DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

13
1 Muandishi: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH Mfasiri: Abu Farida Muhammad Basawad Web Site: http://www.qssea.net Tarehe: 22nd June, 2020 Dhul Qa’dah, 1, 1441 H UISLAMU hutoa mwongozo kwa wafuasi wake katika awamu zote na shughuli za ki- maisha, katika mas’ala, vifaa vya uundaji na vile vile vya kiroho. Mafundisho yake ya kimsingi kuhusu uchumi yametajwa katika vifungu kadhaa vya Qurân. Mbali na kudharau ustawi wa vifaa vya kujimudu, inatambua (4/5) kuwa: اَ يه فيۡ مُ وهُ قُ زۡ ٱرَ ا وٗ م َ ي قيۡ مُ كَ لُ ّ ٱَ لَ عَ ج ي ّ ٱلُ مُ كَ ل َ وۡ مَ أ٥ "Bidhaa zako ambazo Mungu ametengeneza kama njia ya kujikimu kwako." [An-Nisâ’ 4:5] Na inaamuru: اَ يۡ نْ ٱَ مينَ كَ يب صيَ نَ نسَ تَ َ و "Wala usisahau fungu lako la dunia." [Al-Qaswas 28/77] Walakini, imetilia mkazo katika sehemu mbili kwa mwanadamu, kwa kuwakumbusha yakuwa: ٖ ق َ لَ خۡ ةي مينَ خير ٱ ي ۥُ َ اَ مَ ا وَ يۡ نْ ٱ ي اَ اتينَ ءٓ اَ نّ بَ رُ ولُ قَ ن يَ اسي مّ ٱَ مينَ ف٢ نّ م مُ هۡ مينَ و ي اتَ ءٓ اَ نّ بَ رُ ولُ قَ ي ٱ ي َ وٗ ةَ نَ سَ ا حَ يۡ نْ ٱ ي اَ ن ي ارّ ٱَ ابَ ذَ ا عَ قينَ وٗ ةَ نَ سَ ةي حَ خير٣ ۡ مُ هَ لَ ك ي ئ َ لْ وُ أ ي ابَ يسۡ ٱُ يع يَ ُ ّ ٱَ و ْ واُ بَ سَ ا كّ يم مٞ يب صيَ ن٤ “...Na wapo baadhi ya watu wanao sema: Mola wetu Mlezi, tupe duniani! Naye katika Akhera hana sehemu yoyote. Na katika wao wapo wanao sema: Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto! Hao ndio watakao pata sehemu yao kwa sababu ya yale waliyo yachuma. Na Allâh ni Mwepesi wa kuhisabu.” [Al-Baqarah: 200-2] Katika aya nyengine tunaona imewekwa wazi na dhahiri yakwamba, yote yanayopatikana ardhini, baharini na hata mbinguni yameumbwa na Mwenyezi Mungu kwa faida ya mwanadamu; au yakwamba yote yaliyo duniani, mbinguni, baharini, kwenye nyota na sehemu nyengine yamefanywa kuwa wanyenyekevu kwa mwanadamu na Mwenyezi Mungu. Inabaki kwa mwanadamu kujua na kufaidika kutokana na uumbaji wa Mwenyezi Mungu, na kufaidika kwa njia ya kimantiki, ikizingatia siku za usoni. Sera ya kiuchumi ya Uislamu pia imeelezewa katika Qur’ân, kwa maneno mengi yasiyokuwa na shaka:

Transcript of DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

Page 1: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

1

Muandishi: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH Mfasiri: Abu Farida Muhammad Basawad Web Site: http://www.qssea.net Tarehe: 22nd June, 2020

Dhul Qa’dah, 1, 1441 H

UISLAMU hutoa mwongozo kwa wafuasi wake katika awamu zote na shughuli za ki-maisha, katika mas’ala, vifaa vya uundaji na vile vile vya kiroho. Mafundisho yake ya kimsingi kuhusu uchumi yametajwa katika vifungu kadhaa vya Qurân. Mbali na kudharau ustawi wa vifaa vya kujimudu, inatambua (4/5) kuwa:

لكم قييما وٱرزقوهم فييها تي جعل ٱلللكم ٱل مو

٥أ

"Bidhaa zako ambazo Mungu ametengeneza kama njia ya kujikimu kwako." [An-Nisâ’ 4:5]

Na inaamuru:

نيا يبك مين ٱلد ٧٧ول تنس نصي"Wala usisahau fungu lako la dunia." [Al-Qaswas 28/77]

Walakini, imetilia mkazo katika sehemu mbili kwa mwanadamu, kwa kuwakumbusha yakuwa:

رةي مين خلق نيا وما لۥ في ٱلأخي ينا في ٱلد ن ٢٠٠فمين ٱلناسي من يقول ربنا ءات ومينهم منيا حسنة وفي ٱلأيقول ربنا ءاتي رةي حسنة وقينا عذاب ٱلناري نا في ٱلد ئيك لهم ٢٠١خي

ولأ

سييع ٱليسابي وٱلل ا كسبوا يم يب م ٢٠٢نصي“...Na wapo baadhi ya watu wanao sema: Mola wetu Mlezi, tupe duniani!

Naye katika Akhera hana sehemu yoyote. Na katika wao wapo wanao sema: Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na

adhabu ya Moto! Hao ndio watakao pata sehemu yao kwa sababu ya yale waliyo yachuma. Na Allâh ni Mwepesi wa kuhisabu.”

[Al-Baqarah: 200-2]

Katika aya nyengine tunaona imewekwa wazi na dhahiri yakwamba, yote yanayopatikana ardhini, baharini na hata mbinguni yameumbwa na Mwenyezi Mungu kwa faida ya mwanadamu; au yakwamba yote yaliyo duniani, mbinguni, baharini, kwenye nyota na sehemu nyengine yamefanywa kuwa wanyenyekevu kwa mwanadamu na Mwenyezi Mungu. Inabaki kwa mwanadamu kujua na kufaidika kutokana na uumbaji wa Mwenyezi Mungu, na kufaidika kwa njia ya kimantiki, ikizingatia siku za usoni.

Sera ya kiuchumi ya Uislamu pia imeelezewa katika Qur’ân, kwa maneno mengi yasiyokuwa na shaka:

Page 2: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

2

غنيياءي مينكم ٧ك ل يكون دولة بي ٱل

“... ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu ...” [Al-Hashr 59:7]

Usawa wa wanadamu wote katika utajiri na faraja, hata ikiwa ni katika hali bora, haina dhamana kuwa ni miongoni mwa uzuri usiochanganyika kwa ubinadamu. Kwanza, kwa sababu vipaji vya asili havilingani miongoni mwa watu tafauti, kiasi cha kwamba hata ikiwa lau mtu angeanzisha kikundi cha watu wenye usawa kamili, hivi karibuni mfujaji wa mali atatumbukia kwenye shida na ataangalia tena kwenye bahati nzuri za wenzake kwa uchoyo na wivu. Kwa kuongezea, kwa misingi ya kifalsafa na ya kisaikolojia, inaonekana yakwamba kwa faida ya jamii ya wanadamu inafaa kuwe na viwango katika utajiri, fakiri akiwa na hamu na motisha ya kufanya kazi kwa bidii. Kwa upande mwengine, ikiwa kila mtu ataambiwa yakwamba hata kama atafanya kazi zaidi ya kile kinachotakiwa kwake kama kazi yake, hatapata malipo na atabaki kama wale ambao hawafanyi zaidi ya kazi zao, mtu atakuwa mvivu na asojali, na kipawa chake kikatokomea kwenye bahati mbaya ya ubinadamu.

Kila mtu anajua yakwamba maisha ya wanadamu ni yenye kuendelea daima, kwa njia ya utawala na unyonyaji mmoja baada ya mwengine wa vitu vyote ambavyo Mwenyezi Mungu alivyoviumba, haliyakuwa mtu anaona yakwamba wanyama wengine wote hawakubadilika chochote katika maisha yao tangu Mwenyezi Mungu alipoumba vizazi vyao. Sababu ya tafauti hii kama ilivyogunduliwa na wanabiolojia ni kujumuika kwa wakati mmoja kwenye mazingira ya kijamii, ushirikiano, na uhuru wa mashindano kwenye watu wa jamii moja, yaani, wanadamu na haliyakuwa wanyama wengine wakiwa wanateseka kutokana na ukosefu wa mahitaji yote au baadhi yake yenye umuhimu. Mbwa, paka na nyoka, kwa mfano, hawaundi hata familia; wanaendeleza kabila zao kwa njia ya “mapenzi” yasokuwa na gharama na ya muda mfupi. Wengine, kama vile kunguru na njiwa huunda familia kwa njia ya wanandoa, na juu ya hayo, hata kama mume husaidia katika ujenzi wa kiota, kila mshiriki wa wanandoa hutegemea pato lake mwenyewe kwa kukimu maisha yake. Labda ushirikiano wa kijamii ulioendelea zaidi hupatikana miongoni mwa nyuki, chungu na mchwa (chungu weupe): Hao wanaishi ki-Jumuiya, na usawa kamili katika maisha yao, tena juu ya hayo, bila ya mashindano yoyote miongoni mwa jamii zao, na kwa sababu hiyo haiwezekani kwa mwenye akili zaidi au mwenye bidii zaidi kuishi kwa raha kuliko wengine. Kwa sababu hii, hakuna mageuzi wala mabadiliko, maendeleo machache kwenye aina yoyote ya vizazi hivi, kama walivyo kinyume cha vizazi vya wanadamu. Historia ya zamani ya mwanadamu inaonyesha yakwamba kila maendeleo na kila uvumbuzi wa njia za faraja uljitokeza kupitia ushindani na hamu ya uboreshaji, na pia kupitia kwenye viwango vya utajiri au umaskini miongoni mwa watu, mmoja juu ya mwengine. Ndio, uhuru uliokamilika ungewaongoza watu wenye tabia za kishetani kuwadhalilisha wahitaji, na kuwafyonza pole pole. Kwahivyo ilihitajika katika kila ustaarabu wa maendeleo na kila utamaduni uliostawi kuwalazimisha washiriki wake baadhi ya majukumu (kama vile amri ya ulipaji wa kodi, marufuku ya kupatikana njia ya kuomba usaidizi kwenye dhulma na ulaghai n.k.), na kupendekeza baadhi ya vitendo vya ziyada (kama kutoa swadaka na kugharimika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu), lakini juu ya hayo, kuwa na uhuru mwingi wa mawazo na vitendo kwa washiriki wake, ili kila mmoja ajinufaishe mwenyewe, familia yake, marafiki zake na jamii nzima kwa ujumla. Hii ndiyo dharura ya Uislamu, na pia ni yenye kuafikiana na hali za kimaumbile.

Page 3: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

3

Ni juu ya msingi wa kanuni hii ya maadili yakwamba Uislamu umeunda mfumo wake wa uchumi. Ikiwa inawastahamilia walio wachache katika matajiri, inawawekea majukumu yaliyo mazito: wanapaswa kulipa kodi kwa niyaba ya masikini, na wanazuiliwa kutekeleza njia mbaya za ukandamizaji, kuhodhi na kujilimbikizia mali. Kwa mwisho huu kutakuwa na baadhi ya maagizo au amri za makatazo, na pia baadhi ya mapendekezo - kwa kutoa swadaka na kuchinja - pamoja na ahadi ya malipo ya kiroho (mengine ya kidunia). Kwa kuongezea, inafanya, kwa upande mmoja, tafauti kati ya kiwango cha chini cha lazima na upendeleo wa kiwango cha juu, na kwa upande mwengine kati ya amri hizo na maagizo ya kisheriya yenye kuambatanishwa na vikwazo vya bidhaa na mengine yasiokuwa hayo, lakini kwa ambayo Uisilamu unajidhihirisha yenyewe kwa ushawishi na elimu peke yake.

Kwanza tutaelezea kwa maneno machache tabia hii ya maadili. Vielelezo vingine vitatuwezesha kuelewa vizuri maana yake. Masharti ya msisitizo zaidi yameajiriwa na Uislam kuonyesha yakuwa kuomba misaada ya wengine ni jambo la kuchukiza na itakuwa ni aibu siku ya Kufufuliwa; bado wakati huo huo sifa isiyo na kifani imetolewa kwa wale wanaokuja kusaidia wenzao, watu walio bora kwa kweli ni wale ambao wanaojitolea na wakawapendelea wengine juu ya nafsi zao. Vile vile uchoyo na

ufujaji, zote mbili, zimekatazwa. Siku moja Mtume wa Uislam ( وسلم عليه الله صلى )

alikuwa na haja ya pesa nyingi kwa sababu fulani za umma. Mmoja wa marafiki zake akaleta kiyasi fulani cha kutoa kama mchango wake, na aliposhurutishwa na Mtume

( موسل عليه الله صلى ), akajibu: "Sikuacha nyumbani isipokuwa mapenzi ya Mwenyezi

Mungu na Mtume wake.” Mtu huyu alipokea sifa za dhati kutoka kwa Mtume ( الله صلى

وسلم عليه ). Zaidi ya hayo, katika tukio jengine, swahaba wake mwengine, aliyekuwa

mgonjwa sana, alimwambia alipokuja kumjulia hali yake: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Mimi ni mtu tajiri, na ninataka kurithisha kila kitu nilicho nacho kwa ustawi wa

watu maskini." Mtume (صلى الله عليه وسلم) akamjibu: “Hapana, ni bora kuwaachia

jamaa zako njia ya kujitegemea ya kimaisha kuliko yakwamba wawe ni wenye kuwategemea wengine wakalazimika kuomba.” Hata kwa theluthi mbili na kwa nusu ya

mali, maneno ya Mtume (صلى الله عليه وسلم) yalikuwa: “Hiyo ni nyingi sana.” Wakati

pendekezo lilipowasilishwa ili kutoa theluthi moja ya mali hiyo kwa hisani, alisema:

“Kweli, hata thuluthi ya tatu ni kiasi kikubwa." (cf. Bukhari). Siku moja Mtume ( صلى .alimuona mmoja wa maswahaba zake akiwa amevalia mavazi duni (الله عليه وسلم

Alipoulizwa, alijibu: “Ewe Mjumbe wa Allâh! Mimi si masikini; nimependelea tu kutumia utajiri wangu kwa masikini badala ya kujitumilia mimi mwenyewe.” Mtume

akasema: “Hapana; Allâh anapenda kuona juu ya mtumwa Wake (صلى الله عليه وسلم)

athari za fadhila ambazo amempa!” (taz. Abu Dawud na Tirmidhi). Hakuna ubishi katika mwelekeo huu; kila moja ina muktadha wake na inahusiana na kesi tafauti za mtu binafsi. Tumepewa nafasi ya kuamua mipaka ya chaguo la busara kwa ziada ya kiwango cha lazima, kwa kutazama watu wengine wa jamii.

MIRATHI

Katika hali zote mbili, haki ya mtu binafsi ya kujitolea mali yake, na haki ya mali inayokusanywa ya kila mtu, kwa kiyasi cha makadirio ya mtu kuwa ni muhusika katika jamii, ni lazima aridhike wakati huo huo. Tabia za kibinafsi zinatafautiana sana.

Page 4: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

4

Ugonjwa au ajali nyengine vilevile zinaweza kumuathiri mtu kwa kila sehemu. Kwa hivyo inahitajika yakwamba nidhamu fulani zinapaswa kuwekwa kwake kwa faida ya ukusanyaji.

Kwa hivyo Uislamu umechukua hatua mbili; kwanza usambazaji wa lazima wa mali ya mtu aliyekufa kati ya ndugu zake wa karibu, na pili kizuizi juu ya uhuru wa mirathi kwa kupitia nyaraka za mirathi na hati ya wasiya. Warathi wa kisheria hawahitaji wasiya wowote wa umiliki, na urathi wa mali ya marehemu kwa viwango vilivyopangwa na sheria. Hati ya Wasiya inahitajika tu kwa niaba ya wale ambao hawana haki ya kurithi kutoka kwa mtu aliyekufa.

Kuna usawa katika jamaa za kitengo hicho-hicho kimoja, na mtu hawezi kumpa mtoto mmoja wa kiume (mkubwa au mdogo) zaidi ya mwingine, iwe mkubwa wa watoto. Gharama za kwanza juu ya mali iliyoachwa na marehemu ni gharama za mazishi yake. Kilichobaki hapo kinakwenda kwa wadai wake, deni likipewa kipaumbele juu ya “haki” ya warathi. Katika nafasi ya tatu, hati yake ya wasiya inatekelezwa, kwa kipimo na kiwango ambacho isizidi theluthi moja ya mali inayopatikana (baada ya mazishi na malipo ya deni). Ni tu baada ya kutimiza majukumu haya ya awali ambapo warathi huzingatiwa. Mwenzi (wa kiume au wa kike) wa maisha, wazazi, vizazi (wana na binti) ndio warathi wa daraja la kwanza, na wanarithi katika hali zote. Ndugu na dada, na jamaa wengine wa mbali wanarithi kutoka kwa mtu aliyekufa tu kwa kukosekana kwa jamaa wa karibu. Kati ya hawa jamaa wa mbali tunapata wajomba, shangazi, binamu, mpwa na wengine.

Bila ya kuingia katika maelezo ya kiufundi, sheria fulani za kimsingi zinaweza kuelezewa. Mwuaji huwekwa kando na urathi wa muathirika wake mwenyewe, hata ikiwa mahakama itaamua yakwamba ilikuwa ni kesi ya kifo kwa ajali ya hiari (bahati mbaya). Wazo la msingi linaonekana kuwa ni kuzuia majaribu yote ya kumuua jamaa

tajiri kwa kuzingatia urathi wa mapema. Mtume ( وسلم عليه الله صلى ) pia, amekataza

urathi kati ya jamaa wa dini tafauti, hata kati ya mume na mkewe. Walakini, haki ya kutoa zawadi na hati ya wasiya inaweza kutolewa katika suala hili; kwa mfano, mume wa Kiislamu anaweza kurithisha hata kwenye kitanda chake cha mauti, sehemu ya mali yake kwa niaba ya mke wake ambaye sio Mwislamu. Kwa nguvu ya hali ya kimataifa na kisiasa ya nyakati zao, wanavyuoni wa Kiislamu wa zamani wameanzisha kizuizi kingine, v., Tofauti ya eneo (kwa mfano, utaifa wa kisiasa) kama kizuizi cha urathi. Ni dhahiri mikataba ya kisheria inaweza kudhibiti swali la sheria za kibinafsi za kimataifa, kwa maana tofauti, juu ya msingi wa kutendeana.

Katika nchi ambazo sheria ya urathi wa Kiisilamu haitekelezwi na serikali, bado haki ya hati ya wasiya inatambulika, wenyeji wa Waislamu wanaweza, na ni lazima, watumie kifaa hicho, ili kutekeleza jukumu lao la kidini kuhusu utaftaji wa mali zao baada ya kifo chao.

WASAYA

Tumeelezea hivi karibuni tu yakwamba haki ya urathi kwa njia ya wasiya inafanya kazi tu katika mipaka ya theluthi moja ya mali hiyo, kwa niaba ya watu mbali ya wadai na warathi. Madhumuni ya hukumu hii yanaonekana kuwa mara mbili: Kwanza, kumruhusu mtu kurekebisha mambo, katika hali za kushangaza, wakati hukumu ya kawaida inaposababisha ugumu; na theluthi moja ya mali hiyo inatosha kutekeleza majukumu yote ya maadili. Kusudi jengine la sheria ya wasiya ni kuzuia mkusanyiko wa mali

Page 5: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

5

mikononi mwa wachache, jambo ambalo lingetokea ikiwa mtu atatoa mali yake yote kwa njia ya wasiya kwa mtu mmoja, na kumtenga kabisa jamaa yake wa karibu. Uislamu unapenda ugawanyaji wa mali kati ya idadi kubwa ya watu iwezekanavyo, kwa kuzingatia masilahi ya familia.

+18042928373

MALI YA UMMA

Mtu pia ana majukumu kama muhusika wa familia kubwa, yaani, jamii na Jimbo ambalo analoishi mtu. Katika mviringo wa uchumi, mtu hulipa ushuru, ambao serikali inasambaza kwa faida ya ukisanyaji huo.

Viwango vya ushuru hutafautiana kulingana na aina anuwai za vyanzo vya mapato, na inatupa moyo kufahamu yakwamba Qur’ân, ambayo inayotoa maelekezo swahîh kuhusu matumizi ya bajeti, haikutangaza hukumu wala viwango vya mapato ya Serikali.

Katika hali ya kuheshimu uadilifu wa mafundisho ya Mtume (صلى الله عليه وسلم) na

warathi wake wa karibu, ukimya huu wa Qur’ân unaweza kufasiriwa kama kutoa hiyari kwa serikali kubadili sheria za mapato kulingana na hali, kwa maslahi ya watu.

Katika wakati wa Mtume, kulikuwa na ushuru wa kilimo, na wakulima walikabidhi sehemu ya kumi ya mavuno, maadamu ilikuwa ni juu ya kiwango cha chini kisichotozwa ushuru na walimwagilia maji ardhi zao kwa maji ya mvua au ya chemchemi, na nusu ya kiwango hicho kwa upande wa visima kama njia ya umwagiliaji. Katika biashara na unyanyasaji katika migodi, mtu alilipa 2 1/2% ya thamani ya bidhaa. Ama kuhusu ushuru wa uingizaji kutoka nchi za nje, kuhusu viongozi wa misafara ya nchi za ng’ambo kuna ukweli wa kuvutia ambao unaopaswa

kuletwa kwa faida ya kupatikana faraja. Katika zama za Mtume ( وسلم عليه الله صلى ),

hawa walikuwa wanapewa zaka kama sehemu ya kumi ya mavuno kama ushuru wa forodha; Khalifa Umar aliwapunguzia wageni nusu ya ushuru huo, kuhusu aina fulani za vyakula na vinywaji zilizoingizwa katika mji wa Madinah (kama ilivyopokewa na Abu ‘Ubaid). Utangulizi huu wa mamlaka makubwa huangazia juu ya kanuni muhimu za

sera ya hazina ya Uislamu. Wakati wa Mtume ( وسلم عليه الله صلى ), kulikuwa na ushuru

wa mifugo ya Ngamia, Kondoo na Mbuzi, na Ng'ombe maadamu walikuwa wakilishwa kwenye malisho ya umma na walizidi kwa idadi kiwango cha chini kisichotozwa ushuru. Msamaha uliwekwa zaidi kwa wanyama wa mzigo na wale walioajiriwa kwa kulima na unyunyizaji wa maji.

Kulikuwa na ushuru wa 2 1/2% juu ya akiba na juu ya fedha na dhahabu. Hili lililazimisha watu kutumia utajiri wao kwa kuongezeka, na sio kujiingiza katika shughuli za kuhodhi kusikofaa.

MATUMIZI YA SERIKALI

Qur’ân (9: 60) imefaradhisha kanuni zinazosimamia bajeti ya matumizi ya Jimbo katika Uislamu kwa maneno yafuatayo:

يقابي إينما ٱل وبهم وفي ٱلر يلفقراءي وٱلمسكييي وٱلعميليي عليها وٱلمؤلفةي قل ت ل دق ص

علييم حكييم ي وٱلل ين ٱلل فرييضة م بييلي ي وٱبني ٱلس غريميي وفي سبييلي ٱلل ٦٠وٱل

Page 6: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

6

“Wa kupewa sadaka (yaani; kodi juu ya Waislamu) ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia (kodi), na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa (yaani; watumwa na wafungwa wa kivita), na wenye madeni, na

katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Allâh ni Mwenye kujua Mwenye hikima.” [At-Tawbah

9:60]

Hivi vichwa vinane vya matumizi yenye kushughulikia mahitaji yote ya shughuli za ukusanyaji, vinahitaji ufafanuzi wa kuwawezesha kupata ufahamu wa anwai zao kamili na matumizi.

Neno swadaqât, ambalo tunatafsiri kama kodi ya Jimbo kwa Waislamu, na ambalo ni aina nyengine ya neno la zakat, inamaanisha ushuru uliolipwa na Waislamu kwa serikali yao, katika nyakati za kawaida, iwe kwenye kilimo, biashara ya migodi, tasnia, ufugaji wa Ng'ombe, akiba au vichwa vingine. Hizi huondoa kodi ya muda iliyowekwa katika nyakati zisizo za kawaida, mapato yanayotozwa kwa wasio Waislamu, - wahusika au wageni wa nchi za ng’ambo, - na pia michango yote isiyo ya lazima. Vitabu vya

taratibu za kisheriya vya Uislamu wa mapema, na haswa maneno ya Mtume ( صلى الله .hayakuacha shaka yakuwa neno swadaqât lilitumika kwa maana hii (عليه وسلم

Haikuhusu swadaka hata kidogo, ambayo haiwezi kuwa ya lazima wala iliyodhamiriwa kwa kulingana na idadi na wakati wake wa malipo. Kiwango cha sawa kwa swadaqât ni “infaq fl sabil Allah”, matumizi katika njia ya Mwenyezi Mungu, au tatauwu, swadaka ya hiari.

Aina mbili za kwanza za wahitaji (fuqara ') na masikini (masâkin), ambazo karibu

zinafanana, hazikuelezewa na Mtume (صلى الله عليه وسلم); kuna ikhtilafu kubwa ya

maoni. Kulingana na maneno na mazoezi ya mara kwa mara ya khalifa Umar, (yaliyorekodiwa na Abu Yousuf katika kitabu chake cha Kitab-al-Kharaj na Ibn Abi Shaibah katika Musannaf yake), fuqara 'ni masikini miongoni mwa Waislamu, na masakin ni miongoni mwa wasio Waislam wanaoishi katika eneo la Kiislamu, kama vile Mayahudi. Katika Futuh al-Buldan yake, Baladhuri anatoa mfano mwingine wa khalifa huyo huyo, aliyepeana pensheni kwa Wakristo wa Jabiyah (Syria) kutoka kwenye swadaqât yaani; mapato ya zakât. Mwanachuoni ash-Shâfi-i alidhani yakwamba maneno hayo yanafanana kabisa, na kwamba Mwenyezi Mungu, kwa fadhila Zake, aliwataja majina mara mbili ili apate kufanya mpango wa malipo mara mbili. Kulingana na mamlaka hii, kwa kuwa kila mmoja wa vichwa vinane kwenye Âya ya Qur’ân anapaswa kupokea moja ya nane ya mapato ya Serikali, maskini angepokea nane-mbili. Kuwa iwe kile mbili-nane. Iwe itakavyokuwa, jukumu la kwanza la Nchi ni kuona yakwamba hakuna mkaazi kwenye ardhi ya Kiislamu aliyenyimwa njia ya kujipatia riziki: chakula, mavazi, malazi, nk.

Jambo linalofuata linahusu mishahara ya watendaji: watozaji, wahasibu, wadhibiti wa matumizi, wakaguzi wa wahasibu, nk Ikiwa ukweli utaambiwa, aina hii inajumuisha utawala mzima (wafanyi kazi wa serikali), raiya, jeshi na kidiplomasia, kama mtu anavyoweza kuona maelezo ya aina ya wenye kufadhiliwa. Mwanahistoria, al-Baladhuri (katika al-Ansab yake) amehifadhi hati ambayo khalifa Umar aliyomuamuru gavana wake wa Syria: "Tuletee (Madinah) mtaalam wa ki-Giriki, ambaye anayeweza kutupangia vizuri hesabu za mapato yetu”. (hisaba faraidina). Hatuhitaji mamlaka bora kwa kudai yakwamba wasio Waislamu hawangeweza kuajiriwa tu katika usimamizi wa Jimbo la Kiisilamu, lakini pia kuwa wanufaike na swadaqât iliyotozwa Waislamu pekee.

Page 7: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

7

Jamii ya wale ambao nyoyo zao zinapaswa kupatanishwa zinaweza kueleweka kwa urahisi na neno la kisasa "fedha za siri". Katika kitabu chake al-Ahkam as-Sultaniyah, Mwanachuoni Abu-Ya’la al-Farra’ amesema: “Kwa wale ambao nyoyo zao zinapaswa kushindwa, ni wa aina nne:

1. Wale ambao nyoyo zao zinapaswa kushindwa kwa kuja kwao kuwasaidia Waislamu;

2. Au kwa kuwazuia kuwadhuru Waislamu;

3. Kwa kuwakaribisha waingie kwenye Uislamu; na

4. Kwa kuwaalika kupitia kwao, jamii zao na familia zao kuukubali Uisilamu. Ni halali kugharimika kwa kila mmoja wao wakiwa ni Waislamu au washirikina.

Kwa kutaja kifungu cha maneno “kuziacha huru shingo”, mtu mara nyingi ataelewa matumizi ya aina mbili: ukombozi wa watumwa, na kuwakomboa wafungwa wa kivita mikononi mwa adui. Kulingana na sheria ya Kiislamu (Qur’ân 24/33), kila mtumwa ana haki ya kununua dhamana yake kwa kulipa thamani yake kwa bwana wake; na ili kupata kiasi kinachohitajika anaweza kumlazimisha bwana wake ampe vifaa vya kufanyia kazi, na katika kipindi hiki hahitaji kumtumikia bwana wake. Zaidi ya hayo, kama tulivyo ona hivi punde, ni jukumu la serikali kutenga kila mwaka katika bajeti kiasi fulani cha kusaidia watumwa kununua uhuru wao (kujikomboa). Hati ya wakati wa Khalifa wa Umaiyad, 'Umar ibn' Abd al-Aziz (iliyopokewa na Ibn Sa'd), inasema, yakwamba malipo ya kujikomboa na serikali ya Kiislamu ni pamoja na kuwakomboa hata wasio Waislamu ambao wangelikuwa wamefanywa kuwa ni wafungwa na adui.

Orodha ya wale walio na deni kubwa ina, kulingana na mazoea ya zama zinazotambiliwa kuwa bora, mfululizo kamili wa maombi: mmoja aliwasaidia wale ambao waliopata shida kama vile mafuriko, mitetemeko ya ardhi, nk. Haiwakusudii maskini, ambao tayari waliotajwa mwanzoni mwa Âyah, lakini kwa wale matajiri walioathirika kutokana na hali mbaya, zaidi ya uwezo wao. Khalifa 'Umar alianzisha sehemu maalum katika Hazina ya Umma, ili kukopesha pesa, bila ya riba, kwa wale ambao walikuwa na mahitaji ya muda mfupi na kutoa dhamana muhimu ya ulipaji. Khalifa mwenyewe alikuwa akiuomba msaada kwa mahitaji yake ya kibinafsi. Inajieleza yenyewe bila ya kusema yakwamba “utaifa” wa kukopesha bila ya riba ndio kiambatanishi muhimu cha uharamu wa riba katika Uislamu. Khalifa huyo huyo alikuwa akikopesha pesa za umma hata kwa wafanyabiashara kwa muda maalum, na hazina ikishiriki pamoja nao kwa asilimia ya hisabu zao pindi wanapofunga takwimu za biashara mwisho wa mwaka, hawashiriki katika faida tu, bali pia itokeapo hasara. Maombi mengine ya matumizi ya Jimbo hili yalikuwa ni kwa aina ya bima ya jamii. Ikiwa mtu akipatikana na hatia ya mauaji bila kukusudia na hakuweza kulipa pesa za damu, inayohitajika katika sheria, kwa kujitegemea yeye mwenyewe, serikali ikamsaidia chini ya kichwa hiki cha bajeti, kama inavyothibitishwa na kesi kadhaa za

kitendo cha Mtume (صلى الله عليه وسلم). Tutarejelea jambo hili tena, baadaye kwa

undani zaidi.

Kifungu cha maneno “katika njia ya Allâh”, katika istilahi ya Kiisilamu, inaashiria katika tukio la kwanza, ulinzi wa kijeshi na matumizi kwa wafanyikazi, vifaa, n.k Lakini, kwa kweli, istilahi hiyo inatumika kwa kila aina ya kazi za uhisani, kama vile kuwasaidia wanafunzi, kutoa hiba (usaidizi wa kifedha) na misaada katika njia za kidini kama vile ujenzi wa misikiti, nk.

Kifungu cha mwisho kinahusu mawasiliano na msongamano wa watalii kwa maana pana: ujenzi wa madaraja, barabara, hoteli, mikahawa, usalama wa njia (wakiwemo

Page 8: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

8

polisi) mipango ya usafi, uchukuzi wa wasafiri, na kila faraja inayotolewa kwa wageni wakati wa safari zao, ikiwemo kujitolea kuwakirimu bila malipo na kulingana na njia zinazopatikana. Zamani ukarimu kama huo ulikuwa ukihakikishiwa kwa muda wa siku tatu katika kila mahali pa makaazi.

Ili kushukuru fadhila hizi za mwelekeo wa Qur’ân, mtu lazima ukumbuke yakwamba wakati huo ulikuwa ni mwanzoni mwa Uislamu, karne kumi na nne zilizopita. Hapakuwa na mengi ambayo yaliyoweza kuongezwa kwenye vichwa hivi vya matumizi. Ilionekana kana kwamba imeafikiana vilivyo katika nyakati zetu katika Jimbo linaloendelea na kustawi, wakiwa katika kujihusisha kikamilifu juu ya ustawi wa raia wake.

KODI ISIYO YA KAWAIDA

Swadaqât zilikuwa ndizo kodi za pekee katika Taifa wakati wa Mtume ( صلى الله عليه na Makhalifa wa waongofu. Katika nyakati za baadaye, katika matukio ya mahitaji (وسلم

maalum, wanavyuoni walikubali uwezekano wa kisheria wa kutoza malipo ya nyongeza, juu ya msingi madhubuti wa uwekevu, kwa dharura yenye uwezekano. Ushuru kama huo unaitwa Nawa'ib (majanga).

BIMA YA JAMII

Hatari peke yake zinazojumuisha malipo makubwa kutoka kwenye vifaa vya bima, na hizi hutofautiana kulingana na nyakati na hali za kijamii. Miongoni mwa Waarabu wakati wa kuanza kwa Uislamu, maradhi ya kila siku hayakujulikana, na huduma ya matibabu haikugharimu utendakazi wowote; mtu wa kawaida alikuwa akijenga nyumba yake na mikono yake mwenyewe, na hakuwa akilipa hata sehemu kubwa ya vifaa. Kwa hivyo ni rahisi kuelewa ni kwanini mtu alikuwa hana haja ya bima dhidi ya ugonjwa, moto, nk. Badala yake, bima dhidi ya kushikwa mateka na dhidi ya mauwaji ndiyo

yaliyokuwa mahitaji ya kweli. Tayari katika zama za Mtume (صلى الله عليه وسلم), nukta

hii ilipata mvuto wa tanabuhi; na mielekeo kadhaa ilifanywa ambayo iliyokuwa na minyumbuko ya mahitaji zaidi na mabadiliko ya hali za mazingira. Kwahivyo, katika Katiba ya Jiji la Jimbo la Madinah la mwaka wa kwanza wa Hijrah, bima hii iliitwa ma’aqil na ilifanya kazi kwa njia ifuatayo. Ikiwa mtu alifanywa kuwa mfungwa wa ki-vita na adui, malipo ya kikombozi yalihitajika kwa ununuzi wa ukombozi wake. Vivyo hivyo, mateso yote ya mwili au mauaji yanayoweza kushukiwa yanahitaji malipo ya uharibifu au pesa za damu. Hii mara nyingi ilikuwa ikizidi uwezo wa mtu anayehusika,

mfungwa au muhalifu. Mtume ( وسلم عليه الله صلى ) alipanga kuwepo na bima ya ubia juu

ya msingi wa maafikiano katika pande mbili: washiriki wa kabila wanaweza kutegemea hazina kuu ya kabila lao, ambayo kila mtu alichangia kulingana na uwezo wake; na ikiwa hazina ya kabila ilithibitisha kutokuwa na uwezo, makabila mengine yanayohusiana au makabila ya jirani yaliwajibika kutoa misaada kwa wenzao. Mfumo maalum wa wenye mamlaka ya uongozi ulianzishwa kwa kupanga muungano wa makundi na kuwa kundi lililokamilika. Huko Madinah, makabila ya wa-Answari

yalijulikana sana; Mtume ( وسلم عليه الله صلى ) aliwaamuru wakimbizi wa Makkah waweko

pale, ambao asili zao walikuwa ni makabila tafauti ya Makka, au walikuwa ni watu wa Abyssinia, au Waarabu waliotoka maeneo tafauti, wote wanapaswa kuunda “kabila” jipya lao, kwa lengo la bima ya kijamii iliyosemwa.

Page 9: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

9

Baadaye katika zama za Khalifa ‘Umar, maafikiano ya kuwepo kwa makubaliano baina ya makundi ya bima yalipangwa juu ya msingi ya wataalamu wenye ujuzi, usimamizi wa idara za kijeshi na za kiraiya, ambazo kila mmoja wao alipokuwa, au hata kwenye sehemu walizotoka. Wakati wowote inapohitajika, serikali kuu au ya mkoa hujitokeza kwa usaidizi wa vikundi hivyo, kama tulivyoelezea hapo juu wakati wa kuzungumzia kuhusu matumizi ya Serikali.

Kimsingi, bima inaashiria upunguzaji wa mzigo wa mtu binafsi kwa watu wengi iwezekanavyo, ili kupunguza uzito wa mzigo wa kila mmoja. Badala ya kampuni za kibepari za bima, Uislamu ulipendelea kuandaa bima juu ya msingi wa ushirikiano wa pande mbili na umoja, na kusaidiwa na mageuzi ya kimaendeleo kwenye makundi kufikia kilele katika Serikali Kuu.

Kundi kama hilo linaweza kujihusisha na biashara kwa msaada wa pesa zilizokaa tu ambazo hazijatumika, ili ziongezeke na kuwa nyingi. Wakati unaweza kuja, ambapo washiriki wa kundi wakaweza kusamehewa kabisa, kutokana na kulipa michango zaidi, na wanaweza hata kupokea kiasi fulani kama faida ya biashara. Iinakuwa ni jambo la kawaida kwa vikundi hivi vya misaada ya pande mbili vinaweza kupata bima dhidi ya hatari za kila aina, kama vile ajali za trafiki, moto, hasara katika uchukuzi, na kadhalika. Vilevile linakuwa ni jambo la kawaida kwa biashara ya bima kuweza “kutaifishwa” kwa hatari zote au aina fulani, kwa mfano, kwa sababu za muda mfupi kama vile kutuma mizigo, nk.

Bila kuingia katika maelezo ya kiufundi, inaweza kuelezewa yakwamba bima ya ubepari, ambayo mtu aliye na bima hashiriki katika faida za kampuni kulingana na michango yake, haivumiliwi katika Uislamu. Kwani, bima kama hiyo hufanya aina ya mchezo wa bahati nasibu.

Katika mapito, tunaweza kutaja taasisi nyengine ya kijamii ya wakati wa Khalifa ‘Umar. Alikuwa ameandaa mfumo wa malipo ya uzeeni kwa wenyeji wote wa nchi - na kulingana na Kitab al-Amwâl cha ibn Zanjuwaih na ar-Risalah al-‘Uthmaniyah cha al-Jahiz, hata wasiokuwa Waislamu walikuwa miongoni mwa wenye kunufaika na pesa hizi za uzeeni - kiyasi cha kwamba muda mchache tu pindi anapozaliwa mtoto, ataanza kupokea kiinua mgongo fulani. Wazee walipokea kiwango cha chini cha kuweza kukimu mahitaji muhimu ya kimaisha. Hapo mwanzoni, Khalifa alikosea mahali fulani miongoni mwa aina tafauti za vikundi vya wastaafu; na kama kiwango cha chini kilikuwa 1, basi aliyebahatika zaidi alipokea 40; lakini hadi mwishoni mwa maisha yake, aliamua kuzingatia usawa kamili, lakini alikufa kabla ya mageuzi haya yalipoweza kuanzishwa. Taasisi hii, iliyopewa jina la “Diwan” na 'Umar, inaonekana

asili yake ilianzia wakati huohuo wa Mtume (صلى الله عليه وسلم), kama taarifa ifuatayo

inavyodokeza: “Msingi wa shughuli hii ni hadithi ambayo Mtume (صلى الله عليه وسلم)

alimchagua Mahmiyah ibn Jaz' kuwa msimamizi wa serikali ya tano ya ngawira iliyotekwa kwenye Banu’l-Mustaliq; na kwa hakika Mahmiyah alikuwa anasimamia serikali ya tano ya mali za ngawira. Sadaqat ( ushuru wa zakat) zilisimamiwa kando, na

zilikuwa na kazi zao fulani. Mtume (صلى الله عليه وسلم) alikuwa akitumia Swdaqât kwa

watoto Mayatima, wanyonge na masikini: ikiwa yatima atafikia umri wa kubaleghe na akaanza kuwajibika na huduma za jeshi (Jihad), alikuwa akihamishwa kutoka kwenye orodha ya wenye kunufaika wa sadaqat hadi kwenye ile ya fay’, juu ya hayo, iwapo atakataa kushiriki kwenye huduma za kijeshi, hatofaidika tena kutokana na Swadaqât na ataamrishwa atafute ajira yake mwenyewe.” (cf. Sarakhsi, Sharh as-Siyar al-Kabir, ed. Munajjed, $ 1978).

Page 10: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

10

MCHEZO WA KAMARI

Katika kuharamisha haya, [Qurân 5:90] imeziainisha kama “kazi za Shetani”; na hii imetokana na sababu inayokubalika. Inatambuliwa yakwamba maovu mengi ya kijamii hutokamana na usambazaji mbaya wa mali ya kitaifa, baadhi ya watu wanakuwa matajiri sana na wengine masikini sana na kwa sababu hiyo wanaangukia kuwa waathiriwa kwenye unyanyasaji wa matajiri. Katika michezo ya bahati nasibu na kamari, kuna jaribio kubwa la ushawishi wa pato la haraka na rahisi, na mara nyingi pato la rahisi ni baya kwa jamii. Tuchukulie yakwamba katika mashindano - ya Farasi na wengineo - na katika bahati nasibu, ya umma au ya kibinafsi, na pia michezo mingine yote ya bahati, wananchi hutumia pauni milioni 3 kila wiki - kama ilivyo katika nchi fulani - kwa muda wa miaka kumi tu, jumla ya Pauni Millioni 1,560 hukusanywa kutoka kwa idadi kubwa ya wenyeji na kugawanywa tena miongoni mwa idadi ndogo ya kejeli. Chini ya asilimia moja ya watu huneemeka kwa gharama ya asilimia 99 iliyobaki. Au kwa matamshi mengine, asilimia 99 hufukarishwa ili kuwatajirisha asilimia 1, na asilimia hii 1 ya mamilioni zimeundwa na kuangamiza kwa mpangilio wa makusudi asilimia 99. Ema iwe ni michezo ya kamari, ikiwemo bahati nasibu, ya kibinafsi au kutaifishwa, ubaya wa kulimbikiza mali mikononi mwa wachache, kwa jasho la idadi kubwa sana, inafanya kazi kwa nguvu kamili. Kwahivyo, jumla ya uharamu wa michezo ya bahati nasibu na kamari katika Uislamu. Kama ilivyo katika bima za ubepari, michezo ya kubahatisha hubeba hatari za upande mmoja.

RIBA YA PESA ZA MKOPO

Labda hakuna dini duniani ambayo haijakataza riba. Tabia tofauti ya Uisilamu ni kwamba haujakataza mapato ya aina hii tu, lakini pia ilirekebisha sababu zinazopelekea uwepo wa taasisi hii mbaya katika jamii ya wanadamu.

Hakuna mtu anaelipa riba kwa hiari juu ya kile anachokikopa: yeye hulipa tu kwa sababu anahitaji pesa na anagundua yakwamba hangeweza kuipata bila kulipa riba.

Uislamu umeweka wazi tafauti kati ya faida ya kibiashara na riba juu ya kukopesha

pesa. Allâh (تعالى) Amesema:

ا يبو م ٱلر ٱليع وحر حل ٱلل ٢٧٥ وأ

“Lakini Allâh ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba.” [Al-Baqarah 2:275]

Baadaye kidogo (2/279), Akasema:

ين فإين رب م ذنوا بيم تفعلوا فأ ي ٱل ي لل ليكم ل م فلكم وإن تبت ۦ ورسولي مو

رءوس أ

٢٧٩تظليمون ول تظلمون “Basi mkitofanya jitangazieni vita na Allâh na Mtume wake. Na mkitubu, basi

haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.” [Al-Baqarah 2:279]

Page 11: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

11

Msingi wa marufuku ya riba vilevile ni kuhatarisha upande mmoja. Kwani wakati mtu anapokopa kiasi fulani kwa lengo la kupata ongezeko, inawezekana yakwamba hali isilete ishara ya nafasi nzuri ya kufaulu kwa mapato ya kutosha kuweza kulipa riba iliyoahidiwa, mkopeshaji asishiriki katika hatari ya ukandamizaji.

Haiwezekani kumlazimisha mtu kujinyima mwenyewe pesa zake, ili kukopesha wengine bilashi na bila ya riba. Tumeelezea kuwa Uislamu umeamuru yakwamba mojawapo ya mashtaka juu ya mapato ya Jimbo ni uwajibu wa kusaidia wale ambao waliojilimbikiza madeni makubwa kwa hayo, Hazina ya Umma hupanga mkopo usokuwa na riba, pamoja na kwa kuongeza mikopo inayotolewa na watu wahisani au mashirika, kuwasaidia wale ambao ni wenye kuzihitaji. Jambo la msingi ni msaada wa pande mbili na ushirikiano.

Kwa upande wa mikopo ya kibiashara, vilevile kuna mfumo wa mudarabah, ambao mtu hukopesha pesa na akashiriki kwa usawa katika faida na pia katika hasara. Ikiwa, kwa mfano, watu wawili wataanzisha shirika, kila mmoja akatoa nusu ya mtaji na kazi, usambazaji wa faida hautokuwa mgumu. Walakini, ikiwa mtaji utatoka kwa kundi moja na kazi kutoka kwa kundi jengine, au ikiwa hayo makundi mawili yatatoa mtaji lakini moja tu likafanya kazi, au viwango vyao vya ushirika visiwe sawa, kwa hali hiyo malipo ya kuridhisha ya kazi, kwa msingi wa masharti yaliyokubaliwa hapo awali yatazingatiwa kabla ya usambazaji wa mapato na faida hayajatekelezwa. Hapana shaka tahadhari zote zinazowezekana huchukuliwa, ili kuzuia hatari, lakini Uislamu unaamrisha yakwamba kwa ushirikiano wote wa mikataba, faida na vilevile hasara zinapaswa kuhusishwa na vyama vyote viwili vilivyoekeana mikataba.

Kwa kadiri benki zinavyohusika, shughuli zao kimsingi ni za aina tatu: kutoa pesa kutoka sehemu moja hadi nyengine, kuhakikishia usalama wa akiba ya wateja, na kukopesha wengine pesa kwa faida. Gharama za utenda kazi hubebwa na wale wanaotumia huduma ya benki. Suali linabaki la mikopo kwa biashara, tasnia au kazi nyengine yoyote ya biashara. Ikiwa benki inashiriki katika faida ya wadeni wake na pia katika hatari zao, Uislamu unaruhusu shughuli kama hizo za benki, vinginevyo sivyo.

Nguvu ya kujiamini imetokana na ujasiri. Ikiwa benki za akiba za serikali zitatangaza mwishoni mwa mwaka, na sio mwanzoni mwake, yakwamba wako katika nafasi ya kulipa kiyasi cha asilimia kadhaa na kadhaa ya faida kwa wateja, jambo hilo, sio tu kuwa itakuwa halali kulingana na Uislam, bali umma pia haungekuwa na kusita kuweka akiba zao na benki za serikali, licha ya ukimya hapo mwanzo kuhusiana na wingi wa faida inayotarajiwa. Kwani, kwa kawaida, mtu huwa na imani na huduma ya jamii.

Kwa kumalizia, msingi wa ushirikiano wa pande mbili katika faida na hasara ni lazima zitekelezwe katika mikataba yote ya kibiashara.

TAKWIMU

Katika mipango yote, inahitajika kuwa na wazo la rasilimali inayopatikana. Mtume

( وسلم عليه الله صلى ) alipanga sensa ya idadi ya Waislamu, kama al-Bukhari alivyotuarifu.

Katika ukhalifa wa ‘Umar, sensa ya wanyama, miti ya matunda, na bidhaa nyengine ziliandaliwa; na katika mikoa mipya iliyopatikana, ardhi zenye rutuba zilipimwa. Kwa roho safi, iliyojaa wasiwasi juu ya ustawi wa umma, khalifa ‘Umar alikuwa na tabia ya kuwaalika wawakilishi wa watu wa mikoa tafauti, baada ya ukusanyaji wa ushuru, ili kujua ikiwa wana malalamiko yoyote dhidi ya tabia za wakusanyaji ushuru katika mwaka mzima.

Page 12: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

12

MAISHA YA KILA SIKU

Huwenda tukaweza kumaliza maelezo haya mafupi kwa kutaja marufuku aina mbili zenye umuhimu mkubwa, zenye kujenga kwa hakika sifa muhimu za tabia katika maisha ya kila siku ya Mwislamu, michezo ya bahati nasibu na vileo. Tumekuwa na hafla ya kujadili michezo ya bahati nasibu, ambayo mtu hutumia wakati kwa mfululizo wakati wa mwaka mzima bila ya kupata chochote kwa malipo. Ni hasara iliyoje kwa wale ambao ni dhaifu kiuchumi! Matumizi ya Pombe yana tabia ya kipekee yakuwa matumizi yake kwa kiasi kidogo humfanya mtu asijali chochote na kudhoofisha azimio lake la kuacha kulewa; na mtu anapokuwa amelewa, hupoteza udhibiti wa matendo yake. Mtu anaweza kisha kupotea pesa bila kugundua. Juu ya uovu huu, kutofuata kanuni za usafi kunaweza kuongezewa katika athari mbaya ya vileo ambavyo huambukizwa kwa watoto na vizazi vya baadae pia.

Aya moja ya Qur’ân (2/219) inazungumzia, kwa maneno ya kufurahisha:

ي ٱ و لمري ٱلونك عني يس كب مين لميسييلناسي وإثمهما أ قل فييهيما إيثم كبيير ومنفيع ل

فعيهيما ٢١٩ن“Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa

na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake.”

[Al-Baqarah 2:219]

Qur’ân haikatai yakwamba kuna baadhi ya faida fulani katika matumizi ya pombe, lakini inatangaza kuwa ni maasiya dhidi ya Aliyeweka Sheriya (Allâh). Katika Âyah nyengine (5/90) imeishusha daraja hadi kwenye kiwango sawa na ibada ya sanamu, na kuitangaza kuwa ni kazi ya mikono ya Shetani;

ها يأ يين ٱ ي ٱو لمر ٱ ءامنوا إينما ل نصاب ٱ و لميسي

زلم ٱو ل

ين عملي ل يطني ٱريجس م لش

يبوه ٱف ٩٠لعلكم تفليحون جتن“Enyi mlioamini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga

ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.” [Al-Mâ’idah 5:90]

Na kuongezea, iwapo mtu angependelea kuwa na furaha katika Milimwengu miwili, atapaswa kujiepusha na michezo ya bahati nasibu na vinywaji vya ulevi (Hamidullah, 1969).

Page 13: DR. MUHAMMAD HAMIDULLAH

13

References:

Hamidullah, M. 1388H/1969), “. The Economic System of Islam” in Introduction to Islam, Paris,

Centre Culturel Islamique (New Enlarged edition), (first published in 1957