MEM BULLETIN 74.pdf

download MEM BULLETIN 74.pdf

of 14

Transcript of MEM BULLETIN 74.pdf

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    1/14

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali

    kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizar a ya Nishati na MadiniWasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263

    au Fika Osi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    HABARI ZA

    NISHATI &MADINI

    Toleo No. 74 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Julai 3 - 9, 2015Bulletinews

    http://www.mem.go.tz

    SomahabariUk.2

    Hasara za kutokupitishwa miswada

    ya sheria za Petroli, Teiti hizi hapa;

    Hasara za kutokupitishwa miswada

    ya sheria za Petroli, Teiti hizi hapa;Maamuzi ya kuwekeza katikanchi huangalia mfumo wakisheria wa nchi hususani sheriaza sekta husika, na kwa kuwa nchiimeshaandaa miswada ya sheriazinazohusiana na mafuta na gesiasilia, kusitisha kuzipitisha sheriahizo kwa sasa kutaathiri mipangoya majadiliano kuhusu uendelezajiwa gesi asilia iliyogunduliwa

    baharini kwa kuwa wawekezajiwengi watasubiri kuona sheriampya ili kufanya maamuzi ya

    uwekezaji.

    Utekelezaji wa miradiinayofadhiliwa na MCC(Compact II) utakwama kwavile sharti moja wapo ni uwepowa sheria ya gesi asilia, kwa vilemuda wa mwisho wa Bodi yaMCC kupitisha miradi hiyo nimwezi Septemba, 2015.

    Kupoteza fursa ya mabadiliko(window of change) ambayoipo kwa sasa. Serikali iliyopomadarakani ina nia thabiti yakuona mabadiliko ya kweli yakisheria kwenye sekta ya mafutana gesi asilia.

    Kutachelewesha utekelezaji wampango kabambe wa matumiziya gesi asilia nchini kwenye

    uzalishaji wa umeme, viwandani,majumbani na kwenye magari.Matumizi haya yanatarajiwakuleta mapinduzi ya kiuchuminchini.

    Kukosekana kwa sheriainayosimamia masuala ya uwazikwenye sekta ya uziduaji (mafuta,gesi asilia na madini) kamaambavyo ingekuwa baada yakupitishwa kwa sheria.

    Itakumbukwa kuwa, 16 Juni, 2015, Serikali iliwasilisha miswada miwili ya (Petroleum na TEITI) ili kuomba Bunge lijadili na kuweza kupitisha kwa ajili yakusimamia shughuli za mafuta na gesi asilia na uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uziduaji.

    Muswada wa sheria umejumuishamasuala mengi yaliyokuwakwenye mikataba, na kuachamasuala machache yatakayohitajimajadiliano. Muswada huu

    usipopitishwa kuwa sheriavipengele hivyo vitaendeleakujadiliwa kwenye mikataba.

    Muswada wa sheria unaanzishamdhibiti (PURA) atakayesimamiashughuli zote za utafutaji na

    uzalishaji wa mafuta na gesiasilia, ambaye hatakuwepo ikiwakazi hizi zitatekelezwa na sheriailiyopo.

    Muswada wa sheria umewekamazingira yatakayowezeshawazawa kushiriki kikamilifukatika shughuli za mnyororowa thamani katika tasnia yamafuta na gesi asilia. Fursa hiiitacheleweshwa hadi tuwe nasheria na kanuni muafaka.

    Muswada wa sheria umejumuisha masuala mengi yaliyokuwa kwenye mikataba, na kuacha masualamachache yatakayohitaji majadiliano. Muswada huu usipopitishwa kuwa sheria vipengele hivyovitaendelea kujadiliwa kwenye mikataba.

    Bandari ya Tanga kuanzakushusha mafuta

    1 2

    6

    5

    3

    7

    4

    8

    9

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    2/14

    2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Bandari ya Tanga kuanza kushusha mafuta

    Na Asteria MuhozyaTanga

    Kufuatia kuongezeka kwakiwango cha mafutayanayoingizwa nchini kupitia

    mfumo wa Uagizaji waMafuta wa Pamoja nchini

    (BPS), bandari ya Tanga itakuwa ya pilikupokea shehena ya mafuta kwa kutumiamfumo huo, baada ya Wizara ya Nishatina Madini kuona umuhimu wa kuwa namiundombinu mingine nje ya Jiji la Dar esSalaam.

    Hayo yameelezwa na Waziri wa

    Nishati na Madini, George Simbachawenewakati wa kikao baina yake na Uongoziwa Mkoa wa Tanga, Taasisi za Serikalizinazoshughulika na masuala ya mafutana wadau wa mafuta mkoani Tanga hivikaribuni, kabla ya kukagua bandari yaTanga na miundombinu ya kuhifadhi

    mafuta katika Bohari ya kampuni ya GBPna kampuni ya TSN group wamiliki wabohari ya TAPCO.

    Akizitaja faida za kutumia bandari hiyoalieleza kuwa, ni pamoja na kuongezekakwa uhakika wa upatikanaji na usambazajimafuta, kupunguza msongamano uliopokwa kutegemea Bandari ya Dar es Salaam,kupunguza gharama za usambazaji

    mafuta ikiwemo pia kukuza uchumi waMkoa wa Tanga na hivyo kuchangia zaidi

    katika Pato la taifa.Simbachawene alisema hiyo ni fursanzuri kwa serikali na kueleza kuwa,itashirikiana kwa karibu na wadau wotewalio tayari kufanya kazi katika sekta hiyo,na hivyo kuutaka mkoa huo kuipokeashughuli hiyo kikamilifu kwani ni sehemuya mafanikio ya mkoa huo kiuchumi.

    Simbachawene aliongeza kuwa,uwepo wa fursa ya bandari ya Tangautasaidia kukuza uchumi, hivyo kuzitakaIdara na Taasisi za serikali zinazohusikana masuala hayo kutoa ushirikiano kwamkoa huo ili kuweza kufikia malengotarajiwa. Wizara itakuwa karibu sana namkoa wa Tanga katika suala hili, Idarana taasisi zinazohusika tushirikiane kwa

    karibu zaidi, alisema Waziri.Vilevile, Simbachawene alisema

    shughuli ya uhifadhi wa mafuta itaanzakwa kutumia miundombinu ya bohariza kampuni ya GBP zenye uwezo wakuhifadhi lita milioni 26, wakati bohariza mafuta za kampuni nyingine zitafuatabaadae baada ya kukamilika kwa kazi yakuzifanyia tathmini ili kujiridhisha kuhusuuwezo wa kuhifadhi mafuta.

    Aidha, Waziri alichukua fursa hiyokukipongeza kikosi kazi cha wataalamukutoka Wizara ya Nishati na Madini,EWURA, PICL, TRA TBS, GAPCO,GBP na AGUSTA Energy kwa ajiliya kukamilisha taratibu za kuiwezeshabandari ya tanga kupokea shehena yamafuta mwezi Julai.

    Akizungumza katika kikao hicho,Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalulaalieleza namna kila mdau alivyopangakufanya kazi ili kutekeleza jambo hilokwa ufanisi na kuongeza kuwa, Mkoaumejipanga vizuri na zoezi la upakuajimafuta na kueleza kuwa, litafanyikakikamilifu.

    Waziri, tayari mkoa umejipangakujua nani atafanya nini katika zoezizima la kushusha mafuta baada ya meliya kwanza kuwasili hapa. Tunajua faidatutakazopata kutokana na shughuli hizikufanyika, hivyo mkoa upo tayari kupokeamafuta, alisema Magalula.

    Naye Mkurugenzi mtendaji waKampuni ya GBP, Badar Masoudaliipongeza Wizara kwa jitihada zakuwakutanisha wadau wa mafuta katikautaratibu huo na kueleza kuwa, ni uamuziutakaosaidia kukuza uchumi wa jiji hilo.

    Badar aliongeza kuwa, kampuniyake imepanga kuendelea kuboreshamiundombinu ya uhifadhi mafutakwa kuweka vifaa vya kisasa na hivyo

    kuipongeza Serikali kwa kukubali kuifanyabandari ya Tanga kuwa ya pili nchini kwakupokea mafuta.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni GBP ya Tanga, BadarMasoud (katikati), akimwongoza Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene, (kulia) kutembelea Bandari ya Tangaitakayotumika katika shughuli za kushusha mafuta jijini humo.Wengine nyuma ni wadau wa Mafuta Tanga, Taasisi za Serikalizinazoshughulika na masuala ya mafuta na Uongozi wa Mkoawa Tanga.

    Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene (wa pili kushoto) akikaguamiundombinu ya kuhifadhi mafuta katika Bohari ya Kampuni ya GBP ya Tanga.Nyuma ya Waziri ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula. Wengine kutoka kulia niMeneja Mkuu wa PICL, Michael Mjinja, Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya PetroliWizara ya Nishati na Madini, Mhandisi, Hosea Mbise na Mkurugenzi Mtendaji wa

    Kampuni ya GBP ya Tanga, Badar Masoud. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa GBP, Boharihiyo ina uwezo wa kuhifadhi lita milioni 26 za mafuta.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari ya GBP ya Tanga, Badar Masoudakimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawenewakati akikagua miundombinu ya kuhifadhi mafuta katika Bohari yaKampuni ya GBP , Tanga. Wengine katika picha ni Baadhi ya watendajiwa Wizara na wadau wa mafuta mkoa wa Tanga zikiwemo Taasisi zaSerikali.

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    3/14

    3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Tahariri

    MEM

    Na Badra Masoud

    FIVEPILLARS OFREFORMS

    KWA HABARI PIGA SIMUKITENGO CHA MAWASILIANO

    BODI YA UHARIRI

    MHARIRI MKUU:Badra MasoudMSANIFU: Essy Ogunde

    WAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya, GreysonMwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James

    na Nuru Mwasampeta

    INCREASE EFFICIENCY

    QUALITY DELIVERYOF GOODS/SERVICE

    SATISFACTION OFTHE CLIENT

    SATISFACTION OFBUSINESS PARTNERS

    SATISFACTION OFSHAREHOLDERS

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Karibuni wawekezajimuwekeze katika umeme!!

    Wiki hii Tanzania ilipokea ujumbe wa wafanya-biashara wa Makampuni zaidi ya 30 kutokanchini Korea wakiwa wamefuatana na wa-tendaji wa Serikali ya nchi hiyo lengo likiwani kutafuta maeneo mbalimbali ya uwekezaji

    ikiwamo sekta ya nishati ya umeme.

    Ujumbe huo wa Korea uliwakutanisha wadau katika sektambalimbali ambapo walitaka kupata taarifa ya fursa zilizopokatika sekta za gesi, mafuta na umeme ambapo miongoni mwataarifa zilizotolewa katika ujumbe huo kutoka Korea ni fursazilizopo katika uwekezaji katika sekta ya nishati ya umeme.

    Kama tunavyoelewa kwamba nishati ya umeme ni muhimukatika kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa letu nauwekezaji katika sekta hiyo unahitaji mitaji mikubwa kutokanana gharama zake kuwa kubwa hivyo ni wajibu wetu kuwavutiawawekezaji wa ndani na nje ya nchi kushirikiana na Serikalikupitia TANESCO kuwekeza katika umeme pamoja na miun-dombinu yake.

    Kama tunavyoelewa nchi yetu imebarikiwa kuwa na vyan-zo vingi vya umeme ambavyo ni pamoja na maji, gesi, makaa

    ya mawe, joto ardhi, jua, upepo, bayogesi n.kTutakumbuka kwamba Tanzania ilitunga sera ya uwekezajikwa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi mwaka 2009,sera hiyo ilifuatiwa na sheria ya (PPP-Public Private Petner-ship) mwaka 2010 ambayo baadaye mwaka 2014 ilifanyiwamarekebisho.

    Lengo kubwa la sera na sheria hii ya PPP ilikuwa ni ku-wavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katikamiradi mikubwa na ya kimkakati kama ya umeme hususankatika ujenzi wa mitambo ya kuzalisha, kusafirisha na kusam-baza umeme.

    Kwa sasa Wizara inayo miradi mingi ambayo ipo katikamipango ya kuendeleza sekta ndogo ya umeme lakini kuto-kana na upungufu wa bajeti ya kutosha katika kutekeleza mi-

    radi hiyo hivyo, inatubidi tuingie ubia na sekta binafsi katikakutekeleza miradi hiyo.Hivyo, basi hatuna budi kuitangaza na kuwavutia wawekeza-

    ji kuingia ubia na TANESCO katika kuwekeza kwenye miradiyote ya umeme ambayo inahitaji wabia ili miradi hiyo iwezekutekelezeka kwa maslahi ya taifa letu.

    Tunawakaribisha wawekezaji mbalimbali kuja nchini ku-wekeza katika miradi ya umeme kwani mazingira ya uwekeza-ji ya nchi yetu ni mazuri kwa uwekezaji hususan utulivu naamani.

    Kwa moyo mkunjufu tunawakaribisha wawekezaji Tan-zania waje tushirikiane katika kuendeleza sekta ya umemeambayo ndiyo mhimili na kichocheo kikubwa katika kukuzauchumi wa taifa la Tanzania na watu wake.

    TEL-2110490

    FAX-2110389

    MOB-0732999263

    Na Greyson Mwase,Dar es Salaam

    Wizara yaNishati naMadini naTaasisi zakeimeendelea

    kungara katika maonesho yakimataifa ya Saba Saba ( Dar esSalaam International Trade Fair)yanayoendelea katika viwanjavya Mwalimu Nyerere jijini Dares Salaam na kuwa kivutio chawananchi wengi.

    Maonesho hayo yaliyoanzaJuni 28, 2015 na kutarajiwakumalizika Julai 07, 2015,yaliiwezesha Wizara kutumiafursa hiyo kutangaza fursa zauwekezaji nchini katika sekta zanishati na madini.

    Wageni waliotembelea bandahilo ni pamoja na ujumbe wawawekezaji na wafanyabiasharawa nishati kutoka Korea ambapowalisema kuwa wamebaini fursanyingi katika sekta ya nishati nakuahidi kuendelea kujifunzafursa hizo na kuwekeza.

    Akizungumza katikamahojiano maalum mmojawa wafanyabiashara haoambaye ni Makamu wa Raiskatika kampuni ya Energyand Minerals ResourcesDevelopment Associations yaKorea Dk. Song Jae Ki alisemakupitia maonesho ya sabasabawamejifunza fursa nyingihususan katika sekta ya nishati.

    Dk. Jae Ki alisemawamebaini kuwa nchi ya

    Tanzania ina vyanzo vingivya nishati ya umeme ambapoikiwa wawekezaji wengiwatahamasishwa kuwekezakatika vyanzo hivyo, taifa laTanzania linaweza kupiga hatuakubwa kiuchumi.

    Aliongeza kuwa Tanzania ninchi yenye amani na salama kwauwekezaji na kuahidi kutangazafursa hizo kwa wawekezajiwengine ili kukuza uchumi wanchi.

    Wakati huo huo wakazikutoka jijini Dar es Salaamwakizungumza kwa nyakatitofauti walipongeza Wizaraya Nishati na Madini kwa

    juhudi zakekatika kuelimisha

    umma hususankupitia maonesho

    mbalimbali ya kitaifa.Antony Lyimo mkazi wa

    jijini Dar es Salaam alisemaamejifunza fursa mbalimbalipamoja na taratibu za kufuatakatika uwekezaji wa madini.

    Alisema wananchi wengihawakuwa na uelewa wa taratibuza kufuata katika uendeshaji washughuli za madini ikiwa nipamoja na uombaji wa leseni nautunzaji wa mazingira.

    Wananchi wengi tulikuwahatuna uelewa wa taratibuza kuomba leseni, lakini sasatunaweza kuomba leseni wakatiwowote, alisisitiza.

    Naye Ramsey Yusuphalipongeza jitihada za Wizarakatika kuboresha huduma zaleseni kwa kuanzisha mfumo wamtandao ambao unawezeshawateja kupata huduma zaleseni kupitia mtandao badala yakufunga safari hadi ofisini.

    Aliongeza kuwa, mfumohuo utapunguza rushwa namalalamiko ya kucheleweshewaleseni.

    Mtaalam kutoka Idara ya Madini Mhandisi Rayson Nkya(Katikati) akimwonesha Makamu wa Rais wa Kampuni yaEnergy and Minerals Resources Development Associationya Korea, Dk. Song Jae Ki (Kulia) moja ya machapishoya Wizara ya Nishati na Madini kwenye Maonesho yaKimataifa ya Sabasaba (Dar es Salaam International Trade

    Fair; DITF) yanayoendelea katika viwanja vya MwalimuNyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Godfrey Fwenikutoka Idara ya Madini ya Wizara.

    Nishati na Madini yangara maoneshoya kimataifa ya Sabasaba

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    4/14

    4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akisalimiana na baadhi yawananchi wa Kijiji cha Chogola, wilaya ya Mpwapwa wakati wa ziara yake yaKukagua Utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini, inayofadhiliwa na Wakala waNishati Vijijini (REA) na kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO).

    Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Chogola, Wilaya ya Mpwapwa wakishangiliajambo, wakati Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akihutubiakatika mkutano huo wakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Miradi yaUmeme vijijini inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwana Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO).

    Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Wilaya ya Mpwapwa, LawrenceKateba akiongea jambo wakati ziara ya Waziri wa Nishati na Madini, George

    Simbachawene akikagua Utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini , Awamu ya Pili, inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwa na Shirika laUmeme Nchini, (TANESCO).

    Simbachawene awatoa hofuwananchi tozo ya mafuta

    Na Asteria Muhozya, Mpwapwa

    Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ame-waeleza wananchi umuhimu wa tozo iliyoongezwa katikamafuta ya petroli na dizeli na kueleza kwamba ina umuhimumkubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kusaidia us-ambazaji wa umeme ambapo mahitaji ya nishati hiyo ni

    makubwa.Simbachawene aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano

    wake na wananchi wa Kijiji cha Chogola, Kata ya Masa, Wilayani Mpwapwawakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijiji-ni, Awamu ya Pili inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) nakutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).

    Simbachawene aliongeza kuwa, fedha hizo zinatarajiwa kutekeleza mi-radi mingi zaidi ya umeme kwani, kadri miaka inavyosonga ndivyo mahitajimakubwa ya nishati hiyo yanayozidi kuongezeka.

    Alisema kuwa, Serikali imetangaza kuongeza tozo ya mafuta ya petroli

    na dizeli ili fedha zitakazopatikana kwenye tozo hiyo zitunishe Mfuko wakusambaza umeme vijijini na kuongeza kuwa, tozo ya mafuta imepanda ku-toka sh 50 kwa lita hadi 100 kwa lita, ikiwa ni ongezeko la sh 50 kwa lita.

    Aidha, Simbachawene alitumia fursa hiyo, kuwaomba Wabunge wa Jam-huri ya Muungano wa Tanzania kukubali kuijadili miswada ya Mafuta nagesi Asilia katika kipindi hiki kabla ya Uchaguzi Mkuu na kueleza kuwa,sheria ya Petroli ya mwaka 1980 na 2008 hazitoshi kuwaongoza wataalamhivyo uwepo wa sheria mpya ni muhimu kwa kuwa, zitasaidia kuwaongozawataalamu kutengeneza mikataba katika sekta ndogo ya gesi asilia na mafuta.

    Hakuna dhamira mbaya, wananchi wanahitaji maendeleo kupitia ra-silimali hizi. Wabunge turudi bungeni tutunge sheria kuhusu masuala haya.Tutapoteza fursa ya kuingia katika soko. Sheria ina michakato, tumezingatiahayo na tumeshirikisha wadau, alisisitiza Simbachawene.

    Katika hatua nyingine, Simbachawene amesema kuwa, Serikali imefanyakazi kubwa katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Kusambazaumeme vijijini na kuongeza kuwa, miradi ya umeme ni endelevu na hivyokuwataka wananchi ambao hawajafikiwa na huduma hiyo kuwa wavumilivu.

    Maendeleo ni mchakato, Serikali imefanya kazi kubwa kupeleka umemevijijini, zoezi hili litaendelea kwa awamu kwasababu si rahisi jambo hili ku-fanyika kwa mara moja,alisisitiza Simbachawene wakati akiwahutubia wa-nanchi wa Kijiji cha Chipogoro, Wilayani Mpwapwa.

    Aidha, aliwataka wananchi kuwa wavumilivu na changamoto hiyo yanishati ya umeme na kueleza kuwa, tatizo hilo lipo karibu kuisha kutokanana ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi asilia (50.5tcf) ambacho kitasaidiakuzalisha nishati hiyo na ziada kuuzwa ili kusaidia katika kuimarisha uchumiwa nchi.

    Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene , akiwahutubia wananchi

    wa Kijiji cha Chogola wakati wa ziara yake ya Kukagua Utekelezaji wa Miradi yaUmeme Vijijini, Awamu ya Pili, inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini nakutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    5/14

    5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Meneja Mradi wa Kituo cha KuzalishaUmeme wa gesi cha Kinyerezi-1,Mhandisi Simon Jilima wa Tanescoakitoa maelezo kuhusu maendeleoya ujenzi kwa ujumbe kutoka Serikaliya Msumbiji. Ujumbe huo ulikuwanchini hivi karibuni kujifunza jinsiSerikali ya Tanzania inavyotekelezakwa ufanisi miradi ya kipaumbeleiliyoko chini ya Mpango wa MatokeoMakubwa Sasa (BRN).

    Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu kutoka Serikali ya Msumbiji, Bi. CristinaMatuse ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Tume ya Mipango ya Msumbiji,akitoa neno la shukrani baada ya kutembelea mradi wa umeme waKinyerezi-1 ambapo aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutekeleza mradihuo mkubwa kwa fedha za ndani.

    ZIARA YA UJUMBE WA SERIKALI YA MSUMBIJI

    KINYEREZI I, JIJINI DAR ES SALAAM

    u

    u

    Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa UmemeNchini (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mrambaakifafanua jambo kuhusu uendeshaji wa kituo chaumeme wa gesi Kinyerezi utakavyoendeshwa kisasawakati wa ziara ya wajumbe wa Serikali ya Msumbiji.

    Kaimu Meneja wa Kampuni Tanzu ya Usambazaji waGesi (GASCO), Mhandisi Kapuulya Musomba akiwaelezawageni kutoka Msumbiji kuhusu usambazaji wa gesi kwaajili ya mitambo ya umeme ya Kinyerezi.u

    PICHA ZOTE KWA HISANI YA KITENGO CHA MAWASILIANO PDB PICHA ZOTE KWA HISANI YA KITENGO CHA MAWASILIANO PDB

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    6/14

    6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Baadhi ya Viongozi wa Dini katika Kijiji cha Chogola wakimwombea Waziri wa

    Nishati na Madini, George Simbachawene wakati wa ziara yake ya kukaguaUtekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini (REA), inayofadhiliwa na kutekelezwa naShirika la Umeme Nchini (TANESCO), katika kijiji hicho.

    Waziri wa Nishati na Madini akipokea zawadi ya Silaha za Jadi kutoka kwa baadhiya viongozi wa kijiji cha Chogola, ikiwa ni ikiwa ni ishara ya uongozi. Viongozi haowalitoa zawadi hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Miradi yaUmeme Vijijini, Awamu ya Pili, inayotekelzwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)na kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini,

    Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene akipokea zawadi ya Bibliakutoka kwa baadhi ya Viongozi wa Dini katika Kijiji cha Chogola wakatialipotembelea Kijiji hicho wakati wa ziara ya kukagua Utekelezaji wa Miradi ya

    Umeme Vijijini inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwa naShirika la Umeme Nchini, (TANESCO).

    Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati, Mhandisi Sosthenes Masollaakiwaelimisha wananchi Kijiji cha Chogola kuhusu masuala ya Madini, wakati ziaraya Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akikukagua Utekelezaji waMiradi ya Umeme Vijiji, Awamu ya Pili, inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini(REA) na kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO).

    Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Kanda ya Kati, MhandisiDeogratius Ndamgoba, akiongea jambo na wananchi wa Kijiji cha Kijiji chachogola wakati ziara ya Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene

    akikukagua Utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijiji , Awamu ya Pili, inayofadhiliwana Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini,(TANESCO). Wengine wanaomsikiliza ni watumishi wa TANESCO Dodoma na Ofisi

    Baadhi ya Watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Ofisi ya MadiniKanda ya Kati na wananchi wa Kijiji cha Chogola wakimsikiliza Waziri wa Nishatina Madini, George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akiwahutubia wakati

    wa ziara yake ya Kukagua Utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini, Awamu ya Pili,inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini na kutekelezwa na Shirika la UmemeNchini (TANESCO).

    ZIARA YA WAZIRI DODOMA

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    7/14

    7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Mhandisi katikaKampuni ya TSNGroup, ambao niwamiliki wa bohariya kuhifadhi mafutaya TAPCO MhandisiMichael Shimiu,(watatu kulia)akimweleza jamboWaziri wa Nishatina Madini, GeorgeSimbachawene (wapili kushoto) naujumbe wake wakatiwalipoitembeleaKampuni hiyo kuonamiundombinu yakuhifadhi mafutaya Kampuni hiyo.Kushoto ni Mkuu wa

    Mkoa wa Tanga SaidMagalula na kuliani Mkurugenzi waTSN Group, FaroukBaghoza.

    Meneja Biashara sehemu ya Mafutaya Petroli wa Kampuni ya Lake

    Gas, Jamal Yahaya, akimwoneshaWaziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene na ujumbewake, Matanki ya kuhifadhi gesiya kampuni hiyo (hayapo pichani)wakati Waziri alipotembeleakampuni hiyo mkoani Tanga.

    u

    u

    u

    Baadhi yaMatanki yakuhifadhimafuta yakampuni yaTSN Group,wamiliki waBohari yaTAPCO.

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    8/14

    8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Baadhi ya Wananchi wa Kijiji chaChipogoro, Wilaya ya Mpwapwawakifuatilia hotuba ya Waziriwa Nishati na Madini, GeorgeSimbachawene wakati wa ziarayake ya kukagua Utekelezajiwa Miradi ya Umeme VijijiniAwamu ya Pili inayofadhiliwa naWakala wa Nishati Vijijini (REA) nakutekelezwa na Shirika la UmemeNchini, (TANESCO).

    Wananchi wa Jamii ya Kimasai, wakicheza ngoma wakati wa ziara ya Waziri wa Nishatina Madini, George Simbachawene kukagua Utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijiniinayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Pili na kutekelezwa na Shirika laUmeme Nchini, (TANESCO).

    Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka kwa

    baadhi ya wazee wa Kijiji cha Chipogoro, wakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji waMiradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Pili inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) nakutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO).

    Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Kanda ya Dodoma, Mhandisi Zakayo Temuakiongea jambo wakati wakati wa wakati wa ziara yake ya kukagua Utekelezaji wa Miradi yaUmeme Vijijini Awamu ya Pili inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwa

    na Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO). Kushoto (jukwaani) ni Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akifuatilia. Wengine ni maofisa wa Wizara

    Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akiongea na wananchi wakati wa ziarayake mkoani Dodoma

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    9/14

    9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Mtaalam kutoka Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Vito na AlmasiNchini ( TANSORT) Dorcus Moshi (katikati) akiwaelimisha watotowaliotembelea banda hilo aina za madini yanayopatikana nchiniTanzania.

    Mmoja wa wakina mama kutoka Kikundi cha Wachimbaji MadiniWanawake Tanzania, (Tanzania Women Mining Association) ShamshaDiwani (katikati) akitoa maoni yake mara baada ya kutembelea bandaa Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Vito na Almasi Nchini ( TANSORT)

    kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katikaviwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

    Baadhi ya wananchi wakiangalia aina za madini ya mawe katika banda la Wakala wa JiolojiaNchini (GST), kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vyaMwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

    Afisa Uokoaji katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Evarist Mwanakatwe (katikati)

    akielezea mikakati ya mgodi huo katika uimarishaji wa usalama katika shughuli za madini.Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Philipo Mathayo (kushoto)akielezea sera ya madini katika kuimarisha shughuli za uchimbaji madini nchini.

    Afisa Uokoaji kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Evarist Mwanakatwe (kulia) akielezeakazi ya uokoaji inavyofanywa na mgodi huo pindi yanapotokea maafa.

    u

    SABASABA 2015

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    10/14

    10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Na Greyson Mwase,Dar es Salaam

    Imeelezwa kuwa Mgodi wa Dhahabuwa Geita (GGM) katika kipindi chamiaka miwili ( 2013 2014) ulitumiashilingi bilioni 22.4 kwa ajili ya

    kuboresha huduma za jamii katika mji waGeita.

    Hayo yalisemwa na Afisa Mazingirawa mgodi huo, Paskazia Mwesiga katikaMaonesho ya Kimataifa ya Sabasabayanayoendelea katika viwanja vyaMwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

    Alisema fedha hizo ni msaada katikakuunga juhudi za serikali , asasi zizizo zakiserikali, na mashirika yanayofanya kazina jamii na kujitoa katika kufikia Malengoya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo yaMilenia.

    Alisema kuwa uwekezaji huu katikahuduma za jamii unalenga mahitaji navipaumbele vya jamiii wilayani Geitaambapo ndipo mgodi unapoendeshashughuli zake.

    Akielezea miradi iliyotekelezwaMwesiga alisema shilingi bilioni 10.1

    zilitumika kwa ajili ya ujenzi wa shule yawasichana ya Nyankumbu na kuongezakuwa ujenzi wa shule hiyo umekamilika

    na kukabidhiwa rasmi kwa serikali.Alisema kuwa lengo la kujenga shule

    hiyo ni kuboresha elimu katika mkoawa Geita kwa kuhakikisha kuwa elimu

    bora inatolewa katika shule za sekondarihususan katika masomo ya sanyansi.

    Aliongeza kuwa mgodi bado unafanyajitihada katika ujenzi wa kituo cha afyakitakachokuwa kinahudumia wanafunzina jumuiya ya wananchi waishio katikaeneo la Nyankumbu.

    Mwesiga aliongeza kuwa mradimwingine ni wa maji ambao ulitumiashilingi bilioni 10, ambapo tangi namitambo ya kusafisha maji vilijengwa nakusisitiza kuwa mradi umekamilika.

    Aliongeza kuwa mazungumzo naserikali ya Tanzania yamekamilikaambapo mgodi wa Geita utashirikikuweka mtandao wa usambazaji wa majiili kuhakikisha kuwa wakazi wa Geitawanapata maji yaliyo safi na salama.

    Aliendelea kutaja miradi mingine kuwani pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumbakatika Bonde la Tarzan uliogharimushilingi bilioni 1.1 ambapo umekamilikana nyumba kukabidhiwa kwa wananchi;

    zahanati ya Nyakabale ambapo ujenziwake uligharimu shilingi milioni 330.

    Aliongeza kuwa nyumba za watumishi

    kwa ajili ya zahanati hiyo zimekamilikapamoja na ufungaji mtambo wa umeme wa

    jua na kusisitiza kuwa kisima kinajengwakwa ajili ya wakazi wa Nyakabale.

    Mwesiga alisisitiza kuwa, katika juhudiza kupambana na ugonjwa wa Malaria,mgodi ulitumia shilingi milioni 220 kamagharama ya kunyunyuzia dawa kwa kaya200.

    Alitaja mradi mwingine kuwa ni wa

    kudhibiti UKIMWI ulioanza mwaka2002, na kusisitiza kuwa mgodi kwakushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti

    Maambukizi ya UKIMWI (TACAIDS)uliboresha mradi huu kwa kupanda MlimaKilimanjaro Kilimanjaro Challenge nakukusanya fedha ambazo zinaelekezwakatika mapambano dhidi ya UKIMWI.Kupitia mradi huu jumla ya shilingimilioni 250 zilipatikana.

    Mwesiga alitaja miradi mingine kuwani pamoja na wa mafunzo jumuishi yaufundi katika madini uliogharimu shilingi

    milioni 93 na mradi wa ajira kwa wahitimuwa vyuo vikuu uliogharimu shilingi milioni340.

    Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akiongea na wakati wa ziara yakeya kukagua Miradi ya Umeme vijijini Awamu ya Pili, inayofadhiliwa na Wakala waNishati Vijijini (REA) na kutekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).

    Na Asteria Muhozya, Tanga

    Imeleezwa kuwa, matumizi ya nishati ya gesi ni muhimukwa kuwa yatasaidia kutokomeza uharibifu wa maz-ingira unaofanywa kutokana na matumizi ya kuni namkaa unaotumika kwa ajili ya matumizi ya majumbani

    Hayo yameelezwa hivi karibuni na Waziri wa Nishati naMadini, George Simbachawene wakati wa ziara yake katikakampuni ya Lake Gas, jijini Tanga , alipokuwa Jijini humokukagua miundombinu ya kuhifadhi mafuta na bandari yaTanga itakayotumika kushusha shehena ya mafuta.

    Aidha, Simbachawene alisema kuwa katika hali halisiukilinganisha gharama za matumizi ya mkaa na gesi, gesi inagharama nafuu zaidi, hivyo matumizi yake yanampunguziamtumiaji wa kipato cha chini gharama za maisha.

    Ukweli ni kuwa, matumizi ya mkaa yana gharamakubwa kuliko gesi. Kwanza mkaa ni nishati inayoishi kwamuda mchache sana ukilinganisha na gesi, alisema Sim-

    bachawene.Simbachawene alitumia fursa hiyo kuipongeza kampu-

    ni hiyo kutokana na shughuli zake za kuingiza gesi nchini,ikiwemo mipango yake ya kuwakopesha walimu vijijini gesiili waweze kutumia nishati hiyo badala ya kuni na mkaa nakuahidi kuisadia kampuni hiyo kuweza kuingiza kiasi kikub-wa zaidi cha gesi.

    Nawapongeza sana kwa ubunifu wenu huu wa ku-wawezesha wananchi kuachana na matumizi ya mkaa am-

    bayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu mazingira.Lakini pia niwapongeze kwa kuwezesha upatikanaji wa ajirakwa vijana kutokana na uwepo wa kampuni hii. Serikali ita-shirikiana nanyi katika hili, aliongeza Simbachawene.

    Simbachawene asisitiza utumiaji

    wa gesi kuokoa mazingira

    GGM yatumia bilioni 22.4kuboresha mji wa Geita

    Afisa Mawasiliano katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Suzan Mwita(kushoto) akitoa maelezo kwa maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madiniwaliotembelea banda la mgodi huo.

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    11/14

    11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    http://www.mem.go.tz

    Na Bibiana Ndumbaro.

    Wafanyakazi waShirika la Madini laTaifa (STAMICO)wameaswa kufanyakazi kwa kujituma

    na kuepuka ufanyaji kazi wa mazoeaili kuwa mfano wa kuigwa katikautekelezaji wa majukumu yao kwakuzingatia kauli mbiu ya matokeomakubwa sasa (BRN).

    Mkurugenzi wa Utawala naUsimamizi wa Rasilimali Watu waWizara ya Nishati na Madini, MrimiaMchomvu ametoa rai hiyo hivi

    karibuni wakati akizindua Baraza laWafanyakazi la STAMICO, katikahafla makao makuu ya Shirika hiloyaliyopo jijini Dar es Salaam.

    Bw. Mchomvu amesema uundajiwa Baraza la Wafanyakazi sehemu yakazi utasaidia kuongeza ushirikishwajiwa watumishi katika kupanga nakutekeleza majukumu yaShirika, kuletausawa katika kujadili mambo muhimu,kutoa ushauri juu ya tija na ufanisiwakazi ikiwemo maboresho ya miundona kanuni za Utumishi na masharti yakazi.

    Mrimia amesema ana matumainimakubwa na STAMICO kwamba

    itaendelea kujiimarisha katikakusimamia na kuendesha miradi yake

    ili ianze kupeleka fedha Hazina badala

    ya kuendelea kuitegemea Serikali katika

    kujiendesha.

    Naye Kaimu Mkurugenzi wa

    STAMICO Zena Kongoi amesema

    STAMICO inatambua umuhimu wa

    Baraza la Wafanyakazi mahali pa kazi

    kwani lina wajibu wa kutengeneza

    mazingira mazuri ya kufanyia kazi na

    kuwapatia staili muafaka wafanyakazi

    wake.Aidha alitoa rai kwa Baraza na

    Chama cha Wafanyakazi TAMICOkuwakumbusha wafanyakazi kutambuawajibu wao mahala pa kazi kwanihakuna haki ya mfanyakazi bila wajibu.

    Shirika liko katika mchakato wakufanyia maboresho stahili mbalimbaliya wafanyakazi, ili kuongeza moralikwa wafanyakazi na hivyo kuongezaufanisi katika kazi. Alisisitiza BiKongoi

    Kwa upande wa Tume ya Usuluhishina Uamuzi (CMA) MkurugenziMsaidizi wa Elimu Kazi na MafunzoBw. Andrew Mwalisi aliipongezaSTAMICO kwa kuingia katikaorodha ya Mashirika yenye Baraza laWafanyakazi jambo ambalo litaongezatija na mahusiano mazuri kazini. Piaaliwaasa wana STAMICO kuzingatiaDhana ya Utawala Bora ili kuifanyaSTAMICO isonge mbele.

    STAMICO imeunda baraza lawafanyakazi kwa mujibu wa sheria yautumishi wa umma na. 8 ya mwaka2002 na kulizindua rasmi tarehe 30mwezi wa sita mwaka huu.

    Baraza hilo lina wajumbe 37wakiwemo wajumbe wanaoingia kwanyadhifa zao kupitia Kurugenzi naVitengo, Wawakilishi wa Halmshauriya TAMICO-STAMICO na Wajumbewa kuchaguliwa.

    MCHOMVU AZINDUA BARAZA

    LA WAFANYAKAZI STAMICO

    Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Nishati na Madini (MEM)Bw.Mrinia Mchomvu (kulia)akiwahutubia wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa STAMICO wakatiakizindua Baraza hilo. Bwana Mchomvu alizindua Baraza hilo kwa niaba ya Kaimu Katibu Mkuu wa WizaraMhandisi Ngosi Mwihava. Kushoto ni wajumbe wa Baraza wakisikiliza Hotuba ya Mgeni Rasmi

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    12/14

    12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Wakaguzi wa Mazingira kutoka TMAA wa pili kutoka kushoto Bi Monica Augustino, Abel Maluluna Nchagwa Marwa wakikagua na kupitia baadhi ya Nyaraka zinazohusu shughuli za utunzajiEndelevu wa Mazingira katika mgodi wa BulyanhuLu.

    Wataalamu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini Tanzania (TMAA) wakifafanua masualambali mbali juu ya shughuli za Wakala katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya SabaSabayanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mhandisi Baraka Manyama, Eva Mow,Zephania Henry, Mhandisi Asanterabi Solomon na Omar Ryakyaaya.

    Wataalam katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamojakwenye banda la TMAA viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kwenye Maoneshoya Kimataifa ya Biashara (SabaSaba).

    Mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Yusuph Msembele (Katikati) akimwonesha mmoja wawafanyabiashara kutoka Korea (kulia, anayepiga picha machapisho hayo) machapisho ya Idara

    ya Nishati.

    Afisa wa Huduma kwa Wateja kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Lucas Kusare ( wapili kutoka kulia) akiwaonesha wafanyabiashara wa nishati kutoka Korea mfano wa mtambo

    wa kuzalisha umeme kwa njia ya maji katika Banda la TANESCO kwenye Maonesho yaKimataifa ya Sabasaba (Dar es Salaam International Trade Fair; DITF) yanayoendelea katikaviwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

    Mmoja wa wafanyabishara wa nishati kutoka Korea akiangalia vinyago kwenye banda la Kituocha Jimolojia Tanzania (TGC) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba (Dar es SalaamInternational Trade Fair; DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dares Salaam

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    13/14

    13BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim (mwenyeKibagharashia) na Mratibu wa Ubia wa Sekta za Umma na Binafsi (Public Private Partnership PPP), Laurian Rwebembera wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katikaJukwaa la Biashara baina ya Tanzania na Korea, lililofanyika hivi karibuni katika Hoteli yaSerena jijini Dar es Salaam.

    Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga (Kushoto) na Kaimu Naibu MkurugenziMtendaji Uzalishaji (Tanesco), Mhandisi Nazir Kachwamba, wakifuatilia mada zilizokuwazikiwasilishwa katika Jukwaa la Biashara baina ya Tanzania na Korea, lililofanyika hivi karibunikatika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

    Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Uzalishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),Mhandisi Nazir Kachwamba akiwasilisha mada kuhusu Miradi ya Umeme na fursa za uwekezajizilizopo katika sekta hiyo.

    Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (Kushoto) Badra Masoud, akifuatilia mada zilizokuwazikiwasilishwa katika Jukwaa la Biashara baina ya Tanzania na Korea lililofanyika hivi karibuni

    katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

    Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Wachimbaji Wadogo, Julius Sarota (Kulia)akifuatilia mada mbalimbali katika Jukwaa la Biashara baina ya Tanzania na Korea lililofanyika

    hivi karibuni katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

    Meneja Mkakati kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Bw. George Kibakayaakiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji kwenye Mafuta na Gesi nchini Tanzania.

    MKUTANO WA KIBIASHARA TANZANIA/KOREA

  • 7/18/2019 MEM BULLETIN 74.pdf

    14/14

    14 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    HABARI ZA NISHATI/MADINI

    Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za Wizara kwenye Mitandaoya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani ya Nishati na MadiniKaribu tuhabarishane na

    tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

    Maendeleo ya taifalolote dunianihutegemea kwakiasi kikubwauwepo wa umeme

    wa uhakika na wa kutosha jambolinalosababisha Serikali ya Tanzaniakuona umuhimu wa kukaribishamakampuni mbalimbali binafsikuwekeza katika sekta ya umeme

    hususan katika uzalishaji umeme.Kwa sasa mahitaji ya umeme

    nchini yamefikia MW 935 hukumahitaji ya umeme kwa mwaka2020 yanatarajiwa kufikia 3,423 naifikapo mwaka 2025 mahitaji yaumeme yanatarajiwa kufikia 4,574lakini lengo la Serikali ni kwambaifikapo mwaka 2025 taifa liwe nauwezo wa kuzalisha MW 10,000.

    Ili kufikia kiasi hicho chaumeme kinachohitajika kwamiaka ijayo, Serikali imeshaanzakufanya jitihada mbalimbali zakuhakikisha kiasi cha uzalishajiumeme kinaongezwa na hasa katikakujenga mitambo hiyo ya kuzalishaumeme na miongoni mwa ujenziwa mitambo ya kuzalisha umemeiliyoanza kujengwa ni pamoja na

    mtambo wa kinyerezi I ambapoutazalisha MW 150.

    Aidha, Serikali imeendeleakuwavutia wawekezaji wa ndanina nje ya nchi ili kushirikiana naSerikali (TANESCO), kuwekezakatika sekta ndogo ya nishati yaumeme hasa katika uzalishaji,usafirishaji na usambazaji umemekama ifuatavyo:-

    Maeneo ya kipaumbele katika

    uwekezaji Sekta ya Umeme

    S/

    NO

    PROJECT

    DESCRPTION

    SOURCE OF

    FUNDING

    PROJECT

    COST

    STATUS

    1 Kinyerez i I - 150MWgas red power plant

    GoT USD 183m Construction 84%completed

    2 Kinyerezi II 240MW gas redpower plant

    GoT - 15%JBIC 85%Contractor:SumitomoCorporation

    USD 344million GoT is soliciting fundsfor nancing the 15%of the contract value ofthe project

    3 Kinyerezi III 600MW gas redpower plant

    China PowerInvestment (CPI)

    USD 401million JV Company formedand feasibility study isunder review

    4 Kinyerezi IV 330MW gas redpower plant

    Poly TechnologyInc. of China

    USD 400million. Preliminary feasibilitystudy is under review

    5 Somanga Fungu320MW Gas FiredPower Plant

    Kilwa Energy- IPP

    USD 365.6Million

    Investor workingwith banks to achievenancial closure

    6 GeoWind 50MWWind Power Plant atSingida

    Exim Bank ofChina

    USD 136Million

    Discussion to concludenancial closure is inprogress

    7 150MW Solar PV inShinyanga

    Not yet secured USD 185million Under System reviewand equipment design

    8 400MW gas redpower plant atMtwara withSymbion (T)

    Symbion USD396.577million

    Feasibility study isunder review

    9 87MW hydropowerplant to bedeveloped atKakono in KageraRegion

    Not yet secured Estimatedcost USD379.4million

    Feasibility Studycompleted Solicitationof nancing in progress

    10 44.8MWhydropower p lantto be developed atMalagarasi river inKigoma

    Not yet secured Estimatedcost: USD149.5million

    Feasibility StudycompletedSolicitation of nancingin progress

    11 400kV Iringa Shinyangatransmission project(Backbone)

    IDA, AfDB, JICA,EIB and KoreaEDCF

    USD 470Million

    Construction 20%completed

    12 400kV North EastGrid Dar Chalinze

    Tanga - Arusha

    GoT - 15%Exim Bank ofChina 85 %

    USD692.7million

    GoT is soliciting fundsfor nancing the 15%of the contract value ofthe project

    13 200kV Makambako Songea transmissionline

    SIDA & GoT USD111.43million

    Distributioncomponent 5%completed

    14 400kV North WestGrid Phase 1: Mbeya- Sumbawanga

    Financing notrmed

    USD259.2million

    Contract for upgradingthe feasibility studyfrom 220kV to 400kVby SWECO Signed

    15 400 kV Singida-Arusha transmissionline

    AfDB, JICA USD 258.82million

    Valuation of propertiesfor compensation hasstarted

    16 400 kV Chalinze-

    Dodomatransmission line

    Financing not

    rmed

    Estimated USD

    175 million

    Procurement of

    Consultant forfeasibility study is inprogress

    17 220 kV Bulyanhulu-Geita transmissionline

    Arab Bankfor EconomicDevelopment inAfrica (BADEA),OFID & GoT

    USD 30million Contract signing withConsultant for projectsupervision completed

    18 220kV T/L Geita Nyakanazitransmission line

    KfW, AFD, EU &GoT

    Euro 29million& TZS 5billion

    Contract signingwith Consultant forproject supervision isunderway

    19 Improving thereliability of Electricpower supply in thecity of Dar es Salaam

    Finish EUR.21.8million

    Construction 60%completed

    20 Tanzania Energ yDevelopment andAccess ExpansionProject (TEDAP) -Transmission

    IDA USD34,252,345.78

    Construction 70%completed

    21 Tanzania Energ yDevelopment andAccess ExpansionProject (TEDAP) -Distribution

    IDA USD43,543,460.07

    Construction 60%completed

    22 Electricity V AfDB & GoT USD51.25million

    Construction 75%completed

    S/NO

    PROJECTDESCRPTION

    SOURCE OFFUNDING

    PROJECTCOST

    STATUS

    23 New 132kVKilimanjaro ArushaTransmission Lineand Rehabilitation ofKiyungi Substation.

    Korean Export-Import Bankthrough EDCF

    USD20,176,384

    Construction 85%completed

    24 Rehabilitation ofHale Hydro Plant21MW

    Co-nanced bySIDA (60% grant)and GoT (40%commercial loan)

    SEK 197 Million The contract for thetechnical consultanthas been signed

    25 Rehabilitation and

    Upgrade of GridNetwork.

    AFD EUR. 53.0M Procurement of

    Consultant forsupervision of theproject is underway

    26 Project forReinforcement ofPower Distributionin Dar es salaamRegion

    JICA Japanese Yen4.41 Billionequivalent toUSD 38 Million

    Contract signingwith Consultant forproject supervision isunderway

    Maeneo hayo ndiyo maeneo ya kipauembele katika uwekezaji kwenye sekta yaumeme hivyo Kampuni yoyote ya ndani na nje ya nchi zinakaribishwa kushirikiana naSerikali/TANESCO kuwekeza ili kufikia malengo na dira ya taifa ili ifikapo mwaka2025 Tanzania iwe taifa la kipato cha kati na kichocheo kikubwa cha kufikia malengohayo ni kuwapo kwa umeme wa uhakika na wa kutosha pamoja na kuwapo kwamiuondombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme bora na wa kutosha.