MEM 78 Online

download MEM 78 Online

of 5

Transcript of MEM 78 Online

  • 8/20/2019 MEM 78 Online

    1/10

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali

    kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizar a ya Nishati na MadiniWasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263

    au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    HABARI ZA

    NISHATI &MADINI

    Toleo No. 78 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Julai 31 - Agosti 5, 2015Bulletinews

     

    http://www.mem.go.tz

     

    REA yataka ushirikiano taasisi

    za Kifedha, Sekta Binafsi

    TPDC yaeleza mafanikio yake  S o ma hab ar i  U k . 10 

    Umeme ni eneolinalohitaji kuendelezwakwa ushirikiano naSekta Binafsi, Taasisi zaKifedha na Washirika waMaendeleo ili kuongezakasi ya kuviunganishivijiji na nishati hiyo”Mhandisi Ngosi Mwihava

    Endapo wadau haowatashirikiana naREA, mradi huo utaletamatokeo makubwa zaidiya yaliyopatikana sasa nahivyo kuweza kuyafikiamaeneo ambayohayajafikiwa na nishatihiyo”.Edmund Mkwawa

    Serikali peke yakehaiwezi kufanya kazi hiyotunahitaji kushirikianana Sekta Binafsi, Taasisiza Kifedha na Washirikawa Maendeleo. Uhakikawa umeme utawezeshawananchi wengi zaidikujiingiza katikashughuli za kiuchumi”.

    Dkt. Lutengano Mwakahesya

    Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava,(katikati) katika picha ya pamoja na Washirika wa Maendeleo.

    Washiriki wa kikao kazi baina ya REA Taasisi za Kifedha, Washirika waMaendeleo, Taasisi Binafsi, Wizara na Taasisi za Serikali.

     S o ma hab ar i  

    U k . 2 

  • 8/20/2019 MEM 78 Online

    2/10

    2   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Asteria Muhozya,Dar es Salaam

    T

    aasisi za Kifedha, Sekta Binafsina Washirika wa Maendeleonchini, wameshauriwa kutumiafursa zilizopo katika sektaya nishati hususani umeme

    kushirikiana na serikali kupitia Wakalawa Nishati Vijijini (REA), ili kuongezakasi ya kuviunganisha vijiji vingi zaidi na

    umeme, ikiwemo kuwezesha mapinduziya maendeleo kupitia nishati hiyo.

    Hayo yamebainishwa kwa nyakatitofauti kwenye kikao kazi kilichoandaliwana REA, kikijumuisha Taasisi za Kifedha,Sekta Binafsi, Washirika wa Maendeleo,Washirika katika tasnia ya nishati, nawawakilishi kutoka Wizara na Taasisiza Serikali, kwa lengo la kujadili na

    kuangalia namna sekta hizo zinavyowezakushirikiana pamoja ili kuongeza nguvuya kuhakikisha Tanzania hususan vijiji

    vinaunganishwa na nishati ya umeme ilikuchochea shughuli za kiuchumi vijijini.

    Akifungua kikao hicho, Kaimu KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati na MadiniMhandisi Ngosi Mwihava, alisema,miradi ya kuviunganisha vijiji na nishati yaumeme ni eneo linalohitaji kuendelezwakwa ushirikiano na wadau hao ili kuongezakasi ya uunganishaji umeme.

    Alisema kuwa, tangu Wakalahuo kuanzishwa mwaka 2007 kasiya kuviunganisha vijiji na umemeimeongezeka, na kuongeza kuwa, jitihadakubwa imekwishafanywa na Serikalina endapo wadau hao wataunganishanguvu, azma ya serikali kuhakikisha

    kuwa ifikapo mwaka 2030 taifa zima liwelimeunganishwa na nishati hiyo litafikiwaharaka kwa kuwa REA itakuwa na vyanzo

    vingi vya fedha.Mwihava aliongeza kuwa, serikali

    imefanikiwa kuimarisha miundombinu

    ya uzalishaji umeme jambo ambalolimewezesha kiwango cha uzalishajikuongezaka kutoka megawati 891 mwaka2005 hadi 1,226.3, Machi 2015.

      “Ikiwa vijiji vyetu vitaunganishwana nishati hiyo, hali hiyo itachocheashughuli za kiuchumi kufanyika ikiwemokuanzishwa kwa viwanda vidogo katikamaeneo ya vijijini, na kuongeza hudumaza kisasa za kiuchumi zinazotumia nishatihiyo. Umeme ni maendeleo na ili tuendeleetunahitaji umeme,” alisema Mwihava.

    Naye Mwenyekiti wa Bodi ya REA,Edmund Mkwawa, alieleza kuwa, endapowadau hao watashirikiana na REA, mradihuo utaleta matokeo makubwa zaidi yayaliyopatikana sasa na hivyo kuwezakuyafikia maeneo ambayo hayajafikiwa

    na nishati hiyo. Aliongeza kuwa, zipofursa nyingi ambazo taasisi hizo zinawezakuzitumia kupitia miradi mbalimbaliambayo itawezesha kupata faida na hivyo,kikao hicho kitawawezesha wadau haokutambua fursa hizo.

    Kwa upande wake Mtendaji Mkuuwa REA, Dkt. Lutengano Mwakahesyaalitumia fursa hiyo kuwashukuru wadauwote ambao wamewezesha Wakala huokuunganisha miji, vijiji na nishati hiyo

    kufikia asilimia 40 na kueleza kuwa,Wakala huo utaendelea kutafuta wafadhiliili kuweza kufanikisha malengo yake yakuhakikisha kwamba taifa linaunganishwana umeme.

    Aliongeza kuwa, serikali peke yakehaiwezi kufanya kazi hiyo na kuelezakuwa, uhakika wa uwepo wa umemeutawezesha wananchi wengi zaidikujiingiza katika shughuli za kiuchumi.

    Kwa upande wake Afisa Mwandamizianayeshughulikia nishati kutoka Benkiya Maendeleo ya Afrika (AfDB), StellaMandago, alizitaka taasisi hizo kufanyakazi na Wakala huo kwani zipo fursanyingi na hivyo itawezesha taasisi hizokupanua wigo wa shughuli zao kiuchumikupitia nishati ya umeme.

    REA yataka ushirikiano taasisi za Kifedha, Sekta Binafsi

    Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati

    na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava,(katikati) katika picha ya pamoja nabaadhi ya watumishi wa Wakala waNishati Vijijini (REA)

    Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishatina Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava,(katikati) katika picha ya pamoja nawawakilishi wa Taasisi za Kifedha.

    Afisa Mwandamizi anayeshughulikia nishatikutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), StellaMandago, akisisitiza jambo katika kikao hicho.

    Sehemu ya washiriki wakifuatilia kikao kazi baina yaREA, taasisi za Kifedha, Washirika wa Maendeleo, TaasisiBinafsi, Wizara na Taasisi za Serikali, kilicholenga kujadilina kuangalia namna sekta hizo zinavyoweza kushirikianapamoja ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme.

  • 8/20/2019 MEM 78 Online

    3/10

    3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Tahariri

    MEM

      Na Badra Masoud

    FIVEPILLARS OFREFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI

    MHARIRI MKUU: Badra MasoudMSANIFU: Essy Ogunde

    WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, GreysonMwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James

    na Nuru Mwasampeta

    INCREASE EFFICIENCY 

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OFTHE CLIENT

    SATISFACTION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OFSHAREHOLDERS

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Taasisi za Kifedha, SektaBinafsi tuunganishe nguvu

    kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Wachimbaji Madini watakiwakuendana na mabadiliko ya teknolojia

    Na Greyson Mwase,Handeni-Tanga

    W

    achimbaji waMadini nchiniwametakiwak u e n d a n a

    na teknolojiainayokua kila kukicha ilikuwezesha sekta ya madini kuwana mchango zaidi katika pato lataifa.

    Rai hiyo ilitolewa na AfisaMadini Mkazi kutoka Ofisiya Madini- Handeni mkoaniTanga, Frank Makyao wakatiwa ufunguzi wa mafunzo juu yamatumizi ya huduma za leseniza madini kwa njia ya mtandaoyaliyokutanisha wachimbaji wamadini Kanda ya Masharikiyaliyofanyika hivi karibuni mjiniHandeni

    Lengo la mafunzo hayo

    lilikuwa ni kuwapa uelewa wamatumizi ya huduma za leseniza madini kwa njia ya mtandaoijulikanayo kama Online MiningCadastre Transactional Portal.

    Makyao alisema kuwani vyema wamiliki wa leseniza madini wakaachana na

    mfumo wa zamani wa kutumiamakaratasi katika huduma zaleseni kwani mfumo wa kisasawa huduma za leseni kwa njia yamtandao utawawezesha kupataleseni kwa wakati na uwazi zaidi.

    “Kwa mfano kuanzia sasamtaweza kufanya malipo yaleseni zenu kwa njia ya M-Pesa,Airtel Money na Tigo Pesa haliitakayowezesha ofisi za madinikupata mapato zaidi,” alisisitizaMakyao.

    Makyao aliendelea kusemakuwa wachimbaji wa madiniwanatakiwa kuchangamkiamafunzo yanayotolewa na

    wataalam kutoka Wizara yaNishati na Madini na kuanzakutumia huduma hiyo maramoja ili kurahisisha utendaji waowa kazi.

    Alisema biashara katikanchi nyingi duniani imekuwaikifanyika kwa njia ya mtandao

    na kuwataka wachimbaji wamadini kuchangamkia fursahiyo ili waweze kuendana naushindani wa biashara ya madiniduniani.

    Aidha aliwataka wachimbajiwa madini kufuata sheria zamadini katika uombaji na umilikiwa leseni za madini pamoja nakushirikiana na serikali kwakulipa kodi na tozo mbalimbalikama Sheria ya Madini yaMwaka 2010 inavyowataka ilisekta hiyo iwe na mchango zaidikatika ukuaji wa uchumi waTaifa.

    Wiki hii tumeshuhudia Serikali kupitia Wakalawa Nishati Vijijini (REA), ikiingia katika hatuanyingine ya kuzitaka Sekta Binafsi, Taasisi zaKifedha na Washirika wa Maendeleo kuunganisha

    nguvu ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji zaidina nishati ya umeme.

    Tumeshuhudia jitihada kadhaa ambazozimefanywa na Serikali kuhakikisha kwambataifa letu linazalisha umeme wa uhakika na wakutosha na inapiga hatua kubwa ya kiuchumi nakimaendeleo kupitia nishati ya umeme.

    Katika kikao kazi na wadau hao, Serikali kupitiaREA, halikadhalika Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) walijaribu kueleza kwa undani namnasekta hizo zinavyoweza kushirikina katika tasniahiyo na bado wakaendelea kunufaika kutokana na

    fursa nyingi za kiuchumi na kibiashara.Kutokana na takwimu kadhaa, tangu kuanzishwa

    kwa Wakala huo mwaka 2007, umesaidia kwakiasi kikubwa kuongeza kasi ya kuviunganisha vijijina umeme. Aidha, imeelezwa kuwa, jitihada zaSerikali za kuimarisha miundombinu ya umeme,zimewezesha uzalishaji kuongezeka kutokamegawati 891 mwaka 2005 hadi 1,226.3 mweziMachi , 2015.

    Ni wazi kuwa endapo jitihada hizo ambazozimefanywa na Serikali na baadhi ya Washirikawa Maendeleo, zitaongezewa nguvu zaidi kwaushirikiano na sekta binafsi , Taasisi za Kifedha naWashirika wa Maendeleo ambao bado hawakokatika muungano huo, watawezesha azma yaSerikali ya kuviunganisha vijiji na nishati hiyokufikiwa kwa haraka zaidi.

    Shime Sekta Binafsi, Taasisi za Kifedha naWashirika wa Maendeleo wakati wa kuiwezeshaTanzania kujenga uchumi imara na kuwezeshamapinduzi ya kimaendeleo ni kupitia Nishati hiyo nisasa. Ushirikiano wenu ni muhimu ili kuhakikishaTaifa linazalisha umeme mwingi, wa uhakika na

    wa gharama nafuu kwa wananchi wake.

    Afisa Madini Mkazi- Ofisi ya Madini Handeni, Frank Makyao (kulia)akifungua mafunzo kuhusu huduma za leseni za madini kwa njia yamtandao yaliyokutanisha wachimbaji wa madini kanda ya masharikimjini Handeni. Kutoka kushoto ni wawezeshaji wa mafunzo hayokutoka Wizara ya Nishati na Madini, Pendo Elisha na Charles Gombe.

  • 8/20/2019 MEM 78 Online

    4/10

    4   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

     

    Mpango Kazi wa Ushiriki wa Watanzaniakatika Tasnia ya Mafuta na Gesi Asilia

    Na Rhoda James

    Wizara ya Nishatina Madini nchiniimejipanga kuimarishaUshiriki wa Watanzaniakatika Tasnia ya Mafuta

    na Gesi Asilia. Katika kufanikisha azmahiyo, Mpango Kazi ambao unaainishamaeneo ya kimkakati ambayo Wizaraitaanza kuyafanyia kazi umeandaliwa. Vilevile, Wizara itaunda Kitengo Maalumucha Kusimamia Masuala ya Ushiriki waWatanzania (Local Content Unit).

    Kamishna wa Nishati na Petroli waWizara ya Nishati na Madini, MhandisiHosea Mbise alisema hayo hivi karibuni

    katika kikao chake na watumishi wa sektahiyo jijini Dar es Salaam.Kikao hicho kinafuatia ushauri

    uliotolewa na uongozi wa juu wa Wizarakujadili mikakati ya utekelezaji wa masualayaliyoainishwa katika Sera ya Ushiriki waWatanzania (Local Content Policy, 2015)na Sheria (Petroleum Act, 2015 and TEITIAct, 2015) kwa lengo la kuimarisha Ushirikiwa Watanzania katika Tasnia ya Mafuta naGesi Asilia.

    Mwasilisha mada kutoka Wizara yaNishati na Madini, Neema Lugangiraalisema kikao hicho pia kilijadili nakuboresha Mpango Kazi husika pamojana mambo mengine ili kuweka mikakati yautekelezaji.

    Lugangira pia alisema kuwa ipo haja yaWizara kuunda jukwaa tofauti zikiwemo jukuwaa la Kushauriana katika Masualaya Ushiriki wa Watanzania (Local Content

    Consultative Forum) na kauandaa warsha

    (Local Content Workshop) yenye lengo lakujenga na kuimarisha uelewa wa Ushiriki

    wa Watanzania katika tasnia hiyo ya

    Mafuta na Gesi Asilia. Aidha, maazimio

    mbalimbali yalifikiwa katika kikao hichoyakiwemo kuboresha taarifa za mitandao

    pale Sera zinapoboreshwa, kuandaa kitabu

    cha Ushiriki wa Watanzania katika Tasniaya Mafuta na Gesi Asilia katika lugha yaKiswahili na Kiingereza na uandaaji wa barua kwenda kwa wadau wote kwa ajiliya kuwataarifu juu ya masuala ya Ushirikiwa Watanzania katika tasnia ya Mafuta naGesi Asilia.

    Akifunga kikao hicho Mhandisi Mbisealiwaasa watumishi wote wa Wizara

    kushirikiana kikamilifu katika kufanikishamikakati hiyo ili kutekeleza Mpango Kazihuo.

    Wa pilikutokakulia niMwasilishajimadakutokaWizara yaNishati naMadini,NeemaLugangiraakifafanua

     jambokatika kikao

    hicho.

    Katika ni Kamishna wa Nishati na Petroli wa Wizara yaNishati na Madini, Mhandisi Hosea Mbise pamoja nawatumishi wa sekta hiyo wakijadili Mpango Kazi wa Ushirikiwa Watanzania katika Tasnia ya Mafuta na Gesi Asilia.

    ipo haja ya Wizara kuunda jukwaa tofauti zikiwemo jukuwaa la Kushauriana katika Masuala ya Ushiriki waWatanzania (Local Content Consultative Forum) nakauandaa warsha (Local Content Workshop)

  • 8/20/2019 MEM 78 Online

    5/10

    5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Mradi wa umeme Vijijini kuboreshwaNa Mohamed Saif 

    Serikali inaendelea na mkakati wakewa kuhakikisha miradi ya umemenchini inakamilika kwa wakatiuliopangwa ili kuleta matokeoyaliyokusudiwa.

    Kaimu Katibu Mkuu wa Wizaraya Nishati na Madini, Mhandisi NgosiMwihava alisema hayo hivi karibuni jijiniDar es Salaam wakati wa mkutano wakena Ujumbe wa Benki ya Dunia uliolengakujadili programu ya upanuzi wa Mradi waUmeme Vijijini ujulikanao kama TanzaniaRural Electrification Expansion Program(TREEP).

    Mhandisi Mwihava alisema kuwanishati ya umeme ina umuhimu wa kipekeekatika kuleta maendeleo ya kiuchumi ikiwani pamoja na kupunguza umaskini. “Serikaliinatambua umuhimu wa nishati ya umemekwa maendeleo ya taifa,” alisema MhandisiMwihava.

    Akizungumzia mapendekezoyaliyotolewa na ujumbe huo kuhusuprogramu hiyo ya TREEP, aliagizaMaafisa waliohudhuria mkutano huokupitia mapendekezo husika ili kwendasawa na Mpango wa Matokeo MakubwaSasa (BRN). “Mpango wa MatokeoMakubwa Sasa (BRN) kwa sekta ya nishatiumeainisha vyema namna miradi yaumeme nchini inavyotakiwa kukamilika,”alisema Mhandisi Mwihava.

    Akizungumza katika mkutano huo,

    Mtaalamu Mwandamizi wa masualaya Nishati wa Benki ya Dunia, NataliaKulichenko alisema matarajio ya programuya TREEP ni kuongeza na kuboreshaupatikanaji wa umeme vijijini, kuongezausambazaji wa umeme mbadala vijijini nakuimarisha uwezo wa sekta ya nishati ilikukidhi mahitaji ya umeme vijijini.

    Alisema kupitia ushirikiano mzuri baina ya Benki ya Dunia, Wizara ya Fedha,Wizara ya Nishati na Madini na taasisizilizo chini yake, malengo na matarajio

    ya programu hiyo yatafikiwa kamainavyokusudiwa.

    Naye Kamishna Msaidizi wa Umeme,Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi

    Innocent Luoga alisema ni vyemampango huo wa TREEP ukazingatiaunafuu wa gharama za uunganishwaji waumeme kwa wateja.

    Alisema gharama za kuunganishiwaumeme zinapaswa kuwa nafuu ilikuwawezesha wananchi wengi zaidikupata huduma husika.

    Wachimbaji Kaskazini wafurahia huduma za leseni kwa mtandaoNa Greyson Mwase, Arusha

    Wachimbaji wamadini kutokaKanda ya Kaskaziniw a m e f u r a h i s h w ana mafunzo

    yanayoendeshwa na Wizara ya Nishatina Madini huhusu huduma za leseni zamadini kwa njia ya mtandao.

    Wakizungumza kwa nyakati tofautimkoani Kilimanjaro na Arusha wachimbajihao walisema kuwa wamefurahishwa nauhudi za Serikali katika kuboresha huduma

    za leseni ikiwa ni pamoja na kuwapatiamafunzo.

    Mmoja wa wachimbaji kutokaSame, Kilimanjaro Richard Mbwamboakizungumza kwa niaba ya wachimbajiwenzake alisema kuwa, mafunzo hayoyatawawezesha kutumia mtandao katikakutuma maombi ya leseni za madini

    na hivyo kupunguza gharama ambazo

    walikuwa wakizipata awali.Akizungumzia huduma mpya ya leseniza madini kwa njia ya mtandao alisemakuwa huduma hiyo ni nzuri kwa kuwaitaongeza kasi ya upatikanaji wa leseni zamadini na kuongeza mapato kwa Serikali.

    Mbwambo alisema, awali wachimbajiwa madini walishindwa kuomba leseniza uchimbaji wa madini kutokana naupatikanaji wake kuwa mgumu, kutokanana kusafiri umbali mrefu hadi ofisi za madinizilizo mbali na hivyo kuingia gharamakubwa wakati wa ufuatiliaji wa leseni hizo ,hali iliyowakatisha tamaa wachimbaji wengiya kuomba leseni.

    Naye Naamin Samuel ambaye nimchimbaji wa madini ya Gypsum kutokaSame, Kilimanjaro aliongeza kuwa baada yakupata elimu na kuanza kutumia hudumaza leseni za madini kwa njia ya mtandaowataweza kulipa fedha kwa wakati kupitia

    mitandao ya simu ikiwemo Airtel Money,M-Pesa na Tigo Pesa.

     Kwa upande wake Jumaa Ally ambayeni mchimbaji wa madini ya Tanzanite kutokaMirerani aliishauri Serikali kuendelea kutoamafunzo zaidi kwa wachimbaji wa madininchini kote ili waanze kutumia hudumahiyo.

    Alisema huduma ya leseni za madinikwa njia ya mtandao itapelekea Serikalikuwa na kumbukumbu sahihi ikiwa nipamoja na kukusanya fedha zaidi itokanayona kodi kwani wachimbaji wengi sasa

    wataweza kulipa kwa wakati.

    Wakati huohuo, akielezea manufaa yahuduma ya leseni za madini kwa njia yamtandao mtaalam kutoka Wizara ya Nishatina Madini, Kitengo cha Leseni CharlesGombe alisema mfumo huo utaongezauwazi na kasi ya utoaji wa leseni za madiniambapo wateja wataingiza maombi yaleseni wenyewe, hivyo kupunguza tatizo lamlundikano wa maombi kwenye ofisi zamadini.

    Aliongeza kuwa wateja na Serikaliwatakuwa na uhakika na maombiyatakayowasilishwa yakiwemo maombiya kuhuisha na kuhamisha lesenipamoja na kuwa na uhakika wa malipoyatakayofanyika kupitia mfumo huo.

    Aliendelea kusema kuwa watejawatapata taarifa za leseni zao kila wakatina kujua wanapotakiwa kufanya malipo yaleseni au watakapotakiwa kutuma taarifa zautendaji kazi.

    Kaimu Katibu MkuuWizara ya Nishati naMadini, Mhandisi NgosiMwihava (kulia) katikapicha ya pamoja nawataalamu waandamiziwa masuala ya Nishatiwa Benki ya Dunia,Natalia Kulichenko(katikati) na RichardHosier (kulia)wakimsikiliza KamishnaMsaidizi wa Umeme,Mhandisi InnocentLuoga (hayupo pichani)akizungumza wakatiwa mkutano wa kujadiliMpango wa UpanuziMradi wa Umeme

    Vijijini (TREEP).

    Baadhi ya Watendaji waWizara ya Nishati na Madinipamoja na taasisi zilizo chiniyake wakifuatilia madakuhusu mpango wa UpanuziMradi wa Umeme Vijijini(TREEP) iliyowasilishwa nawataalamu waandamiziwa masuala ya Nishati waBenki ya Dunia, NataliaKulichenko na Richard

    Hosier (hawapo pichani).Wa kwanza kushoto niKamishna Msaidizi waUmeme, Mhandisi InnocentLuoga akifuatiwa naMhandisi Victor Labaa.

    Huduma ya

    leseni za madini kwanjia ya mtandaoitapelekea Serikali kuwa nakumbukumbu sahihi ikiwa ni pamoja na kukusanya fedhazaidi itokanayo na kodi.

  • 8/20/2019 MEM 78 Online

    6/10

    6   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Zuena Msuya,

    Dar es Salaam

    Wizara ya Nishati naMadini imelikaribishaShirika la Maendeleola Ufaransa (afd)kuwekeza nchini

    katika miradi mbalimbali ya maendeleohususani umeme.

    Hayo yamebainishwa na KamishnaMsaidizi wa Nishati anayeshughulikiaumeme Mhandisi Innocent Luogawakati wa kikao cha pamoja na ujumbe

    wa afd waliofika Wizarani ili kufahamumaeneo mapya wanayoweza kuwekezapamoja na kufahamu maendeleo yamiradi waliyoifadhili.

    Luoga alisema wataalamu watafanyautafiti katika maeneo ambayo wanaonayanahitaji ufadhili na baada kujadilianana wafadhili ili kufahamu kama miradihiyo ni ya muda mrefu ama mfupi katikautekelezaji wake.

     “Tanzania bado ina maeneo mengiya kuwekeza ili kuwapatia watanzaniaumeme kutokana na kuwepo kwavyanzo mbalimbali vya nishati hiyo.”alisema Mhandisi Luoga.

    Mhandisi Luoga alisema miradiinayofadhiliwa na afd iko katika hatua

    nzuri ya utekelezaji ambapo baadhiya miradi hiyo inatarajiwa kukamilikamwanzoni mwa mwezi Septembamwaka huu ikiwemo ile ya kuimarishaupatikanaji wa huduma ya umeme kwa jiji la Dar es Salaam.

    Alisema mbali na miradi hiyo kwa jijila Dar es salaam, pia miradi mikubwa yaumeme ambayo ipo katika mpango waMatokeo Makubwa Sasa inayotarajiwakuboresha upatikanaji wa huduma yaumeme wa uhakika nchi nzima na kwakipindi cha muda mfupi.

    Kwa upande wake Meneja wa miradiendelevu ya umeme kutoka afd, MaitaneConcellon ameshauri kuwa miradiinayofadhiliwa na Wahisani imalizwe

    kwa wakati ili kutoa imani kwa wafadhilina kwamba wako tayari kuendelea kutoaufadhili kwa Serikali ya Tanzania.

    Aidha wametaka kuharakishwakwa maeneo ya ufadhili pindi maeneoyatakapopatikana ili kuweza kuwekeanamikataba ya namna ya kuitekeleza.

    Vilevile, Concellon amelipongezaShirika la Umeme Tanzania Tanescokwa kazi wanayofanya na kuishaurikuweka wazi mipango kazi yaoikiwemo masuala ya mikataba, na piawashirikiane na kampuni za mawasilinokama TTCL.

      Tayari afd imefadhili miradimbalimbali ukiwemo ule wa Geita- Nyakanazi ambapo pia inatarajiakufadhili miradi mingi zaidi ukiwemowa Tanzania - Zambia.

    Ufaransa kuendelea

    kufadhili miradi ya umeme

    Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika kikao cha pamoja na Ujumbe wa Shirika

    la Maendeleo la Ufaransa waliopo upande wa kushoto waliofika Wizarani kufahamu maendeleo yamiradi walioifadhili pamoja na kutaka miradi mipya ya kuifadhili.

    Wajumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (afd), mwenye nguo ya njano ni Meneja wamiradi endelevu ya umeme kutoka afd, Maitane Concellon na kulia kwake ni Dennis Munuve.

  • 8/20/2019 MEM 78 Online

    7/10

    7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Kitengo cha Leseni, Charles Gombe

    akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Afisa MadiniMkazi – Kilimanjaro kabla ya kuanza kwa uendeshaji wa mafunzo ya huduma zaleseni kwa njia ya mtandao. Mafunzo hayo yanahusisha wachimbaji wa madinilengo likiwa ni kuwapa uelewa wa matumizi ya huduma za leseni kwa njia yamtandao

    Baadhi ya wachimbaji wa madini kutoka wilaya ya Same mkoani Kilimanjarowakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na wataalam kutokaWizara ya Nishati na Madini

    Afisa Madini Mkazi -Mkoa wa Kilimanjaro, Fatuma Kyando akielezea sheria nakanuni za uchimbaji wa madini nchini katika mafunzo hayo

    Mmoja wa wachimbaji wa madini kutoka wilayani Same, mkoani KilimanjaroRichard Mbwambo akiuliza swali katika mafunzo hayo

    Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini (waliokaa mbele) wakiwa katikapicha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo (waliosimama nyuma).

    Mmoja wa wachimbaji wadogo, Naamin Samuel kutoka kampuni ya Kivoroi naNdarauoi akiuliza swali katika mafunzo hayo.

     

    MAFUNZO KWA WACHIMBAJI WA MADINI KUHUSU MATUMIZI YAHUDUMA ZA LESENI ZA MADINI KWA NJIA YA MTANDAO - MIRERANI

  • 8/20/2019 MEM 78 Online

    8/10

    8   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Afisa Madini Mkazi, Mkoa wa Kilimanjaro, Fatuma Kyando akielezeasheria na kanuni za uchimbaji wa madini nchini katika mafunzo ya sikumbili yaliyoshirikisha wachimbaji wa madini Mirerani . Lengo la mafunzohayo lilikuwa ni kuwapa uelewa juu ya huduma za Leseni kwa njia yamtandao.

    Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Kitengo cha Leseni Charles Gombe (kulia)akihakiki Leseni ya mmoja wa wachimbaji (katikati) Kushoto ni Afisa Madini katika Ofisiya Madini, Mirerani, Denis Mrengo

    Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini Alex Magayane (kushoto) akifunguamafunzo hayo.

    Mjiolojia katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi -Mirerani, Amir Chande Ramadhani (kushoto)na Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Kitengo cha Leseni Charles Gombe (kulia)

    wakifuatilia tovuti ya huduma za leseni kwa njia ya mtandao (online mining cadastretransactional portal) kwenye mafunzo hayo.

    Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini (kushoto) Pendo Elisha akitoa

    mada kwa wachimbaji madini (hawapo pichani) kuhusu namna ya kujiunga na huduma yaleseni kwa njia ya mtandao. Wa kwanza kulia ni Mhandisi Migodi katika Ofisi ya Afisa MadiniMkazi –Mirerani, Fedrick Phinius.

    Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwakwa nyakati tofauti.

     u

    MAFUNZO KWA WACHIMBAJI WA MADINI KUHUSU MATUMIZI YAHUDUMA ZA LESENI ZA MADINI KWA NJIA YA MTANDAO - MIRERANI

  • 8/20/2019 MEM 78 Online

    9/10

    9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    “OMCTP- Huduma za

    leseni Kiganjani Mwako”

    Wizara ya Nishati na Madini ilizindua mfumo wa Huduma za Leseni kwa

    njia ya mtandao tarehe 8 Juni, 2015. Uzinduzi huo ulifanyika baada yakipindi cha mwaka mzima wa maandalizi ya mfumo huo wa kielektronikiujulikanao kama Online Mining Cadastre Transactional Portal (OMCTP).Pamoja na malengo mengine, Mfumo huo umeanzishwa ili kutekelezaagizo la Serikali la kutaka Wizara na taasisi za Serikali ziwe zinapokeamalipo ya Serikali kwa njia za kielektroniki.Licha ya kuwawezesha wateja kufanya malipo ya leseni na mrabaha kwa njiaya kielektroniki, mfumo huo wa kielektroniki wa OMCTP utawawezeshawateja waliosajiliwa kutuma maombi ya leseni, kuhakiki taarifa za leseniwanazomiliki, kutuma taarifa za utendaji kazi na kadhalika. Aidha, Mfumowa OMCTP utawawezesha wateja kupata taarifa mbalimbali za sekta yaMadini zikiwamo ramani za kijiolojia na taariza za migodi mikubwa.

    1. UTARATIBU WA KUJISAJILI KATIKA MFUMO WA OMCTPIli kujisajili kwenye mfumo huo wa OMCTP, hatua zifuatazo

    zinahusika.

    1.1. Kujaza na Kuwasilisha Fomu ya Usajilia. Fomu ya kuomba usajili wa OTMCP zinapatikana kwenye tovuti ya

    Wizara au kwenye Osi ya Madini iliyo karibu na wewe. Jaza Fomuhizo kadiri ya maelekezo yaliyomo kwenye Fomu husika;

    b. Wamiliki wa leseni za madaraja A na B wawasilishe maombi yao katikaOsi za Makao Makuu ya Wizara (MEM HQ) wakiambatisha lesenihalisi pamoja na stakabadhi za malipo ya leseni husika kutokea lesenihusika ilipohuishwa kwa mara ya mwisho hadi wakati wa kuombausajili. Leseni zilizopatikana kwa njia ya sihia ziambatishwe na hatihalisi ya sihia (transfer certicate);

    c. Wamiliki wa leseni za madaraja C na D watahudumiwa kupitia osiza madini za mikoani (ZMO/RMO) zinazohusika na usimamizi waleseni husika. Maombi ya usajili yaambatane na leseni halisi pamojana stakabadhi za malipo ya ada kutokea leseni husika ilipohuishwa kwamara ya mwisho hadi wakati wa kuomba usajili. Leseni zilizopatikanakwa njia ya sihia ziambatishwe na hati halisi ya sihia; na

    d. Wamiliki wa leseni watakaotuma mawakala kwa ajili ya kujisajilina mfumo wa OTMCP, ni lazima wawape mawakala husika nguvuza uwakili (Power of Attorney) za kuwaruhusu mawakala husikakushughulikia leseni. Hati halisi ya Nguvu za Uwakili ziwasilishwepamoja na fomu ya kuomba kujisajili kwenye mfumo wa OMCTP.

    e. Wadau wengine ambao hawamiliki leseni, na wangependa kusajiliwa,wawasilishe fomu a usajili pamoja na hati za utambulisho katika Osiya Wizara au Katika osi za Madini za Kanda au Osi za Madini zaWakazi.

    1.2. Uhakiki wa Taarifa Katika Osi ya MadiniMwombaji anapaswa kushiriki katika uhakiki wa taarifa za leseni

    zilizowasilishwa pamoja na maombi ya usajili kama ifuatayo:-a. Asa wa leseni atakuwa na muhtasari wa taarifa za leseni husika

    kutoka kwenye masjala ya leseni (MCIMS) utakaoonesha wamiliki waleseni, malipo ya ada, taarifa zilizopokelewa, nk ili kuoanisha na taarifazilizowasilishwa na mwombaji;

    b. Asa wa leseni atahakiki taarifa za leseni husika na kuhuisha taarifaambazo zinahitajika ikiwa ni pamoja na taarifa za malipo ya ada;

    c. Pindi taarifa za leseni zote za mwombaji zitakapohuishwa kwenyemasjala ya mfumo wa MCIMS, ombi husika la usajili litashughulikiwa.Aidha, mwombaji husika atajulishwa kama kuna mapungufu katikataarifa alizowasilisha na kutakiwa awasilishe upya;

    1.3. Kusajiliwa kwenye Mfumo wa OMCTPa. Asa wa Leseni atamsajili mmiliki wa leseni kuwa mtumiaji wa

    OTMCP baada ya kupokea ombi la usajili na kufanya uhakiki wa taarifaza leseni za mmiliki Mwombaji;

    b. Mwombaji aliyekamilisha usajili kwenye mfumo wa OMCTP atapokeaujumbe wa barua pepe au ujumbe mfupi wa simu (SMS) kuthibitishausajili wake; na

    c. Kabla ya kuanza kutumia huduma ya leseni kupitia mfumo wa OMCTP,msajiliwa atatakiwa kubadilisha namba yake ya siri (password).

    Huduma ya Usajili wa OMCTP inatolewa katika osi ya makao makuu yawizara na kwenye osi 21 za mikoani (RMO na ZMO). Aidha, osi mpyanne zitaanza kutoa huduma hiyo katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

    Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava,akiongea na baadhi ya washiriki wa kikao kazi kilichojadili namna Sekta

    Binafsi, Taasisi za Kifedha na Washirika wa Maendeleo wanavyowezakushirikiana na REA ili kuongeza kasi ya kuviunganisha vijiji na umeme.

    FUATILIA  Kipindi Maalum- Ewura na Uchumi

    Tarehe 3 Agosti, saa 3:00 – 4:00 usiku, Star TV

     Tarehe 5 Jumatano saa 4:00 usiku – 5:00 usiku, TBC1

    Vilevile usikose Mahojiano kuhusu Wakala wa Jiolojia Tanzania(GST) tarehe 3 Agosti, 2015 katika kipindi cha Jambo Tanzania

    TBC1

  • 8/20/2019 MEM 78 Online

    10/10

    10   BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    1.1.1. Utafutaji na Uendelezajiwa Sekta Ndogo ya Mafuta naGesi Asilia Nchini

    Mikataba ya Utafutaji Mafutana Gesi Asilia :Katika kipindi cha2005 – Juni 2015, Serikali ilielekeza

     juhudi za utafutaji mafuta na gesiasilia kwa kuvutia wawekezajikatika kina kirefu baharini namabonde ya ufa. Kwa mara yakwanza Serikali ilitoa leseni zautafutaji mafuta na gesi katikamabonde ya Ziwa Tanganyikakusini, Malagarasi, Kilosa-Kilombero, Pangani, Ruhuhu,Kyela na Tanga. Katika kipindihicho, Serikali ilisaini mikataba26 ya uzalishaji na ugawanajiwa mapato (Production SharingAgreements - PSAs). Idadi hiyoni kubwa ikilinganishwa namikataba 13 iliyosainiwa kati yaMwaka 1952 hadi 2004. Idadihiyo ni asilimia 65 ya mikatabayote 37 iliyosainiwa tangu kuanzashughuli za utafutaji wa mafutanchini Mwaka 1952.

    (i) Ukusanyaji wa Takwimuza Miamba Mitetemo

    (Seismic):Katika kipindi chaMwaka 2005 hadi 2015 TPDCikishirikiana na kampuni zautafutaji mafuta ilifanikiwakukusanya takwimu zamitetemo (2D seismic) za

     jumla ya kilomita 54,978 nakilomita za mraba 34,486 za3D seismic. Takwimu hizozimeweza kuvutia wawekezajikwa wingi na kuongeza kasi yautafutaji wa mafuta nchini.

    (ii) Uchorongaji Visima vyaUtafutaji Mafuta:Katikakipindi cha Mwaka 2005hadi Juni, 2015 idadi ya

    visima vilivyochorongwavilikuwa 45 ambavyo ni sawaasilimia 56 ya visima vyote 90vilivyochorongwa nchini hadisasa. Kati ya hivyo, visima 35viligundulika kuwa na gesi.Idadi hii ni kubwa kwa kipindihiki kuliko wakati mwinginewowote katika historia yautafutaji wa mafuta na gesi hapanchini. Wastani wa uchimbajivisima kati ya Mwaka 1952 na

    Mwaka 2004 ulikuwa chini yakisima kimoja (1) kwa mwaka.Wastani huo kwa kipindi chaMwaka 2005 na Mwaka 2014ulifikia visima 5 kwa mwaka.

    (iii) Ugunduzi wa GesiAsilia:Katika kipindi chaMwaka 2005 hadi 2015,Serikali imepata mafanikiomakubwa ambapo gesi asiliailigunduliwa nchi kavu katikamaeneo ya Mkuranga Mwaka2007, Nyuni Mwaka 2008 naNtorya Mwaka 2012. Aidha,ugunduzi wa kwanza wa gesikatika kina kirefu bahariniulifanyika Mwaka 2010 katikakitalu namba 4 (Kisima chaPweza -1). Kisima hichokilichochea juhudi za Serikaliya Awamu ya Nne katikautafutaji wa mafuta na gesi

     baharini ambapo hadi June,2015 visima 34 vilichorongwa.Hadi kufikia Septemba, 2005gesi asilia iliyogunduliwa nchiniilikuwa ni futi za ujazo trilioni(TCF) 8. Katika kipindi chaMwaka 2005 hadi 2015, hazinaya gesi asilia iliongezeka hadikufikia futi za ujazo trilioni

    55.08 Ongezeko hili ni sawana asilimia 558.8 ya hazinailiyokuwepo Mwaka 2005.

    (iv) Uboreshaji wa MikatabaKifani (Model ProductionSharing Agreements - MPSAs):Serikali iliboresha MikatabaKifani (MPSAs) ili kuhakikishakuwa mikataba hiyo inawianana vivutio vya utafutaji mafutana gesi nchini, mwenendo waupatikanaji mitaji ya utafutajimafuta na gesi duniani na piainawezesha Taifa kupata patostahiki. MPSA ya Mwaka 2004iliboreshwa na kupata MPSA

    ya Mwaka 2008 ambayo piailiboreshwa na kupata MPSAya Mwaka 2013. MPSAhiyo ndiyo inatumika kuingiamikataba ya utafutaji, uzalishajina ugawanaji mapato.

    (v) Kufanyika kwa Duru yaNne ya Kunadi Vitalu vyaUtafutaji wa Mafuta na Gesikatika Kina Kirefu cha MajiNchini:Uzinduzi wa Duru

    ya Nne ya kuitisha zabuniza utafutaji mafuta (FourthPetroleum Licensing Round)kwenye vitalu saba (7) katikaBahari Kuu na kimoja (1)kwenye Ziwa TanganyikaKaskazini ulifanyika hapanchini Mwezi Oktoba, 2013.Katika uzinduzi huo MkatabaKifani 2013 ulitumika.Uzinduzi ulifanywa rasmina Mhe. Dkt. Jakaya MrishoKikwete, Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania.Duru hii ya nne ilikuwa niduru ya kwanza kufanyikanchini baada ya duru nyinginetatu kufanyika nje ya nchi.Kufanyika kwa duru hiihapa nchini kumetoa fursakwa Watanzania kuongezauelewa na kubainisha maeneombalimbali wanayowezakushiriki katika Sekta Ndogoya Mafuta na Gesi Asilia.

    (vi) Mradi wa Ujenzi waMiundombinu ya Gesi Asilia:Mwezi Septemba, 2011Serikali kupitia TPDC ilisainiMkataba wa Usanifu, Ununuzi

    na Ujenzi yaani Engineering,Procurement and Construction(EPC) na “China PetroleumTechnology and DevelopmentCorporation (CPTDC)” kwaajili ya ujenzi wa bomba namitambo ya kusafisha nakusafirisha gesi asilia.

      Mwezi Juni, 2012 Serikali ilisainimakubaliano ya mkopo nafuuna Benki ya Exim ya Chinakwa ajili ya kugharamia ujenziwa mitambo ya kusafisha gesiasilia na bomba la kusafirishagesi asilia kutoka Mnazi Bay- Mtwara na Songo SongoKisiwani (Lindi) hadi Dar es

    Salaam lenye urefu wa kilomita542. Gharama za mradi huoni Dola za Marekani milioni1,225.3, sawa na Shilingi trilioni1.96. Ujenzi wa Bomba hiloumekamilika kwa asilimia 100.Hadi sasa ujenzi wa nyumbaza wafanyakazi katika eneo laSongo Songo Mkoani Lindina MadimbaMkoani Mtwaraumekamilika kwa asilimia100; Mitambo ya kuchakata

    gesi iliyoko Madimba naSongoSongo hadi July, 2015imekamilika kwa asilimia 98.

    (vii) Ukamilishaji wa Visimavya Uzalishaji na Ujenzi waMiundombinu na Matumiziya Gesi Mnazi Bay:visimavinne vya uzalishaji gesi asiliavilivyopo Mnazi Bay Mtwaravilikamilishwa kati ya Mwaka2006 na 2007. Pia, ujenzi wamitambo ya kusafisha gesi asiliayenye uwezo wa kusafisha hadi

    futi za ujazo milioni 10 kwa siku(10 mmscfd) ulikamilishwa.Bomba lenye urefu wa kilometa27 na uwezo wa kusafirisha gesihadi futi za ujazo milioni 70kwa siku (70 mmscfd) kutokaMnazi Bay hadi Mtwara Mjinililikamilika. Mtambo wa kufuaumeme ulisimikwa MtwaraMjini na ufuaji umeme kwakutumia gesi ya Mnazi Bayulianza Mwaka 2006. Vilevile,miundombinu ya kusafirishiaumeme kutoka Mtwarakwenda miji ya Lindi na Masasiilikamilika. Kupitia Mradihuo Miji ya Mtwara, Lindi naMasasi inapata umeme wauhakika tangu Mwaka 2006mradi huo ulipoanza, ambapomatumizi ya gesi kwa siku nifuti za ujazo milioni mbili (2mmscfd).

    (viii) Matumizi ya Gesi AsiliaViwandani, Majumbanina kwenye Magari: Miradimbalimbali ilitekelezwa ilikuhakikisha kuwa gesi asiliainawafikia watumiaji wadogowa viwandani, majumbani,

    kwenye taasisi na watumiajiwa magari katika Jiji la Dar esSalaam. Kabla ya Mwaka 2005kulikua na viwanda viwili (2)tu vilivyokuwa vinavyotumiagesi asilia. Kati ya Mwaka2005 na Juni, 2015 viwanda 38,nyumba 70, Gereza la Keko,hoteli kubwa moja (Serena)viliunganishwa kutumia gesi namagari 60 yaliwekewa mifumoya kutumia gesi asilia.

    Taarifa ya Mafanikio Shirika la

    Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

    Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandaoya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya ‘Nishati na Madini’ Karibu tuhabarishane na

    tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini