mwalimuwakizungu.files.wordpress.com  · Web viewNAME…………………………………INDEX...

71
NAME…………………………………INDEX NO…………..CLASS……….. ADM NO……………DATE…………………………SIGN…………………… 102/1 KISWAHILI KARATASI YA 1 INSHA SAA:1 ¾ MTIHANI WA PAMOJA WA BAHATI CLUSTER, TERM II, 2019 Kenya Certificate of Secondary Education (K.C.S.E) MAAGIZO 1. ANDIKA INSHA MBILI. INSHA YA KWANZA NI LAZIMA. 2. KISHA CHAGUA INSHA NYINGINE MOJA KATI YA HIZO TATU ZILIZOBAKI. 3. KILA INSHA ISIPUNGUE MANENO MIA NNE. 400 4. KILA INSHA INA ALAMA ISHIRINI. 20 5. KILA INSHA LAZIMA IANDIKWE KWA LUGHA YA KISWAHILI. KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE SWALI UPEO ALAMA 1 20 2 20 3 20 4 20 JUMLA 40 1

Transcript of mwalimuwakizungu.files.wordpress.com  · Web viewNAME…………………………………INDEX...

NAME…………………………………INDEX NO…………..CLASS………..

ADM NO……………DATE…………………………SIGN……………………

102/1

KISWAHILI

KARATASI YA 1

INSHA

SAA:1 ¾

MTIHANI WA PAMOJA WA BAHATI CLUSTER, TERM II, 2019

Kenya Certificate of Secondary Education (K.C.S.E)

MAAGIZO

1. ANDIKA INSHA MBILI. INSHA YA KWANZA NI LAZIMA.

2. KISHA CHAGUA INSHA NYINGINE MOJA KATI YA HIZO TATU ZILIZOBAKI.

3. KILA INSHA ISIPUNGUE MANENO MIA NNE. 400

4. KILA INSHA INA ALAMA ISHIRINI. 20

5. KILA INSHA LAZIMA IANDIKWE KWA LUGHA YA KISWAHILI.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE

SWALI

UPEO

ALAMA

1

20

2

20

3

20

4

20

JUMLA

40

1. Andika barua kwa mhariri wa gazeti la Zindukeni ukitoa maoni kuhusu sekta ya usafiri wa pikipiki.

2. Fafanua njia mbalimbali za kustawisha michezo nchini.

3. Andika insha inayoafikia methali, Ukiona vyaelea vimeundwa.

4. Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo:

Nilijaribu kuuinua mguu wangu uliojaa maumivu kutokana na jeraha…..

102/1

KISWAHILI

KARATASI YA 1

INSHA

SAA:1 ¾

BAHATI CLUSTER EXAMINATION

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE

SWALI

UPEO

ALAMA

1

20

2

20

3

20

4

20

JUMLA

40

1. Hii ni insha ya kiuamilifu – Mtahiniwa azingatie vipengele hivi vya kimsingi: -

(a) (i) Sura iwe ya barua rasmi – Anwani mbili.

(ii) Mtajo – Kwa mhariri

(iii) Kichwa cha barua/mada

(iv) Kiwiliwili/Maudhui

(v) Hitimisho – Jina kamili la mwandishi liweko

- Sahihi itangulie

(b) Hoja za kuzingatia.

Maoni yaweza kuwa faida na / au hasara.

Faida.

i. Ajirakwa vijana.

ii. Kupunguza uhalifu.

iii. Usafiri wa haraka.

iv. Usafiri wa kutegemea.

v. Kupenya maeneo yasiyofika magari.

vi. Kuimarisha uchumi wa jamii.

Hasara.

i. Kuongezeka kwa ajali.

ii. Kuongezeka kwa vifo vinavyotokana na sekta ya usafiri.

iii. Kuzidisha msongamano kwenye hospitali.

iv. Kuongeza gharama ya huduma za hospitali.

v. Kuchangia ongezeko la uhalifu/wizi wa pikipiki.

vi. Kuzidisha msongamano wa trafiki.

2. Njoa za kustawisha michezo nchini.

Vidokezo

· Wanamichezo waajiriwe na serikali.

· Waalimu wa michezo wawe wamehitimu.

· Vipawa vya wanamichezo vitambuliwe mapema.

· Vyuo maalumu vya michezo vianzishwe nchini.

· Kufanya somo la michezo kuwa la lazima nchini.

· Kuondoa siasa michezoni.

· Wanamichezo wastaafu wapewe heshima.

· Pawe na bima ya kushughulikia wanaoumia.

· Vifaa vya michezo visitozwe ushuru.

· Kuwe na vifaa vya kutosha na vya kufaa.

Kutuza

Insha kamili iwe na hoja zisizopungua tano na zifafanuliwe.

3. Ukiona vyaelea vimeundwa.

Hii ni insha ya methali.

Maana: Ukiona kitu kimenawiri au kizuri jua kuwa kuna juhudi na wakati uliotumika.

· Mwanafunzi akuze pande zote mbili.

· Mtahiniwa aonyeshe juhudi za aliyeelezwa zilizozaa matunda.

Utahini/usahihishaji

(i) Mtahiniwa akikuza upande mmoja asipite alama kumi.

(ii) Azingatie masharti yote ya insha ya methali.

(iii) Insha hii lazima iwe na kichwa/anwani ambayo ni methali yenyewe.

4. Kisa kionyeshe alivyopata jeraha ( atumie mbinu rejeshi) na akiendeleze kisa bila kuongeza maneno kwenye kianzio au kuongeza maneno.

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA INSHA-2019

UTANGULIZI

Karatasi hii imedhamiria kutathmini uwezo wa mtahiniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi,akizingatia mada aliyopewa .Mawasiliano haya yanategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa, kwa mfano, kutunga sentensi sahihi zenye mtiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawazo asili , ubunifu mwingi na hati nadhifu.Kwa ketegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha,ni lazima kutilia mkazo mtindo ,mada na uwezo wa mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo.Mtahini lazima aisome insha yote huku akizingatia sarufi, hoja ,msamiati ma mtindo ili aweze kuikadiri kwa kurejelea viwango mbalimbali vilivyopendekezwa.Viwango vyenyewe ni A,B’C na D kutegemea uwezo wa mtahiniwa.

VIWANGO MBALIMBALI

KIWANGO CHA D KWA JUMLA MAKI 01-05

1 Insha haieleweki kwa vyovyote vile ama uwezo wa mtahiniwa wakutumia lugha ni hafifu sana hivi kwamba mtahini lazima afikirie kile mtahiniwa anacho jaribu kuwasilisha.

2 Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa

3 Lugha imevurugika ,uakifishaji na insha ina makosa ya kila aina.

4 Kujitungia swali na kulijibu

5 Insha ya urefu wa robo ikadiriwe hapa

NGAZI MBALIMBALI KIWANGO CHA D

D-(D YA CHINI) MAKI 01-02

1 Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile

2 Kujitungia swali tofauti na kulijibu

3 Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya ndimi.

4 Kunakili swali au maswali na kuyakariri

5 Kunakili swali au kichwa tu

D WASTANI MAKI 03

1 Mtiririko wa mawazo haupo

2 Mtahiniwa amepotoka kimaudhui.

3 Matumizi ya lugha ni hafifu mno

4 Kuna makosa mengi ya kila aina

D+ (D YA JUU) MAKI 04-05

1 Insha ya aina hii huwa na makosa mengi ya kila aina .Lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha

2 Hoja hazikukuelezwa kikamilifu / mada haikukuzwa vilivyo.

3 Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha.

4 Mtahiniwa hujirudiarudia

5 Insha yenye urefu wa robo ikadiriwe hapa.

KIWANGO CHA C KWA JIJMLA: MAKI 06-10

1. Mtahiniwa anajaribu kuishughulikia mada japo hakuikuza na kuiendeleza vilivyo.

2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia /hana ubunifu wa kutosha.

3. Mtahiniwa anaakifisha sentensi vibaya.

4. Mtiririko wa mawazo unaanzakujitokeza japo kwa njia hafifu.

5.Insha inamakosa mengi ya sarufi, ya misamiati na ya tahajia (hijai.)

6. Insha yenye urefu wa nusu ikadiriwe hapa.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA C

C-(C YA CHINI) MAKI 06-07)

.

1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake.

2. Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo.

3. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati na insha yake haieleweki kwa urahisi

.

C WASTANI MAKI 08

1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu,

2. Dhana tofautitofauti hazijitokezi wazi.

3. Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha.

4. Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa.

5. Amejaribu kuishughulikia mada aliyopewa

6. Mtahiniwa ana shida ya uakifishaji.

7. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi ya hijai na ya msamiati lakini bado insha inaeleweka.

C+(C YA JUU) MAKI 09-10

1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini kwa njia isiyo na mvuto.

2. Dhana tofautitofauti zinajitokeza japo kwa njia hafifu.

3. Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.

4. Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu.

5. Ana shida ya uakifishaji.

6. Kuna makosa ya sarufi, ya msamiati na ya hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo.

KIWANGO CHA B KWA JUMLA: MAKI11-15

1. Katika kiwango hiki, mtahiniwa anaonyesha hali ya kuimudu lugha.

2. Mtahiniwa anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi vizuri.

3. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha.

4. Mada imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.

5 Insha ya urefu wa robo tatu ikadiriwe katika kiwango hiki.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA B

B-(B YA CHINI): MAKI 11-12

1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofautitofauti akizingatia mada.

2. Mtahiniwa ana mtiririko mzuri wa mawazo.

3. Mtahiniwa anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia.

4. Makosa yanadhihirika/kiasi

B WASTANI MAKI 13

1. Mtahiniwa anadhihirisha haliya kuimudu lugha

2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika akizingatia mada.

3. Mtahiniwa anateua na kutumia mifano michache ya misamiati mwafaka.

4. Sarufi yake ni nzuri.

5. Makosa ni machache/kunamakosa machache

.

B+ (B YA JUU) MAKI 14-15

1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anajieleza waziwazi.

2. Mtahiniwa anawasiliha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.

3.Mtahiniwa ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia.

4. Sarufi yake ni nzuri.

5. Uakifishaji wa sentensi zake ni mzuri.

6. Makosa ni machache ya hapa na pale.

KIWANGO CHA A KWA JUMLA MAKI 16-20

1. Mtahiniwa ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka akizingatia

mada.

2. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato.

3. Ana uwezo wa kutumia tamathali za usemiilikutoa hisia zake kwa njia bora nakwaurahisi.

4. Umbuji wake unadhihirisha ukomavu na ukakamavu wake kimawazo

5. Insha inaurefu kamili

NGAZI MBAL1MBALI ZA KIWANGO CHA A

A-(YA CHINT) MAKI 16-17

I. Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha.

2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anashughulikia mada.

3. Ana mtiririko mzuri wa mawazo

4. Msamiati wake ni mzuri na unaovutia.

5. Sarufi yake ni nzuri.

6. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi.

7. Makosa ni machache yasiyokusudiwa

.

A WASTANI MAKI 18

1. Mtahiniwa anawasilishaujumbe vizuri kulingana na mada.

2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato/kunasa.

3. Anatoa hojazilizokomaa.

4. Anatumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia zaidi.

5.Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi.

6. Makosa ni nadra kupatikana

.

A+(AYAJUU)MAKI 19 -20

1. Mawazo yanadhihirika zaidi na mada imeshughulikiwa vilivyo.

2. Anajieleza kikamilifu akitumia Iugha ya mnato.

3. Hoja zake zimekomaa na zinashawishi.

4. Msamiati wake ni wa hali ya juu na unaovutia zaidi

5. Sura yake ninzuri zaidi/kabisa

6. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentesi kiufundi.

7.Makosa yote kwa jumla hayazidi matano.

VIWANGO MBALIMABLI KWA MUHTASARI

Kiwango

NGAZI

MAKI

A

A+

A

A-

19-20

18

16-17

B

B+

B

B-

14-15

13

11-12

C

C+

C

C-

09-10

08

06-07

D

D+

D

D-

04-05

03

01-02

USAHISHAJI NA UTUZAJI KWA JUMLA

Mtahini ni sharti aisome insha yote akizingatia vipengee muhimu. Vipengee hivi ni maudhui, msamiati,mtindo, sarufi na hijai

MADHUI

1. Maudhui ni hoja au mambo yanayozungumziwa, kuelezewa au kuhadithiwa kwa mujibu wa mada iliyoteuliwa.

2.Maudhui ndio hasa uti wa mgongo wa insha yoyote ile.

3.Ubunifu wa mtahiniwa hukisiwa kwa kutathmini uzito wa maudhui yake kulingana na mada teule

MSAMIATI

Msamiati ni jumla ya maneno yatumiwayo katika lugha husika, Mtahinwa anatarajiwa kutumia msamiatiunaooana na mada teule. Kutegemea ukwasi wa lugha alionao, mtahiniwa anatarajiwa kuikuza mada kwa kuifinyanga lugha kiufundi. Ni muhimu kuelewa kwamba kutokana namaendeleo na ukuaji wa teknolojia na mawasiliano, maneno mapya yanaibuka kila uchao.

MTINDO

Mtindo unahusu mambo yafuatayo.

Mpangilio wa kazi kiaya.

Mtiririko na mshikamano wa mawazo kiaya na katika insha nzima.

Hati nzuri na inayosomeka kwa urahisi.

Matumizi ya tamathali za usemi, kwa mfano, methali, misemo, jazanda nakadhalika.

Kuandika herufi vizuri kwa mfano Jj, Pp. Uu, Ww na kadhalika.

Sura ya insha

Unadhifu wa kazi ya mtahiniwa.

SARUFI

Sarufi ndio msingi wa 1ugha. Ufanisiwa mawasilianohutegemea uwezo wa mtahiniwa wa kutunga sentensi sahihi zenye uwiano wa kisarufi. Mtahini ataonyesha makosa yote ya sarufi yake katika insha anayosahihisha. Makosa ya sarufihuweza kutokea katika:

(i)Matumizi yaalama za uakifishaji.

(ii)Kutumia herufi kubwa au ndogo mahali pasipofaa.

(iii)Matumizi yasiyofaa ya ngeli na viambishi, viunganishi, nyakati, hali, vihusiano na kadhalika.

(iv)Mpangilio wa maneno katika sentensi.

(v)Mnyambuliko wa vitenzi na majina

(vi)Kuacha neno linalohitajika au kuongeza neno lisilohitajika katika sentensi.

(vii)Matumizi ya herufi kubwa:

a) Mwanzo wa sentensi

b) Majina yapekee.

c) Siku za juma,mwezi n.k.

i) Majina ya mahali, mji, nchi, mataifa na kadhalika.

ii) Mashirika, masomo, vitabu n.k.

iii)makabila, lugha nk.

vi)Jina la Mungu.

v) Majina ya kutambulisha hasa wanyama wa kufugwa, kwa mfano yale ya mbwa, popi, simba, Tomi na mengineyo

vi)majina ya watu (binadamu)

MAKOSA YA HIJAI/TAHAJIA

Haya ni makosa ya maendelezo. Mtahini anashauriwa asahihishe huku akiyaonyesha yanapotokea kwa mara ya kwanza tu. Makosaya tahajia huweza kutokeakatika:

(a) Kutenganisha neno kwa mfano‘aliye kuwa’

(b) Kuunganisha maneno kwa mfano ‘kwasababu’.

(c) Kukata silabi visivyo afikapo pambizoni kama vile ‘ngan –o’

(d)Kuandika herufiisiyofaa kwamfano ‘ongesa’ badala ya ‘ongeza’

(a) Kuacha herufi katika neno kwa mfano ‘aliekuja’ badalaya ‘aliyekuja’.

(f) Kuongeza herufi isiyohitajika kama vile ‘piya’ badala ya ‘pia’.

(g) Kuacha alama inayotarajiwa katika herufi kama vile ji.

(11) Kukosa kuandika kistari cha kuendelezea neno afikiapo pambizoni au kukiandika mahali pasipofaa.

(i). Kuacha ritifa au kuiandika mahali pasipofaa, kwa mfano ngombe,n.k

(j) Kuandika maneno kwa kifupi kama vile k.v., k.m., .y.v., n.k. na kadhalika.

(k) Kuandika tarakimu kwa mfano 27-08-2010.

ALAMA ZA KUSAHIHISHA

= Hupigwa chini ya sehemu ambapo kosa la sarafi limetokea kwa mara ya kwanza tu .

- Hupigwa chini ya sehemu au neno ambalo kosa la hijai imetokea kwa mara ya kwanza tu.

· Hutumiwa kuonyesha hoja inapokamilikia pambizoni kushoto.

^ Hutumiwa kuonyesha kuachwa kwa neno/maneno.

· Hutumiwa kuonyesha msamiatibora. Alama hiihutiwa juu ya neno lenyewe.

X Hutumiwa kuonyesha msamiati usiofaa. Alama hii hutiwa juu ya neno lenyewe.

Maelezo mafupi yanahitajika kuhusu tuzo lililotolewa. Kila ukurasa uwe na alama ya katikati ili

kuthibitisha kuwa mtahini ameupitiaukurasa huo.

UREFU

Mtahiniwa akiandika insha iliyo na maneno yafuatayo atakuwa ametimiza kiwango kilichoonyeshwa:

a)1-174 -robo-asizidi alama 05/20

b)175-274 –Nusu-asizidi alama 10/20

c)275-374 Robo tatu-asizidi alama 15/20

d)Zaidi ya 375-Kamili

NAME…………………………………INDEX NO…………..CLASS………..

ADM NO……………DATE…………………………SIGN……………………

102/2

KISWAHILI

KARATASI YA 2

SAA: 21/2

MTIHANI WA PAMOJA WA BAHATI CLUSTER, TERM II, 2019

Kenya Certificate of Secondary Education (K.C.S.E)

Maagizo

1. Andika jina lako na namba yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.

2. Tia sahihi yako na tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.

3. Jibu maswali yote. Andika majibu yako katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali.

4. Karatasi hii ina kurasa kumi na mbili zilizopigwa chapa.

5. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

Kwa matumizi ya mtahini pekee

SWALI

UPEO

ALAMA

1

15

2

15

3

40

4

10

JUMLA

I. UFAHAMU(ALAMA 15)

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuatia

Kitengo cha familia Kimesakamwa na wimbi kali la mabadiliko katika jamii. Namna ambavyo familia zinaendeshwa siku hizi ni tofauti na taratibu za azali. Waama hakuna kipenge cha maisha yetu ambacho hakijaathiriwa na kile ambacho kimekuja kujulikana kama ‘usasa’.

Familia nyingi hasa katika maeneo ya mijini zinategemea sana watu wa kuajiri kuzishughulikia. Wazazi wengi hawatengi muda wa kukaa nyumbani na watoto ili kuwapa mwongozo na mapenzi yaliyo muhimu katika hatua mbalimbali za ukuaji wao. Wazazi huondoka mapema sana kwenda kazini na kurejea wakiwa wamechelewa mno. Watoto wao wakati huo huwa ama hawajaamka au tayari washalala. Kwa upande mwingine wapo wazazi ambao wanafanya kazi katika miji iliyo mbali na wanapokaa watoto wao au nchi za kigeni. Uhusiano kati ya mzazi na mtoto unakosa rotuba ya kuuneemesha na matokeo yake huwa ni vijana waliokosa mwelekeo. Walivyosema Waswahili, samaki hukunjwa akiwa bado mbichi. Tabia za watoto hawa zinaweza tu kuandaliwa katika maadili wakiwa wadogo.

Tofauti kati ya wazazi, Pamoja na kuzaliwa kwa watoto nje ya ndoa kumebadilisha sura ya kitengo cha familia. Tofauti na zamani, hii leo utapata familia ambazo zinaendeshwa na mzazi mmoja – anaweza kuwa baba au mama tu. Ni kweli kwamba mtoto huhitaji malezi ya wazazi wote wawili. Mwongozo wa ushirikiano wa wazazi wote wawili ni imara na bora zaidi kuliko wa mzazi mmoja. Hii haimaanishi kuwa mtoto hawezi kulelewa vizuri na mzazi mmoja au vibaya na wazazi wote. Mtoto huweza kukosa huduma za kimsingi kwa kosa lisilo lake.

Jukumu la jamii katika malezi ya watoto limepungua. Zamani malezi ya mtoto yalikuwa jukumu la kila mwanajamii. Mtoto alipothubutu kufanya kosa aliweza kuadhibiwa palepale na mwanajamii yeyote ambaye hakusita kujitwika jukumu la mzazi. Hata hivyo hali ni tofauti hii leo. Kumwadhibu mtoto wa mtu ni kichocheo tosha cha kuleta mfarakano usiokwisha katika jamii. Kila mtu anauchelea ugomvi wa kujitakia. Kila mtoto sasa anaelewa na vipimo vya mzazi wake na siyo vya jamii pana. Watoto nao wamegundua hili na hawakusita kujivika mavazi mawili tofauti, zuri mbele ya wazazi wao na jinginelo popote pasipo hao wazazi. Sasa wazazi wanaweza kuishi na wahalifu waliokubuhu bila kufahamu.

Jambo lingine linalohusiana na hilo ni kutupiliwa mbali kwa tamaduni za Kiafrika. Ni kama jamii iliyotupa jongoo na mti wake. Si siri kuwa kuna masuala ya kitamaduni yaliyopitwa na wakati na ambayo inahalisi kuyapiga teke. Hata hivyo hatuwezi kukitia kila kipengee cha tamaduni zetu jalalani. Utamaduni wetu mbali na kututambulisha kama jamii, pia hutekeleza jukumu adhimu la kutuwezesha kuyaona mambo kwa mtazamo mmoja. Mtazamo huo mmoja ndio unaotupa umoja wetu. Hatuwezi kuwa na utangamano bila kuwa na uzi unaotufunga Pamoja. Maadili ya jamii hayawezi kubainika bila ya watu kuwa na Mwongozo na mtazamo mmoja kuhusu hali yao ya maisha.

Familia za kisasa zina idadi ndogo za watu ikilinganishwa na hapo awali. Hali ngumu ya maisha imewasukuma watu katika kupata watoto wachache ambao wanaweza kumudu kuwalea vizuri. Nako kupungua kwa nafasi za ajira kunawazuia vijana kuingia katika nikahi mapema. Hali hii imechangia katika kupunguza idadi ya watu na pia kupunguza kasi za uchipukaji wa familia mpya. Hali ngumu ya maisha imepunguza upana wa familia kama ilivyokuwa awali. Siku hizi mtu na mkewe au mumewe Pamoja na watoto wanaikamilisha familia. Vikoa vimekwisha na kubaki kuwa kila mtu na lake. Wengine hawako tayari kuwatilia pondo ndugu zao.

Maswali

1. Kwa mujibu wa taarifa eleza matatizo yanayoweza kuikabili familia inayoendeleshwa na mzazi mmoja.(alama 2) .........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

2. Ni nini kiini cha utengano wa wazazi katika ndoa.(alama 1) ........................................................................................................................................................................................................................................................................................................

3. Jadili nafasi ya utamaduni katika kuijenga jamii bora kwa kurejelea makala. (alama 2)

................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

4. Kwa nini familia za kisasa zina idadi ndogo ya watu?(alama 2)

.................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

5. Taja huku ukitoa mifano ya tamathali zozote tatu za lugha zilizotumiwa katika taarifa. (alama 3)

..............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa kifunguni.(alama 5)

i. Kimesakamwa –

.........................................................................................................................................................................................................................................................

ii. Mfarakano usiokwisha

............................................................................................................................................................................................................................................................

iii. Wahalifu waliokubuhu

..............................................................................................................................................................................................................................................................

iv. Vikoa vimekwisha

...............................................................................................................................................................................................................................................................

v. Kujivika mavazi mawili

..................................................................................................................................................................................................................................................................

2. UFUPISHO

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yafuatayoKi1a walimwengu wanapotajiwa kuwa shambulizi la kigaidi limetokea mahali fulani, wimbi la taharuki huwakumba. Mashambulizi ya kigaidi yameongezeka katika siku za hivi majuzi ambapo kundi Ia watu linalohisi kuwa linaonewa na kukandamizwa huitumia mbinu ya kushambulia kwa kuvizia, hasa kutumia mabomu au kuteka ndege na kutishia kuilipua na wakati mwingine kuilipulia angani. Kuna mabomu yaliyotegwa na kulipuka katika maegesho ya magari au kwenye vizuizi vya magari. Mengine hutegwa na kulipuliwa katika afisi, mikahawa, makao ya watu, n.k. Katika baadhi ya mashambulizi, wapo waliojitoa mhanga ambao hujilipua katika shambulizi

. Makundi ya watu wanaohasimiana ndio chanzo cha matendo ya kigaidi. Kundi linalohisi kuwa linaonewa au ambalo kweli linaonewa na ambalo ni dhaifu kuliko lile jingine, hufanya juu chini kushambulia kisirisiri. Nia ni kulipisha kisasi kwa jambo wanalohisi wamehiniwa. Kwa kuwa kundi hilo hudhani kuwa dhaifu halina njia wala uwezo wa kuyakabili moja kwa moja matendo waliyotendewa au wanayoendelea kutendewa, njia ya pekee, kwa maoni yao, huwa hii ya kushambulia kwa kushitukiza. Kiini cha uonevu kinaweza kuwa dini, uchumi, maamuzi ya kisiasa au jambo lingine lolote lile. Kinachobainika katika suala zima Ia mashambulizi ya kigaidi ni kuwa lipo jambo ambalo linazikera nyoyo za kundi fulani Ia watu walio wanyonge ambao huona kuwa njia ya pekee ya kudhihirisha hisia zao ni kupitia mashambulizi ya aina hii.

Mashambulizi ya aina hii yana athari zake nyingi. Kuna watu wanaouawa na wengine wengi kulemaa. Maisha ya watu hawa au jamaa zao wanaowategemea hubadilika na kujaa mvurugano uliokithiri. Kuna watoto ambao ndoto zao za kupata elimu zimetumbukia nyongo baada ya wazazi wao kuzikwa hai katika vifusi. Mbali na kukosa elimu na mahitaji mengine ya kimsingi, watoto hawa hupatwa na matatizo ya kisaikolojia baada ya kuona maafa yaliyowafika wavyele wao. Hata wale wanaosalimika kutoka kwenye vifusi hivi hawaishi kuandamwa na majinamizi yasiyoisha.

Mashambulizi ya kigaidi hayaathiri tu watu pamoja na kuharibu mali ya thamani ya lukuki ya pesa. Zipo athari nyingine hasi ambazo hudhihiri. Kwa mfano usalama wa nchi huwa mashakani. Wananchi na wageni vilevile hujihisi kuwa dhaifu na dhalili katika nchi illyovamiwa. Serikali husika hujikuta katika shutuma kwa kushindwa kutambua mipango hiyo mapema na kuzuia hasara ya nyoyo na mali. Aidha, jamii ya kimataifa huiona nchi hiyo kama yenye kukosa usalama na hivyo kuwaonya raia wake dhidi ya kuizuru. Iwapo nchi husika inategemea utalii kama kitega uchumi muhimu, basi hukosa wateja na waajiriwa katika sekta hii kupigwa kalamu.

Tatizo la ugaidi si Ia nchi moja au mataifa fulani mahususi wala hakuna nchi au taifa linaloweza kudai kuwa haliwezi kukabiliwa na tishio la kigaidi. Kuanzia Dar es Salaam, Nairobi hadi New York na London au hata Cairo hadi Riyadh na Baghdad, sote tunakabiliwa na tatizo hili hili. Hakuna ajuaye lini, vipi au wapi magaidi wamedhamiria kutekeleza unyama huu.

Labda swali Ia kujiuliza ni kwamba; Je, upo uwezekano wa mwenendo huu wa kuwaangamiza watu, wengi wa wahasiriwa wakiwa wale wasio na hatia, kudhibitiwa na kumalizwa kabisa? Serikali za nchi mbalimbali zimejaribu kutumia uwezo wao wa kiuchumi na kiteknolojia ili kujaribu kuiondoa hali hii. Njia waliyoitumia ni ya mtutu wa bunduki ambapo makombora mazito yaliyogharimu pesa nyingi yanadondoshwa katika makao ya washukiwa. Hata katika hatua hii nayo, upo uwezekano mkubwa wa kuuawa watu wasio na hatia vilevile. Pia ni wazi kwamba uhasama unalipwa kwa uhasama na matokeo yake ni ulipizaji kisasi usioisha. Amani inakuwa nadra. Juhudi za ulimwengu kulaani vitendo hivi ni nzuri ila hazitoshi. Utumiaji nguvu kutafuta ufumbuzi wa kitendawili hiki si suluhisho. Kama wanavyoeleza wanasosholojia, kila kitendo kina sababu zake zilizofichama. Sababu hizo ndizo kichocheo cha vitendo vinavyojidhihiri. Hivyo basi jukumu lipo katika kutambua vichochezi vya mashambulizi na kujitahidi kuvitatua kwa njia ya mashauriano yaliyojengwa katika nia safi ya kuleta usawa na usalama duniani.

Wapo watu wanaoona kuwa vitendo vya mataifa yaliyoendelea kwa nchi changa ndivyo kilele cha ugaidi. Watu wanaona kuwa tabia ya mataifa hayo yenye uwezo kiuchumi na kiteknolojia kuamua na kudhibiti sera na imani za nchi changa ni ugaidi uliokubuhu. Vikwazo hivi huwaacha viongozi hoi na wananchi kuteseka kufuatia ulazimishaji wa sera za kiuchumi na kisiasa zisizohusiana na mahitaji ya watu wa nchi husika wala kuambatana na mahjtajj ya nchi hizi. Hii ni hali inayoyatia mataifa yanayoendelea katika wasiwasi usioisha kutokana na dhiki zisizoisha kusababishwa na mataifa ya kigeni.

II. UFUPISHO

a) Kwa kutumia maneno yasiyozidi 80, fupisha aya ya pili, tatu na nne.(alama 10)

alama1, mtiririko

Matayarisho

...................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

Jibu

...............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

b) Eleza njia zinazotumiwa na mataifa ulimwenguni kupambana na ugaidi. (Maneno 40)alama 5; 1 ya mtiririko

Matayarisho

..............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

...............................................................................................................................................

Jibu

...............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

(a) i.Taja vigezo viwili vya kuanisha irabu.(alama 1)

.....................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

ii. Tofautisha sauti zifuatazo.(alama.2)

a. /a/ na /i/

...............................................................................................................................................

b. /e/ na /o/

......................................................................................................................................

(b) Ainisha aina za vivumishi katika sentensi ifuatayo.(alama. 2)

Mwalimu mzee alitufundisha vizuri ile mada ngumu.

...........................................................................................................................................................................................................................................................

i. i.Eleza maana ya kirai. (alama.1)

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

ii. Tunga sentensi iliyo na kirai kivumishi na kirai nomino chenye muundo wa W+ V (alama 1)

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

(c) Andika sentensi hii upya bila kubadilisha maana ukitumia “O” rejeshi. (alama 2)

Mwanafunzi alitumwa nyumbani juzi na hajapata karo hadi leo.

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

(d) Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika hali ya udogo wingi.

Kono lake lilivimba baada ya kuumwa na jibwa.(alama 2)

....................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

(e) Tunga sentensi iliyo: (alama 3)

Kitenzi kishirikishi kikamilifu

....................................................................................................................................................................................................................................................................................

Kivumishi kimilikishi nafsi ya pili wingi

...............................................................................................................................

Kiwakilishi cha nafsi ya tatu tegemezi wingi.

...................................................................................................................................................................................................................................................

(f) Kanusha sentensi ifuatayo kisha ueleze maana yake katika hali kanushi (alama 2)

Angeongoza darasa lake, angepewa tuzo.

........................................................................................................................................

..............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

(g) Onyesha sehemu za kisarufi katika neno lifuatalo.(alama 2)

Kililiwa

....................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

(h) Kanusha katika hali timilifu wakati uliopita.

Kamati ya uchaguzi iliandaa ripoti kuhusu utovu wa nidhamu shuleni.(alama 2)

......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

(i) Changanua kwa kutumia mchoro wa matawi

Hatukuondoka na yeye japo tulirudi naye.(alama 4)

(j) Tumia kiambishi KA katika sentensi ili kuleta dhana ya:(alama 2)

i. Wakati usiodhihirika

..................................................................................................................................................................................................................................................

ii. Kuonyesha matokeo yanayosababishwa na kitendo.

...............................................................................................................................................................................................................................................

(k) Chane kwa mtama_________________ kwa udongo.(alama 1)

(l) a. Eleza maana ya fungu tenzi.(alama 1)

................................................................................................................................................................................................................................................................................b.Taja aina mbili za fungu tenzi. (alama.2)

..........................................................................................................................................................................................................................................................................

(m) Geuza sentensi hii hadi usemi halisi.

Wanakijiji walikuwa wanataka kujua iwapo vipakatalishi vya shule za msingi vingeweza kuinua kiwango cha elimu. (alama 3)

........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

(n) a. Eleza maana ya yambwa. (alama 1)

........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................b. Tunga sentensi iliyo na: shamirisho kipozi na chagizo cha kiasi kamili. (alama.2)

.............................................................................................................................................................................................................................................................................

(o) Tunga sentensi kwa kutumia kiunganishi cha wakati.(alama 2)

...............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

(p) Andika visawe vya maneno yaliyopigigwa mstari . (alama 2)

Tulienda kusali siku ya Jumapili.

........................................................................................................................................

SWALI LA 4: ISIMU JAMII

Eleza changamoto zinazokumba ukuaji wa lugha ya Kiswahili nchini Kenya. ( alama 10)

_________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________

________________________________________________________________________

102/2

KISWAHILI

KARATASI YA PILI

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA KISWAHILI

UFAHAMU

1.- Mtoto anaweza kukosa huduma za kimsingi

- Watoto hukosa mwelekeo

2x1=Alama 2

2.Tofauti kati ya wazazi/wazazi kutoelewana katika ndoa1x1 = Alama 1

3.– Utamaduni huwezesha jamii kuyaona mambo kwa mtazamo mmoja.

- Hutuwezesha kuwa na umoja

- Hututambulisha Kama jamii

- Hukuza maadili miongoni mwa wanajamii

Zozote 2x1 = Alama 2

4 - Kwa sababu ya hali ya ngumu ya maisha inayowafanya watu kupata watoto wachache wanaoweza kumudu kuwalea

- Kupungua kwa nafasi za ajira huwazuia vijana kuingia kwa nikahi mapema.

2x1 = Alama 2

5.Misemo – kuingia katika nikahi →kuolewa

Methali – samaki hukunjwa akiwa bado mbichi

Tashhisi – kitengo cha familia kimesakamwa na wimbi kali la mabadiliko

3x1 = Alama 2

6 (a)Kimesakamwa – kimesongwa / kimekabiliwa sana.

(b)Mfarakano usiokwisha – ugomvi usio na kikomo

(c)Wahalifu waliokubuhu – wahalifu / watenda maovu waliobobea / waliozoea

(d)Vikoa vimekwisha – utangamano / ujamaa umekwisha

(e)Kujivika mavazi mawili – Kuwa na tabia aina mbili – nzuri na mbovu

5x1 = Alama 5.

IIUFUPISHO

(a)- Makundi ya watu wanaohasimiana ndio chanzo cha ugaidi.

-Nia huwa ni kulipiza kisasi kwa vile kundi moja hujihisi kuwa dhaifu.

- Kiini cha uhasama huwa dini, uchumi au siasa

- Mashambulizi haya huwa na athari nyingi k.v.

-Watu kuuawa

-Ulemavu

-Kuvuruga maisha ya watu

-Elimu huvurugwa

-Matatizo ya kisaikologia

-Kuharibu mali

-Usalama wa nchi huwa mashakani

-Utalii huathiriwa

Hoja zozote 9 x1 = 9

Utiririko 1x1 = Alama 1

(b)Njia zinazotumiwa kupambana na ugaidi

-Kutumia mtutu wa bunduki / kushambulia magaidi

-Kulaani vitendo vya kigaidi

-Kujaribu kutambua vichochezi vya mashambulizi na kujaribu kuvitatua kwa mashauriano

-Kuwekewa vikwazo kwa mataifa yaliyo na magaidi

4x1 = Alama 4

Utiririko = Alama

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

(q) i.Taja vigezo viwili vya kuanisha irabu.(alama 1)

mkao wa midomo

sehemu ya ulimi kinywani

ii. Tofautisha sauti zifuatazo.(alama.2)

a. /a/ na /u/

/a/ ni sauti ya chini kati ilhali /u/ ni sauti ya nyuma juu

/a/ midomo hutandazwa ilhali /u/ midomo huviringwa

b. /e/ na /o/

/e/ sauti ya mbele kati /o/ sauti ya nyuma kati

/e/ midomo hutandazwa /o/ midomo huviringwa

(r) Ainisha aina za vivumishi katika sentensi ifuatayo.(alama. 2)

Mwalimu mzee alitufundisha vizuri ile mada ngumu.

Mzee – kivumishi jina, ile- V kionyeshi/ kiashiria, ngumu- sifa,

ii. i.Eleza maana ya kirai. (alama.1)

fungu la maneno lisilo na muundo wa kiima kiarifa au kipashio cha kimuundo cha sentensi ambacho hakiwasilishi maana kamilifu.

ii. Tunga sentensi iliyo na kirai kivumishi na kirai nomino chenye muundo wa W+ V (alama 1)

Mwanafunzi yule mwerevu alisoma kile kizuri.

Kirai kivumishikirai nomino(W+V)

(s) Andika sentensi hii upya bila kubadilisha maana ukitumia “O” rejeshi. (alama 2)

Mwanafunzi alitumwa nyumbani juzi na hajapata karo hadi leo.

Mwanafunzi aliyetumwa nyumbani juzi hajapata karo hadi leo.

(t) Badilisha sentensi ifuatayo iwe katika hali ya udogo wingi.

Kono lake lilivimba baada ya kumwa na jibwa.(alama 2)

Vijikono vyao vilivimba baada ya kumwa na vijibwa.

(u) Tunga sentensi iliyo: (alama 3)

Kitenzi kishirikishi kikamilifu.

Mama angali nyumbani.

Kivumishi kimilikishi nafsi ya pili wingi

Vitabu vyenu vinahitajika.- mzizi –enu uwepo.

Kiwakilishi cha nafsi ya tatu tegemezi wingi.

Wanasoma vitabu vyao. Kiambishi wa

(v) Kanusha sentensi ifuatayo kisha ueleze maana yake katika hali kanushi (alama 2)

Angeongoza darasa lake, angepewa tuzo.

Asingeongoza darasa lake, asingepewa tuzo.

Maana: aliongoza vizuri na akapewa tuzo

(w) Onyesha sehemu za kisarufi katika neno lifuatalo.(alama 2)

Kililiwa

Ki- ngeli

li- wakati uliopita

l- mzizi

iw - kauli

a-kiishio

(x) Kanusha katika hali timilifu wakati uliopita.

Kamati ya uchaguzi iliandaa ripoti kuhusu utovu wa nidhamu shuleni.(alama 2)

Kamati ya uchaguzi ilikuwa haijandaa ripoti kuhusu utovu wa nidhamu shuleni.

(y) Changanua kwa kutumia mchoro wa matawi

Hatukuondoka na yeye japo tulirudi naye.(alama 4)

S1 +U + S2

S1---- KN--0

KT-----T+H+W

U---japo

KN--O

KT-------T+W

Mwanafunzi achore mchoro wa matawi

(z) Tumia kiambishi KA katika sentensi ili kuleta dhana ya:(alama 2)

iii. Wakati usiodhihirika

Mwalimu kaondoka.

iv. Kuonyesha matokeo yanayosababishwa na kitendo.

Alisoma sana akapita mtihani

(aa) Chane kwa mtama shumbi kwa udongo.(alama 1)

(ab) a. Eleza maana ya fungu tenzi.(alama 1)

Ni kitenzi kilichoundwa kwa viambishi tofautitofauti.

b.Taja aina mbili za fungu tenzi. (alama.2)

fungu tenzi kama sentensi sahili

fungu tenzi kama kishazi tegemezi

(ac) Geuza sentensi hii hadi usemi halisi.

Wanakijiji walikuwa wanataka kujua iwapo vipakatalishi vya shule za msingi vingeweza kuinua kiwango cha elimu. (alama 3)

“Vipakatalishi vya shule za msingi vitaweza kuinua kiwango cha elimu?” wanakijiji waliuliza.

(ad) a. Eleza maana ya yambwa. (alama 1)

yambwa ni nomino tendwa au tendewa

b. Tunga sentensi iliyo na: shamirisho kipozi na chagizo cha kiasi kamili. (alama.2)

Mwanafunzi alisoma kitabu mara tatu.

Kitabu- kipozi

Mara tatu- chagizo cha kiasi

(ae) Tunga sentensi kwa kutumia kiunganishi cha wakati.(alama 2)

Mwizi aliwawaiba kondoo halafu akawachinja.

Kisha,baadaye

(af) Andika visawe vya maneno yaliyopigigwa mstari . (alama 2)

Tulienda kusali siku ya Jumapili.

Kusali- kuomba, kuabudu

Jumapili- dominika

SWALI LA 4: ISIMU JAMII

Eleza changamoto zinazokumba ukuaji wa lugha ya Kiswahili nchini Kenya. ( alama 10)

____________________

1. Athari za lugha ya kwanza / kigeni.

2. Kinadunishwa – Kiswahili huhusishwa na wasiosoma.

3. Matumizi ya sheng’

4. Ukosefu wa vifaa kama vile vitabu

5. Vyombo vya habari.

6. Ukosefu wa utafiti.

7. Vipindi vichache shuleni.

8. Sera mbovu ya lugha nchini

Ondoa nusu ( ½ ) alama kwa kila kosa la hijai – hadi 4

Ondoa nusu ( ½ ) alama kwa kila kosa la sarufi hadi makosa 4.

(Hoja zozote 5x2)

NAME…………………………………INDEX NO…………..CLASS………..

ADM NO……………DATE…………………………SIGN……………………

102/3

KISWAHILI

KARATASI YA 3

SAA: 21/2

MTIHANI WA PAMOJA WA BAHATI CLUSTER, TERM II, 2019

Kenya Certificate of Secondary Education (K.C.S.E)

MAAGIZO:

1) Jibu maswali Manne pekee.

2) Swali la kwanza ni la Lazima.

3) Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki, yaani; Hadithi Fupi, Fasihi Simulizi, Riwaya na Ushairi.

4) Usijibu maswali Mawili kutoka Sehemu moja.

5) Maswali yote yajibiwe kwa lugha ya Kiswahili.

6) Karatasi hii ina kurasa 6 zilizopigwa chapa.

7) Watahini lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa na kuwa maswali yote yamo.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI

SWALI

MADA

TUZO

1

TAMTHILIA

2

RIWAYA

3

HADITHI FUPI

4

USHAIRI

5

FASIHI SIMULIZI

JUMLA

SEHEMU YA A:TAMTHILIA

1. Lazima

K. Pauline: Kigogo

Majoka alitumia njia nyingi kudhibiti uongozi wake. Thibitisha ukweli huu. (alama 20)

SEHEMU B: RIWAYA

K.Matei: Chozi la Heri

Jibu swali la 2 au 3

2. Wanawake wamesawiriwa kwa mtazamo chanya katika jamii ya chozi la Heri. Jadili ukweli huu kwa kutoa ithibati mwafaka. (alama. 20)

3. “Ni mara ngapi mimi na babako husafiri na kukupagaza ulezi wa ndugu zako hawa? …umeweza kumuelekeza… katika kipindi hiki ambacho anatafuta utambuaji. Wewe pekee ndiwe dawa ya hasira … ya kivolkano. Bila wewe malezi ya hawa wadogo wako yangekuwa magumu.”

a)Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

b)Tambulisha mbinu tatu za sanaa zilizotumika katika dondoo hili. (alama 3)

c)Eleza sifa sita za mhusika “babako” aliyerejelewa katika dondoo hili. (alama 6)

d) “Ulezi ni ujima”. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea dondoo hili na riwaya yote kwa jumla. (alama 7)

SEHEMU YA C:HADITHI FUPI

A. Kochokocho A na D. Kayanda(Wah.): (Tumbo Lisilishiba na Hadithi Nyingine)

Jibu swali la 4 au 5

4. Jadili matatizo yanayokumba sekta ya elimu huku ukirejelea hadithi zozote tano katika diwani ya Tumbo Lisiloshiba.(alama. 20)

5. “…hata mapenzi yako yawe mazito namna gani…ni bora kuliko kasoro ya mapenzi.”

a)Eleza muktadha wa dondoo hili. (al. 4)

b)Tathmini umuhimu wa mnenewa.(al 6)

c)Thibitisha ukweli kuwa mapenzi yanayorejelewa yaligeuka na kuwa mazito kuliko ilivyotarajiwa na yakawa na kasoro nyingi. (al.10

SEHEMU YA D: USHAIRI

Jibu swali la 6 au 7

6. Soma shairi hili kisha ujibu maswali.

Jicho, tavumiliaje, kwa hayo uyaonayo?

Kicho, utasubirije, maonevu yapitayo

Kwacho, lijalo na lije, nimechoka vumiliyo

Naandika!

Moyo, unao timbuko, maudhui tuyasikiayo

Nayo, visa na mauko, wanyonge wayakutayo

Kwayo, sina zuiliko, natoa niyahisiyo

Naandika!

Hawa, wanotulimiya, dhiki wavumiliayo

Hawa, mamiya mamiya, na mali wazalishayo

Hawa, ndo wanaoumiya, na maafa wakutayo

Naandika!

Hawa, sioni wengine,kwao liko angamiyo

Hawa, uwapa unene, watukufu wenye nayo

Hawa, bado ni wavune, kwa shida waikutayo

Naandika!

Bado, wawapo mabwana, wenye pupa na kamiyo

Bado, tafauti sana, kwa pato na mengineyo

Bado , tuling’owe shina, ulaji pia na moyo

Naandika!

Maswali

a)Shairi hili laweza kuwekwa katika bahari zipi? Thibitisha kila jibu lako (ala4)

b) Eleza dhamira ya mshairi (ala2)

c)Onyesha mifano miwili ya uhuru wa kishairi jinsi ulivyotumika katika shairi (ala2)

d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (al.4)

e) Tambulisha kwa mifano mbinu zozote mbili za sanaa katika shairi. (ala2)

f) Fafanua sifa za kiarudhi zilizotumika katika ubeti wa tano. (al.3)

g) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi. (ala3)

i) Zuiliko

ii) Wavune

iii) Wenye pupa na kamiyo.

7. Soma shairi hili kisha ujibu maswali.

Amka!

Uondoe utandu machoni

Uone mtandao duniani

Uchawi wa karne hii

Uunganishavyo watu.

Amka!

Uwe mtu mpya

Uabiri mtandao ulimwenguni

Ukuvushe milima na mabonde

Ujuane na watu.

Amka!

Uwe na yako anwani

Udhibiti wavuti mkononi

Uone na uonekane kote

Uzungumze na watu

Ufurahie malimwengu

Amka!

Uone huu ulimwengu

Ulivyofanywa mdogo sasa

Ulivyopea kimawasiliano

Unganike na watu.

Amka!

Ukalie tarakilishi

Uangaze usioyajua

Uwasiliane kwa meme

Uunganike na watu.

Amka!

Uone nukulishi

Ubebe yako rununu

Useme na ulimwengu

Useme na watu

Maswali

a)Lipe shairi hili anwani mwafaka.(al. 2

b)Shairi hili ni la aina gani? Thibitisha.(al.2

c)Andika maneno manne yanayotaja teknolojia ya kisasa.(al.2

d)Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari.(al.4

e)Eleza toni ya shairi hili.(al.2

f)Tambulisha nafsi neni na nafsi nenewa.(al.2

g)Tambulisha kwa mifano mbinu mbili za lugha katika shairi hili.(al.2

h)Ni nini maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumika katika shairi. (al.4 )

i) Uchawi wa karne katika shairi

ii) Ukavushe milima na mabonde

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

(a)Eleza sifa nne za kimtindo zinazopatikana katika methali za Kiswahili.(alama 8)

(b) Eleza mbinu tatu ambazo hutumiwa kuzua misimu.(alama 6)

(c)Ni jukumu la jamii kudumisha fasihi simulizi. Dhihirisha.(alama 6)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

102/3

KISWAHILI

FASIHI

JULAI-2019

MUDA 2½

BAHATI CLUSTER EXAMINATIONS

MAAGIZO:

8) Jibu maswali Manne pekee.

9) Swali la kwanza ni la Lazima.

10) Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki, yaani; Hadithi Fupi, Fasihi Simulizi, Riwaya na Ushairi.

11) Usijibu maswali Mawili kutoka Sehemu moja.

12) Maswali yote yajibiwe kwa lugha ya Kiswahili.

13) Karatasi hii ina kurasa 6 zilizopigwa chapa.

14) Watahini lazima wahakikishe kurasa zote zimepigwa chapa na kuwa maswali yote yamo.

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA BAHATI CLUSTER, JULAI 2019 (II)

1)Njia alizotumia Majoka kudhibiti uongozi wake

· Majoka anatumia vyombo vya habari kufanya matangazo yake: mwezi mzima wa kusherehekea uhuru pamoja na kuzaliwa kwake bila kujali watu watakula nini wasipofanya kazi.

· Majoka anapanga mauaji ya wanaompinga. Ajali iliyosababisha kifo cha jabali, kiongozi wa chama cha Mwenge, (Uk. 35).

· Majoka anatumia Vyombo vya dola( askari) kuwafurusha waandamanaji pamoja na kuwaangamiza. Vijana watano waliuawa wakati wa maandamano.

· Anatangaza kuwa maandamano ni haramu huku akiwataka polisi kutumia kutumia nguvu zaidi. Kenga anasema, “Tangaza kuwa maandamano ni haramu, kisha uwaamuru maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi.”

· Anapanga kutumia wahuni kunyamazisha watetezi wa wachuuzi wa Sagamoyo. Kenga anataka kumwangamiza Tunu anaposema, “Lazima tuwawekee vidhibiti mwendo na hatimaye tuwakomeshe kabisa.”

· Anatoa amri ya kuwazuia wahisani wa wapizani wake kwa kudai kuwa Sagamoyo ina uwezo wa kujitegemea. Majoka anasema, “Na hawa wafadhili wao nao lazima wavunje kambi zao. Sagamoyo twajiweza.”

· Majoka anatoza kodi zaidi ya inavyohitajika. Wachuuzi wanalipa kodi na kitu juu yake. Anaongeza mishahara ya walimu na wauguzi lakini anaongeza kodi kwa asilimia kubwa.

· Wasamoyo hawapewi uhuru wa kumchagua kiongozi wanaomtaka. Anapanga kuwa mtoto wake Ngao Junior atatangazwa kuwa mrithi wake.

· Majoka anazima uhuru wa vyombo vya habari. Anatoa amri ya kufungwa kwa Runinga ya Mzalendo kwa kutangaza moja kwa moja maandamano yaliongozwa na Tunu.

· Anawaamrisha askari kuwatawanya waandamanaji kwa vitoa machozi na risasi.

· Anamrisha lini watu watazikwa:Majoka anaagiza Chopi kuhakikisha maiti ya Ngurumo imezikwa siku hiyo hiyo kabla ya jua kutua kwani hataki kilio wakati wa sherehe.

· Majoka anafuga chatu, nyoka hatari na wenye sumu kali ambao huzunguka na hata kuwaangamiza Wasagamoyo ovyo. Ngao Junior na Ngurumo wanaangamizwa na chatu.

· Kutoa amri za kikatili:Katika siku ya kusherehekea uhuru, Majoka alimtaka mkuu wa polisi, Bwana Kingi kuwapiga risasi Tunu na Sudi kwa kuandaa mkutano nje la Soko la Chapakazi.

· Propaganda:Nyimbo za kizalendo zinachezwa katika redio baada ya matangazo maalum ni njia mojawapo ya kuwafumba macho Wanasagamoyo. Nyimbo hizi zinalenga kuwafanya wananchi kuona kuona kuwa Majoka anaendeleza demokrasia.

· Kutumia vikaragosi: Ngurumo pamoja na walevi wenzake wanaimba wimbo wa kumsifu Majoka kule mangweni.

· Kutumia uongo:Jamii ya Majoka inaeneza uongo kuwa wapinzani wote ni watu ambao si wazaliwa wa jimbo la Sagamoyo na wanapaswa kuhama. (Uk 51-52).

· Kutoa chatu kama kafara: Baada ya kifo Ngurumo, Majoka anamweleza Chopi kuwa lazima chatu mmoja atolewe kafara ili watu wajue kuwa usalama upo.

· Kutumia wahuni kueneza uvumi:Majoka anatumia wahuni kueneza uvumi kuwa Sudi na Ashua ndio wanaowinda nafsi ya Tunu.

· Kuchagua mashauri kutoka familia: Mashuri wake mkuu Bwana Kenga alikuwa ni binamu yake. Alikuwa nanamtumia kushawishi wasagamoyo kama Sudi ili wakubali matakwa yake.

· Kumia vitisho:Alitishia Tunu, Sudi na Ashua walipoenda ofisini mwake.

· Kupanga mauaji ya wapinzani: Majoka anapanga njama ya kuua Tunu ingawa kwa bahati yake Tunu, Chopi aliyepewa maagizo hakuyatimiza ipasavyo. Majoka na Kenga wanakubaliana kumuua Chopi ili asitoe siri zao.

· Kuwaua wapizani wake: Majoka alishiriki kwenye njama za kumuua Jabali ambaye aliuawa kwa ajali.

· Kuwazawadi wafuasi wake: Kenga alikuwa amegawiwa kipande cha ardhi katika soko la chapakazi. Mkewe Ngurumo mama Pima alipewa kibali cha kuuza pombe haramu.

(Zozote 20x1)

2) Mtazamo chanya wa wanawake

· Amekengeuka: Terry anamwonya Ridhaa mumewe kutoshiriki imani za kishirikina maana zilimtia wasiwasi bure.

· Wasomi: Wanawake waliosoma ni kama: Apondi, Neema, Bi.Tamasha, Tamira, Umulkheri, mamake Zohali.

· Wapenda masomo: Tila, Chandachema, Mwanaheri, Tuama, Rehema, Pete. Hata kama wengine hawakuweza kuendelea na masomo.

· Wavumilivu:Mwekevu kustahimili matusi ya wanaume na kutengwa na wanawake alipokuwa anapigania uongozi. Chandachema kuvumilia mengi baada ya kifo cha nyanyake.Neema alivumilia kero za wanajamii waliomwonea kwa kukosa mtoto.

· Faraja katika ndoa/mwamba katika ndoa: Licha ya mwangeka kuwa na jumba kubwa na kuishi na babake alihitaji mtu “…alihitaji mtu wa kumpembeja, kumliwaza…mwenzi katika uzazi na malezi (uk.110). Ridhaa anamhimiza Mwangeka kuoa tena. Kiriri alimsihi Annete asiondoke na kumwacha pweke. Lunga alikufa baada ya mwaka mmoja wa kuachwa na Naomi.

· Mwenye bidii kazini: Mwekevu alitia bidii kazini mwake akiwa mkurugenzi wa shirika la Chemichemi. Kwa bidii yake watu walipata maji ya visima.

· Mwenye bidii masomoni: Umulkheri alitia bidii masomoni na kuwa mhandisi. Wengine kama Neema, Apondi walitia bidii masomoni na kupata ajira.

· Mwenye bidii ya kupata riziki na kukimu familia: Mamake Kairu alifanya biashara yake ya kuuza samaki. Halua mkewe Shamsi licha ya ugumu wa maisha alijibidiisha kupata riziki.

· Amewajibika kama mzazi: Mamake Tindi na Lemi aliwaruhusu kwenda matembezini lakini akawaonya wasichelewe kurudi nyumbani. Walipokosa kurudi alienda kuwatafuta. Mamake Kairu alihakikisha mtoto wake ako shuleni na kusoma licha ya ukosefu wa fedha.

· Amewajibika kazini: Selume hangeondoka hospitalini baada ya zamu yake kabla ya kumtembeza muuguzi mwenzake (Meko) kwa wagonjwa.

· Amewajibika katika kuwadhibu watoto: Mamake Mwangeka na mamake Mwangemi waliwadhibu wana wao kwa kumuiga babu yao.

· Mcha Mungu: Wanawake katika makundi mbalimbali ya kidini walihusika pakubwa katika ugavi wa chakula cha msaada kwa wahasiriwa wa vita vya baada ya uchaguzi. Walikuwa wa CWA, Women’s Guild, Mothers Union. Lily Nyamvula alikiri kuwa mwokovu (born again) na hakutaka mumewe kufanya kazi ya uanajeshi.

· Watumishi wa Mungu kwa kuwa watawa: Mtawa Pacha, Cizarina na Anastacia ni watawa waliotumikia Mungu kila siku bila kuolewa.

· Wakarimu/wahisani:Wanawake wajane walikuwa wameanzisha makao ya watoto mayatima ya Jeshi la Wajane wa Kristu. Waliwapa hifadhi watoto wenye mahitaji kama Chandachema.

· Viongozi: Mwekevu alichaguliwa kama kiongozi wa Wahafidhina. Tamasha alikuwa Mwalimu mkuu wa shule ya Kilimo. Mamake Zohali alikuwa mwalimu mkuu wa shule ya upili.

· Msiri: Mamake Kipanga hakumweleza mwanawe kuhusu babake. Mamake Sauna hakumwambia kwa muda mrefu kuwa Maya hakuwa babake mzazi.

· Jasiri: mamake Kairu aliongoza wanawe kumzika mwanawe aliyefia mgongoni. Mwekevu alipigania uongozi kwa ujasiri mkubwa.

· Mwenye utu: Wanawake kadhaa wameonyesha utu kwa kuwasaidia waliokuwa na mahitaji. Wao ni kama: Nyanyake Chandachema, Neema, Apondi, Mwalimu Dhahabu n.k.

· Msamehevu: Umulkheri pamoja na nduguze walimsamehe mama yao Naomi na kuamua kumtafuta.

· Hatibu mzuri: Rachel Apondi alitoa hotuba nzuri ili kuwahimiza walinda usalama kuwajibika zaidi.

· Wenye adabu njema/busara: Selume aliongea akiwa mbali kabla ya kuingia kibanda cha Kaizari kwenye kumjulia hali mkewe na binti zao. Alijua kuwa vibandani hakukuwa na faragha.

(Zozote 20x1)

3)

a)Muktadha (al. 4)

· Maneno haya yalisemwa na Rachel Apondi. Alikuwa akimwambia mtoto wake wa kupanga Umulkheri. Walikuwa katika hoteli ya Majaliwa walipokuwa wakisherehekea siku yake Umu ya kuzaliwa. Apondi anamshukuru Umulkheri kwa kuchangia katika ulezi wa dadake Sophie aliyekuwa mwepesi wa hasira.

b)Mbinu tatu za lugha (al.3

· Swali la balagha “…kukupagaza ulezi wa ndugu zako hawa?”

· Istiari-Ndiwe dawa ya hasira

· Utohozi-Kivolkano (volcano) (3x1)

c)Sifa za Mwangeka(al. 6

· Mcha Mungu: Anashukuru Mungu baada ya kupata Umu ambapo anaona ni binti wa kufidia mwanawe Becky aliyekufa kwa ajali ya moto.

· Mvumbuzi:Anavumbua gari kwa jina Ngokoo ambalo Mwangeka anadai ndilo lilikuwa ka kwanza la Kiafrika.

· Mwenye ukiwa na upweke: Anaishi kwa ukiwa na upweke nyumbani kwake kutokana na kifo cha mkewe na mtoto.

· Mwenye msimamo thabiti:Licha ya kushawishiwa na mkwewe aache kazi ya uanajeshi kwa kuwa inahusisha uuaji, haachi kamwe.

· Mzalendo:Anadhihirisha uzalendo wake kwa kutaka kuwahudumia watu wengi katika udumishaji wa amani kama mwanajeshi katika Mashariki ya kati.

· Mwenye bidii:Anasoma kwa bidii mpaka akajiunga na chuo kikuu na kusomea shahada ya uhandisi.

· Mwenye mapenzi ya dhati kwa babake na mtoto wake wa kupanga Umulkheri: Anamkumbatia babake kwa mapenzi baada ya kuwasili kwa ndege katika uwanja wa kimataifa wa Ndege wa Rubia.

· Mtambuzi: anatambua kwamba babake amezeeka zaidi na kushabihiana na babu yake Mwangeka, Mzee Msubili.

· Mtundu: Kwa utundu wa kitoto ananyang’anywa babake stethoskopu na kuitia katika shingo ya yeye Mwangeka, kisha anamlaza babake kama mgonjwa ili amtibu.

· Mwenye wasiwasi alipokuwa mdogo: Ana mashaka na udhaifu kutokana na kutokuwepo na babake Ridhaa alipokuwa ameenda katika shughuli za kimatibabu.

· Mlezi Mwema: Akishirikiana na Mke wake Apondi wanamlea Umulkheri, Sophie na Ridhaa na kumsomesha hadi anafanikiwa.

· Mkarimu: alionyesha ukarimu mkubwa sana kwa Umulkheri. Aidha baada ya Dick naye kupatikana, Mwangeka na mkewe walimtunza pia kama mwana wao.

· Mdadisi: Kabla ya kujenga jumba lake alifanya utafiti wa kutosha kuhusu ardhi aliyotaka kununua. (6x1)

d)Ulezi ni ujima

Ulezi ni ujima inamaanisha kuwa ulezi ni wa watu wengi wakishirikiana; kwa ujumla si wa mtu mmoja au wazazi pekee. Yaani kila aliyewajibika anapaswa kuchangia. ( Tanbihi:Mwanafunzi aonyeshe isipokuwa mzazi mtoto alilelewa na watu wengine)

· Umulkheri alilelewa na mamake Naomi kwanza. Baadaye anachukuliwa kama mtoto wa kupanga na Mwangeka na Rachel Apondi ambao wanamlea na kumsomesha.

· Umulkheri aliwalea dadake Sophie na kumshauri wakati wazazi wake walikuwa wamesafiri. Ulezi huu ulisaidia kudhibiti hasira za Sophie.

· Chandachema alilelewa na jirani Satua kwa muda mfupi. Baadaye akatunzwa na nyanyake. Nyanyake alipoaga akajikuta akillelewa na Tenge na mke wake Kimai. Mwishowe alijipata katika makao ya watoto ya Jeshi la Wajane wa Kristu akilelewa na wasimamizi wa shirika hilo.

· Zohali alilelewa na wazazi wake na alipotoroka nyumbani alilelewa na Mtawa Pacha aliyemtoa katika aibu ya kukaa mitaani.

· Sauna alilelewa na mamake na baba wa kambo Maya bila kujua kuwa si babake mzazi.

· Mwaliko alilewa na dadake Umu baada ya mamake kuondoka.Baadaye akalelewa na watawa wa Benefactor kama Anastacia. Mwishowe akalelewa na Mwangemi na mkewe Neema.

· Mwangeka na Mwangemi waliadhibiwa na babu yao Mwimo msubili kwa sababu ya kumuiga. Babu anahusika na malezi ya wajukuu wake na kuwaadabisha.

· Mwalimu Dhahabu alichangia kaika ulezi wa mwanafunzi wake Umu. Alimshauri awe makini darasani. Pia alimkutanisha na wazazi wake wa kupanga.

· Pete alilelewa na nyanyake baada ya wazazi wake kutengana kwa sababu baba alisingizia kuwa si mtoto wake kwani hafanani naye.

· Cynthia analelewa na Neema baada ya wazazi wake kufariki. Anamlea kama mtoto wake.

· Riziki Immaculata, kitoto kilichookotwa na Neema kikiwa kimetupwa njiani kinapelekwa katika makao ya watoto ya Benefactor na kuanza kulelewa na Mtawa Cizarina. (7x1).

Hadithi fupi

4)Matatizo yanayoathiri sekta ya elimu

Mwalimu mstaafu

· Watoto wasioelewa masomo bado kushinikizwa kuendelea na masomo na walimu wao. Kipawa cha Jairo kingegunduliwa mapema na aelekezwa na kushauriwa ipasavyo. Mwalimu Mosi alimshauri aendelee na masomo licha ya kwamba hakuwa anaelewa.

· Wanafunzi kupewa matumani yasiyo na msingi. Jairo alipewa matumaini kuwa ujinga wake utaisha na aweze kupata mia kwa mia.

· Wanafunzi kuwalaumu walimu kwa matatizo wanaojiletea. Jairo anamlaumu mwalimu Mosi kwa sababu ya ufukara wake ambao umesababishwa na ulevi.

· Wanafunzi kupuuza ushauri wa mwalimu na kujipata kwa matatizo. Jairo alipuuza ushauri wa Mwalimu Mosi. Alishauriwa aepukane na ufuska lakini akadida.

· Wanafunzi kufukuzwa shuleni kwa kukosa vifaa muhimu. Binti wa Jairo Sabina alifukuzwa shuleni kwa kukosa vitabu vya hisabati. Mwalimu Mosi alienda mjini ili akanunue. Hii husababisha muda wa masomo kupotea.

Mapenzi ya Kifaurongo

· Wazazi kukosa pesa za kugharimia mahitaji ya wanafunzi. Dennis Machora alikosa chakula na mavazi mazuri akiwa chuo kikuu.

· Wanafuzi kujihusisha na mapenzi ya uongo wakiwa chuoni: Dennis alidanganywa na Penina na kukubali kuwa mpenzi wake wakiwa chuoni lakini baadaye akafukuzwa kama mbwa alipokosa kazi. Mapenzi kama haya hupoteza muda wa wanafunzi.

· Ukosefu wa ajira:Wanafunzi kusomeshwa masomo yanayowaelekeza kupata kazi za kiofisi wala sio kujiajiri. Dennis alitafuta kazi aliyosomea kwa miaka kadhaa bila kupata.

· Wahadhiri wasiowajibika: Badala ya Dkt Mabonga badala ya kuwajibika kuyajibu maswali ya wanafunzi anawatusi. Anatumia lugha changamano ambayo baadhi ya wanafunzi hawaelewi.

· Wanafuzi wazembe: Katika kujibu swali la mwanafunzi Dkt. Mabonga anaashiria kuwa baadhi ya wanafunzi ni wazembe “kupiga ubwete” kwani wengine hawataki kufanya utafiti ili waelewe alichokuwa anasema mwalimu. Wanataka waelezwe kila kitu kama watoto. “Wanafunzi wa chuo kikuu si watoto” (uk. 14).

· Wanafunzi kutoka tabaka la chini kujitenga. Hawataki kutangamana na wengine. Dennis anaingiliana na wanafunzi wengine kwa nadra sana.

Shogake Dada ana Ndevu

· Wanafunzi wanafiki wanaodanganya wazazi wao. Safia anadanganya wazazi wake ili Kimwana akubaliwe wadurusu pamoja. Badala ya kusoma walikuwa wanajihusisha na mapenzi.

· Wanafunzi kujihusisha na mapenzi kiholela: Safia na Kimwana wanajihusisha na mapenzi huku wakisingizia kuwa wanasoma.

· Wanafunzi kufa huku wakijaribu kuavya mimba. Safia alienda kiliniki kuavya mimba lakini akafa.

· Wanafunzi kutumia dini kufunika uovu wao. Safia alikuwa anajifunika gubigubi na kuacha macho pekee hata akiwa ndani mwa nyumba. Kimwana naye alikuwa anavaa buibui ili kuficha jinsia yake.

· Wazazi kutokuwa makini kuchunguza wanayofanya watoto wao. Bwana Masudi na Bi. Hamida hawakuwa makini kuhakikisha kama kweli Safia walikuwa wanadurusu.

· Wazazi kuamini watoto zaidi katika maswala ya masomo yao bila uhakika. Safia alifaulu kuwadanganya wazazi wake.

Mtihani wa Maisha

· Wafunzi kukata tamaa ya kuishi baada ya kufeli mtihani:Samueli anafanya jaribio la kujiua baada ya kukosa kufaulu katika mtihani wake.

· Wanafunzi wanaodaiwa karo hawapewi matokeo ya mtihani: Mwalimu mkuu wa shule alikosomea Samueli alikuwa na daftari iliyokuwa na majina ya wale waliodaiwa na shule ambao hawangepata matokeo yao.

· Wanafunzi kutozingatia masomo: Shuleni Samueli hakuzingatia masomo. Alikuwa anaitwa na wanafunzi wengine “Rasta” kwa sababu ya mahoka yaani vituko vyake.Hajui mito katika bara la Afrika iko katika sehemu ipi. Anajidanganya kuwa anajua. (uk.135)

· Wanafunzi kuwadanganya wazazi kuhusu matokeo ya mtihani: Samueli hakusema ukweli kuhusu matokeo yake lakini alidanganya wazazi wake.

· Wazazi kuwaona wanafunzi walioanguka mtihani kama bure na wasio na faida. Wanashindwa kuwashauri. Babake Samueli anamtusi Samueli. “Anafaida gani huyu…sikuzaa mwana nilitoa maradhi tumboni.”

Mame Bakari

· Wanafunzi kutendewa uhalifu/kubakwa: Sara alibakwa siku moja jioni alipokuwa anatoka shuleni. Hii ni ishara ya ukosefu wa usalama kwa wanafunzi.

· Masomo ya ziada/twisheni:Aghalabu masomo haya huwa yanaripiwa na huweza kuwa mzigo kwa wazazi wengine. Pia masomo haya hufanywa jioni wakati watoto wengine wameenda nyumbani.Hii huhatarisha usalama wa mwanafunzi. Sara alibakwa alipokuwa anatoka masomo ya ziada.

· Mimba za mapema: Baada ya kubakwa Sara alipata mimba na hili lilisababisha kukatiza masomo yake pengine kwa muda.

· Msongo wa mawazo (stress): Sara baada ya kugundua kuwa ni mja mzito alikuwa anajifungia chumbani na kulia na kuomboleza kwa sababu ya msongo wa mawazo.

· Kufukuzwa shuleni kwa sababu ya ujauzito: Kulingana na maelezo ya Sara wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni walifukuzwa. “Hii ni skuli ya wanafunzi, mama, sio wazazi” angeambiwa Sara na Mwalimu mkuu. (Hoja zozote 20x1)

5. a)Muktadha wa dondoo hili

· Mnenaji ni Dadi alikuwa anamwambia Kidawa katika hadithi ya Masharti ya Kisasa. Alikuwa akimjibu wakati Kidawa alimjia na kumuuliza iwapo kama angeweza swala la mapenzi. Dadi alikuwa ametafuta mapenzi kwa Kidawa kwa siku nyingi lakini akakataa.

b)Umuhimu wa Kidawa

· Anawakilisha mwanamke wa kisasa ambaye anataka kuolewa lakini kwa masharti.

· Mfano wa wanawake wa kisasa wanaoweza kufanya kazi usiku na mchana na anayependa mitindo ya mavazi ya kisasa.

· Ni mfano wa wanawake wenye msimamo thabiti. Tokea mwanzo alimwambia Dadi yeye ni mwanamke wa kisasa na hakubadilisha msimamo huo.

· Ni kieleleza cha wanawake wanaoamini kuwa lazima wawe na mchango katika kutwalia jamii hata kama itawabidi wafanye kazi usiku.

· Ni mfano wa wanawake wenye bidii katika maisha. Anafanya kazi za nyumbani, ya umetroni na mchana anauza bidhaa.

· Ni kielelezo cha wanawake waaminifu katika ndoa licha ya kuwa alikuwa anafanya kazi usiku wakati mwingine. Alihiari kujiuzulu wakati aliona ndoa yake iko hatarini.

· Ni mwangwi wa mabadiliko katika ndoa. Anadhihirisha kuwa siku za mwanamke kuonewa na kunyanyaswa zimeisha.

c)Mapenzi kuwa mazito (kuwa na ugumu)

· Masharti ya kidawa yamlemea Dadi anashindwa kufanya kazi za nyumbani. Aiona kuwa kazi za nyumbani zilipaswa kuwa za mke.

· Kwa sababu ya kumshuku mkewe Dadi alishindwa kuongea na mkewe kuhusu wasiwasi aliokuwa nao.

· Fasheni za kisasa na kujipondoaalikopenda Kidawa zilimfanya Dadi kuwa na wasiwasi kwamba anafanya hivyo ili afurahishe wanaume wengine.

· Maneno ya “kutembeza bidhaa” mitaani ilimuudhi sana Dadi kila wakati Kidawa alipoyatumia.

· Dadi alishindwa kula chakula alichoandaliwa na Kidawa kwa sababu alikuwa anafikiria jinsi mkewe anavyomwendea kinyume.

· Wakati Kidawa alimuuliza Dadi kama anapendeza baada ya kuvaa, Dadi alishindwa kumjibu. Hakutaka kumsifu mkewe kwani alidhani anaenda kustarehe na wanaume wengine.

· Dadi alichukizwa na tabia ya mkewe kusimama na kuongea na wanaume wengine

· Kanzu ya Kidawa kumfika magoti Dadi aliona itawafanya wanaume wengine kumtumbulia macho kwa kumtamani. Kidawa aliamini mwanamke ana haki ya kuvaa anavyopenda.

· Kidawa alimkashifu mumewe kwa kutofuata masharti ya ndoa na hata akikumbushwa hujifanya hayafahamu.

· Kidawa anamkashifu Dadi kwa kusususia kula chakula na kukosa kuondoa vyombo juu ya meza.

· Dadi alimnyamazia mkewe baada ya kukashifiwa kutofuata masharti ya ndoa.

· Dadi alienda hadi shuleni anakofanya kazi ya umetroni mkewe ili kumchunguza kama alikuwa na uhusiano na mwalimu mkuu.

6. Ushairi

(a)Tarbia-Lina mishororo minne katika kila ubeti

Msuko-Kibwagizo kimefupishwa

Ukara-Vina vya nje vinatiririka katika beti zote ilhali vya ndani havitiririki.

Kikwamba-Katika beti 3-5 neno moja ndilo linaanza kila mshororo.

Sakarani-Kuna bahari kadhaa katika shairi.

(b)Kuwahimiza watu (hasa wanyonge) wainuke na kupinga maovu na maonevu wanayofanyiwa na matajiri wenye uwezo.

(c)Inkisari km vumuliyo-kuvumilia manaandika.

Mazida kurefusha k.m angamiyo,vumiliyo n.k

Tabdila k.m mamiya dadala ya mamia

(d)Hawa wanaotulimia wanavumilia dhiki

Wao ni wengi na ndio huzalisha mali.

Wao ndio wanaoumia na kupata mateso/taabu

Wanayokumbana nayo.Ninaandika /ninasema

(e)Takriri-hawa,bado,mamiya.

Balagha-uyaonaje?

Inkisari-Hawa,ndo

Kinaya watukufu wenye nayo

(f)Kuna mishororo minne

Kuna vipande vitatu katika mishororo ya kwanza mitatu na kimoja katika kibwagizo

Vina vinatiririka/vinafanana

Mizani2,-6-8

2-6-8

2-6-8

4

(g)(i)Cha kunizuia /kizuizi/kizingiti/uogozi/hofu/pingamizi

(ii)Wachovu/dhaifu/hafifu

(iii)Walio na tama kubwa /walafi/mabwanyenye

7. Ushairi

a) Anwani mwafaka:

· Teknolojia

· Teknolojia ya kisasa

· Njia mpya ya mawasiliano

· Usasa katika kuwasiliana

b)Shairi hili ni huru kwani halizingatii arudhi: (2x1)

· Mishororo imetofautiana katika beti mbalimbali. Mf. Ubeti 3 unamishororo 6

· Mizani inatofautiana katika mishororo katika beti mbalimbali.

c)Andika maneno manne yanayotaja teknolojia ya kisasa:( 4x1/2)

· Mtandao

· Wavuti

· Tarakilishi

· Nukulishi

· Rununu

· Meme

d)Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari.

· Mshairi anasema kuwa tuzinduke tupate kunufaika kwa matumizi ya nukulishi. Tubebe simu za mikononi ili tuwasiliane na ulimwengu wote wa watu uliomo.

e)Eleza toni ya shairi hili. (al.2

· Toni ya kuamrisha. Anaarisha watu wazinduke na kutumia teknolojia.

f)Eleza nafsi neni na nafsi nenewa.(al.2

· Nafsi neni-mweledi wa teknolojia/mwenye ujuzi wa teknolojia ya kisasa.

· Nafsi nenewa-mtu mpya/asiye na ufahamu mpana wa teknolojia

g)Mbinu za lugha

· Jazanda-Uchawi wa karne(uvumbuzi wa ajabu)

· Takriri-Amka, useme

h)Maana ya vifungu vifuatavyo:

· Uchawi wa karne -uvumbuzi/ uundaji wa mambo mapya ya kiteknolojia katika karne hii.

· Ukavushe milima na mabonde-Uweze kuwasiliana na wengine ulimwengu kote (pembe zote za dunia/walio mbali)

· Uwasiliane kwa meme-Uwasiliane kwa barua iitwayo meme kwa kutumia mtambo wa talakilishi.

8. Fasihi simulizi

(a)Eleza sifa nne za kimtindo zinazopatikana katika methali za Kiswahili.(alama 8)

(i)Takriri:urudiaji wa maneno

-Bandu bandu huisha gogo

-Haraka haraka haina Baraka

(ii)Taswira (picha)

-Njia mbili zilimshinda fisi

-Paka akiondoka panya hutawala

(iii)Sitiari:mithilisha kitu kimoja na kingine moja kwa moja

-Mgeni ni kuku mweupe

-Ujana ni moshi

(iv)Kejeli/dhihaka

-Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti

-Maskini akipata matako hulia mbwata!

(v)Balagha:maswali yasiyohitaji jibu kwa vile jibu ni bayana

-Umekuwa mumumenye kuharibikia ukubwani?

-Pilipili usiyoila yakuashiani?

-Angurumapo samba mchezo ni nani?

(vi)Tashbihi:ulinganisho kwa kutumia kilinganishi

-Mapenzi ni kama majani popote penye rotuba hujiotea.

-Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza.

(vii)Kweli kinzani:hali inayopingana

-Mpanda ngazi hushuka.

-Kuinamako ndiko kuinukako

(viii)Chuku:maneno yasiyo ya kweli

-Polepole za kobe hufikisha mbali.

-Ukiwa makini utayaona macho ya konokono

(ix)Kinaya;kinyume na matarajio

-Ngoja ngoja huumiza matumbo

(iix)Tashihisi/uhaishaji/uhuishaji

-Sikio la kufa haliskii dawa

-Siri ya mtungi muulize kata {Zozote 4x2.sifa alama 1mfano1

(b).Eleza mbinu tatu ambazo hutumiwa kuzua misimu.(alama 6)

1. Kutumia tanakali-neno mtutu-Bunduki/ hali ya kuachilia risasi

(ii)Utohozi wa maneno

Gava-Government.

Hedi-Head

Fadhee -Father

(iii)Maneno ya kawaida kupewa maana mpya

Toboa-faulu

Chuma -Bunduki

(iv)Matumizi ya tabdila

Njaro-Ndaro

(v)Kufupisha maneno

Kompyuta -komp.

(vi)Kutokana na umbo/rangi ya kinachorejelewa

Mfano Blue -Noti ya kitambo ya shilingi ishirini

Tangi-Mtu mwenye umbo nane

(vii)Kutumia isitara au jazanda

Golikipa-nyani

Mtu mlafi-Fisi

(viii)Kuunda maneno mapya kabisa;. mfano

Kuhanya-Usherati

keroro-Pombe

Kusikia ubao-Hisi njaa

Ni kubaya-hali si nzuri [ 3x2]

(c).Ni jukumu la jamii kudumisha fasihi simulizi. Dhihirisha.(alama 6)

(i)Kuendelea kufundisha Fasihi Simulizi shuleni

(ii)Kufanya Fasihi Simulizi kuwa hai kiutendaji kupitia shehere na hafla tofauti za kiserikali

(iii)Kuhifadhi tanzu mbalimbali ili vizazi vijavyo viweze kuzifahamu mfano kwa kurekodi

(iv)Kufanya utafiti wa kina kuhusiana na tanzu za Fasihi simulizi.

(v)Kuhakikisha kuwa lugha za kiasili hazififii kwa vile ndizo chanzo cha Fasihi simulizi(vi)Kuonyeshwa kwa fani mbalimbali za Fasihi simulizi kwenye vyombo vya habari kama kama runinga.

(vii)Kuhimiza wanajamii hususan viongozi kuwasilisha ujumbe wao kwa kutumia fani za Fasihi simulizi kwa mgano hotuba, ulumbi, mawaidha nk.

(viii)Kuhimiza wanajamii kuionea fahari jadi hii na kushiriki kikamilifu katika matumizi ya fani mbalimbali mfano nyimbo.

(ix)Kusisitiza uendelezwaji wa fani zake katika mashindano ya shule na hata baina ya shule tofauti kimaeneo na kitaifa. [6x1]

1