu ya Pili ya Ruzuku imelenga kusaidia vikundi vya akina mama na kupanua uchimbaji, uchenjuaji pamoja na kuongeza thamani madini.
Suala la ufuatiliaji limeboreshwa pia ambapo, tofauti na ilivyokuwa katika awamu ya kwanza, ambapo Benki ya TIB ndiyo ilikuwa na wajibu wa kutoa ruzuku pamoja na ufuatiliaji wa utendaji wa walionufaika, katika awamu ya pili ufuatiliaji utafanywa na Idara ya Madini iliyo chini ya Wizara na TIB itabaki na wajibu wa kutoa ruzuku.
Kamishna Masanja alisema kuwa mabadiliko yote haya yanalenga kuboresha zoezi la utoaji ruzuku ili liwe lenye tija zaidi.
Kutokana na dhamira hiyo njema na jitihada za wazi zinazofanywa na Serikali, tunawaasa Wachimbaji Madini wadogo hususan wale walionufaika na watakaoendelea kunufaika na Ruzuku pamoja na misaada mingine mbalimbali inayotolewa na Serikali kuitumia vema ili kukuza kipato chao na hivyo kunufaika kimaisha wao binafsi na hata kunufaisha Taifa zima.
Si vema jitihada hizi za Serikali zikaachwa na kupotea bure. Si vema walengwa wa Ruzuku kubweteka tu pasipo kuonyesha jitihada kwa kuhakikisha kuwa ruzuku hiyo inaleta tija katika maeneo yao ya kazi na hivyo kuipa moyo Serikali kuendelea kuongeza kiwango na idadi ya wanopata ruzuku katika kila awamu.
Kwa walengwa kutokutimiza wajibu wao ipasavyo, ni wazi malengo yanayotazamiwa kufikiwa hayatafikiwa.
Iwapo malengo mazuri yaliyokusudiwa na Serikali hayatafikiwa, wa kulaumiwa watakuwa walengwa wenyewe, yaani Wachimbaji Madini wadogo. Hii ni kwa sababu upande wa Serikali umekwishaonyesha dhamira yake ya dhati kuwasaidia na hata utekelezaji wake tumeshuhudia kuwa unafanyika.
Kazi kwenu Wachimbaji Madini wadogo, msibweteke, Msituangushe.
TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
M ashine ya kupima madini ya metali katika banda la Wakala wa
Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) imekuwa kivutio katika Maonesho ya kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Viongozi mbalimbali na wananchi walifurika katika banda la TMAA ili kupima thamani za madini kupitia mashine hiyo ambapo walipimiwa viwango vya madini yaliyopo katika pete, mikufu, hereni, n.k 
Akielezea uwezo wa
maabara ya Wakala katika kupima na kutoa majibu kwa wakati, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Wakala huo, Yisambi Shiwa alisema Wakala una vifaa vya kisasa na wataalam waliobobea katika kufanya uchambuzi wa sampuli za madini ya aina mbalimbali.
Alisema maabara ya Wakala huo inatambulika kimataifa kwa namba ISO 17025 na ni moja ya maabara chache duniani ambazo zinakidhi vigezo vya kimataifa
Aliongeza kuwa maabara hiyo kwa sasa inapokea sampuli za madini kutoka ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na sampuli kutoka bara la Ulaya na Amerika.
Akielezea mafanikio ya Wakala huo, Shiwa alisema
Wakala umewezesha Serikali kupata takwimu sahihi za madini yanayozalishwa na kuuzwa nje ya nchi kutoka kwa wachimbaji wakubwa, wa kati na wadogo ambazo husaidia serikali kuratibu mipango mbalimbali ya maendeleo.
Aliongeza kuwa kaguzi za Wakala zimesaidia ukusanyaji wa kodi mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wa madini kulipwa kwa wakati na ustahiki.
Alisisitiza kuwa Wakala umefanikiwa kudhibiti utoroshwaji wa madini kwenda nje ya nchi, ambapo hadi sasa madini yenye thamani ya shilingi  bilioni 15.7 yalikamatwa kupitia madawati ya ukaguzi ya Wakala yaliyopo katika viwanja vya ndege. Madini hayo yalitaifishwa na kupigwa mnada na serikali.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava ( wa pili kutoka kulia) katika picha ya pamoja na wataalam kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA). Kutoka kushoto Mhandisi Baraka Manyama, Omari Rwakyaya na Mhandisi Yisambi Shiwa.
 
HABARI ZA NISHATI/MADINI
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM); mara baada ya kuwasili katika banda la Wizara wakati wa maonesho ya kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Rayson Nkya (kushoto) akitoa maelezo ya Sera ya Madini kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) mara Kaimu Katibu Mkuu alipotembelea banda la Wizara .
Mtaalam katika Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), Jumanne Shimba (kulia) akimweleza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) jinsi mashine ya kukata madini inavyofanya kazi.
Mtaalam kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Melania Nyimbo (kulia) akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) bahasha yenye machapisho mbalimbali kutoka wakala huo.
 
 
 
Washiriki katika Banda la Wizara ya Nishati na Madini katika picha ya pamoja wakiwa wameshika Tuzo ya ushindi na Cheti mara baada ya Wizara kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Wizara na Wakala wa Serikali kwa mwaka 2015, wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba ( Dar es Slaam International Trade Fair (DITF) yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere  jijini Dar es Salaam.
Washiriki katika Banda la Wizara ya Nishati na Madini kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wakiwa katika picha ya pamoja na Tuzo pamoja na Cheti cha Ushindi.
Washiriki katika Banda la Wizara ya Nishati na Madini katika picha ya pamoja wakiwa wameshika Tuzo na Cheti mara baada ya Wizara kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Wizara na Wakala wa Serikali kwa mwaka 2015 katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba Biashara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi Tuzo ya Ushindi Afisa Habari wa Wizara ya Nishati na Madini Greyson Mwase baada ya Wizara kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Wizara na Wakala wa Serikali kwa mwaka 2015, wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya (Sabasaba) .Wengine wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (TAN TRADE), Jacqueline Maleko (wa pili kulia) na Afisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini Robert Mwasenga.
 WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAPATA TUZO MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA (SABASABA)
      u
HABARI ZA NISHATI/MADINI
Mtaalam kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Ayoub Shija akielezea shughuli za mgodi huo katika banda la Wizara ya Nishati na Madini
Afisa Mawasiliano kutoka Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Nchini (TEITI), Godwin Masabala akitoa maelezo  jinsi taarifa za mapato yatokanayo na rasilimali za gesi na madini zinavyokusanywa.
 WIZARA YA NISHATI NA MADINI YATOA ELIMU MAONESHO  YA KIMATAIFA YA BIASHARA (SABASABA) 2015 DAR
      u
      u Mtaalam katika Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Rayson Nkya (kushoto) akielezea Sera ya madini kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (SabaSaba ) katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Steven Lowoko akitoa maelezo kwa kutumia mfano wa mtambo wa kufua umeme kwa kutumia maji unavyofanyakazi kwa baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la TANESCO.
 u
 u
HABARI ZA NISHATI/MADINI
Afisa Huduma kwa Wateja katika Shirika la Umeme Nchini(TANESCO), Lucas Kusare (katikati) akielezea shughuli za shirika hilo kwa mmoja wa
Afisa Uokoaji katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Evarist Mwanakatwe (kulia) akielezea shughuli za uokoaji zinavyofanyika katika mgodi huo pindi majanga yanapotokea.
Mtaalam kutoka Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), Jumanne Shimba (kulia) akielezea shughuli za kituo hicho kwa mwananchi aliyetembelea katika banda la Wizara ya Nishati na Madini.
Baadhi ya wananchi wakiangalia aina mbalimbali za madini katika banda la Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)
Mtalaam kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Kankila Wakimbili akielezea shughuli za Wakala huo kwa wananchi waliotembelea banda
Mtaalam katika Chuo cha Madini Dodoma(MRI), Mkunde Msaky (kulia) akielezea fani zinazotolewa na Chuo hicho kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
SABASABA 2015, DAR ES SALAAM
 
HABARI ZA NISHATI/MADINI
Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya ‘Nishati na Madini’ Karibu tuhabarishane na
tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
M aendeleo ya taifa lolote duniani hutegemea kwa kiasi kikubwa uwepo wa umeme
wa uhakika na wa kutosha jambo linalosababisha Serikali ya Tanzania kuona umuhimu wa kukaribisha makampuni mbalimbali binafsi kuwekeza katika sekta ya umeme
hususan katika uzalishaji umeme. Kwa sasa mahitaji ya umeme
nchini yamefikia MW 935 huku mahitaji ya umeme kwa mwaka 2020 yanatarajiwa kufikia 3,423 na ifikapo mwaka 2025 mahitaji ya umeme yanatarajiwa kufikia 4,574 lakini lengo la Serikali ni kwamba ifikapo mwaka 2025 taifa liwe na uwezo wa kuzalisha MW 10,000.
Ili kufikia kiasi hicho cha umeme kinachohitajika kwa miaka ijayo, Serikali imeshaanza kufanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kiasi cha uzalishaji umeme kinaongezwa na hasa katika kujenga mitambo hiyo ya kuzalisha umeme na miongoni mwa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme iliyoanza kujengwa ni pamoja na
mtambo wa kinyerezi I ambapo utazalisha MW 150.
Aidha, Serikali imeendelea kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kushirikiana na Serikali (TANESCO), kuwekeza katika sekta ndogo ya nishati ya umeme hasa katika uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme kama ifuatavyo:-
Maeneo ya kipaumbele katika
GoT USD 183m Construction 84% completed
2 Kinyerezi II – 240MW gas red power plant
GoT - 15%  JBIC – 85% Contractor: Sumitomo Corporation
USD 344million GoT is soliciting funds for nancing the 15% of the contract value of the project
3 Kinyerezi III – 600MW gas red power plant
China Power Investment (CPI)
USD 401million JV Company formed and feasibility study is under review
4 Kinyerezi IV – 330MW gas red power plant
Poly Technology Inc. of China
USD 400million. Preliminary feasibility study is under review
5 Somanga Fungu 320MW Gas Fired Power Plant
Kilwa Energy - IPP
USD 365.6 Million
Exim Bank of China
7 150MW Solar PV in Shinyanga
Not yet secured USD 185million Under System review and equipment design
8 400MW gas red power plant at Mtwara with Symbion (T)
Symbion USD 396.577million
Feasibility study is under review
9 87MW hydropower plant to be developed at Kakono in Kagera Region
Not yet secured Estimated cost USD 379.4million
Feasibility Study completed Solicitation of nancing in progress
10 44.8MW hydropower p lant to be developed at Malagarasi river in Kigoma
Not yet secured Estimated cost: USD 149.5million
Feasibility Study completed Solicitation of nancing in progress
11 400kV Iringa  – Shinyanga transmission project (Backbone)
IDA, AfDB, JICA, EIB and Korea EDCF
USD 470 Million
Construction 20% completed
GoT - 15% Exim Bank of China – 85 %
USD 692.7million
GoT is soliciting funds for nancing the 15% of the contract value of the project
13 200kV Makambako – Songea transmission line
SIDA & GoT USD 111.43million
Distribution component 5% completed
Financing not rmed
USD 259.2million
Contract for upgrading the feasibility study from 220kV to 400kV by SWECO Signed
15 400 kV Singida- Arusha transmission line
AfDB, JICA USD 258.82 million
Valuation of properties for compensation has started
16 400 kV Chalinze- Dodoma transmission line
Financing not rmed
17 220 kV Bulyanhulu- Geita transmission line
Arab Bank for Economic Development in Africa (BADEA), OFID & GoT
USD 30million Contract signing with Consultant for project supervision completed
18 220kV T/L Geita  – Nyakanazi transmission line
KfW, AFD, EU & GoT
Euro 29million & TZS 5billion
Contract signing with Consultant for project supervision is underway
19 Improving the reliability of Electric power supply in the city of Dar es Salaam
Finish EUR. 21.8million
Construction 60% completed
20 Tanzania Energy Development and Access Expansion Project (TEDAP) - Transmission
IDA USD 34,252,345.78
Construction 70% completed
21 Tanzania Energy Development and Access Expansion Project (TEDAP) - Distribution
IDA USD 43,543,460.07
Construction 60% completed
Construction 75% completed
STATUS
23 New 132kV Kilimanjaro – Arusha Transmission Line and Rehabilitation of Kiyungi Substation.
Korean Export- Import Bank through EDCF
USD 20,176,384
Construction 85% completed
24 Rehab il itat ion o f Hale Hydro Plant 21MW
Co-nanced by SIDA (60% grant) and GoT (40% commercial loan)
SEK 197 Million The contract for the technical consultant has been signed
25 Rehabilitation and Upgrade of Grid Network.
AFD EUR. 53.0M Procurement of Consultant for supervision of the project is underway
26 Project for Reinforcement of Power Distribution in Dar es salaam Region
 JICA  Japanese Yen 4.41 Billion equivalent to USD 38 Million
Contract signing with Consultant for project supervision is underway